Sultani Jamsheed hakukana kiti cha Usultani wa Zanzibar

Sikiliza ushuhuda ktk Mazungumzo 'Live' ya BBC na wakazi wa Zanzibar walioona kwa macho yao nini kilitokea Zanzibar Stone Town, Darajani , Bambi n.k siku Mapinduzi yalipotokea Januari 1964 na pia Historia nzima chini ya utawala wa Kisultani

Na pia kama wakazi wa Zanzibar wanawaza kurudishwa Utawala wa Kisultani au la. Endelea kusikiliza mazungumzo ktk iplayer BBC:

http://www.bbc.co.uk/iplayer/console/p003qfx1 Heart and Soul Return to Z'bar (jumla dakika 28)
http://www.bbc.co.uk/iplayer/console/p003md9n Heart and Soul return to Z'bar 2 (jumla dakika 28)
 
..yeyote yule anayeyakana Mapinduzi na kuutambua "Uhuru" wa 1963 kwa namna moja ua nyingine anamkubali Sultani kama kiongozi halali wa Zanzibar.

..Katiba ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi ilikuwa inamtambua Sultani kama mtawala wa Zenj, na chini yake alikuwepo Waziri Mkuu. wakati huo pia Zanzibar ilitambulishwa kama "Sultanate of Zanzibar."
 
Hivi vitisho muwatishe wanaoogopa; i'm not one of them.

Mfalme Victor Emmanuel wa Nyumba ya Kifalme ya Savoy Italia. Baada ya vita ya pili ya dunia Waitalia waliamua kupiga kura ya maoni juu ya kuchagua ufalme au kuwa jamhuri. Kwa asilimia 54 wakachagua republic na hivyo kuvunja utawala wa kifalme. Kutokana na kura hiyo ufalme wa Savoy uliodumu kwa muda mrefu duniani at the time ukaamuliwa kufukuzwa Italia na kukimbilia Misri. Ilikuwa ni mwa 2000 ndiyo ukoo wao ukaruhusiwa kurudi na mrithi wa kiti cha Savoy akapewa masharti ya kukikana daima na milele kiti cha ufalme wa italia.

Kuamini kuwa haikuwa sawa ni jambo moja; kuamini kuwa wana haki ya kurithi kiti hicho ni jambo jingine. Hata mimi naweza kuamini kuwa mapinduzi yalivyofanyika haikuwa sawa; lakini ni jambo jingine kuamini kuwa Sultani abakie kuwa Sultani!

Kuna Mfalme kule Barotseland Zambia mpaka leo anasema ile ni nchi kamili kufuatilia mkataba wa zama za ukoloni na Kaunda alikataa. Je unataka kusema madai yake hayo basi atarudi?

Tanzania Mwalimu alifuta Uchifu lakini mpaka leo kuna machifu na watoto wao hawakubaliani na uamuzi ule. Unataka kusema nao tutakuja kuwarudisha.

Mifano yako inathibitisha ninachokisema.

Ni wewe uliyeyaingia maneno hayo kwa sababu huwezi kufikiria nje ya vitu hivyo. Kwa hiyo watu wasitoe maoni kwa sababu wanahusika ni waarabu na waislamu?

hofu yako wewe usitupandikizie wengine. Nani kakuambia kuwa Sultani ni Muarabu?

watisheni hao hao wenye kuogopa kuusogelea ukweli![/QUOTE]

Ni mategemeo yangu kuwa Wazanzibar hawatadanganywa na opinion zako ambazo hakuna evidence ila upendavyo...lol

Wazanzibar wakiendelea kugawanywa in the name of hypothetical enemy called sultan ..ntawahesabu kama wajinga.
 
..yeyote yule anayeyakana Mapinduzi na kuutambua "Uhuru" wa 1963 kwa namna moja ua nyingine anamkubali Sultani kama kiongozi halali wa Zanzibar.

..Katiba ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi ilikuwa inamtambua Sultani kama mtawala wa Zenj, na chini yake alikuwepo Waziri Mkuu. wakati huo pia Zanzibar ilitambulishwa kama "Sultanate of Zanzibar."

