Super El nino 2026/2027.. El nino ya kihistoria

Super El nino 2026/2027.. El nino ya kihistoria

Japo kilevi ila ngoja niseme kitu, kipindi hicho nilikua na miaka 12 tu, ilipiga mvua ya mawe kama siku 5 mfululizo , siku ya sita ikapungua kidogo kutoka nnje tulikuta mashamba na uwanja umegeuka bahari, mifugo ilikufa , baadhi ya watu walio kuwa mabondeni walikufa , baada ya mvua kukata ikashuka njaa ya kufa mtu, wanyama na watu wengi walikufa , kitu kilituokoa ni mahindi ya yanga , na mchele wa kitumbo kw zile familia zilizo jiweza kidogo.



MwKa uliofuatakukashuka wale wadudu wanaoshambulia mazao wakijani , njaa ikawa juu ya njaa , hata mchicha pori ilikua ni ngumu kuupata
_133228338_mediaitem133228337.jpg
3a229aa0-2774-11ee-b1d7-8fdc93c2782e.jpg (1).webp
 
Utabiri wa sasa unaonyesha kuwepo kwa "Super El Niño" inayokuwa kwa kasi kubwa na inayoweza kuweka historia.
Hali hii inatokea katika Bahari ya Pasifiki na inatarajiwa kufikia kilele mwishoni mwa mwaka 2026, kisha kuendelea hadi mapema msimu wa kuchipua wa mwaka 2027. Wanasayansi wa hali ya hewa wanaonya kuwa mfumo huu unakua haraka kuliko kawaida na unaweza kufikia viwango vya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu kumbukumbu zilipoanza kuwekwa mnamo mwaka 1950.

Makubaliano ya hivi karibuni ya kielelezo kutoka taasisi kubwa kama Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha NOAA na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) yanaonyesha uwezekano wa asilimia 96 hadi 97 kwa El Niño hii kudumu msimu wote wa baridi wa kizio cha kaskazini.

Aidha, kuna uwezekano wa asilimia 81 kwamba itaimarika na kuwa ya nguvu kubwa sana. Joto la juu la maji ya bahari tayari limevuka wastani kwa nyuzi joto +1.94 °C, huku joto la chini ya maji likifikia rekodi ya nyuzi joto 6 juu ya wastani.

Kutokana na joto hili kubwa linalotolewa kutoka baharini, kuna uwezekano mkubwa kuwa mwaka 2026 utaweka rekodi mpya ya kuwa mwaka wa joto zaidi duniani.

Wataalamu wanakadiria kuwa athari kamili ya ongezeko hili la joto itafikia kilele chake mnamo mwaka 2027. Hali hii inaweza kusukuma wastani wa joto la dunia hadi nyuzi joto 1.7 juu ya viwango vya kabla ya mapinduzi ya viwanda.

Mkondo wa hewa wa Pasifiki utabadilisha mzunguko wa unyevunyevu duniani na kusababisha mabadiliko makubwa ya hali ya hewa. Maeneo ya Kusini mwa Marekani, California, na Texas yanakabiliwa na hatari kubwa ya mvua kubwa na mafuriko, wakati Kaskazini mwa Marekani kukiwa na hali ya hewa ya wastani.

Kwa upande mwingine, hatari kubwa ya ukame mkali na mawimbi ya joto inatabiriwa kwa nchi za Australia, Kusini-Mashariki mwa Asia, India, na maeneo ya Kusini mwa Afrika.
Hata hivyo, maeneo ya Afrika Mashariki, sehemu za Kati na Mashariki mwa Asia, pamoja na maeneo makubwa ya Amerika Kusini yanatarajiwa kupokea mvua kubwa kupita kiasi.
Hali hii itaongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya mafuriko katika mikoa hiyo.
Ngoja niwatonye wazee kule kijijini wasiuze mahindi yote, maana hawachelewi kubakiza debe mbili tu za kula 🫩😒😒
 
Hii kitu hua nasikia wazee wananambia ishatokea miaka ya 90 huko kwa hiyo hii ndo itakuwa super kuliko ile...
1998 hii ilikuwa balaah ikaja kujirudia 2012 , 2022 na kidogo 2024.

Ila 1998 ilikuwa mvua kubwa kuliko kawaida mkoani kwetu nilishuhudia mwezi December mvua haikunyesha siku mbili tu mwezi mzima.
Mvua ilikuwa ikianza kunyesha usiku mnanaamka nayo nje kila mahali maji yanatembea tuliteseka sana. Mazao mengine yote yalisombwa na maji watu wakaponea kulima viazi na maharage ya kiangazi. Wakulima wengi walihamia kuvua kambale.
 
Serikali hii ya kijinga itapata kisingizio cha kutojenga barabara Kwa wakati kutokana na mvua.
Miradi yote ya barabara inaenda kufa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom