Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Januari 10, 2022. Shahidi namba 8 aendelea kutoa ushahidi. Kesi imeahirishwa hadi kesho 11/01/2022

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,805
4,487
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 10/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

1641805247788.png

Picha: Baadhi ya watu waliohudhuria mahakamani

Updates
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 kamili

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha jopo la mawakili
  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala, Naomba Kuwatambulisha:
  • Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Seleman Matauka
  • Sisty Aloyce
  • Faraji Mangula
  • Michael Mwangasa
  • Gaston Garubindi
  • Maria Mushi
Jaji anaita washtakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya uamuzi Mdogo, Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: nasi pia tupo tayari Kupokea Uamuzi na Kuendelea Jaji anaandika kidogo.

Mahakama ipo kimya!

Jaji anaendelea sasa.

Jaji: Ni kweli Shauri hili Lina kuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo. Kama ambavyo Mahakama Ilihairisha Mwaka Jana, Uamuzi huu Unatokana na Kupigwa kwa Kupokelewa Vielelezo ambavyo Vilikuwa vimetolewa na ASP Jumanne.

Na Kwamba aliomba Kutoa Vielelezo baada ya Kufanya Upekuzi na Kwamba Upekuzi huo Ulifanyika Mbele ya Mwenye Nyumba Mariam Juma na Mjumbe wa Nyumba kumi pamoja na Mke wa Mshtakiwa Na Kwamba alijaza Certificate of Seizure Kwa Mlolongo wa Mali ambazo alizo kamata kama ambavyo nimeziorodhesha, Na Kwamba Baada ya Kufanya Upekuzi huo alizo weka alama X/ HD Na baadaa akamkabidhi Mtunza Vielelezo Kituo cha Polisi Kati Na Kwamba alivichukua na Kwenda Kutunza Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam Tarehe 17 December 2021.

Jaji: Notebook Nyekundu hakutoa Hapa Mahakamani, na Kwamba Baada ya yeye Kupitia na Kugundua haina Uhusiano na Kesi hii alicha Kuitoa hapa Mahakamani.. Na alikuwa anavitaja Vielelezo Kwa Kutumia Alama ya X/HD.

Alipokuwa anavitoa hapa Mahakamani alipingwa na Mawakili wa Utetezi, Wote Walipinga Vielelezo Vyote vilivyokiwa vinaombwa Kutolewa hapa Mahakamani.. Hata hivyo Kila Wakili akisimama na Kutoa Hoja zake.. Kwa Maana hiyo Mahakama haitaenda kwa Kila Wakili Bali kwa Hoja Moja moja.

Jaji: Chain of Custody, Competence ya Vielelezo Vyenyewe na Shahidi aliyekuwa anaomba Kutoa Mahakamani.. Si Jambo Jipya hapa Mahakamani.. Mahakama hii kwa kutumia Experience ya huko Nyuma. Sheria Inaelezea Kwamba Upokelewaji wa Vielelezo Mahakamani Kupitia Sheria Kesi ya SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER, CHARLES GAZILABO AND THE OTHER THREE.

Katika Mashauri yote Mawili Mahakama imeeleza Kwamba Vielelezo Inaweza Kupokelewa Baada ya Vitu Vitatu.. Kutumia Criteria ya Competence, Mahakama ilieleza Kuwa test ipo katika Mambo Matatu yanaitwa Authentication. Lazima atambue Unique features, Unique features ya Kielelezo hicho, Atambue Chain of Custody.. Kwa Maana hiyo Mapingamizi yaliyoletwa yameltwa kwa Jambo Moja la Competence.

Jaji; Mhakama Ita adopt namna ambavyo Mapingamizi yameletwa kwa Chain of Custody na Competence. Issue ya Chain of Custody imeelezwa na Mawakili Wote wa Utetezi. Nitaamua kwa Kufuata Ishu kama ambavyo zime letwa na Mawakili Wa Utetezi.

Maelezo Ya Jumla yanaeleza Chain of Custody ni nini.? Na Wakili Nashon Nkungu Alieleza nini Maana ya Chain of Custody.. Mahakama inakubaliana Kwamba ni namna ambavyo Kielelezo kilikamatwa na Kikitunzwa wapi Kama ambavyo Kilikuwa Mahakamani.

Kielelezo Ambacho Kilikuwa kimelengwa Kuletwa hapa Mahakamani Kilichezewa na Kwamba hii inaonyesha kwamba Vielelezo Vilikuwa Pamoja ndiyo Maana Notebook Nyekundu Imetolewa.

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi walikuja na Hoja Kadhaa Kwa Mujibu wa Sheria Vielelezo ambavyo vimekamatwa Kwamba Vielelezo ambavyo Vimekuwa Commited Vinatakiwa Kuja Vyote Mahakama Kuu.

Kwa Sheria Ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 inataka Afisa wa Polisi ambaye anataka Kutoa Kielelezo Mahakamani anatakiwa arudishe kwa mtu aliyepata Kwake Kama hajarudisha inaonyesha Kielelezo hicho Kimechezewa.

Inaonyesha kuwa shahidi Namba nane hakutoa Hoja zake kwanini Kielelezo Hicho Hakikuletwa Mahakamani.. Waliendelea Kujikimbusha Mahakama Kwamba PGO 229 Afisa wa Polisi anatakiwa Kushika Kielelezo Hicho Mpaka atakapo Kitoa Mahakamani. Na Kwamba Wakati anakamatwa aliamini kina husika ndiyo Maana alikikamata, Hivyo si Sawa kutokutoa hapa Mahakamani.

Jaji: Wakili Malya alisema Kwamba haieleweki Huenda Kwamba Kielelezo hicho Kilikuwa kinamnufaisha Mshitakiwa namba Moja.. Kwa Hoja wakasema Kwamba Wanaomba Mahakama Ione kwamba Kielelezo Kimechezewa.

Kwa sababu Vielelezo hivi Vingine vilikamatwa na Note Booka Nyekundu basi Mahakama Ione kuwa Vielelezo Hivyo Vimechezewa.. Kwa Upande wa Mawakili Wa Mashtaka Walisema Kwamba Mawakili Wa Utetezi Wametafsiri Vibaya. Kwamba Upande wa Mashtaka hawalazimishwi Kutoa Vielelezo Vyote Mbele ya Mahakama..

Shahidi aliona Kwamba Kielelezo hicho hakihusiki hapa Mahakamani.. Kwa Maelezo hayo waliendelea Kusema Kusema Kielelezo Kipokelewe Mahakamani Kama ambavyo Vilikamatwa Sasa Hapa Mahakamani, Mahakama ni kweli Inaona kwamba Kielelezo Hicho hakikutolewa Hapa Mahakamani Kutokana na Shahidi Namba 08 alisema Kwamba hakutoa Kielelezo hicho hapa Mahakamani Kwa sababu aliona Kwamba haihusiani na Kesi hapa Mahakamani.

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi wana maoni kuwa Vielelezo Vyote ambavyo Vimekuwa Commited Vinatakiwa Kuja Mbele ya Mahakama Kuu na Kama siyo basi Mchakato wa Kurudisha Kielelezo Hicho Ulipaswa uwe Umefuatwa Kwa Namna hiyo Waliomba Mahakama Ikatae Vielelezo Vyote.

Ukisoma pande zote Mbili ni wazi Kuwa Kielelezo Hiki Kwa Kutolewa Kwake Kimekiuka Sheria Ukizingatia Kuwa Kilikuwa tayari imekuwa Commited.

Jaji: Kifungu cha 246 CPA na Kanuni ya 8 ya Mwaka 2016 inasema Kuwa Vielelezo Vyote ambavyo Vimekuwa Commited kutoka Kwenye a Mahakama ya Hakimu Mkazi ni Vile ambavyo Mkurugenzi wa Mashtaka atataka kuvitumia Hakuna Sheria inayosema Kwamba Kila Kielelezo ambacho Kimekuwa Commited Kinatakiwa lazima Kiletwa Mahakamani.. Ni wazi atakuwa amepitia Kielelezo hicho Kuona Kama kinatengeneza Kesi au hakitengenezi kesi.

Siyo lazima Kwa Ushahidi au Shahidi Ambao amekuwa Commited Anatakiwa lazima aje Kutoa Ushahidi Mahakamani.. Katika Mazingira hayo basi Mahakama Inaona kwamba Pingamizi hili limekosewa Mahakama Inaona Pingamizi hili halina Msingi na Kutupilia Mbali.

Jaji: Kuhusiana na Chain of Custody imeelezwa Kwamba Kielelezo Kutoka sehemu Moja kwenda sehemu Nyingine Mahakama lazima itazame sana Endapo Mnyororo Wa Kielelezo Kutoka Sehemu Moja kwenda Sehemu Nyingine Inapokuwa Umevunjika Basi Upande wa Mashtaka Wanakuwa Wamekuwa wameshindwa.

Hakuna Maelezo Yaliyotolewa na Shahidi Namba 08 Kwamba aliwezake Kutoa Kielelezo Hicho kutoka kwa sergeant Johnson.. PGO 229 2(c) PGO Hiyo inasema Kwamba Funguo ya Chumba Cha Vielelezo Inatakiwa itajwe ni nani alikuwa anatunza Kwa Kushindwa Kueleza Hilo wanaona Kwamba Chain of Custody imevunjika.

Jaji: Bwana Kidando Nayeye alitoa Maelezo yake Kwamba Pingamizi hili limekosa Substance Kwamba PGO ya 229 4(a) inavyotakiwa Kidando alieleza Namna ambavyo Shahidi namba 08 aliviepeleka Kwa Sarjent Johnson na Kwenda Kuchukua Tarehe 17 December 2021.

Na Kwamba Shahidi ajahojiwa Kuona ambavyo Ushahidi Wake Unavyotetereka, Akaendelea Kusema Kwa Kina Kuwa Shahidi alieleza kwa Kina namna ambavyo alitunza Kielelezo hicho hapa Mahakamani. Akaomba Mahakama Itumie Sheria Kesi ya IGNATUS MKOKA, Kesi namba 245 ya Mwaka 2013, Pia akaomba Mahakama Itumie sheria Kesi ya KENNEDY SHAYO 84 ya 2017 Ukurasa Wa 31 na 34.

Na Akaendelea Kusema Kwamba Shahidi anaeleza Mahakama Vile Vielelezo ambayo alivi kamata na kuvitunza kwa sergeant Johnson.

Jaji: Upande Wa Utetezi Walisema Kwamba Utunzaji wa Vielelezo Katika Sheria Imetungwa kulinda Vielelezo Visichezewe.. Na Kwamba Sheria inasema Kwamba Polisi anatakiwa kuwa Na Notebook namna ambavyo alikuwa anaviorodhesha.

Na Kwamba Shahidi Hakuonyesha Paper Trade na Vithibitisho Vya paper havikuonyesha kama ambavyo inatakiwa.. Wakaomba kutumia Kesi ya ILUMINATUS MKOKA, Pamoja na Kesi ya MAYALA MBITI 177 ya 2015 Ukurasa wa 6.

Jaji: Kuhusiana na Kesi ya KENNEDY SHAYO wakaomba Kwamba Kesi hiyo I aunga Mkono Hoja za Utetezi, Kwa sababu Bunge liliona kuwa Kielelezo ambacho ni Nguo kuna dalili za kuchezewa. Na Kwamba Mnyororo huo unakuwa Umevunjika.

Na Kuhusiana Kupokelewe kwa Vielelezo hivyo kuwa Vitaathiri Washtakiwa au lah.. Walisema Kuwa Bunge linapotunga Sheria na Sheria hiyo Inapokuwa haifuatwi basi Washtakiwa Wanakuwa wameathirika.

Kwenye suala hili ni seme ni kweli Kwamba suala la Upokelewaji wa Vielelezo Limeelezwa..Na suala Zima La Upokelewaji wa Vielelezo Inategemea Ambavyo Vielelezo vimetunzwa Na Chronological paper Trade inaonyesha namna ambavyo Kielelezo Kilikuwa kimekamatwa Mpaka Kutunzwa.

Jaji: suala Zima La Upokelewaji wa Vielelezo Na Chain of Custody Limeelezwa na Sheria Kwa Kifungu cha 38 cha CPA, Sura ya 322, Sheria Ya Polisi na Polisi Wasaidizi, PGO ya 229 Suala la Kufuatwa kwa Mnyororo Wa Kielelezo Kuna Vipingili Vingi.

Unapokuwa Unaangalia Kipengele Kimoja kikiwa Kimekatika Kimoja basi Mnyororo huo Unakuwa Umekatika.. Katika Kushughulika na Vielelezo Hivyo kuwa Vipo namba ambavyo Vinakatwa Mpaka Vinafika Mahakamani. Siyo Sahihi Shahidi Mmoja tu anapotoka Ushahidi Kueleza Kwa niaba ya wengine Kuhusiana na Mnyororo Kuvunjia au kutovunjika.

Jaji: Kwenye kesi ya CHARLES GAZILABO Mahakama Ilitoa Uamuzi Kwamba Mahakama ya Rufani inaamini uthibishwaji wa Utunzaji wa Mnyororo Hauwezi Kuthibitishwa na Shahidi Mmoja, Kwamba Mahakama Itaweza Kuona baada ya Ushahidi Wote Kutolewa.

Katika Kesi ya CHRISTINA Vs JAMHURI Ukurasa Wa 5 na 7 Kufuatia Mfano huu Mahakama Ya Rufani inasisitiza Kuwa Kama Hakuna Ushahidi Wa Moja Kwa Moja Kwamba Mnyororo Ulichezewa. Na Kwamba Kama Upande Wa Jamhuri hawatoleta Mashahidi Wengine Kuthibitisha Mnyororo huo basi Mahakama Inaweza Kusema Mnyororo huo haujathibitishwa.

Jaji: Kwenye kesi ya ABASI KONDO Vs JAMHURI Kesi 472 ya 2017.. Pia Mahakama Ya Rufani Imetoa Malekezo Kwemye kesi ya ANANIA Vs JAMHURI Mahakama Iliyoketi Dar es Salaam.. Hizo authorities nilizosema hapo Juu ni Authorities ambazo zimetolewa na Mahakama Ya Rufani.

Kwa Maana hiyo Mahakama Ya Chini inapotoa Maamuzi lazima Izingatie Maamuzi hayo ya Juu.. Katika Mazingira hayo basi Kwa Kutizama Shahidi ambaye amekuja Kutoa Ushahidi Hapa Mahakamani Kwamba Vielelezo ambavyo alivikamata hakubaki navyo Bali alimkabidhi sergeant Johnson.

Jaji: Kwakuwa Bado Upande wa Jamhuri hawajashindwa Kumuita sergeant Johnson, bado hajaitwa Mahakamani Kutoa Ushahidi hatuwezi Kusema Kuwa Shahidi aliyepo Mahakamani ameshindwa Kutoa Mnyororo Wa Ushahidi.

Jaji: Kuhusiana na Mwaliko niliopata kutumia Kesi ya MKOKA NA MAYALA MBITI nakubalina na Upande wa Utetezi kuwa Kanuni zilizotumika katika Mashauri hayo ni mazuri lakini Ikumbukwe Maamuzi hayo Yalifanyika baada ya Ushahidi Huo Kutolewa. Naona Hoja za Utetezi Zimeletwa Kabla ya Wakati labda kama ingeletwa wakati wa Final Submission. Kwa sababu hiyo Mahakama haiwezi Kuzingatia na Kwa sababu hiyo Pingamizi hili nalitupilia Mbali.

Jaji: Ikumbukwe Pia Shahidi aliyopo Mahakamani, yeye ndiye aliye fanya Search na alizikamata.. Hoja za Kwamba Shahidi amethibitisha Kwamba Mali ambazo zinatolewa Mahakamani ni Mali ya JWTZ wakati Hakuna Mahala aliyothibitisha Kuwa Vielelezo hivyo ni Mali ya JWTZ na pia hakuna.

Mahali ambapo JWTZ walikuja Kuthibitisha Kuwa ni Mali yao Aliendelea Kusema Wakili JOHN Mallya Kuwa Shahidi alishindwa Kutaja Vizuri Hapa Mahakamani, Ikumbukwe ni Vifaa Vya Kijeshi na Vina Majina yake ya Kijeshi.

Akatoa Mfano Kuwa Shahidi amesema Kuwa Kielelezo ni PONJOL wakati ni Sleeping Bag.. Akaendelea Kuomba Mahakama Kwamba Shahidi ameshindwa Kuvitambua Vielelezo Hivyo Na Kwamba Vielelezo Ambavyo Vilitolewa Hakuna sleeping Bag na akaomba Kwa kusema shahidi hana Knowledge ya kutosha.

Jaji: Shahidi alisema Vielelezo ni Mali ya JWTZ na JKT wakati Shahidi hajawahi Kufanya Kazi JKT wala JWTZ.. Kwa Sababu Vielelezo hivyo ni Vya Jeshi na Shahidi hana Knowledge Basi Mahakama Isipokee Vielelezo hivyo Kwa sababu Shahidi Siyo Competent.

Kwa upande wa Mashtaka walikuja Kusema Kwamba likuwa Kutoa Ushahidi Wa Kile ambacho alikikamata, Na Kwamba Kwa Hatua ya sasa siyo Sawa Kutoa Ushahidi Wa Kitaalamu.. Na Kwamba aliendelea Kusema Kwamba A shahidi alivitambua kwa Alama alizo weka yeye Mwenyewe ambayo ni X /HD.

Shahidi alieleza Kwa Kina Kuwa aliweka alama hiyo baada ya Kuvikamata, Aliomba Mahakama Ione kwamba Shahidi huyo ameweza Kutambua Vielelezo hivyo.. Kwa sasa Mahakama Inatazama kama Vinaweza Kupokelewa na siyo Kuthibitisha Kuwa ni Mali ya Jeshi au siyo Mali ya Jeshi.

Jaji: Mallya hajaonyesha Kuwa yeye alivitambuaje hapa Mahakamani.. Wakasema Kuwa Imeelezwa kwenye kesi ya Jamuhuri Vs CHARLES GAZILABO, Kwamba Mahakama Ishughulike na Kuvipokea. Kuhusu alama aliyoweka aliomba Kusema kwamba Mahakama Ione Vielelezo Hivyo Vilishughulikiwa Vizuri.

Katika Rejoinder Walieleza Upande wa Utetezi Ni kwamba Kwakuwa Shahidi alitaja Kwa Majina Vielelezo Hivyo basi alionyesha kuwa anavitambua.. Maelezo ambayo yameletwa pande zote mbili Kuwa Kukosekana Kwa Uelewa Kuhusu Vielelezo hivyo Inatosha Kum' disqualify.

Jaji: Upande wa Mashtaka Wanasema Kwamba Suala la Utalaam siyo Suala la Sasa.. Katika Kesi ya SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER VS DPP inasema Kwamba Katika Ushahidi Kuna Identification ikifanyika inatosha.. Utambuzi Kwa Kuangalia features pekee.

Kwa Alama ambayo Shahidi ameiweka yeye Mwenyewe, ambayo Nimeweka hapo Juu kuwa Kielelezo Kinaweza Kutambuliwa kwa unique features Features ambayo ni Mabaka inapatikana Katika Vielelezo Vyote Lakini Features ambayo ni X/HD ilikuwa inatosha.

Nafahamu maelezo ambayo yanasema kuwa features X /HD siyo Features ya Kisheria.. Mahakama Inaona Hoja hii itashughulika nayo katika Hoja inayofuata.. Hoja ya Utaalamu tuta shughulika nayo baadae siyo kwa sasa.

Jaji: Hoja ya Kidaftari cha Five star, Kuhusu Kikaratasi ambacho Kilikuwa ndani yake, Kuwa hakikufuata Mchakato wa Sheria Juu ya Kuongeza Kielelezo.. Upande wa Mashtaka hawajafuata Utaratibu Wa Kisheria Kutumia Kifungu cha 289 cha CPA sura ya 20 Juu ya Kutaarifu Mahakama Katika Kuingiza Kielelezo Ambacho hakikukuwa Commited.

Vielelezo ambavyo Havikuwa Commited katika Trial Court.. Kidando Wakati anajibu alieleza Mahakama Kuwa suala Zima La Commital Limeelezwa Katika Kanuni ya 8(2) ya 2019 GN ya 277 Katika Ukurasa Wa 32,33 wa Commital Proceedings, Inaonyesha Kuwa Ilishatajwa.. Katika hali hiyo Waliomba Mahakama Ipokee Kielelezo hicho.. Katika Kesi ya RONJINO walisema Kwamba Haihusiki na urodheshwaji wa Vielelezo.

Jaji: Upande wa Utetezi Wakasema Kuwa Kielelezo ambacho Kinatajwa hakikupokelewa, Wakaomba Mahakama Kuwa katika Certificate of Seizure Kuna Vingine vimetwajwa. Kwa Kuangalia kwa Ujumla naona kuwa ni Kweli Vielelezo vinavyolengwa Kutolewa hapa Mahakamani havikutolewa hapa Mahakamani haviku Orodheshwa wakati wa Commital.

Kifungu cha 246 linataka Kuwa Kielelezo au Ushahidi Wowote unapotakiwa Kupokelewa Mahakamani Unatakiwa uwe Umekuwa Commited Mahakamani.

Jaji: Nikisona Kanuni ya 8(2) ya Mahakama hii inataka Mahakama hii Kusoma Maelezo Kwa Lugha wanayo ufahamu, Kusoma Ushahidi Wanaoshtakiwa nao, Nyaraka za Ushahidi Unaotarajiwa Kutolewa Mbele ya Mahakama. Kinachotakiwa Kufanywa na Mahakama Husika ni Kusoma Mashtaka, Kusoma Ushahidi lakini pia Kusoma Nyaraka zinazo Contain Substance ya Ushahidi unapotakiwa Kusomwa Mahakamani Kinachotakiwa Kufanywa ni Kungaliwa Kama Ni kweli kilisomwa?

Hayo ndiyo Masharti ambayo yapo Kifungu 289 (1) Hakuna Shahidi atakayeitwa kama Ushahidi Wake haukusomwa wakati wa Commital, Shahidi ataitwa endapo Kama Ushahidi Wake Ulisomwa na Ushahidi huo ulienda Upande wa Mashtaka.

Katika Haki hiyo Basi kumbe kinachotakiwa ni Shahidi Kuitwa bila Kutolewa Notisi Upande wa Utetezi, Kama Kuna nia ya Kumuita shahidi huyo na Mahakama Ita angalia Notisi hiyo ni toshelezi au Siyo toshelezi.

Hakuna Takwa la Kisheria Kuwa kuna Takwa la Kuleta Kielelezo ambacho ni physical.. Kwa Maelezo hayo naona Hakuna Sheria ambayo imevunjwa.

Jaji: Na Upande wa Mashtaka Waliomba Kwamba Ili Kusudi tukubali au Kupokea Kielelezo chochote lazima Pawe na Sheria inayokataza.. Kama Hakuna Sheria Wala Sheria Kesi Mahakama Hii itakuwa Inafanya Makosa Kukataa Kielelezo.

Kwa Upande wa Mashtaka Hawalazimishwi Kusoma Kielelezo ambacho ni Physical Vielelezo Vyote ambavyo vinalengwa Kutumika hapa Mahakamani, Hakuna Sheria ambayo imevunjwa. Na Sheria ambayo zimeorodheshwa hazikatazi.. Kwa Maana hiyo Naitupilia Mbali Hoja hii.

Jaji: Lakini pia Suala La Mr. Mallya aliomba Mahakama Kuwa Kidaftari ambacho Kilikuwa Commited siyo Kilicho letwa hapa Mahakamani, Mahakama imeombwa Kwenda kwenye Committal Bundle kungalia kama Kielelezo Hicho Kilikuwa Commited.

Mahakama Imeona Kilikuwa Commited na Kiliorodheshwa na Karatasi zimo ambazo zinamichoro Michoro.. Kwa Hoja hiyo ya Malya Pia siyo ya Msingi, Katika Mazingira hayo Basi Mahakama hii Imeona Hoja yake haina Msingi.

Jaji: Mr Mallya ni Kama alitaka Ku' impeachment Kumbukumbu za Mahakama, na Mahakama inaona hoja aliyoleta haina Msingi.

Jaji: Kuhusiana na Kibali cha Kufanya Seizure of certificate Kwamba Baada ya Kukamata Vielelezo hivyo vitakiwa Kupelekwa Kwa Hakimu.. Kuhusiana na Kibali cha Kufanya Seizure of certificate Kwamba Baada ya Kukamata Vielelezo hivyo vilitakiwa Kupelekwa Kwa Hakimu.

Hoja za Kupinga Za Bwana Kidando PGO 226 (2)c Kwamba Afisa wa Upelelezi alikuwa anahusika na Kukamata na Kuhifadhi.

Kesi ya Mbowe Vs DPP ya 420/2018 Mahakama ya Rufani ilisema kwamba kutokutolewa Kwa Taarifa kwa Hakimu haizuii Ushahidi Kupokelewa.

Jaji: Kuhusiana na Kesi ya Mbowe Waliomba Mahakama Ione kuwa Kesi hiyo siyo relevant, Mahakama Ione kuwa Kutofuatwa kwa Utaratibu Wa Kuvalidate search.. Nakubalina na Utetezi Kuwa Search inatakiwa Kuwa Validated na Hakimu Kama ambavyo PGO 226 (2)c na Kifungu cha 38 (2) kwamba.

kama hukupata Kibali cha Search basi Unatakiwa Kupeleka Vielelezo Kwa Hakimu kwa ajili ya Ku validate.. Nakubakina kuwa Hakimu anatakiwa Kutoa Kibali cha Ku Validate Search Nakubalina na Utetezi Kuwa Kesi ya Mbowe ni Distinguishable.

Lakini Ikumbukwe Kuwa Kesi hiyo ilielekeza Kuwa ipo Kesi Nyingine, VUYO Vs DPP ya 334 ya 2016 Kutokana na Maamuzi hayo ya Mahakama ya Rufani kuwa siyo Automatic kuwa Kielelezo hicho Kisipokelewe Mahakamani Bali Kitaangaliwa Kielelezo Kupokelewa Kwake Kuna Muathiri Mshtakiwa.

Ndipo Inapoweza Kuoekana Kuwa Kutofuatwa Kwa Kifungu hicho Kumeathiri Mshtakiwa.. Katika Mazingira hayo Mahakama Inaona pia Pingamizi hilo halina Msingi.

Jaji: Katika Hoja Nyingine ya Vielelezo Ambavyo vinalengwa Kutolewa Mahakamani Vinatakiwa kuwa Labeled Kwa Kufuata Sheria na Mahakama Iliombwa Kungalia PGO 229 (10) Inaeleza namna ya Kuweka alama katika Nguo kama label ya Kielelezo.

Na label ya X/HD siyo Moja ya label ambayo inatajwa katika Sheria.. Kanuni zinasisitiza Kuwa Alama inayowekwa ni Kwa ajili ya Kutofautisha. Imeelezwa kuwa Kilicho fanyika siyo labeling Bali ni Kuharibu Kielelezo Kuwa Jambo hili limefanyika bila Kuwepo Kwa Mashahidi waliokwepo.

Kukiuka Masharti ya PGO hii ni Kukiuka Sheria hii.. Kwenye Hoja hii Wakili wa Serikali alisema Kuwa Vielelezo ambavyo vinalengwa Kutolewa hapa Mahakamani, zilikuwa Labeled na Kumsaidia Shahidi Kukumbuka Vielelezo Hivyo. Kwamba Vielelezo ambavyo Vinatolewa hapa Mahakamani labeling ilikuwa sahihi.. Na wakaomba kuwa Hoja hii haina Msingi na Mahakama Itupilie Mbali.

Jaji: Katika PGO hii Imelekeza Vielelezo Ambavyo ni Nguo Vinatakiwa Kuwa Lebeled, Mahakama imeelezwa Kuwa inatakiwa kuwekwa label kwa kamba ambayo itapita katika Vishikizo na Ining'inie.. Eneo la Ku label Limeelezwa Vizuri.

Exhibit ambayo inatakiwa Labeled inatakiwa Kuwa Paper Pin, PGO 229(8) Kuwa label hiyo inatakiwa Kuwa ni Minor number, na Vingine.. Kutokana na Malekezo hayo ya Kisheria yaliyoelezwa katika PGO Hiyo ni wazi Kuwa Alama iliyowekwa siyo alama ambayo PGO 229 Imeitambua na kuelekeza.

Hata Kama alama hiyo Ingekuwa imevumiliwa basi Kama Ingekuwa Alama hiyo iliwekwa Mbele ya Mashahidi hao basi ingevumilia. Katika Utaratibu huo Mahakama ina Maoni Kwamba alama hiyo iliyowekwa Imekiuka PGO 229 Kwa Maana hiyo inaathiri Afya ya Kielelezo hicho na Kuathiri Competence.

Jaji: Nakubaliana na Upande Wa Utetezi Kama ambavyo Wameieleza Mahakama Kuwa panapokuwa pamefanyika Upekuzi katika Nyumba, Box au Eneo Afisa ambaye amekamatwa Mali anatakiwa Kutoa Risiti Juu ya Mali alizokamata.

Jaji: Nanukuu Kifungu cha 38 (3) ya CPA, Kifungu Kingine Kinachohusika Kutolewa na Risiti ni Kifungu cha 35(3) ya Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322. Kifungu pia cha 22(3)d cha Sheria ya Uhujumu Uchumi inasema Pia Kuwa ni lazima. Kutoa Risiti.

Jaji anasoma kwa kiingereza

Lakini pia PGO ya 226 (2,5) na yenyewe inasema Kuhusiana na Utolewaji wa Risiti Na Mwisho Guidelines ya Mahakama Chapter 05.

Jaji: Hakuna Sehemu inayosema Kuwa pale Mahala ambapo Risiti haijatolewa basi Seizure Certificate Itumie Kama mbadala wa Risiti.. Kwa Upande wa Utetezi walikataa Mwaliko huo Kwa Kuomba Mahakama Ikatae Mwaliko huo Kwamba Risiti na Seizure Certificate ni Nyaraka Mbili tofautiParagraph ya 5 (f) inasema Kuwa inatakiwa Kutolewa Risiti Ya Mali zilizokuwa zinakamatwa.

Jaji: Katika Eneo hilo Mahakama Ina maoni kuwa suala la Risiti Mahakama imewekwa wazi na ni Muhimu itumike... Suala la Seizure Certificate Kutumika badala ya Risiti Kuna Maamuzi Ya Mahakama Ya Rufani ya ANDREA AGUSTINO na Wenzake Ikiwa imeamliwa huko Tanga katika Rufani ya Jinai.

Mahakama ilipo itwa Kuona Kuwa Risiti Itumike Mbadala wa Certificate of Seizure.. Basi ni wazi Kuwa a Mahakamani ya Rufani Ilisha ona kuwa Jambo hili ni Vitu Viwili tofauti na Mahakama Inaona Kuwa Kutokutolewa Kwa Risiti Ni Mambo Mawili tofauti.

Jaji: tumeona Kutokutolewa kwa Risiti Kuna athari, Mahakama ya Rufani Iliyoketi Iringa Quote with Approval katika Kesi ya PATRICK JEREMIAH Vs JAMHURI 34 / 2016 Kwa sababu hiyo Mahakama hii Inaona Kuwa Kushindwa Kutoa Kwa risiti ni Fatal na Jambo hili lina athiri Admissibility.

Jaji: Katika hali ya Kawaida Mahakama Ilitakiwa Kuishia Hapa, Lakini Kuna Mwaliko Wa Kibatala Kuwa Mahakama Izingatie Kuwa unatafuta NINI kila Inapokuwa Sheria Inakiukwa lakini Wanapewa nafasi Upande wa Mashtaka.

Nimeona Hakuna Cha Ku Reconcile Katika Maamuzi ambayo Nimeshayatoa, Maamuzi yote niliyo yatoa ni Maamuzi Halali hivyo Mahakama Inaona Hoja hiyo halikuwa na Mashiko na Naitupilia Mbali.

Jaji: Mahakama inaona Hoja zote zilizo letwa na Upande wa Utetezi Hazi kuwa na mashiko isipokuwa mapingamizi mawili ya labeling na kutokutoa Risiti.. Na kwa mapingamizi haya mahakama inaona yana Merit na sababu nilizo toa mahakamani Nakataaa vielelezo Hivyo NINATOA AMRI.

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Tuna shahidi Mmoja Namba 08 aliyekuwa anatoa Ushahidi Wake, Tupo tayari Kuendelea Wakili Peter Kibatala: Na sisi Pia tupo tayari Kuendelea Shahidi anapanda upyaaaa Kizimbani.

Wakili Peter Kibatala: OBJCECTION Shahidi anazungumzia Kielelezo ambacho Kimekataliwa punde tu Mahakamani, Naona wanaongoza Kwa mlango wa nyuma.

Wakili wa Serikali : Mheshimiwa Jaji Mimi sioni Kama Kuna Sheria inakataza Juu ya Swali hilo

Kibatala: Sija Object Swali Bali Majibu ya Shahidi, anazungumzia Kidaftari ambacho Kimeshakatazwa na Mahakama Jaji: Mimi sioni Kama Kuna tatizo na hilo kama anaongelea Jambo ambalo limekatazwa Mahakama Itaona Mbeleni..

Shahidi: Nimefuatilia Baadhi ya Maeneo ambayo yalikuwa yamechorwa na Taarifa za baadhi ya Maeneo Uhalifu ulikuwa umepangwa

Wakili wa Serikali: Lini na Wapi?

Shahidi: Tarehe 24 August 2020 Nilifika Eneo Moja ambalo lilikuwa Kwenye Mchoro.

Shahidi: Tarehe 25 August 2020 anakamatwa Mtuhumiwa Mwingine anayeitwa Justin Kaaya ambaye alikuja Kuachiwa Baaadae..

Wakili wa Serikali: Kwanini Justin Kaaya aliachiwa

Shahidi: Aliachiwa baada ya Ushahidi Kuonyesha hausiki na Tuhuma tuliokuwa tunampeleleza

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine Ulifanya?

Shahidi: Upelelezi Uliendelea katika Kutafuta Taarifa za Watuhumiwa Wengine tuliokuwa tunawatafuta Ambapo Tarehe 10 September 2020 Tulimkamata Mtuhumiwa Mwingine aliyekuwa anaitwa Khalid Ally Athuman ambaye na Yeye aliachiliwa baada ya Upelelezi Kufanyika..

Wakili wa Serikali: Kwanini Khalid Ally Athuman alikamatwa?

Shahidi: Alikamatwa kama Mtuhumiwa ambaye alikuwa analengwa Kushiriki Kwenye Kikundi, pia aliwahi Kuwa ni Mwanajeshi wa Kikosi cha 92 KJ alimakatwa hapa Dar es Salaam eneo la Kinondoni.

Wakili wa Serikali: Baada ya Ukamatwaji Khalid Ally Athuman Kitugani Kingine Ulifanya

Shahidi: Tarehe 19 September 2020 Tulimkamata Gabriel Muhina huko Tabora, aliwahi Kuwa Mwanejeshi wa JWTZ katika Kikosi Cha KJ 92

Wakili wa Serikali: Mlimkamata kwa Tuhuma gani?

Shahidi: Kwa tuhuma Za Kutaka Kwenda Kushiriki Vitendo Vya Kigaidi Vilivyokuwa Vinataka Kutendwa Hapa Nchini.

Wakili wa Serikali: Gabriel Muhina sasa hivi Yupo wapi?

Shahidi: Tulimuachia baada ya Upelelezi Kufanyika

Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo Nini Kilifuata

Shahidi: Kuna Mtuhumiwa Tulimkamata Tarehe 20 September 2020 Jijini Mwanza MALIMA BURONGO. Aliwahi Pia akiwa Mwanajeshi wa JWTZ Kikosi cha 92 KJ, Nikiwa Mwanza nilitembelea Maeneo Ya Mabatini, Mwanza na BOT kwa kufatisha Mchoro uliokuwa kwenye Kidaftari.. MALIMA BURONGO Tulimkamata Maeneo ya Pasiansi.

Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo Kitu gani kiliendelea

Shahidi: Tarehe 22 July 2021 Usiku aliletwa Mtuhumiwa Namba Nne ambaye ni Freeman Aikael Mbowe ili nimuhoji Baada ya Kuletwa Mbele yangu na Yeye Kunipatia Majina particular zake zote. Ndipo Nilimuonya kwa Makosa ya Kula Njama Kutenda Ugaidi, Chini ya Sheria Ya Kuzia Ugaidi..

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumuonya?

Shahidi: alipomaliza Kutaja Majina yake, Wakili wake Fredrick Kihwelo hakuwepo na hakuweza Kupatikana Wakili wake. Hivyo Mpaka Kesho Yake Tarehe 22 July 2021 hiyohiyo ndipo alipatikana Wakili wake, Siku fanikiwa Kumuhoji Mtuhumiwa, alisema Mpka atakapofika mahakamani ndipo atakapo toa Maelezo yake.

Wakili wa Serikali: Umekuwa Ukieleza kuhusiana na Khalfani Bwire, Hebu Onyesha Hapa Mahakamani Yupo sehemu gani?

Shahidi: Ni yule aliye Vaa Tshirt yenye Maandishi ya Njano.

Wakili wa Serikali: Wakati Unaandika Seizure Certificate Uliandika HALIFANI BWIRE elezea Jina hilo ulilipata wapi..

Shahidi: Ni Kutokana na matamshi aliyokuwa anataka Mwenyewe..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu Kwa sasa Katika Examination inchief.

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji tunapendekeza tupate mapumziko kwa dakika 45 Mpaka Saa 7 na nusu turudi..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi, Walikuwa wametushiriksha.

Jaji: basi tuna break Kwa muda wa dakika 45, tutarudi saa saba na nusu

Jaji anatoka
---

Jaji amerejea Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Kwa Mara Nyingine.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Kama awali, Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia Quorum yetu ipo Vilevile tupo tayari Kuendelea.

Wakili Nashon Nkungu: Shahidi Habari

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Maswali yangu nitataka majibu kwa Sauti

Shahidi: Ndiyo nitajibu

Wakili Nashon Nkungu: Kwamba Uki husika Kukamata Washitakiwa Wa Kwanza, Pili na Watatu

Shahidi: Sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Hata Mahita alieleza hivyo

Shahidi: Mie sijui Kama Mahita kasema hivyo

Wakili Nashon Nkungu: Na ulikuwa na Mahita

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Mahita anasema Mlifika Kituoni

Shahidi: Ndiyo Kituoni tulifika.

Wakili Nashon Nkungu: Mweleze Mheshimiwa Jaji Kama ni Muhimu kumuandikisha Mtuhumiwa Kwenye Detention Register Mtuhumiwa anapo fikishwa Kituo cha Polisi

Shahidi: Kufikishiwa na Kupokelewa ni Vitu Viwili tofauti.

Nkungu: Unaweza Kumfikisha Mtuhumiwa na asipokelewe?

Shahidi: Mtuhumiwa anapokelewa Kituo cha Polisi ndiyo anarekodiwa

Nkungu: Mweleze Mhe Jaji Kama ni Kitu chepesi Kwa Askari Kwa Vitu anavyofanya Kwa Kutumia Memory Yake

Shahidi: Ni Vyepesi Kwakuwa ni Moja ya Sifa ya Askari.

Wakili Nkungu: Unafahamu Kwamba PGO inasema Kinyume Kwamba Askari hategemewi Kutumia Kumbukumbu zake?

Shahidi: Mie sifahamu, ila nafahamu Sifa ya Askari ni Kumbukumbu

Wakili Nkungu: Kwa hiyo PGO inaposema Kuwa Askari asitegemee Memory yake inadanganya?

Shahidi: Haidanganyi

Wakili Nashon Nkungu: Mida ya Kukamata, Kusachi na Kuchukua Vielelezo Ni Mida sahihi au makadirio?

Shahidi: Mida Sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo Mida yote Mliyokuwa Mnaandika Ilikuwa ni Muda sahihi na Siyo Makadirio.

Shahidi: Ni Mida sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba 12 na 13.

Nashon Nkungu: Ulielezea kuwa Mlifika Rau Madukani Saa Saba Kamili Mchana, ni kweli?

Shahidi: Kimyaaaaaaaa!

Wakili Nashon Nkungu: Kwa kuwa hatukadirii tuambie ilikuwa Saa Saba na Dakika Ngapi?

