Rais Dkt. Mwinyi aishukuru Qatar kufadhili mradi wa kurudisha shule watoto, Zanzibar

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na mtoto wa Amiri wa zamani wa Qatar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makumbusho ya Taifa Mhe. Sheikha Al Mayassa bint Hamad bin Khalifa Al Thani katika hoteli ya Sheraton ambapo ndipo linapofanyika Jukwaa la Doha (Doha Forum) tarehe 10 Desemba, 2023.

Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Mhe. Sheikha Al Mayassa kwa niaba ya Serikali ya Qatar kupitia mradi wa miaka mitatu wa “Out Of School Children” (OOSC) uliofadhiliwa na Qatar Fund for Development ambao umetekelezwa kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa UNICEF pamoja na Education Above All Foundation (EAA).

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa baada ya kuwarudisha shuleni watoto zaidi ya 35,500 Unguja na Pemba na kuendelea na masomo.

Rais Dk. Mwinyi pia amependekeza kwa Mhe. Sheikha mpango wa kubadilishana wanafunzi katika fani ya Ukutubi kutoka Zanzibar kuja kujifunza na kubadilishana uzoefu na maarifa katika Maktaba ya Doha.

Kabla ya kumaliza mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi amemweleza Mhe. Sheikha kuwa Zanzibar ina utajiri wa Mambo ya Kale hivyo kutokana na uzoefu mzuri wa Qatar katika masuala hayo, ingekuwa ni fursa nzuri kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) hii itawawezesha wataalamu kutoka Qatar kubadilishana uzoefu.

IMG-20231210-WA0088.jpg
IMG-20231210-WA0087.jpg
IMG-20231210-WA0089.jpg
 
Rais Mwinyi kamwakilisha Rais wa JMT lakini anafanya shughuli zisizo za SMZ. Zile za Tanganyika nani anazifanya?

Vituko katika Muungano haviishi, tunahitaji Tanganyika. Rais SSH anasaidia sana kuidai Tanganyika

Pascal Mayalla JokaKuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom