Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,577
- 46,556
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya hewa ya El Niño kuanzia Septemba na kuendelea hadi Oktoba, Novemba na Desemba 2026, huku athari zake zikitarajiwa kuendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2027.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Agosti 18, 2027 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Ladislaus Chang’a amesema uwepo wa El Niño yenye nguvu unaweza kusababisha vipindi vya mvua kubwa pamoja na kuanza mapema kwa mvua za msimu katika baadhi ya maeneo.
Chang’a amezitaka Idara na Taasisi mbalimbali Nchini, ikiwemo Mamlaka za Bandari, reli, usafiri wa anga pamoja na Sekta ya Afya, kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
“Tunatoa maangalizo mawili la kwanza ni kutokana na uwepo wa El Nino yenye nguvu kubwa kuelekea Mwezi Oktoba, Novemba na Disemba na mwanzoni mwa 2027 vipindi vya mvua kubwa vinaweza kuanza Septemba pamoja na mvua za vuli, pia kuwepo kwa El Nino kunaweza kusababisha kuanza mapema kwa mvua za msimu,”.