Sufi/sufu inapatikana kwa wingi mkoa gani?

Boutafrica

JF-Expert Member
Dec 11, 2014
949
2,065
Kuna Rafiki yangu flan amenipigia simu kutoka Botswana anahitaji Sufi au sufu lile zao linalofanana na pamba.

Kiufupi ameniambia anahitaji tone 60 kwa awamu hii ya kwanza then awamu ya pili atahitaji tone 140 december mwaka huu.

Tone 1 anainunua kwa Tshs 600,000
na haijalishi upo mkoa gani kikubwa akukute nao huo mzigo.

Sasa kiukweli mimi sifahamu ni mkoa gani unapatkana hilo zao kwa wingi so naomba kwa anaejua zaidi mkoa inapopatikana hii product hapa Tanzania.

Kama unafahamu ilipo au unaweza kuipata nichek inbox nikuunganishe nae.
 
Mkuu sufu inatokana na manyoya ya wanyama, kondoo, sungura n.k
Sasa umesema unataka inayotokana na pamba?
 
Kama ndo zile zinazotoka kwene mti wa msufi nenda Tanga hasa Korogwe japo kwasasa misufi mingi watu wameiua au kuikata baada yakuona haina ishu
Namsaidie Na Maeneo Aende Kwamdulu, Kwakombo Atapata Nyingi Hapo Korogwe. Morogoro Pia Tungi Atapata
 
Hiyo Sufi inapatikana ktk maeneo kunakolimwa Zao la Mkonge au Kakao.Nenda mji unaitwa Maramba utaipata kwa wingi.Mji huu upo wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 
Utatumia zaidi ya laki 6 kupata hiyo tani 1 ya sufi. Hii ni biashara kichaa haifai
Nimewasiliana nae muda huu kuhusu bei kulinganisha na ugumu wa upatkanaji amenijib kwamba ngoja afanye calculation then kesho atajibu khs kuongeza kiwango cha bei.
 
Sawa mkuu,so huko kyela inapatikana maeneo mbali sana mashambani au?
Hiyo miti Kyela imeadimika sana,mitunda na mitumbati ilitumika sana kutengenezea mitumbwi kwa ajili ya kubhigilila (kuvulia) samaki mitoni na ziwani. Ila njia ya Malinyi nimeiona ona
 
Back
Top Bottom