Tatizo kubwa la vijana wa leo huko Zanzibar kama MrFroasty ni kuwa hawaelewi sababu hasa zilizosababisha kwanza, Mapinduzi na pili, Muungano. Marehemu Karume aliyeelewa umuhimu wa Mapinduzi hakusita kuukaribisha Muungano kama njia pekee ya kuhakikisha Usultani unapewa kisogo Zanzibar. Muungano kwa hivi sasa ndicho kisiki kinachomnyima usingizi Sultani Jamsheed na watu wake popote walipo - Ulaya, Omani au Zanzibar. Kama fisi anavyosubiri mkono wa binadamu udondoke ndivyo Sultani Jamsheed pamoja na warithi wake wanavyosubiri Muungano uvunjike. Wazanzibari wote wanatakiwa kwanza waufahamu ukweli huu halafu ndio waanze kujadili mambo ya maridhiano/mapatano. Nje ya hapo ni kudanganyana na mwisho wa siku si ajabu tukashuhudia historia ikijirudia na safari hii sina hakika kama atajitokeza Field Marshall Okello mwingine.
 
vyanzo vyangu maeneo ya mashariki ya kati vinadokeza kuwa Jamsheed amepigwa marafiki na mabinamu zake wa Oman kuzungumza na vyombo vya habari hususan masuala ya Zanzibar. Hivyo, ni vigumu kweli kumpata. Mambo yote yanayomhusu yeye yanapitia Oman na hata uwekezaji wake n.k kwenye eneo letu unapitia Oman...
 
Tatizo kubwa la vijana wa leo huko Zanzibar kama MrFroasty ni kuwa hawaelewi sababu hasa zilizosababisha kwanza, Mapinduzi na pili, Muungano. Marehemu Karume aliyeelewa umuhimu wa Mapinduzi hakusita kuukaribisha Muungano kama njia pekee ya kuhakikisha Usultani unapewa kisogo Zanzibar. Muungano kwa hivi sasa ndicho kisiki kinachomnyima usingizi Sultani Jamsheed na watu wake popote walipo - Ulaya, Omani au Zanzibar. Kama fisi anavyosubiri mkono wa binadamu udondoke ndivyo Sultani Jamsheed pamoja na warithi wake wanavyosubiri Muungano uvunjike. Wazanzibari wote wanatakiwa kwanza waufahamu ukweli huu halafu ndio waanze kujadili mambo ya maridhiano/mapatano. Nje ya hapo ni kudanganyana na mwisho wa siku si ajabu tukashuhudia historia ikijirudia na safari hii sina hakika kama atajitokeza Field Marshall Okello mwingine.

Sultan arudi zanzibar baada ya miaka 50 ya mapinduzi? na watu wazenj wakubali tu?

Tupeni data kama kuna movement yeyote chini ya sultan ambayo imedeclare kurudi zanzibar?

Hypothetical enemy?? sidhani kama wazanzibar watadanganyika kirahisi hivyo, your line of thinking ni kama kusema eti queen atarudi Tanzania ikiwa ccm itakosa madaraka?? kidding

Wabara wanataka ku-colonize zanzibar sasa wanaweka hypothetical enemy hakuna kitu kama hicho..
 
Sikiliza Mag3 usizungumze kitu usichokijua hakuna mtu asiyeijua historia ya mapinduzi wala kuifahamu nini historia ya zanzibar. Kwa taarifa yako watoto wadogo wanafahamu what is going on. Kuanzia leo hizi propaganda zenu za ugozi nawapeni references tu mjitosheleze kujua what is going on in the Zanzibar Island. Tuache kupiga kelele zisizo za msingi tuangalie facts and figures.

Kwa kuanzia someni thesis ya jamaa juzi juzi amemaliza PhD mwaka 2009 huko Columbia University Marekani.

http://www.columbia.edu/cu/history/resource-library/Daly_thesis.pdf

Mnaweza kutrace reference kama kweli JF ni wasomaji.

Humo ndani ya Thesis mtajua ni akina nani waanzilishi wa ASP, ZNP , ZPPP

Pili nani aliyepindua zanzibar and why?

Tatu Zanzibar ilikuwaje na nini chanzo za mapinduzi.