Shahidi: Nilikuwa siangalii Muda Kuangalia Dakika Nakumbuka ni Saa Saba Mchana tu.

Wakili Nashon Nkungu: Sasa Ulisema Mlifika Saa Saba Mchana Rau Madukani Mkapaki gari

Shahidi: Ni Kweli

Wakili Nashon Nkungu: Na Ukasema Kingai akamtuma Mahita Kuangalia kama wale Watu Bado Wapo

Shahidi: Sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Kisha Mahita akarudi

Shahidi: Sahihi

Nashon Nkungu: Sasa Kwa Kukadiria Ulichukua Dakika ngapi

Shahidi: Hatufanyi Kazi kwa Kukadiria

Wakili Nashon Nkungu: Nikisema Ulichukua Muda wa Nusu Saa Nitakuwa Sahihi

Shahidi: Wewe Ndiyo Umesema ila Sisi hatufanyi Kazi Kwa Kukadiria au Kungalia Muda wa Kila Kitendo

Wakili Nashon Nkungu: Alipo rudi akasema Wale Watu wapo

Shahidi: Ni sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Nyinyi Sasa mkatelemka Mkaanza Kuji panga

Shahidi: Ni sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Kwa kukadiria Mazoezi yite haya Sita yalifanyika kwa Muda gani?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Kama hutaki Kujibu ni ruksa pia unaweza Kuiambia Mahakama Kwamba hutaki Kujibu..

Shahidi: Vyote Vili fanyika ndani ya Saa Moja

Wakili Nashon Nkungu: Baada ya Matukio yote Kufanyika, Sasa Mkawapekua wale Watuhumiwa, Ni sahihi?

Shahidi: Ndiyo tuliwapekua.

Wakili Nashon Nkungu: Hapa Nimeshika Vielelezo P11 na P12 nakuletea Karibu Uvione na Kuvitambua

Shahidi: Ndiyo nimevitambua

Wakili Nashon Nkungu: Mwambie Mheshimiwa Jaji hii imeandikwa P ngapi

Shahidi: imeandikwa P 12.

Wakili Nashon Nkungu: Na hii Imeandikwa Ngapi Ukitizama

Shahidi: Nimeona ni Exhibit P 11

Wakili Nashon Nkungu: Sehemu za Muda ambao Upekuzi Ulifanyika Unasomeka Saa ngapi?

Shahidi: Saa Saba Mchana

Nkungu: Hapo panasomeka hivyo?

Shahidi: Ni 13:00 Mchana

Nkungu: Sasa 00 ni saa Saba Kamili mchana?

Shahidi: Ndiyo

Nkungu: Sasa ni sahihi kwamba upekuzi (Search) ilianyika kabla hamjafika?

Shahidi: Sasa sisi tulifika Saa saba mchana

Wakili Nashon Nkungu: Sawa, Mimi nitaishia hapo.. Lakini anaendelea tena..

Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kuwa zaidi ya Mara Moja Mlienda na Watuhumiwa Moshi Police Central

Shahidi: Ni kweli.

Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kuwa Nyie Mlitembea na Watuhumiwa na Mkawarudisha Kituoni, ingepata Nguvu kama Ungetupa Detention Register Ya Moshi?

Shahidi: Nguvu ni huu Ushahidi Ninaotoa hapa

Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu Kuwa Detention Register Ni Muhimu Kama Mtu alifika Kituoni na Kutoka

Shahidi: Ni Muhimu Kuonyesha Kumbukumbu

Wakili Nashon Nkungu: Na Pia ni Ushahidi?

Shahidi: Kama Utaamua huo ndiyo Ushahidi.

Wakili Nashon Nkungu: kutokwepo kwa Nyaraka Hakuna Mtu Mwingine Kwa Hakika ataeleza Kuwa Watu hawa walifikishwa Moshi

Shahidi: Sasa Mimi si Nipo hapa Ndiyo Nina Uhakika..

Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo Nyaraka hizi ni Urembo

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Ushahidi Wa Nyaraka Muhimu zinazoelezwa na Sheria hujatoa hapa Mahakamani

Shahidi: Mimi sijaleta Nyaraka hiyo

Wakili Nashon Nkungu: Wakati Mpo Moshi Watuhumiwa Walikuwa Wanalala wapi?

Shahidi: Sijui Kama Walilala Maana yake walikaa Kituo cha Polisi.

Wakili Nashon Nkungu: Na baada ya Mambo yote Uliyo ya eleza Kule Moshi Uliaafiri kuja Dar es Salaam

Shahidi: Ni sahihi tulisafiri

Wakili Nashon Nkungu: kama Kweli Mlisafiri na Kama Kweli Mlisafiri Muda huo, Si tungeona kwenye Polisi Log book

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Nyinyi Safari Yenu Mlisafiri Kwa Gari ya Polisi?

Shahidi: Ndiyo Kwa Gari ya Polisi

Wakili Nashon Nkungu: Je Unafahamu Kuwa Kama Mnasafiri kwa Gari ya Polisi, kila Safari Kuna watu wanatoa Vibali Vya Nyinyi Kusafiri, Je Unafahamu?

Shahidi: Ndiyo Nafahamu.

Wakili Nashon Nkungu: Mweleze Mheshimiwa Jaji Kama ulisema Safari Yenu Ilikuwa authorized na nani

Shahidi: Sikusema

Nkungu: Unafahamu Kuwa Mnapo Anza Safari CRO officer anatakiwa Kurekodi Muda na Dhumuni la Safari kabla hamjaanza Safari

Shahidi: Nitegemea Safari Inaanzia Wapi

Wakili Nashon Nkungu: Inaweza Kuwa recorded au Siyo lazima?

Shahidi: Inategemea Siyo Lazima Wakili Nashon

Nkungu: Je Unafahamu Gari ya Polisi Inapoyoka Nje ya Mkoa inatakiwa Kupata Ruhusa ya IGP Shahidi Si Kweli

Wakili Nashon Nkungu: Je Unafahamu Kuwa Mnapo Pata hitilafu Gari hiyo inatakiwa Kuripotiqa Kwenye Kituo Cha Karibu

Shahidi: Si Kweli Wakili

Nashon Nkungu: Unaifahamu Police Form Fomu EMI?

Shahidi: Hapana sihifahamu

Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli Kwamba Gari zote za Polisi Zina Registration namba

Shahidi: Ndiyo Zina Registration Namba

Wakili Nashon Nkungu: Na Kweli Hapa Mahakamani Hukutoa Registration ya gari yoyote ya Polisi mliyotumia

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Unakumbuka Kuwa Tarehe 9 Mwezi August 2020 Mliwapeleka Watuhumiwa Mbweni?

Shahidi: Si Kweli Tarehe 09 August 2020 sikuwapeleka Watuhumiwa Mbweni

Wakili Nashon Nkungu: Lakini Unakumbuka Kuwa uliwapeleka Watuhumiwa Mbweni

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Sasa Unakumbuka Registration namba ya Gari Mliyotumia kuwapeleka Watuhumiwa Mbweni?

Shahidi: Sikumbuki

Wakili Nashon Nkungu: Lakini wewe Ukisema hapa Moja ya Sifa ya Polisi ni Kuwa na Kumbukumbu

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Sasa hapa Kuna Kauli Mbili Za Mashahidi, Ni sahihi Kwamba Mlikuwa kwenye gari ya Pamoja wewe na Mahita Mkitoka pale Rau Madukani

Shahidi: Ni sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Na Watuhumiwa?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Na Kwamba Mlikuwa Mkiwauliza Maswali Mbalimbali

Shahidi: Hapana Siyo Maswali Mbalimbali

Wakili Nkungu: Mahita anasema Kwenye Ushahidi Wake Kuwa aliwauliza Kuhusu Mwenzao wa tatu yupo wapi

Shahidi: Ndiyo hilo waliulizwa

Wakili Nkungu: Ni sahihi Kwamba Ulisema Wali Jibu kuwa hawajui Kuwa aliondokaje ondokaje Katika lile eneo?

Shahidi: Ni sahihi Wali Jibu hivyo.

Wakili Nkungu: Tuambie nani Muongo kati yako wewe na Mahita aliyesema Wali Jibu tumeamwacha pale Rau Madukani na wewe Waliokujibu kuwa hatujui..

Shahidi: Hakuna Muongo

Wakili Nkungu: Je, Shahidi Unafahamu Kuwa Watuhumiwa wanakataa kuwa Hakuna Sehemu yoyote mliyozunguka nao.

Shahidi: Mie Nimeeleza Ushahidi Wangu

Wakili Nashon Nkungu: Na Moja Sehemu Mliyo enda Aishi Hotel

Shahidi: Ndiyo tulifika

Wakili Nashon Nkungu: Mlijua Mnaenda Aishi Hotel

Shahidi: Ndiyo Kwa Kuongozwa na Watuhumiwa

Wakili Nashon Nkungu: unajua Kuwa Hotel ni Private Premises

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: unajua Kuwa Mlitakiwa kuwa na search Warrant.?

Shahidi: Sisi hatukuingia Ndani ya Hotel, Kiongozi Wetu alishuka akasogea Maeneo yale ila Hakuingia Ndani

Wakili Nashon Nkungu: Bado Upo Serious Unataka Mahakama Iamini Mlienda Aishi Hotel Kumtafuta Mtuhumiwa

Shahidi: Ni Jambo linalohitaji Utaalamu siyo Kama Unavyotaka wewe.

Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli Kwamba hamkuweza Kuandika Maelezo Kwa sababu Mlikuwa bado Mnamtafuta Moses Lijenje

Shahidi: Pamoja na Shauri Kufunguliwa Dar es Salaam, nilieleza.

Wakili Nashon Nkungu: Hiyo ndiyo Sababu Pekee iliyowafanya Mvunje Sheria?

