Simulizi ya Mzinga

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,867
Mzinga Canon) ambao unapatikana katika bustani ya ofisi za Jiji la Tanga katika mtaa wa (Uhuru) Independence Avenue. Kwa wale wakaazi wa Tanga au waliowahi kufika pale, pasi shaka walishaona kitu kama hicho eneo lile.

Simulizi hii nzuri kabisa, imekaririwa kutoka kwa mwandishi James Mgaya Kutoka kwenye jarida la Urithi la mwaka 2003.

Wengine hudhani ni pambo tu, kwa sasa unaonekana ni chakavu na ni dhahiri kabisa ni kutokana na kukosa matunzo. Ila kuna historia kubwa sana nyuma ya mzinga huo chakavu.

Katika nusu ya kwanza ya karne ya 19 kabila la wasegeju walioshi katika eneo la pwani waligawanyika sehemu kuu mbili wakiwa na viongozi wao wa kimila au machifu wao mbalimbali.

Baadhi yao waliishi upande wa kaskazini eneo la chongoleani na Mnyanjani, na hawa waliitwa waboma, na wengine waliishi kusini, ndumi na Mwambani, na hawa waliitwa wakamadhi.

Jamii hizi zilikuwa na ugomvi na vurugu za mara kwa mara, kuna wakati kulitokea vita kati ya Abdallah Mwakete chifu wa Waboma na Chifu wa Wakamadhi aliyeitwa Mwakinoba.

Hali ya vurugu vita na uhasama ilikuwa mbaya kiasi cha kwamba liwali wa Tanga aliamua kutuma taarifa kwa Sultan Majid bin Said wa Zanzibar kwani kwa kipindi hicho Mwambao wote wa Pwani ulikuwa chini ya Usultani.

Sultani alitoa tamko na kutuma askari kutoka Zanzibar hadi Tanga kukomesha vita hiyo na hatimaye walifanikiwa kuyakomesha mapigano na pia walifanikiwa kuwatia mbaroni machifu wote wawili waliosababisha mapigano.

Ukiachilia mbali machifu wale, pia kuna watu wengine wawili walikamatwa ambao ni Mwabohero na Mwinyimakame, wote walipakiwa ndani ya jahazi na kupelekwa Unguja kukutana na Sultani.

Wakati Jahazi limefika maeneo ya Pangani chifu wa Waboma Abdallah Mwaketa alitupwa baharini ingawa hadi leo hii haijaelezwa ni kwa sababu gani, wengine watatu walifikishwa hadi katika kasri la Sultani, naye aliwahukumu kila mmoja kifungo cha miaka 9 jela.

Mwakomba na Mwabohero walifia gerezani, Mwinyimakame peke yake ndio alifanikiwa kutoka gerezani kati ya wote wale na akafanikiwa kurudi Mwambani Tanga.

Baada ya muda Zanzibar ilipata Sultani Mwingine, Sultani Seyyid Bargash bin Said. Mwinyimakame ni mtu mjanja mjanja, alipopata habari kuwa Zanzibar imepata utawala mpya, aliamua kufunga safari hadi Zenji kwenda kutoa heshima mbele ya mtawala huyo mpya.

Alipotaka kurudi Tanga, Sultani Bargash aliamua kumpatia zawadi, yeye Mwinyimakame aliomba apewe zawadi ya Mzinga. Lakini Sultani alijua huyu jamaa ni mtata sana, aliona akimpa mzinga mzima basi anaweza akazua balaa, hivyo akaagiza apatiwe mzinga wa zamani usioweza kufanya kazi.

Mwinyimakame alifurahia zawadi ile na kuchukua mzinga ule na kurejea nao Tanga. Kwa miaka kadhaa, mzinga ule ulikuwa kule Mwambani kwake, miaka ya baadae ulichukuliwa na kuwekwa mbele ya jengo la Bwana Shauri, D.C.

Ambapo jengo hilo baadae lilikuja kubadilika kuwa jingo la Manispaa ya mji wa Tanga, na sasa hivi ni Jengo la Halmashauri Jiji la Tanga, kwa hakika, hadi hivi sasa mzinga huo utaukuta ukifika hapo.

Picha: Urithi Tanga Museum.

FB_IMG_1695538812459.jpg
FB_IMG_1695538817119.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stori yako haijamtaja mwinyi makame alikuwa ni nani,inaonesha tu alikamatwa pamoja na hap wengine,alikiwa na ushawishi gani mpaka sultani ampokee na kumpa zawadi??
 
Stori yako haijamtaja mwinyi makame alikuwa ni nani,inaonesha tu alikamatwa pamoja na hap wengine,alikiwa na ushawishi gani mpaka sultani ampokee na kumpa zawadi??
Ukiachilia mbali machifu wale, pia kuna watu wengine wawili walikamatwa ambao ni Mwabohero na Mwinyimakame, wote walipakiwa ndani ya jahazi na kupelekwa Unguja kukutana na Sultani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshana unaweza kuilinganisha hii historia yako na ile ya vita vikuu vya kwanza vya dunia? Unajua vita ile kwa Tanganyika vilipiganwa katika jiji la Tanga? Enzi hizo Dar ni kijiji cha wavuvi choka mbaya hakina barabara za uhakika na Jiji la Tanga likiwa sio tu na barabara za lami bali pia na Wajerumani walishajenga reli ya kwanza toka Tanga kwenda Moshi. Ile vita ni maarufu kama vita ya nyuki na kuna makaburi ya vita hiyo hapo Tanesco Tanga. Inasemekana huo mzinga ni alama ya ukumbusho wa vita hiyo.
 
Hebu nayo tuipate kwa ukamilifu ili tuweze kupata ukweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom