Super El nino 2026/2027.. El nino ya kihistoria

Utabiri wa sasa unaonyesha kuwepo kwa "Super El Niño" inayokuwa kwa kasi kubwa na inayoweza kuweka historia.
Hali hii inatokea katika Bahari ya Pasifiki na inatarajiwa kufikia kilele mwishoni mwa mwaka 2026, kisha kuendelea hadi mapema msimu wa kuchipua wa mwaka 2027. Wanasayansi wa hali ya hewa wanaonya kuwa mfumo huu unakua haraka kuliko kawaida na unaweza kufikia viwango vya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumbukumbu zilipoanza kuwekwa mnamo mwaka 1950.

Makubaliano ya hivi karibuni ya kielelezo kutoka taasisi kubwa kama Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha NOAA na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) yanaonyesha uwezekano wa asilimia 96 hadi 97 kwa El Niño hii kudumu msimu wote wa baridi wa kizio cha kaskazini.

Aidha, kuna uwezekano wa asilimia 81 kwamba itaimarika na kuwa ya nguvu kubwa sana. Joto la juu la maji ya bahari tayari limevuka wastani kwa nyuzi joto +1.94 °C, huku joto la chini ya maji likifikia rekodi ya nyuzi joto 6 juu ya wastani.

Kutokana na joto hili kubwa linalotolewa kutoka baharini, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwaka 2026 utaweka rekodi mpya ya kuwa mwaka wa joto zaidi duniani.

Wataalamu wanakadiria kuwa athari kamili ya ongezeko hili la joto itafikia kilele chake mnamo mwaka 2027. Hali hii inaweza kusukuma wastani wa joto la dunia hadi nyuzi joto 1.7 juu ya viwango vya kabla ya mapinduzi ya viwanda.

Mkondo wa hewa wa Pasifiki utabadilisha mzunguko wa unyevunyevu duniani na kusababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa. Maeneo ya Kusini mwa Marekani, California, na Texas yanakabiliwa na hatari kubwa ya mvua kubwa na mafuriko, wakati Kaskazini mwa Marekani kukiwa na hali ya hewa ya wastani.

Kwa upande mwingine, hatari kubwa ya ukame mkali na mawimbi ya joto inatabiriwa kwa nchi za Australia, Kusini-Mashariki mwa Asia, India, na maeneo ya Kusini mwa Afrika.
Hata hivyo, maeneo ya Afrika Mashariki, sehemu za Kati na Mashariki mwa Asia, pamoja na maeneo makubwa ya Amerika Kusini yanatarajiwa kupokea mvua kubwa kupita kiasi.
Hali hii itaongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya mafuriko katika mikoa hiyo.
hapa na mimi ningekuwa sina akili kama walivyo baadhi ya members humu wanaokubali na kuamini masimulizi ya vitabu ningesema na kukubali kuwa huo ndo mwisho wa dunia maana ile gharika ya nuhu inarudi tena kuangamiza dunia.
 
Duh nakumbuka el nino ya 1997 arusha ilikua ni kwere bwashee
Barabara Kufungwa:
Barabara kuu ya kuelekea Moshi na Dar es Salaam ilikatika maeneo kadhaa kutokana na mafuriko.
Mawasiliano Kukatika:
Madaraja mengi yalizolewa na maji, na kuacha baadhi ya wilaya kama Monduli na Karatu zikiwa hazifikiki kwa urahisi.

Uharibifu wa Nyumba: Nyumba nyingi za udongo na hata za matofali kwenye mabondia ziliezuliwa au kubomoka kabisa.
 
Utabiri wa sasa unaonyesha kuwepo kwa "Super El Niño" inayokuwa kwa kasi kubwa na inayoweza kuweka historia.
Hali hii inatokea katika Bahari ya Pasifiki na inatarajiwa kufikia kilele mwishoni mwa mwaka 2026, kisha kuendelea hadi mapema msimu wa kuchipua wa mwaka 2027. Wanasayansi wa hali ya hewa wanaonya kuwa mfumo huu unakua haraka kuliko kawaida na unaweza kufikia viwango vya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumbukumbu zilipoanza kuwekwa mnamo mwaka 1950.

Makubaliano ya hivi karibuni ya kielelezo kutoka taasisi kubwa kama Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha NOAA na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) yanaonyesha uwezekano wa asilimia 96 hadi 97 kwa El Niño hii kudumu msimu wote wa baridi wa kizio cha kaskazini.

Aidha, kuna uwezekano wa asilimia 81 kwamba itaimarika na kuwa ya nguvu kubwa sana. Joto la juu la maji ya bahari tayari limevuka wastani kwa nyuzi joto +1.94 °C, huku joto la chini ya maji likifikia rekodi ya nyuzi joto 6 juu ya wastani.