Shahidi: Hatukuvunja Sheria

Wakili Nashon Nkungu: Mliwaandika Maelezo Ndani ya Masaa Manne

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Anita na Esther Maelezo Yao yaliandikwa Wapi

Shahidi: Yaliandikwa Moshi

Wakili Nashon Nkungu: pamoja na Kwamba Kesi ilifunguliwa Dar es Salaam

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Wakati Mnawaandika Maelezo Mlikuwa mnajua Mbowe na Yeye mtuhumiwa?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Na Mliwaandika Maelezo Bila MBOWE Kukamatwa?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo Kutokukamatwa Mbowe Freeman halikukwamisha suala la kuandika Maelezo Wengine?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli Mbowe Ulimuandika Saa 6 Na Dakika 51?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo inawezekana Kuandika Maelezo Usiku

Shahidi: Ndiyo Kutoka Na Upelelezi Ulikuwa bado haujakamilika

Wakili Nashon Nkungu: Ni wewe ndiyo Ulifanya Upekuzi wa Maungoni?

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Na Ulipofika Kiunoni ukahisi ni Kitu Kigumu

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Katika Bastola Kuna Maeneo Matatu ambayo Ndiyo Ukaguliwa fingerprints

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kuwa Finger inaweza Kuonyesha Possession Ya Bastola hiyo

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu Kwamba PGO inasema Kuwa possession ya Bastola inathibitishwa na Finger Prints

Shahidi: Ndiyo.

Wakili Nashon Nkungu: Je umeleta Hapa Mahakamani Ushahidi Wa Finger Prints Kuonyesha Possession Ya hiyo Bastola?

Shahidi: Hapana Siku leta Kwasababu halikuwa na Sababu

Wakili Nashon Nkungu: Ni sahihi Kwamba PGO inasema Silaha (Exhibit) kisiwe Loaded

Shahidi: Inategemea PGO

Wakili Nashon Nkungu: PGO ipi?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Je wewe ulimweleza Sebastian Madembwe Kwamba hatakiwi Kufanya hiki na hiki?

Shahidi: Mimi sijaongea Kuhusu Madembwe na Katika Ushahidi Wangu Sijataja Madembwe

Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu Kwamba Madawa yakikamatwa Yanatakiwa Kupelekwa Kituo cha Karibu yakabidhiwe kwa Officer incharge

Shahidi: Inategemea

Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu Kuwa Mtu (Mtuhumiwa) anapokiri anatakiwa afikishwe kwa Hakimu

Shahidi: Inategemea na Mtu Mwenyewe kama anahitaji

Wakili Nashon Nkungu: Je Unafahamu huo Ukiri wa Mtu wa Tatu unaongeza Nguvu ya Ushahidi.

Shahidi: Ndiyo ni Hitaji la Mtuhumiwa Mwenyewe siwezi Kulazimisha

Wakili Nashon Nkungu: Wakati Adamoo anaandika Ukiri kwa Kushiriki kwake Kuweka Magogo na Ugaidi Hukuona haja ya Kwenda Kwa Mlinzi wa Amani

Shahidi: Mimi si Kuandika Maelezo ya Adamoo

Wakili Nashon Nkungu: Unafahamu Inspector Mahita

Shahidi: ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Na ulisema Ulikuwa naye Mlipofika Kwa Bwire

Shahidi: Ndiyo

Wakili Nashon Nkungu: Ni kweli mlieleza kwenye Ushahidi wako Mlimkamata Bwire na Simu mbili za Techno na Nyingine

Shahidi: Ndiyo.

Wakili Nashon Nkungu: Je ulitoa hapa Mahakamani simu hizo

Shahidi: Hapana

Wakili Nashon Nkungu: Je ulisema zipo wapi simu hizo

Shahidi: Zipo Mahala Salama

Wakili Nashon Nkungu: Ulizihusisha na Mashitaka haya?

Shahidi: Sijasema labda Kuna Mtu Mwingine atakuja

Wakili Nashon Nkungu: nimesikia umehojiwa Kuhusu HALIFAN BWIRE, Je ulisema hapa Mahakamani kuwa Mtu huyu ndiyo Khalfani Bwire?

Shahidi: Sikuwa nimeeleza

Wakili Nashon Nkungu: Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

- Namuona anasimama wakili John Mallya

Mallya: unajua kuna mamlaka inayotoa leseni ya kufanya biashara ya mafuta?

Shahidi: Hapana sifahamu Mallya: inaitwa EWURA leo nitakufahamisha sasa

Mallya: unafahamu kuwa masoko yanasajiliwa?

Shahidi: Hapana sijui

Mallya: basi fahamu, masoko yanasajiliwa na Mamlaka za Serikali.

Mallya: shahidi unajua Kuwa wauzaji wa mafuta uliowataja wana leseni za biashara katika Halmashauri husika?

Shahidi: Sijui Kama wanapewa Leseni.

Mallya: Mimi sasa nakubishia kuwa katika yale Makutano Jirani na BOT Hakuna kituo cha Mafuta, Sasa ithibitishe mahakama kama Kweli Kuna kituo cha mafuta

Shahidi: Kwenye ushahidi wangu nimesema hakuna

Mallya: Wewe unasajili vituo vya mafuta?

Shahidi: Hapana.

Mallya: ulijaribu hata Kununua Mafuta Lita 5?

Shahidi: Hapana

Mallya: Vipi Kama ni Road Show tu?

Shahidi: Sijui sasa wewe

Mallya: umesema Kuwa Pale Arusha ulienda Kwenye Soko Je Ulimtaja hata Kiongozi wa soko?

Shahidi: Hapana

Mallya: ulitaja hata Sanduku la Posta la Soko?

Shahidi: Sijui

Mallya: Shahidi Ushawahi Kufanya Kazi Ofisi za DCI

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Muda gani?

Shahidi: Kwa Miaka 7 Ofisi ya Utawala wa Upelelezi

Mallya: Unakumbuka kesi yoyote ambayo Umeshawahi kupeleleza?

Shahidi: Ni nazo nyingi lakini siwezi Kutaja hapa

Mallya: Vipi Kuhusu Kesi ya Tito Magoti ambayo alikamatwa na ZCO na Baadae Kunyimwa dhamana na akatoka kwa Kulipa pesa Baadae, Ushiriki wako Ukoje?

Shahidi: Siwezi Kueleza hapa hilo

Mallya: Wakati Unatoa Ushahidi Wako Ulisema wewe ni Msukuma

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unafahamu Kuwa Boazi na Yeye ni Msukuma?

Shahidi: Mie sijui

Mallya: Unafahamu pia Kuwa Makonda ni Msukuma?

Shahidi: Mie sijui

Mallya: Vipi Ushiriki wako katika Kumkamata kabsjourno?

Shahidi: Si Kweli.

Mallya: na wala hukwepo Wakati ana +chukuliwa Maelezo?

Shahidi: Sijafanya! Sijafanya! Sijafanya!

Mallya: Mshtakiwa Namba 4 alikuwa na Msaidizi wake anaitwa Ben Saa Nane alikamatwa na Mamlaka za Serikali Ukiwa Ofisi ya DCI

Shahidi: Mie sijui lolote

Mallya: Lakini Ulisikia Kuwa Ben Saanane amepotea..?

Shahidi: Nilisikia Kwenye Vyombo Vya Habari

Mallya: Ukiwa Ofisi ya DCI Ulichukua Hatua gani Baada ya Ben SaaNane Kupotea ukiwa Ofisi ya DCI

Shahidi: Miye siyo Jukumu langu,DCI anajua Kazi yake

Mallya: Mbowe wakati anatekwa Mwanza Simu zake Walizipeleka Wapi

Shahidi: Mimi sijui Nilikutana naye Tarehe 22 July 2021.

Mallya: Nyumbani Kwake Walikamatwa Computer, Rooter na Nyaraka Zingine pamoja na Hizo Simu Mmepeleka wapi? Maana hapa Mahakamani Hakuna.

Shahidi: Wanajua waliovikamata miye sijui lolote

Mallya: Fomu ya Kukamatia Mali unajaza kitu chochote au Kilichoandaliwa Mle?

Shahidi: Kilichoandaliwa Mle

Mallya: zile Particular alizojaza ulijaza kabla ya Kumpekua au Baada ya Kumpekua

Shahidi: Alijaza Mwenyewe

Mallya: alijaza baada ya Kupiga Makofi Kidogo au Kwa hiari yake

Shahidi: Kwa hiari yake

Mallya: Wakati unampekua alijibu anakaa wapi?

Shahidi: Chalinze

Mallya: Ukaamini Anakaa Chalinze

Shahidi: Napokaa haikuwa Muhimu Mallya: Jina lake Muhimu?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Adress yake hukumuuliza? Shahidi: Sikumuuliza

Malya: Maelezo hayo ya Chalinze Ulitoa wapi

Shahidi: Hata Mwenzie alisema hivyo

Mallya: Mheshimiwa Jaji atasoma hapo Umeandika Adress ya wapi wala sikupi faida kukutajia..

Mallya: Mheshimiwa Jaji Naomba Kielelezo P 13

Mallya: Kwemye Maelezo haya Kuna sehemu wamesema Kuwa Walikutana Morogoro Kupanga Ugaidi?

Shahidi: Ndiyo Walikutana Kupanga Ugaidi

Mallya: Sawa, Chukua Maelezo haya Nionyeshe Sehemu palipoandikwa Walikaa Kikao cha Kupanga Ugaidi

Shahidi: anapekua Maelezo, anapekua..

Shahidi: anasoma sasa "hiki kikao walichokutana ndiyo ugaidi wenyewe sasa" Mahakama inaangua kicheko kikubwa sana.

Mallya: haya na vilevile Hawa washtakiwa Wa nashitakiwa Kufanya Vikao Vya ugaidi Dar es Salaam, haya nionyeshe na Dar es Salaam walikaa wapi Kupanga ugaidi

Shahidi: anasoma na Mahakama Inacheka tena kwa sauti sana.

Mallya: Kuna Sheria yoyote inakata Kiongozi Kuwa na Mlinzi?

Shahidi: Hapana, sifahamu..

Mallya: Kuna Sheria Yoyote inakataza Kuwa Mlinzi Ambaye ni Mwanajeshi Mstaafu au aliyeacha kazi

Shahidi: Hapana

Mallya: Ukiwa Ofisi ya DCI Mwezi 9, 2017 Kiongozi Mwenzake alishambuliwa na risasi

Shahidi: Kuhusu kumshambulia Nina Taarifa ila kuhusu report sifahamu Mallya na watu waliomshambulia Tundu Lissu wana mafunzo ya kutumia hizo silaha?