Tutaendelea kuwaletea reference zaidi badala kukaa mkizungumzia conspiracy theory of Jamshid. Kwanza Mwanakijiji Jamshid alikuwa na watoto 6 sasa sijui mmoja wa ziada ametokea wapi? Likewise, nimemuuliza jamaa yangu mmoja yuko london anasema movement zilikuwapo zamani but wengi wa watu waliokuwa proactive hawana nguvu tena kwa sasa. Vilevile jamshid sidhani kama ana mpango huo kwani serikali ya Oman imemzuia kujihusisha na siasa sasa atarudije zanzibar???

But ukweli utajulikana tu ila nawashaurini musome kwanza kabla ya kuja kujadili JF maana tunapoteza nguvu bure JF unless mna hidden ajenda zenu zengine.

Adios kwa leo someni hiyo thesis kwanza na kesho ninawaletea reference nyengine siku njema
 
Sultan arudi zanzibar baada ya miaka 50 ya mapinduzi? na watu wazenj wakubali tu?

Tupeni data kama kuna movement yeyote chini ya sultan ambayo imedeclare kurudi zanzibar?

Hypothetical enemy?? sidhani kama wazanzibar watadanganyika kirahisi hivyo, your line of thinking ni kama kusema eti queen atarudi Tanzania ikiwa ccm itakosa madaraka?? kidding

Wabara wanataka ku-colonize zanzibar sasa wanaweka hypothetical enemy hakuna kitu kama hicho..

Tumaini hawa jamaa inaelekea wana ajenda yao nyengine wape reference wakajisomee. Wanazungumzia vitu wasivyovijua wanasahau katika mapinduzi kuna watu wamechomwa moto, kuna watu wamezikwa kama takataka yaani watu 100 wamezikwa pamoja. Malori yamejazwa maiti. Nyie mnang'ang'ana na Jamshid come on give me a break.

Msizingumzie fitina jamani but zanzibar inahitaji uhuru wake na maendeleo na vijana kweli tunakusudia kuyaleta hayo mambo. Zanzibar mapinduzi ni daima.
 
Mdondoaji.. naweza kuandika narration ya kilichotokea siku ya Mapinduzi kuliko unavyodhania. Mapinduzi ya umwagikaji damu hayana uzuri wa namna yoyote. Lakini wakati mwingine ni ya lazima ili kutengeneza mazingira ya usawa wa kweli (waulize Wamarekani na Waingereza au Wafaransa).

Je unaona ubaya wowote kwa Sultani Jamsheed kukana urithi wa kiti cha Zanzibar yeye na watoto wake milele na akifanya hivyo anaweza kuruhusiwa kurudi Zanzibar kama raia wa kawaida?
 
Ni kweli aisee maana kila ninapo connect dots naona watanganyika wameamua kuwatengenezea "artificial fear/enemy" ili waendeleze ubabe wao huko zenj

Nitawashangaa sana wazenj kama watakuwa wajinga kukubali hizi hadithi za alinacha??

Ingefaa kuwauliza "Je queen anategemea kurudi Tanganyika ikiwa ccm itaondolewa maana ndio iliyomtoa mkoloni?

Umesema kweli wanatetea uwongo bila aibu kwasababu wana agenda zao ..shame on them, amkeni wapenda haki.
 
Mdondoaji.. naweza kuandika narration ya kilichotokea siku ya Mapinduzi kuliko unavyodhania. Mapinduzi ya umwagikaji damu hayana uzuri wa namna yoyote. Lakini wakati mwingine ni ya lazima ili kutengeneza mazingira ya usawa wa kweli (waulize Wamarekani na Waingereza au Wafaransa).

Je unaona ubaya wowote kwa Sultani Jamsheed kukana urithi wa kiti cha Zanzibar yeye na watoto wake milele na akifanya hivyo anaweza kuruhusiwa kurudi Zanzibar kama raia wa kawaida?

Ndio maana mnatengeneza hypothetical enemy ili mumwage damu tena kwa kizingizio cha sultan?

Unajua ukishazoea kula damu ya watu huwezi kuacha mnataka kuwasingizia wazenj kwamba wanataka kurudisha sultan mpate sababu ya kupeleka jeshi lenu na kuwashika wanao dai haki za nchi yao? na kuwaua?

