Super El nino 2026/2027.. El nino ya kihistoria

Super El nino 2026/2027.. El nino ya kihistoria

Duh! Mule sijui kama Kuna kitu kimebaki.
Hata kama kipo hakifai tena
98c6f790-2774-11ee-b1d7-8fdc93c2782e.jpg.webp
 
96 , 97 kama sikosei, nakumbuka tulikua tunamshawishi mama tuende kwa bibi moshi 😆
Hapana,,
1998 nakumbuka na nilikuwa mhanga mmojawapo.
Treni ya mwisho kufanya kazi nilikuwepo nakumbuka tulikuwa tukitoka likizo na ilikwamia maeneo ya bahi dodoma.
Serikali ikasema tukae hapo tusubiri msaada. abiria wengi tuliamua kutembea kundi letu tulikuwa na mbunge wa iramba mashariki wa wakati huo. pesa ilishindwa kufanya kazi yaani hela unayo mahitaji huwezi kupata vijiji vingi vilisombwa na maji.
Tukiwa tunatembea tulipata gari ya

super najmunisa abiria tulikaa mpaka juu ya siti pale ambapo abiria wanaegemea. Sasa maji yamejaa na dereva nadhani alikuwa anabuni tu njia Kuna sehemu gari ilipinduka sababu ya mawe Kuna vijana walikuwa wamekaa juu kule sehemu ya mizgo mmoja alifariki na aliachwa njiani,, kwa sababu maji yalikuwa yanazidi na hayupo aliyekuwa tayari kusimama mafuriko yamkute porini.
Nina hakika mdogo wangu familia hazikutamani kusafiri kwa sababu njia nyingi zilikatika, mawasiliano hayakuwepo na mbaya zaidi barabarani kulikuwa na maiti nyingi zilizosombwa na maji.

El nino na ajari ya Mv bukoba ndio vitu ambavyo rais Benjamin mkapa analaumiwa na waathirika utadhani alisababisha yeye binafsi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom