Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar

Mushi,

Historia ya Tanzania hapo bila historia ya Zanzibar. Kumbukeni hizi nchi mbili ziliungana zikiwa sawa kabisa na kila moja ikiwa na kiti UN. Kwa taarifa yako Zanzibar ilikuwa imelipa ada ya uanchama wa UN kwa miaka 40 chini ya Balozi Hasnuu Makame na baada ya muungano ada ya Zanzibar ndio ilichukuliwa na Muungano.
Historia ya Zanzibar haiwezi kufutwa na Muungano. Acheni ukoloni wa bara hapa. Mimi ni mbara na hata siku moja siwezi kuwaburuza watu wenye Taifa lao na historia yao.

Kumbuka Serikali iliyopinduliwa Zanzibar haikuwa serikali ya waarabu. Ilikuwa serikali ya Waafrika chini ya Shamte kama Waziri Mkuu
 
Ndio maana wanaweka hypothetical enemy hapa kudanganya wabongo, tuwe wapenda haki, hakuna haja ya kuishi kwenye nchi inayo colonize watu wengine, tuungane kwa respect
 
ndugu.
maelezo yako ni mazuri lakini nimewahi kuongea sana hapa, unajua hali ya zanzibar tunaielewa zaidi sisi tunaoishi zanzibar, tunajua tulikotoka na tulipo,ni ukweli usiopingika kwamba wazanzibari wamekumbana na mengi yaliyowafunza katika maisha yao halisi (na sio magazeti).Hivi utaamini kwamba Zanzibar hata mtoto ambae hajafikia umri wa kupiga kura basi anaweza akadanganya umri ,ilimradi tu awakilishe hisia zake kwenye kisanduku cha kura(akapige kura)?, jiulize ni kwanini?.Wazanzibari tunaongelea hali halisi tunayokumbana nayo ,Watanzania bara munaiongelea Zanzibar kwa kuisoma magazetini au kuitembelea wiki moja.
nawasilisha
Bwana under_age inaelekea kuwa kweli wewe bado ni mtoto!
Zanzibar na Pemba tunailewa haswa pengine zaidi ya nyie wenyewe mnovyoielewa.
Matatizo ya Zanzibar yana historia ndefu sana , na tunayo yashughulikia sasa ni matokeo ya matatizo hayo.
Si jambo la kuzua kuwa Zenj lugha za waungwana na watwana bado zipo hadi hii leo, hii ina maanisha ubaguzi ambao bado upo, japo kichinichini.
Wale wa uzao wa kiarabu bado wana hisia ya kurudisha watwala wao wa zamani-Jamshed.
Ndugu yangi mimi nimekaa Pemba kwa miaka 2, pale Chake. nalielwa hili.
Sio bahati mbaya kuwa leo hii kuna kambi zisizo changanyika za CUFPemba na CCM Zanzibar.Trace background ya watu walio ndani ya kambi hizi na utajua naongelea nini.Leo kama Abdalla Natepe atajiunga na CUF basi hiyo ndo itakuwa miujiza ya karne hii.
Fuatilia harakati za Maalim Sherrif akiwa ndani ya utawala wa CCM na hatimaye chama chake cha CUF hatimaye utaelewa kwa nini yeye ndiye kinara wa kuwa rudisha wajomba zake Zanzibar.
 
Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Mzee mwenzangu za leo,

Usulutani Tanzania ulifutwa.

Sultani huyu kwao ni Omani, mwaka alohamisha usulutani wake toka Omani na kuuleta Zanzibar unajulikana.
Pengine badala ya kudai kiti cha usulutani Zanzibar kwa nini asiende kudai huko Omani?
Huko Omani kilmtoa nini?
Zanzibar ni mali yake?
Anaweza dai alinunua kisiwa hicho kwa kipande kirefu sana cha nguo, je thamani ya Wazanzibar waliokuwemo humo kisiwani ni shilingi ngapi??

Au ndo anataka kutuingizia kadi ya Ubwana na Utwana katika maana kwamba alipohamia Zanzibar alikuta ndezi na Watwana???

Hebu asilete za kuleta.

Waingereza walikuja kututawala lakini Masultani wao hawakuhama UK.
Hawa masultani wa Omani wao waliona wamefika pale Zanzibar kiasi cha kuhamisha hata vinyambu vyao toka Omani??

Kuhusu Wazanzibari wachache wanaotaka kutawaliwa! Hiyo si hoja nzito kwani kihistoria na kiuzoefu kuna watu wapendao kujipendeza, hata pale wajuapo fika kwamba mshahara wa kujipendekeza kwao ni utwana wa kizazi.
 
Nonsense, unaongelea mambo mepesi mepesi yanayotokana history, unarudiarudia ujinga kwasababu huna hoja nyingine ya kuulinda muungano, very sad!

Barbados iko chini ya queen wanashida gani, kuna visiwa chungu mzima ziko chini ya queen

Hii habari yako ni very irrelevant na unapotosha watu kwa makusudi kwasababu hakuna mtanganyika anaweza kueleza kwa haki anaitakia nini? zanzibar..kama wanataka ufalme so it be? inakuuma nini? ni choice yao

hata ZNZ ikiwa chini ya sultani haitakuwa na madhara yeyote. ZNZ vunja muungano tumlete sultani tuwe kama barbados
 
Je, Sultani Jamsheed arudishiwe mali aliyonyang'anywa kufuatia mapinduzi ya 1964?
Mwanakijiji.
Hii mada umeiweka kwenye jukwaa la siasa na ni tegemeo langu kwamba utaijadili kisiasa na sio kibarazani barazani.
Serikali ya sasa ya Zanzibar ni ya kidemokrasia na bahati nzuri imepata baraka za CUF na CCM, katiba yetu inazungumzia kuyalinda mapinduzi na inapinga usultani na ilitaifisha ardhi na mali nyingi kama mashamba n.k na kuwekwa chini ya serikali.Sasa be sincere na uwe muwazi , ni kwa kippengele gani sultani anaweza kurudi?
the only posibility ninayoiona ni kupitia kura ya maoni ambayo itahitaji marekebisho ya katiba, let say this is the case , I can guarantee you hakuna kijana wa kizanzibari mwenye habari na usultani. Na let say kumeitishwa referendum na wazanzibari wakasema wanataka utawala wa sultani urudi (which is very unlike case),kuna ubaya gani? si walioamua ni wazanzibari wenyewe, hivi UK si wako na royal system na mbona ni moja ya mataifa yanayoongoza ulimwengu?
Another option ni mapinduzi , nadhani ndugu Tumain ameuliza suali zuri hapa, atapindua kwa kutumia nini wakati yeye mwenyewe ni mkimbizi tu(according to you).
Pia usisahau kwamba Wazanzibari wengi wanaolaani mapinduzi ya 1964 hawaungi mkono utawala wa sultani.
Nawasilisha.
 
Bwana under_age inaelekea kuwa kweli wewe bado ni mtoto!
Zanzibar na Pemba tunailewa haswa pengine zaidi ya nyie wenyewe mnovyoielewa.
Matatizo ya Zanzibar yana historia ndefu sana , na tunayo yashughulikia sasa ni matokeo ya matatizo hayo.
Si jambo la kuzua kuwa Zenj lugha za waungwana na watwana bado zipo hadi hii leo, hii ina maanisha ubaguzi ambao bado upo, japo kichinichini.
Wale wa uzao wa kiarabu bado wana hisia ya kurudisha watwala wao wa zamani-Jamshed.
Ndugu yangi mimi nimekaa Pemba kwa miaka 2, pale Chake. nalielwa hili.
Sio bahati mbaya kuwa leo hii kuna kambi zisizo changanyika za CUFPemba na CCM Zanzibar.Trace background ya watu walio ndani ya kambi hizi na utajua naongelea nini.Leo kama Abdalla Natepe atajiunga na CUF basi hiyo ndo itakuwa miujiza ya karne hii.
Fuatilia harakati za Maalim Sherrif akiwa ndani ya utawala wa CCM na hatimaye chama chake cha CUF hatimaye utaelewa kwa nini yeye ndiye kinara wa kuwa rudisha wajomba zake Zanzibar.

ndugu.
Labda umenisoma sivyo, hakuna atakaekataa mgawanyiko wa Zanzibar kisiasa.Nilichoongelea ni uhali halisi wa maisha ya Zanzibar tunaokumbana nao katika our daily life routine,mfano ni hii post yako.Wengi wenu mnachanganya mambo, mkiona mtu anayalaani au kuyapinga mapinduzi ya 1964 au kuyaita haramu basi munachukulia kwamba anataka kurejesha usultani which is not the case in Zanzibar.Wazee wetu wengi wanalaani Mapinduzi yale kwa vile waliuliwa jamaa zao ambao walikuwa wazanzibari tangu enzi na enzi na sio kwa sababu ya Sultani.Hii ndio hali halisi.
 
Hivi watanganyika tunahangaika nini na Zanzibar????si tuwaachie tuu kanchi kao yatakayotokea huko mbele ya safari hayatuhusu.JK awe mwanaume kama Gobachev avunje muungano ili tuone kilichojiri sio kila siku mara yakhe Seif kasema hivi,Karume kasema vile...sie kwetu TBR pouwa tuwaache watajiju!!!!
 
Mushi,

Historia ya Tanzania hapo bila historia ya Zanzibar. Kumbukeni hizi nchi mbili ziliungana zikiwa sawa kabisa na kila moja ikiwa na kiti UN. Kwa taarifa yako Zanzibar ilikuwa imelipa ada ya uanchama wa UN kwa miaka 40 chini ya Balozi Hasnuu Makame na baada ya muungano ada ya Zanzibar ndio ilichukuliwa na Muungano.
Historia ya Zanzibar haiwezi kufutwa na Muungano. Acheni ukoloni wa bara hapa. Mimi ni mbara na hata siku moja siwezi kuwaburuza watu wenye Taifa lao na historia yao.

Kumbuka Serikali iliyopinduliwa Zanzibar haikuwa serikali ya waarabu. Ilikuwa serikali ya Waafrika chini ya Shamte kama Waziri Mkuu

well said bro, na hata waliouliwa kwenye Mapinduzi wengi wao ni waZanzibari lakini historia na siasa za shule zinatulazimisha tuamini kwamba ni waarabu.La kufanya ni kusahau yaliopita na kujenga Zanzibar mpya, tukikumbatia historia ,itaendelea kutugawa milele na milele.Jambo ambalo nina mia juu ya mia haliwezi kurudi Zanzibar ni usultani, Sijui mleta mada ana ajenda gani ya siri na mjadala huu, lakini sijawahi kumsikia mZanzibari anazungumzia usultani, si maalim Seif, si Karume ,si wananchi wa kawaida.
nawasilisha
 
It takes no time bana! hii si trinity issue is not that difficult?

Rais ninaye mzungumzia ni wa zanzibar wenye jeshi lao (suppose wakijiondoa kwenye muungano) huyu sultani anawezaje kumfukuza rais wa ccm/cuf kutoka oman wherever he is? kama siyo danganya toto eti watanganyika wanawalinda wazenj?

Lindeni vibibi vyenu kule shinyanga vinavyouawa kwa uchawi achani wazenj? after all hatuna resources za kuchezea hivyo?

Huna haja ya ku cherry pick,angalia issue kwa mapana na utaona kuwa zote Shinyanga na Zanzibar ziko kwenye jedwali moja la muungano,hopefully umenipata,wote ni wananchi wa Tanzani wenye unique history lakini wako kwenye union.
 
Mzee mwenzangu za leo,

Usulutani Tanzania ulifutwa.

Sultani huyu kwao ni Omani, mwaka alohamisha usulutani wake toka Omani na kuuleta Zanzibar unajulikana.
Pengine badala ya kudai kiti cha usulutani Zanzibar kwa nini asiende kudai huko Omani?
Huko Omani kilmtoa nini?
Zanzibar ni mali yake?
Anaweza dai alinunua kisiwa hicho kwa kipande kirefu sana cha nguo, je thamani ya Wazanzibar waliokuwemo humo kisiwani ni shilingi ngapi??