Nafikiri tufike mahali tuache huu unazi na unafiki uliopita kiasi? shame on you
 
Mdondoaji.. hiyo Thesis hata siwezi kuendelea kuisoma kwani mara moja imejaa mambo ambayo si ya kweli kihistoria!
 
..yeyote yule anayeyakana Mapinduzi na kuutambua "Uhuru" wa 1963 kwa namna moja ua nyingine anamkubali Sultani kama kiongozi halali wa Zanzibar.

..Katiba ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi ilikuwa inamtambua Sultani kama mtawala wa Zenj, na chini yake alikuwepo Waziri Mkuu. wakati huo pia Zanzibar ilitambulishwa kama "Sultanate of Zanzibar."
jokakuu.
Narejea tena . Zanzibar kuna watu wanayalaani yale mapinduzi lakini hawaukubali usultani na wala hawautaki hata kuusikia , yes i said it (likihitajika darasa hapa nitatoa). Familia yangu upande wa baba ni katika waliopata mateso ya mapinduzi na jamaa wa upande wa mama walikuwa upande wa kupindua(hivyo damu yangu inaingia pande zote mbili za mapiduzi), Naongea kuhusu reality na sio historia ya shule, nashukuru wazee wangu wameishi kwa amani muda wote bila dosari.Kipindi cha mapinduzi kilikuwa kigumu kwao lakini mola aliwasaidia ,sio vyema mkawa mnafanya mzaha na hili jambo, daima wazee wangu walilia na kukosa nguvu pale waliponielezea yaliopita Zanzibar, hata nikafika mahala kuona tabu kuwauliza.Nimesoma mengi kutoka kwao na nikabeba ujasiri wa kuamini kwamba ni mimi na vijana wenzangu ndio wa kuibadilisha Zanzibar. Leo hii kila tukitaka kujaribu kupiga hatua kuna watu kwa makusudi mazima wanafufua chokochoko hizi na zile za kihistoria,Inanikera sana,I must be honest!.Zanzibar ya leo hakuna anaetaka usultani, ni jambo ambalo liko wazi.Nakuombeni Tujadilini mambo yanayoingia akilini.Sikatazi kuongelea historia ya Zanzibar lakini itumiwe kujenga na sio kubomoa!
Zanzibar ni taifa la kidemokrasia linaloongozwa na katiba ya serikali ya MAPINDUZI ya Zanzibar na sio vyenginevyo.
nawasilisha
 
Nakuelewa:

Sikiliza ushuhuda ktk Mazungumzo 'Live' ya BBC na wakazi wa Zanzibar walioona kwa macho yao nini kilitokea Zanzibar Stone Town, Darajani , Bambi n.k siku Mapinduzi yalipotokea Januari 1964 na pia Historia nzima chini ya utawala wa Kisultani

Na pia kama wakazi wa Zanzibar wanawaza kurudishwa Utawala wa Kisultani au la. Endelea kusikiliza mazungumzo ktk iplayer BBC:

http://www.bbc.co.uk/iplayer/console/p003qfx1 Heart and Soul Return to Z'bar (jumla dakika 28)
http://www.bbc.co.uk/iplayer/console/p003md9n Heart and Soul return to Z'bar 2 (jumla dakika 28)
 
Mdondoaji.. hiyo Thesis hata siwezi kuendelea kuisoma kwani mara moja imejaa mambo ambayo si ya kweli kihistoria!

Huendelei kusoma kwasababu umezoea dogmatism, inabidi usome sasa kujua ukweli

Historia inakuwa kweli ikiwa unapenda kusikia kile tu unapenda kusikia?

Hii ni aina mpya ya Great thinker! soma ndugu ili uwe fair..siyo unajaza uwongo watu kwa historia ya la sita, iliyoandaliwa na Mtawala kwa faida yake.
 
Mdondoaji.. hiyo Thesis hata siwezi kuendelea kuisoma kwani mara moja imejaa mambo ambayo si ya kweli kihistoria!