Shahidi: hata Wahalifu wanajua kutumia

Shahidi: Hapana, Ni uhalifu tu unatokea

Mallya: Wakati Mbowe anahutubia Arusha paliwahi Kulipuka Bomu katika Mkutano wake, Ushawahi Kusikia Tukio hilo.?

Shahidi: Hapana sikumbuki

Mallya: Shahidi nitafutie kwenye Kielelezo P 13 sehemu ambayo Ling'wenya alikiri Kufanya Ugaidi kwenye Mikoa ya Mwanza na Mbeya.

- Shahidi anapekua,

Shahidi: Kuna sehemu anaposema Nchi Nzima, Mikoa Unayosema ipo Kwenye Nchi Nzima

Mallya: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji aandike Sehemu inaposomeka Kwamba watafanya Maandamano Nchi Nzima Ndiyo Kupanga Ugaidi Mwanza na Mbeya

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwenye Hati ya Kukamatia Bastola Sehemu zote Umejaza Adamoo ila hapa Umejaza Adamo Je Ulisha wahi Kueleza Utofauti huu?

Shahidi: Hapana Sijaelezea

Mallya: Mheshimiwa Jaji yangu ni Hayo tu

Matata: Kama Aliitwa Kwa VIP Protection, alitumiwa Nauli na Pesa ya Matumizi Njiani?

Shahidi: Kama zina malengo Mazuri Siyo Kosa

Matata: Soma hapo

Shahidi: "Baada ya hapo Mheshimiwa Mbowe alisema Kuwa atarudi Dar es Salaam, Ambapo Kuna Kazi Kubwa ya Kuweka Magogo".

Matata: Kuna sehemu amekiri Kuwa ataweka Magogo Mkoa fulani au Barabara fulani?

Shahidi: Hakuna sehemu iliyoandikwa

Matata: Kuna sehemu Specific ambapo wamesema Kwamba Kuna Maandamano Yatafanyika Mkoa fulani na Mkoa fulani?

Shahidi: Hakuna specific ilipotajwa Mkoa

Matata: Kwa Uelewa Wako Kufanya Maandamano ni Kosa Kisheria au siyo Kosa

Shahidi: Inategemea Maandamano yamefanyikaje

Matata: Nilisikia Unasema Mtu akikiri ni Hitajio lake Kama atahitaji kwenda Kwa Mlinzi wa Amani

Shahidi: Ndiyo Mpaka yeye atakapo hitaji.

Matata: Kwa Kifungu Kipi Cha Sheria

Shahidi: Sikumbuki

Matata: Kwa Sheria Ipi

Shahidi: Sikumbuki Sheria ipi ila Kwa uzoefu wangu

Matata: ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.

Kibatala: nafahamu wewe ni Shahidi Mzoefu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unafahamu kuwa Wanao fuatilia Kesi hii Wanafuatilia Wajibu wa Utendaji Kazi wa Jeshi la Polisi

Shahidi: Miye natimiza Majukumu Yangu kama Shahidi, Suala la Watu wanasema nini huko, siyo Kazi yangu.

Kibatala: Unafahamu Unatakiwa Kuwa na Adabu Unapokuwa Kwenye Kizimba Cha Mahakama na Mchakato huu?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: na Unafahamu Kuwa Unapoambiwa Uje Mahakamani Siku fulani lazima uje?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Uliambiwa Kwamba Mheshimiwa Jaji Alitoa Amri katika Mahakama ya Wazi Kuwa 14 December 2021 alisema Ukija Tarehe 15 December 2021 kuwa Uje na Uthibitisho

Shahidi: Niliambiwa lakini nilikuwa Njiani

Kibatala: haya Iambie Mahakama Ulifanya hivyo Ulipokuwa Mahakamani Kutoa Uthibitisho Kuwa Ulikuwa unaumwa

Shahidi: sikufanya

Kibatala: Kuna Siku yoyote ile Ambayo ulinyoosha Mkono Kumwambia Mheshimiwa Jaji nafahamu Kuna Amri yako?

Shahidi: Sikunyoosha Mkono

Kibatala: Kwa hiyo tukuchukuliaje sasa, Kwamba Umeizoea sana Mahakama?

Shahidi: Si Kweli Kwamba Nimeizoea Mahakama.

Kibatala: haya Iambie Mahakama Ulifanya hivyo Ulipokuwa Mahakamani Kutoa Uthibitisho Kuwa Ulikuwa unaumwa

Shahidi: sikufanya

Kibatala: tulikuwa na likizo ya Mahakama ya wiki 2 Je Ulishawahi Kuandika Barua Kupitia Mawakili wako kuwa Unasababu fulani?

Shahidi: sikufanya

Kibatala : Umefanya kazi kwa Miaka Mingapi huko Polisi

Shahidi: Miaka 20.

Kibatala: Tukupime kwa Uzoefu wako.?

Shahidi: Mie Mwanadamu, huwezi Kunipima Kwa Kukosea Jambo Moja.

Kibatala: Wakati wa Upelelezi Ulikuwa ASP sasa hivi Umepanda Cheo, Je Ulipanda Cheo Lini?

Shahidi: Mwaka Jana Mwezi Sita

Kibatala: Ni sahihi umepandishwa Cheo baada ya Kufanya hizi Shughuli ambazo ziliwapelekea hawa Kupelekwa Mahakamani?

Shahidi: Ni kweli Matokeo yalikuwa yameshatokea

Kibatala: Kingai alikuwa nani Wakati huo wa 2020

Shahidi: Alikuwa ACP Kibatala: na Sasa ni nani

Shahidi: Ni ACP

Kibatala: Kwenye Mkoa alikuwa ni nani

Shahidi: Mpelelezi Wa Mkoa

Kibatala: sasa hivi ni nani

Shahidi: Ni Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa

Kibatala: Nilisikia Mlikuwa Mnafanya kazi na Mahita

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mahita alikuwa nani

Shahidi: Alikuwa Assistant Inspector

Kibatala: Sasa hivi anacheo gani

Shahidi: Inspector

Kibatala: amepanda Cheo au ameshuka cheo

Shahidi: Amepanda Cheo

Kibatala: na Goodluck na Yeye alikuwa nani Shahidi: alikuwa Constable

Kibatala: na Yeye ni nani Sasa hivi

Shahidi: Yupo Kozi anasoma

Kibatala: Nilisikia Kuna Askari Ulisema aaliwekwa Ku Intercept ile Daladala, Je una taarifa za Huyo Traffic?

Shahidi: Sina

Kibatala: Je kazi aliyoifanya ilikuwa ya Msingi au Haikuwa Msingi

Shahidi: alifanya Shughuli ya Muhimu.

Kibatala: Kwa Ushahidi Wako wewe Ukisema kwamba Bwire alipofanyiwa search alikutwa na Simu Mbili za Techno na Bundi?

Shahidi: Ndiyo nilizungumzia ila nikasema Kuhusu Disposal Yake Watakuwa kuzungumzia wengine

Kibatala: Wakati Manazichukua Palikuwa na Shahidi Huru Mwingine?

Shahidi: Hapakuwa na Shahidi Huru yoyote

Kibatala: PGO inaelekeza Nini Kuhusu Kuchukuliwa Mali ya Mshtakiwa?

Shahidi: Inasema Kuwa lazima Pawe na Mashahidi huru

Kibatala: Ila kwa Jambo hili hamkuona Umuhimu wa Shahidi Huru?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Ulimwambia Jaji kwanini Hapakua na Shahidi Huru.?

Shahidi: Sikusema, Mimi sikushughulika na Hizo simu

Kibatala: Nilisikia ulihusika Kukamatwa na Mhina na Khalid, kwa ufahamu wako Walikaa Ndani Wakiwa wamebebeshwa Kesi ya Ugaidi Mpaka Nyie Mlipoamua Muwaachie huru?

Shahidi:
Mwaka Mmoja

Kibatala: Baada ya Upelelezi Kukamilika ndiyo Mkagundua kuwa hawakuwa na Kosa

Shahidi: taratibu zinataka Wakae Ndani Mpaka Upelelezi Unapokamilika.

Kibatala: Jeshi La Polisi limepanga kuwafidia?

Shahidi: Miye siwezi Kuingolea hilo.

Kibatala: Ushawahi Kufuatilia Juu ya Afya Zao hasa Muhina ambaye amepata stress Disorder ambayo Mlimsababishia nyie Ukiongozwa na wewe

Shahidi: Walikuwa ni Wahalifu

Kibatala: Kama Wahalifu Kwanini Mliwaachia

Shahidi: Kwa sababu hapo kuwa na Ushahidi Wa Kutosha.

Kibatala: Sasa Watu ambao Umekosa Ushahidi unawaita Wahalifu?

Shahidi:
Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Kwanini Mahakama Isione Kwamba wewe ni Shahidi ambaye una maslahi Kama Unawaita Watu ambao hawajakuwa Convicted kuwa ni Wahalifu tena amewaaachia Mwenyewe

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Nilisikia Unasema Kuwa Mpango wa Kulipua Vituo Vya Mafuta na Kupanga Magogo Barabarani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Ulisema Lolote hapa Mahakamani Kwamba Ulitoa Taarifa Kwa Ubalozi wa Uingereza Waweze Kuwakinga Watu wao

Shahidi: Si Kufanya

Kibatala: ulitoa Taarifa kwa Ubalozi wa Marekani

Shahidi: Si Kutoa Taarifa popote

Kibatala: Ubalozi Wa Kenya

Shahidi: Si Kutoa Taarifa

Kibatala: zoezi la Wakili wa Serikali Kuchukua Hati ya Mashtaka, Kuhusu Kuandika HALIFANI Je Uliongozwa Kuhusu Kulihanisha Majina

Shahidi: Sikuongozwa Kulinganisha majina.

Kibatala:
Wakati Ling'wenya anatoka Mtwara akasimama Chalinze na Kumchukua Mshtakiwa Wa Pili Kwenda Morogoro kwenda Kwa Urio Je walikuwa tayari Wana Nia Ovu au hawajui

Shahidi: Miye siwezi Kufahamu Kama Walikuwa wana Nia Ovu

Kibatala: Wakati wa Atoka Morogoro Kwenda Moshi walikuwa wa nafahamu kuwa wanaenda Kufanya Matendo ya Ugaidi Moshi

Shahidi:
Walikuwa wanafahamu K

Kibatala: Nani aliyewa Recruit kati ya Mheshimiwa Mbowe au Urio?