Au ndo anataka kutuingizia kadi ya Ubwana na Utwana katika maana kwamba alipohamia Zanzibar alikuta ndezi na Watwana???

Hebu asilete za kuleta.

Waingereza walikuja kututawala lakini Masultani wao hawakuhama UK.
Hawa masultani wa Omani wao waliona wamefika pale Zanzibar kiasi cha kuhamisha hata vinyambu vyao toka Omani??

Kuhusu Wazanzibari wachache wanaotaka kutawaliwa! Hiyo si hoja nzito kwani kihistoria na kiuzoefu kuna watu wapendao kujipendeza, hata pale wajuapo fika kwamba mshahara wa kujipendekeza kwao ni utwana wa kizazi.

Usultani wa Zanzibar uligawanyika toka kwa Usultani wa Omani baada ya ndugu wawili kugombania. Mmoja akabakia yeye na ukoo wake na usultani wa Omani na Muscat wakati yule mwingine ndiyo akabakia na Usultani wa Zanzibar. Sasa Jamsheed hawezi kudai kiti cha Oman kwani kina mwenyewe!!

Mapinduzi ndiyo yameharibu; Muungano ndio ukavuruga kabisa.
 
Kuna kitu kinaitwa "Baraza la Mapinduzi" kule Zanzibar. Kimo kwenye KATIBA zote mbili, ya JMT na ile ya SMZ. Waliomo mle hivi sasa sio waliohusika na mapinduzi. Baraza hili linafahamika jinsi lilivyofanya kazi zake baada ya mapinduzi. Kwa nini bado lipo?
 
MwanaKijiji this is totally unacceptable and it shows at best your facts twisting behaviour which gets too much into you bana mdogo. You will pay for the sin......

Hivi vitisho muwatishe wanaoogopa; i'm not one of them.

Moja, Niambie duniani Kiongozi yeyote aliyepinduliwa na akakubali mapinduzi. Lipi la ajabu kwa Jamshid. Unaleta propaganda mbaya sana ambazo zitabeba ubaguzi wa rangi na nashangaa kwa nini unakuwa IRRESPONSIBLE kiasi hiki.

Mfalme Victor Emmanuel wa Nyumba ya Kifalme ya Savoy Italia. Baada ya vita ya pili ya dunia Waitalia waliamua kupiga kura ya maoni juu ya kuchagua ufalme au kuwa jamhuri. Kwa asilimia 54 wakachagua republic na hivyo kuvunja utawala wa kifalme. Kutokana na kura hiyo ufalme wa Savoy uliodumu kwa muda mrefu duniani at the time ukaamuliwa kufukuzwa Italia na kukimbilia Misri. Ilikuwa ni mwa 2000 ndiyo ukoo wao ukaruhusiwa kurudi na mrithi wa kiti cha Savoy akapewa masharti ya kukikana daima na milele kiti cha ufalme wa italia.

Burundi alipinduliwa Mfalme ' Mwami' Mwambutsya mwaka 1962 na mpaka leo watoto wake wanaamini haikuwa sawa lakini hakuna dalili zozote za Burundi kurudisha Ufalme.

Kuamini kuwa haikuwa sawa ni jambo moja; kuamini kuwa wana haki ya kurithi kiti hicho ni jambo jingine. Hata mimi naweza kuamini kuwa mapinduzi yalivyofanyika haikuwa sawa; lakini ni jambo jingine kuamini kuwa Sultani abakie kuwa Sultani!

Rwanda alipinduliwa Mfalme Kigeli V na mpaka leo yupo Marekani anadai ufalme wake na hakuna Rwanda dalili za kumrejeshea ufalme huo. Walipinduliwa pia kina viongozi wengine na hawakukubali na walidai haikuwa sawa nao watarudi?

Kuna Mfalme kule Barotseland Zambia mpaka leo anasema ile ni nchi kamili kufuatilia mkataba wa zama za ukoloni na Kaunda alikataa. Je unataka kusema madai yake hayo basi atarudi?