Hapo ndipo mnaponishinda wadanganyika mnataka yasemwe mnayotaka nyie msioyataka hamtaka yazungumzwe nakushauri Mwanakijiji isome yote bwana mdogo huyo ameshida tuzo bora anashuka historia ya zanzibar sasa hivi anamalizia PhD yake Oxford University.

Tuseme huyo ni bwana mdogo ana munkari na kitabu ngoja nikuletee gwiji mwengine (Professor Thomas Burgess) wa historia usome ameandika nini maana sasa sijibizani na mtu natoa reference tu. Kamata reference hiyo kama hauna password i search online utaipata but JSTOR ni hazina kubwa ya articles nyingi duniani.

http://www.jstor.org/pss/3097615

Paper Title: Burgess, T., "Cinema, Bell Bottom, and Miniskirts Struggles over youth and citizenship in Revolutionary Zanzibar", Journal of African Historical Studies, Vol 35, No 2-3 (2002)

Ukweli utajulikana tu na sio conspiracy za ajabu ajabu
 
i1658_sultan.jpg

Kwa kadiri ya kwamba Sultani Jamsheed Bin Abdallah anaendelea kujitambua kuwa ni Sultani wa Zanzibar na kwa kadiri ya kwamba uzao wake unakidai kiti hicho kama urithi wa haki yao; na kwa kadiri ya kwamba wapo Wazanzibari ambao wanamtambua Jamsheed kama Sultani wao na ya kwamba wako tayari kurejesha status quo ya 1963 (ambapo Sultani alikuwa ni mfalme wa heshima Kikatiba kama ilivyo Uingereza - japo tofauti kidogo) basi juhudi zote za maridhiano haziwezi kufanikiwa kwani Sultani na uzao wake watakuwa ni kama kivuli juu ya Zanzibar na watu wake.

Ili kuleta mapatano ya kweli (kama anavyosema Lula) basi hatima ya Sultani na uzao wake ni lazima ijadiliwe.

a. Je, ni jinsi gani Bw. Jamsheed anaweza kurudi Zanzibar bila ya kuwa na mamlaka ya Usultani yeye na uzao wake milele?

b. Je, Bw. Jamsheed anaweza kuwa na nafasi yoyote ya heshima katika Zanzibar ukiondoa ya kutambuliwa kama Sultani?

c. Je, akikubali kukana kiti cha Usultani, yeye mwenyewe, wanawe na wale wote walio katika mnyonyoro wa urithi milele anaweza kurudi Zanzibar na sehemu ya upatanishi ni kumrudishia baadhi ya mali zake zilizochukuliwa baada ya mapinduzi ya 1964?

d. Je, aweza kurudi pasipo kuwa na nafasi yoyote ya kisiasa na kukatazwa yeye mwenyewe na warithi wake kushiriki katika uongozi wa chama chochote cha siasa?

e. Je, Bw. Jamsheed katika kuleta mapatano yuko tayari kutambua na kukubali uwepo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Uzao wa Jamsheed (allexperts):

*Prince Sayyid Ali bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Khalifa bin Jamshid Al-Said
*Princess Sayyida Matuqa bint Jamshid Al-Said (1957-)
*Prince Sayyid Abdullah bin Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Wasfi bin Jamshid Al-Said (1972-)
*Princess Sayyida Adla bint Jamshid Al-Said
*Prince Sayyid Gharib bin Jamshid Al-Said

Ningependa CCM na CUF watoe misimamo yao kwa maswali yangu hayo.

Kwa habari zaidi ya line of succession ya Masultani wa Zanzibar BONYEZA HAPA

Hiyo list ya watoto iko wikipedia but sio hizo habari za kuwa Sultan Jamshid anataka kurudi zanzibar tunaomba utupe reference umezitoa wapi???
 
naomba kuuliza, Hivi Jemshid hakuukana usultani Zanzibar, Vipi malkia wa Uiengerza alikana himaya yake kule USA? ikiwa anataka kuendeleza himaya USA, itakubalika?

