Sura ni mwanajeshi ila mawazo ni ya Polepole

Sura ni mwanajeshi ila mawazo ni ya Polepole

Polepole alinyimwa maslahi gani wakati alikuwa Balozi.
sasa we unadhani mpaka aanze kukichafua sababu ilikuwa ni nini? Kutenguliwa ubalozi? Bila shaka ni big no!! Kumbuka anachokisema hata yeye hayuko salama kisheria!! Mi nahisi walimwaga ugali akaamua kumwaga mboga!!
 
Sura kweli ni mwanajeshi,

Sare kweli ni za kijeshi,

Ila mawazo (Talking Points) ni ya ndugu Humphrey Polepole.

Wale wana-CCM ambao walidhani kwamba Polepole ana ushawishi mdogo hapa nchini, kwamba ni mtu wa kupuuzwa walifanya mahesabu yao vibaya mno. Malalmiko yote ya kuharibika kwa Tanzania yanawalenga watu wakubwa wafuatao, Jakaya Kikwete, Edward Lowassa, Benard Membe na Rostam Aziz. Malalamiko ya ndugu H.Polepole yamegeuka kuwa The Official Narrative Against CCM's Rulling Elites, na hamuwezi kufanya lolote lile.

Mwanadamu anaweza kuficha mambo mengi, lakini hana uwezo kuficha JUA, MWEZI na UKWELI.
==========================================================
CCM na Watanzania huwa tuna kumbukumbu ndogo mno kwamba Tanzania hayawezi kutokea machafuko, lakini tunasahau kwamba yaliwahi kutokea huko nyuma zaidi ya mara nne kwa nyakati tofauti. Miaka ya 60 yalitokea, miaka ya 70 yakatokea na miaka ya 80 yakatokea, yakiongozwa na maafisa wa jeshi ambao hawakuridhika na sera za TANU/ASP/CCM.

Utofauti kipindi kile na kipindi hiki ni mmoja tu: UHALALI WA SERIKALI (Legitimacy). Serikali ilikuwa inaungwa mkono na wananchi wengi, hivyo jeshi lingepata shida kutawala hata kama wangefanikiwa. Mzee Nyerere alichokwa na sera zake, lakini watanzania walimuheshimu mno na wengi ndani ya vyombo vya usalama walikuwa na maswali kama:
​
  • Akishaondoka Mzee Nyerere nani atakuwa mbadala wake ?​
  • Huo mbadala wa Mzee Nyerere anaweza kuwa na hulka za kizalendo ? ​
  • Nyerere alikuwa na wafuasi kote Africa, ambao wamepita Tanzania na kuwa hadi maraisi wa nchi mbalimbali, unadhani tukimtoa Mzee Nyerere kinguvu hawataihujumu Tanzania na hata kuvamia nchi kijeshi ?​
  • Vipi kuhusu watanzania wa kawaida, mtawaambia nini kuhusu Nyerere wao ambaye kwao ni kama BABA na MUNGU MTU ?​
Madam Samia na Al-Hajj Kikwete hawana hii HOME FIELD ADVANTAGE, kwasababu wanabadilishika (They're Not Indispensable). Hawana kitu cha ziada ambacho kitafanya watanzania wawalilie zaidi zaidi ya sababu za UDINI na MASLAHI BINAFSI tu.

CCM + TISS, mlionywa sana, miaka na miaka. Haya mnayoyafanya yatakuja kuwatokea puani. Acheni matumizi mabaya ya vyombo vya dola na kuviingiza kwenye siasa za moja kwa moja na kuhujumu watu. Leo hii vyombo hivi vinaanza kufanya siasa dhidi yenu mnalalamika. Tulipofika hapa, sipo pazuri na sidhani kama kuna MWAFAKA WA KISIASA unaweza ukaleta SULUHISHO kwasababu kila upande uko kwenye vita ya uhai wake.

Wale wanaojiita kwamba ni WAZALENDO wanaamini kwamba CCM MTANDAO wakivuka 2025 basi Tanzania imekwisha. Huku CCM MTANDAO wanaamini kwamba wakitolewa MADARAKANI watashughulikiwa ipasavyo kuliko hata ambavyo JPM aliwashughulikia. Mara ya mwisho waliponea chupu-chupu, kipindi hiki watauwawa kabisa au kufungwa.

MWANADAMU HUVUNA ALICHOKIPANDA.......
MIAKA 30 TOKEA 1995, sasa CCM wanavuma walichokipanda miaka yote......
​
Politician wote ni waongo lakini kuna kuzidiana.

Hizi zogo lina tokea karibu na uchaguzi sababu ni vyeo. na ulaji.
Alokuwa hana anataka na alokuwa anwo hataki kuwacha.

Uwongo na ukweli na ghasdia zote zitatumika ukisha uchaguzi kutakuwa kimya.
Mawazo yangu haina haja ya vurugu na matusi na ghasia, watu watoke wote kwa wingi kupiga kura na wasiipigie wa gombeya wa CCM au Haribu Kura.
Maana mshindi lazime apate zaidi ya ailimia 50 ya kura zilopigwa.

Kuhusu utekaji si jambo zuri.
Lakini kote duniani ukiingia katika Deepstate basi ujuwe uta potea.

Kenya watu wanapotea ,Uganda Marekani UK France canada China Uarabuni na kote unakojuwa wewe.
Kote wana mbinu zawo zakupoteza watu.

Tanzani watu wlipotea Kabla ya Uhuru na Baada ya uhuru,
Wakati wa Nyerere,Mwinyi, Mkapa,Kikwete,Magufuli na sasa.
Sema mitandawo na technolgy sasa zimekuwa na watu wanapata habari haraka.
Pia kuhusu polepole hata hawo majirani hawajuwi habari za Polepole wala wahawamjuwi.

Tunaipenda Nchi yetu tufikirie kabla hatuja juta.
 
Back
Top Bottom