Tanzania Mwalimu alifuta Uchifu lakini mpaka leo kuna machifu na watoto wao hawakubaliani na uamuzi ule. Unataka kusema nao tutakuja kuwarudisha.[/quote]

Mifano yako inathibitisha ninachokisema.

Umeandika hii post yako kwa kuwa ni Zanzibar. Kwa kuwa ni Mwarabu. Kwa kuwa ni Muislam.

Ujue wasomaji wako ni waislam na wakristo na watu wa rangi zote.

Ni wewe uliyeyaingia maneno hayo kwa sababu huwezi kufikiria nje ya vitu hivyo. Kwa hiyo watu wasitoe maoni kwa sababu wanahusika ni waarabu na waislamu?

Hii post yako ni irresponsible na ni propaganda za CCM dhidi ya Wazanzibari na umoja wao. Huijui historia ya Zanzibar na unajiweka weka tu matokeo yake unataka kumwaga sumu zile zile za kusema CUF waarabu na watamleta Sultan. Upuuzi kabisa.

hofu yako wewe usitupandikizie wengine. Nani kakuambia kuwa Sultani ni Muarabu?

Kwa taarifa yako ndani ya CUF wote wale ni ASP na hakuna ZNP mle wala UMMA.

Ushindwe na ulegee

watisheni hao hao wenye kuogopa kuusogelea ukweli!
 
hivi mtu anaweza vipi kutawala wakati kuna mwingine anadai haki hiyo ya kutawala kwa kuzaliwa na wapo watu (baadhi ya watawaliwa) wanaomtambua huyo mtu mwingine?

Japokuwa haisemwi hadharani (kwa sababu ya siasa 'maalum' za Zanzibar) Sultan amekuwa katika jitihada nyingi na za muda mrefu za kurejea Zanzibar. Ndani ya Zanzibar bado kuna wale ambao hawayatambui mapinduzi ya 1964 na ndiyo hao wako nyuma ya utawala wa sultan. Kama utakuwa mfuatiliaji makini na mzuri, Sultan ameendelea kuimarisha mazingira ya kuwepo kwake. Hapa Dar ana vitega uchumi vyake kupitia wanafamilia yake. Pale Zanzibar ana mambo mengi tu ambayo anayafanya. Lakini jambo kubwa ambalo linaumiza vichwa ni juu ya ardhi iliyokuwa na mashamba yake, hili ni pasua kichwa, akirudi itakuwaje?
Ukweli Sultan ana uhakika wa kurudisha himaya yake hapo mwaka 'X'.
 
HIvi watu wanataka tuwakumbushe kuhusu Dowans?

Uuuuffffsssssiiii, @#!*x***?, MKJJ hii inahitaji kutungiwa kitabu maalumu
icon14.gif
 
Jmushi.. Muungano ulikusudia kuzuia mara moja jaribio la kumrudisha Sultani kwa nguvu. Serikali ya Karume ilikuwa ni dhaifu sana mwanzoni na isingeweza kuhimili onslaught ya watetezi wa utawala wala wa ZNP na ZPP na Sultani.
Haiba na ubabe wa Karume wakati ule asingekubali kirahisi kuingia katika mikono ya utawala wa mtu mwingine. Kuna nguvu nyingi zinatumika kuonyesha kana kwamba Karume aliburuzwa tu kukubali muungano wakati huo sio ukweli. Nimeifurahia hii topic maana imefungua pazia na kutuonyesha wazi nini kimefichwa nyuma yake maana wengine tunahisia hisia kwamba kuna linalofichwa katika namna huu muungano unavyosemwa vibaya kwamba ndio chanzo cha matatizo ya Zanzibar.
 
Nimepata hint 1995 Sultan aliwahi kuulizwa juu mambo ya kurudi Zanzibar katika idhaa ya BBC.

Kama yupo mwenye mp3 hiyo, tafadhali tuekee hapa tupate kumsikia Sultani mwenyewe.
 
Back
Top Bottom