carbohydates
Senior Member
- Oct 13, 2026
- 118
- 201
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesisitiza mvua kubwa za El Nino zipo na zitakuwa kubwa kuliko zilizotangulia.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a alisema El Nino inaendelea kuimarika na itaendelea kuimarika mwezi ujao na kumairika huko kunadhihirishwa na kuongezeka kwa kiwango cha joto katika maeneo ya Bahari ya Hindi.
“Neno moja leo tuondoke nalo, El Nino ipo tena yenye nguvu kubwa kuelekea mwezi Novemba, kwa sababu hali inazidi kuimarika,” alisema Dk Chang’a wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika kikaokazi Dar es Salaam jana.
Alisema miaka yote ambayo El Niño imepiga nchini na maeneo mengine ya Afrika ya Mashariki, kiwango cha joto bahari kimekuwa kikubwa.
Aliitaja miaka hiyo kuwa ni 1982/1983, 1997/1998, 2015/2016 na 2023/2024, kiwango cha juu cha joto kimekuwa nyuzijoto zaidi ya 2.6 kuelekea kunyesha kwa mvua hizo kubwa za El Nino.
Dk Chang’a alisema mwaka 1982 ilikuwa nyuzijoto 2.2, mwaka 1997 nyuzijoto 2.4, mwaka 2015 nyuzijoto 2.6 na mwaka 2024 nyuzijoto 2.0.
“Na hadi sasa kiwango cha joto ni zaidi ya nyuzijoto 2.6 baharini, hivyo El Nino inaimairika, ipo na itakuwa kubwa kuliko zilizotangulia,” alisema Dk Chang’a.
Alieleza kuwa hali hiyo ya joto inashuhudiwa katika maeneo ya Afrika Mashariki na hii hushuhudiwa hali inapokuwa chanya upande wa Magharibi mwa bahari.
Chanzo : Habar leo