Kutokana na joto hili kubwa linalotolewa kutoka baharini, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwaka 2026 utaweka rekodi mpya ya kuwa mwaka wa joto zaidi duniani.

Wataalamu wanakadiria kuwa athari kamili ya ongezeko hili la joto itafikia kilele chake mnamo mwaka 2027. Hali hii inaweza kusukuma wastani wa joto la dunia hadi nyuzi joto 1.7 juu ya viwango vya kabla ya mapinduzi ya viwanda.

Mkondo wa hewa wa Pasifiki utabadilisha mzunguko wa unyevunyevu duniani na kusababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa. Maeneo ya Kusini mwa Marekani, California, na Texas yanakabiliwa na hatari kubwa ya mvua kubwa na mafuriko, wakati Kaskazini mwa Marekani kukiwa na hali ya hewa ya wastani.

Kwa upande mwingine, hatari kubwa ya ukame mkali na mawimbi ya joto inatabiriwa kwa nchi za Australia, Kusini-Mashariki mwa Asia, India, na maeneo ya Kusini mwa Afrika.
Hata hivyo, maeneo ya Afrika Mashariki, sehemu za Kati na Mashariki mwa Asia, pamoja na maeneo makubwa ya Amerika Kusini yanatarajiwa kupokea mvua kubwa kupita kiasi.
Hali hii itaongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya mafuriko katika mikoa hiyo.
Bora mvua kubwq kupita kias au ukame uliobobea?
 
Barabara Kufungwa:
Barabara kuu ya kuelekea Moshi na Dar es Salaam ilikatika maeneo kadhaa kutokana na mafuriko.
Mawasiliano Kukatika:
Madaraja mengi yalizolewa na maji, na kuacha baadhi ya wilaya kama Monduli na Karatu zikiwa hazifikiki kwa urahisi.

Uharibifu wa Nyumba: Nyumba nyingi za udongo na hata za matofali kwenye mabondia ziliezuliwa au kubomoka kabisa.
Hapo dar ndio itakuwa balaa
 
Asili ya El Niño inatokana na kuongezeka kwa joto la maji ya juu ya bahari kupita wastani wa kawaida katika eneo la katikati na mashariki mwa Bahari ya Pasifiki ya Ikweta.

Hali hii ni sehemu ya mfumo wa asili wa mabadiliko ya tabianchi duniani unaojulikana kama El Niño-Southern Oscillation (ENSO).

Chanzo cha Jina "El Niño"Maana ya neno: Jina "El Niño" linatokana na lugha ya Kihispania likimaanisha "mtoto wa kiume" au "mtoto mchanga".

Wagunduzi:
Jina hili lilitolewa na wavuvi wa nchi za Peru na Ecuador huko Amerika Kusini.

Uhusiano na Krismasi: Wavuvi hao waligundua mkondo wa maji kuwa moto usio wa kawaida mara nyingi karibu na wakati wa Krismasi.
Waliliita jina hilo kwa heshima ya kuzaliwa kwa Mtoto Yesu.

Jinsi El Niño Inavyotokea Kisayansi
Hali ya Kawaida:
Upepo wa kibiashara (trade winds) huvuma kutoka mashariki kwenda magharibi, ukisukuma maji ya moto kuelekea bara la Asia na Australia, na kuruhusu maji baridi kutoka chini ya bahari kupanda juu karibu na pwani ya Amerika Kusini.

Kipindi cha El Niño:
Upepo huu wa kibiashara unalegea au kubadili uelekeo.Mabadiliko ya Joto:

Maji ya moto yaliyokuwa upande wa magharibi yanasafiri kurudi mashariki kuelekea Amerika Kusini.Kiwango cha Joto:

Hali hii ya El Niño huthibitishwa kisayansi pale joto la uso wa bahari linapoongezeka kwa angalau nyuzijoto 0.5°C au zaidi juu ya wastani.
 
Toa ata shuhuda moja mkuu
Japo kilevi ila ngoja niseme kitu, kipindi hicho nilikua na miaka 12 tu, ilipiga mvua ya mawe kama siku 5 mfululizo , siku ya sita ikapungua kidogo kutoka nnje tulikuta mashamba na uwanja umegeuka bahari, mifugo ilikufa , baadhi ya watu walio kuwa mabondeni walikufa , baada ya mvua kukata ikashuka njaa ya kufa mtu, wanyama na watu wengi walikufa , kitu kilituokoa ni mahindi ya yanga , na mchele wa kitumbo kw zile familia zilizo jiweza kidogo.

MwKa uliofuatakukashuka wale wadudu wanaoshambulia mazao wakijani , njaa ikawa juu ya njaa , hata mchicha pori ilikua ni ngumu kuupata
 
Kama shemeji kajenga mabondeni mfikishie taarifa
5ea0c1b6-d611-4529-be1c-4f83f1347a0a.jpg.webp
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom