Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,131
- 35,173
Ubishi, ukaidi na ujeuri wa Wapalestina kutaka kupambana na Israel itapelekea maafa na mateso zaidi kwa watu wasiokuwa na hatia. Ama kwa kupenda au kutokupenda, suluhisho rahisi na lenye kuleta amani mashariki ya kati ni wapalestina kuwa watulivu ili waendelee kukaa pale kwa amani au kuhama kabisa maeneo yale ili kuepusha shari zaidi.
Hizi choko choko za vikundi vya Hamas nk. ni kujilisha upepo na kuongeza mateso, hazina msaada wowote endelevu kwa wapalestina. Wapalestina wakae wakijua, hakuna nchi ya kiarabu itajiingiza kichwa kichwa kuwapigania pale, sio Iran, Lebanon, Syria, Egypt, Jordan au Saudi Arabia ambayo ina muda, nguvu, rasimali au dhamira ya dhati ya kwenda moja kwa moja kuwapigania wapalestina, kila taifa linapambana na hali yake tu.
Hilo eneo la Gaza hapo mashariki ya kati ni dogo sana, kavu mnoo, halina rasilimali zozote muhimu za kiuchumi ukiachilia hizi blah blah za kiimani ambazo zinatumika na pande zote kinafiki tu na kimchongo ili kujitengenezea uhalali wa kumiliki hayo maeneo kwa sababu ya umuhimu wa kihistoria.
Sasa kwanini watu wakae kwa wagombana?
Kwani dunia haina sehemu zingine za kuishi?
Kuna raha gani kuishi katika hali hiyo?
Unaweza kusema au kuwaza kuwa kwanini waisraeli wao wasihamishwe pale? Jibu ni moja tu, Israel kwa sehemu kubwa ndio inapamiliki pale kwa sasa (iwe kwa haki au mabavu), Israel haina muda wa kuchokoza wapalestina ili iendelee kukaa pale bali ina dhamira, muda na nguvu za kutaka kuwakandamiza zaidi na kuwatuliza vilivyo ikiwa wapalestina watataka kuendelea kubakia pale.
Kama kuna wafia dini huku duniani wanaoona ni lazima kuendelea kupigana vita pale mashariki ya kati basi waende wao pale kwa vivuli vya dini yao kupigana na sio kutumia wapalestina kama chambo.
Note:
Taifa la Palestina lina mchanganyiko wa watu wenye imani tofauti tofauti wakiwemo waislamu (97%) na wakristo (3%), wakati taifa la Israel nalo lina waumini wa kiyahudi (81%), waislamu (14%), dini za asili (3%) na wakristo (2%). Lakini kote huko kwa hayo mataifa na hao waumini ukichunguza utagundua miongoni mwao kuna wapagani na wahuni kibao, hivyo tusilazimishe hii vita kuwa ni vita ya kidini wakati ni siasa na tamaa tu.
TUMECHOKA NA VITA
HATUTAKI VITA