Mimi huwa napenda kusoma habari, lakini chache sana huwa naziamini, hivi kufanya master yako kwa kutegemea vitabu (siasa) halafu ujisifu kuwa eti mimi ninajuwa, ndio unajuwa kulingana na kitabu, sio kwa kweli hasa, hebu kasome tena na pitia kwa Mazrui, yule wa Oxford atakupa zaidi
 
Ukweli utajulikana tu na sio conspiracy za ajabu ajabu

Kwa bahati mbaya sisi wengine hatuhitaji kusimuliwa wala kusoma vitabu - historia ya mapinduzi ya Zanzibar tunaijua kwa sababu tulikuwepo. Kama mnaweza kuwasikiliza wazee wenu inabidi mtusikilize na sisi wengine kwani hatuna sababu ya kuvutia upande wowote, sisi si wamba ngoma kama hao wazee wenu.

Mimi ni Mtanganyika asiyeona faida yoyote ya huu Muungano na hata ukivunjika kesho naamini maisha yataendelea kwani tumechoka kuipakata Zanzibar. Mlikuwa na bahati ya kumpata kaka aliyewashika mikono na kuwakingia kifua adui alipotaka kuwaangamiza lakini shukrani tunayopata kila leo ni kutukanwa.

Mdondoaji, hiyo conspiracy za ajabu unazoongelea ni zipi ? Je si kweli kuwa Sultani Jamsheed ana ndoto za kuitawala tena Zanzibar ? Hata Idi Amin ndoto yake ya kurudi kuitawala Uganda haikuzimika hadi siku yake ya mwisho anaingia kaburini, sembuse Sultani ambaye dalili zote zaonyesha anao sympathizers.
 
Wewe ni muongo kabisa kwa experience yangu hakuna hata mtu mmoja aliyekuwapo kipindi cha mapinduzi akawa anajisifia kuwa ameyaona kwani yaliyotokea ni ya kusikitisha. Niliwahi kwenda kumuona mzee mmoja jina namuhifadhi kigamboni ambaye alishiriki mapinduzi akawa hawezi hata kuandika achilia mbali kuona sasa hebu tuambie wewe umeyaonelea wapi acha kutudanganya kaka labda ulikuwa mtoto kipindi hicho.

Tuje katika conspiracy mnasema Jamshid atarudi kwani akirudi atafanya nini zanzibar? Akirudi na asiporudi zanzibar itawasaidia nini wazanzibar? Tangia zamani Tanganyika ilikuwa inatamani kuimeza zanzibar for many reasons, wealth, business, security reasons. ASP imeanzishwa na watanganyika ikijidai eti inatetea haki za wazanzibari. Washirazi walijiunga baada wakawastukia kuwa ni bomu wakaamua kuanzisha Zanzibar People Party (ZPPP). ASP ilingia na conspiracy ya kuwa eti serikali iliyoko madarakani ilikuwa ya vibaraka, baada ya mapinduzi wakadai eti wamemkomboa mwafrika dhidi ya sultani, 1977 wakaja wakasema wamemkomboa mwafrika dhidi ya maadui wa ujamaa, Sasa wanakuja conspiracy nyengine eti sultani anarudi zanzibar hatudanganyiki abaa!!!!

Kuhusu mapinduzi hakuna mtu aliyewaomba watanganyike wapindue zanzibar but kwakuwa nyerere aliona plan zake hazitasimama hadi atakapokuwa na serikali ya wadanganyika wenzie zanzibar ili apate kukitawala kisiwa. Ijapokuwa hamna evidence linking Nyerere na ASP but alifahamu everything going on kuhusu zanzibar angelikuwa muadilifu kweli kwanini hakuyazuia masuala ya uhaini dar akayaacha yaendeleee hali yeye ni waziri mkuu!!!!

Muungano hakuna mtu anautaka kama nyie mmeuchoka zanzibar ndio kabisa wazanzibar hawataki hata kuusikia basi tu ni CCM ndio inashikilia but mie sidhani kuuvunja ni busara la msingi ziwepo serikali tatu na muungano uwe shirikisho au jamhuri na sio hivi. Kila mmoja ajitegemee kivyake whether jamshid amerudi, queen elizabeth ii, babu amerudi zanzibar inachotaka ni maendeleo watu wamechoka!!!! Hatuhitaji sympathy ya mtu tunalolisema ni ukweli tu
 
Back
Top Bottom