Shahidi: aliyewafadhili.

Kibatala: Nani aliye watongoza Ling'wenya na Adam pale Morogoro Kwenda Kufanya Ugaidi, Ni Urio au Mbowe

Shahidi: Ni Urio Kibatala: Urio ana Umri gani

Shahidi: Ni Mtu Mzima.

Kibatala: akitoka Mtu Mwanza akaniomba nimtafutie Watu wa Kumuua Mtu MWZ Je, Mimi niliyewatafuta watu Kwa ajili ya Kwenda Kuua nitakuwa Nina tenda Kosa la Jinai au siyo?

Shahidi: Inategemea Kibatala: Basi Kama nilivyokueleza Mwanzo Watu wanapima weredi wako na Jeshi la Polisi.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Bado nina Maswali Mengi, Naomba tuhairishe hadi Kesho

Jaji anaandika Kidogo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hatuna Pingamizi na Ombi lililo Wasilisha na Wakili Msomi Kibatala Kwa sababu Ule Muda tuliokubaliana umeshafika.

Jaji: Kufuatia Maombi yaliyoletwa na utetezi na Kukubaliwa na upande wa mashtaka nahairisha shauri hili hadi kesho saa 3 Asubuhi.

Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka kesho Asubuhi. Shahidi namba 08 ataendelea kuwa kizimbani hapo kesho.
 
... shukrani makamanda kwa taarifa hii muhimu ya kufungulia mwaka! Tunasubiri maneno mawili, NATOA AMRI, kuona ni amri gani itatolewa na mahakama! Hii kesi so far imevunja rekodi kwa kutolewa amri nyingi ndani ya vipindi vifupi vifupi!
 
Uzi umedoda,,

Nyumbu wako ccm wanamuunga mkono mama ili kumkomoa Ndugai na marehemu!

Je, mabeberu nao wamemsusa Mwamba? Maana siwaoni hapo.
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 10/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

View attachment 2075719
Picha: Baadhi ya watu waliohudhuria mahakamani

Updates
Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 kamili

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha jopo la mawakili
  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naitwa Peter Kibatala, Naomba Kuwatambulisha:
  • Nashon Nkungu
  • John Mallya
  • Dickson Matata
  • Seleman Matauka
  • Sisty Aloyce
  • Faraji Mangula
  • Michael Mwangasa
  • Gaston Garubindi
  • Maria Mushi
Jaji anaita washtakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya uamuzi Mdogo, Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: nasi pia tupo tayari Kupokea Uamuzi na Kuendelea Jaji anaandika kidogo.

Mahakama ipo kimya!

Jaji anaendelea sasa.

Jaji: Ni kweli Shauri hili Lina kuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo. Kama ambavyo Mahakama Ilihairisha Mwaka Jana, Uamuzi huu Unatokana na Kupigwa kwa Kupokelewa Vielelezo ambavyo Vilikuwa vimetolewa na ASP Jumanne.

Na Kwamba aliomba Kutoa Vielelezo baada ya Kufanya Upekuzi na Kwamba Upekuzi huo Ulifanyika Mbele ya Mwenye Nyumba Mariam Juma na Mjumbe wa Nyumba kumi pamoja na Mke wa Mshtakiwa Na Kwamba alijaza Certificate of Seizure Kwa Mlolongo wa Mali ambazo alizo kamata kama ambavyo nimeziorodhesha, Na Kwamba Baada ya Kufanya Upekuzi huo alizo weka alama X/ HD Na baadaa akamkabidhi Mtunza Vielelezo Kituo cha Polisi Kati Na Kwamba alivichukua na Kwenda Kutunza Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam Tarehe 17 December 2021.

Jaji: Notebook Nyekundu hakutoa Hapa Mahakamani, na Kwamba Baada ya yeye Kupitia na Kugundua haina Uhusiano na Kesi hii alicha Kuitoa hapa Mahakamani.. Na alikuwa anavitaja Vielelezo Kwa Kutumia Alama ya X/HD.

Alipokuwa anavitoa hapa Mahakamani alipingwa na Mawakili wa Utetezi, Wote Walipinga Vielelezo Vyote vilivyokiwa vinaombwa Kutolewa hapa Mahakamani.. Hata hivyo Kila Wakili akisimama na Kutoa Hoja zake.. Kwa Maana hiyo Mahakama haitaenda kwa Kila Wakili Bali kwa Hoja Moja moja.

Jaji: Chain of Custody, Competence ya Vielelezo Vyenyewe na Shahidi aliyekuwa anaomba Kutoa Mahakamani.. Si Jambo Jipya hapa Mahakamani.. Mahakama hii kwa kutumia Experience ya huko Nyuma. Sheria Inaelezea Kwamba Upokelewaji wa Vielelezo Mahakamani Kupitia Sheria Kesi ya SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER, CHARLES GAZILABO AND THE OTHER THREE.

Katika Mashauri yote Mawili Mahakama imeeleza Kwamba Vielelezo Inaweza Kupokelewa Baada ya Vitu Vitatu.. Kutumia Criteria ya Competence, Mahakama ilieleza Kuwa test ipo katika Mambo Matatu yanaitwa Authentication. Lazima atambue Unique features, Unique features ya Kielelezo hicho, Atambue Chain of Custody.. Kwa Maana hiyo Mapingamizi yaliyoletwa yameltwa kwa Jambo Moja la Competence.

Jaji; Mhakama Ita adopt namna ambavyo Mapingamizi yameletwa kwa Chain of Custody na Competence. Issue ya Chain of Custody imeelezwa na Mawakili Wote wa Utetezi. Nitaamua kwa Kufuata Ishu kama ambavyo zime letwa na Mawakili Wa Utetezi.

Maelezo Ya Jumla yanaeleza Chain of Custody ni nini.? Na Wakili Nashon Nkungu Alieleza nini Maana ya Chain of Custody.. Mahakama inakubaliana Kwamba ni namna ambavyo Kielelezo kilikamatwa na Kikitunzwa wapi Kama ambavyo Kilikuwa Mahakamani.

Kielelezo Ambacho Kilikuwa kimelengwa Kuletwa hapa Mahakamani Kilichezewa na Kwamba hii inaonyesha kwamba Vielelezo Vilikuwa Pamoja ndiyo Maana Notebook Nyekundu Imetolewa.

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi walikuja na Hoja Kadhaa Kwa Mujibu wa Sheria Vielelezo ambavyo vimekamatwa Kwamba Vielelezo ambavyo Vimekuwa Commited Vinatakiwa Kuja Vyote Mahakama Kuu.

Kwa Sheria Ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 inataka Afisa wa Polisi ambaye anataka Kutoa Kielelezo Mahakamani anatakiwa arudishe kwa mtu aliyepata Kwake Kama hajarudisha inaonyesha Kielelezo hicho Kimechezewa.

Inaonyesha kuwa shahidi Namba nane hakutoa Hoja zake kwanini Kielelezo Hicho Hakikuletwa Mahakamani.. Waliendelea Kujikimbusha Mahakama Kwamba PGO 229 Afisa wa Polisi anatakiwa Kushika Kielelezo Hicho Mpaka atakapo Kitoa Mahakamani. Na Kwamba Wakati anakamatwa aliamini kina husika ndiyo Maana alikikamata, Hivyo si Sawa kutokutoa hapa Mahakamani.

Jaji: Wakili Malya alisema Kwamba haieleweki Huenda Kwamba Kielelezo hicho Kilikuwa kinamnufaisha Mshitakiwa namba Moja.. Kwa Hoja wakasema Kwamba Wanaomba Mahakama Ione kwamba Kielelezo Kimechezewa.

Kwa sababu Vielelezo hivi Vingine vilikamatwa na Note Booka Nyekundu basi Mahakama Ione kuwa Vielelezo Hivyo Vimechezewa.. Kwa Upande wa Mawakili Wa Mashtaka Walisema Kwamba Mawakili Wa Utetezi Wametafsiri Vibaya. Kwamba Upande wa Mashtaka hawalazimishwi Kutoa Vielelezo Vyote Mbele ya Mahakama..

Shahidi aliona Kwamba Kielelezo hicho hakihusiki hapa Mahakamani.. Kwa Maelezo hayo waliendelea Kusema Kusema Kielelezo Kipokelewe Mahakamani Kama ambavyo Vilikamatwa Sasa Hapa Mahakamani, Mahakama ni kweli Inaona kwamba Kielelezo Hicho hakikutolewa Hapa Mahakamani Kutokana na Shahidi Namba 08 alisema Kwamba hakutoa Kielelezo hicho hapa Mahakamani Kwa sababu aliona Kwamba haihusiani na Kesi hapa Mahakamani.

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi wana maoni kuwa Vielelezo Vyote ambavyo Vimekuwa Commited Vinatakiwa Kuja Mbele ya Mahakama Kuu na Kama siyo basi Mchakato wa Kurudisha Kielelezo Hicho Ulipaswa uwe Umefuatwa Kwa Namna hiyo Waliomba Mahakama Ikatae Vielelezo Vyote.

Ukisoma pande zote Mbili ni wazi Kuwa Kielelezo Hiki Kwa Kutolewa Kwake Kimekiuka Sheria Ukizingatia Kuwa Kilikuwa tayari imekuwa Commited.

Jaji: Kifungu cha 246 CPA na Kanuni ya 8 ya Mwaka 2016 inasema Kuwa Vielelezo Vyote ambavyo Vimekuwa Commited kutoka Kwenye a Mahakama ya Hakimu Mkazi ni Vile ambavyo Mkurugenzi wa Mashtaka atataka kuvitumia Hakuna Sheria inayosema Kwamba Kila Kielelezo ambacho Kimekuwa Commited Kinatakiwa lazima Kiletwa Mahakamani.. Ni wazi atakuwa amepitia Kielelezo hicho Kuona Kama kinatengeneza Kesi au hakitengenezi kesi.

Siyo lazima Kwa Ushahidi au Shahidi Ambao amekuwa Commited Anatakiwa lazima aje Kutoa Ushahidi Mahakamani.. Katika Mazingira hayo basi Mahakama Inaona kwamba Pingamizi hili limekosewa Mahakama Inaona Pingamizi hili halina Msingi na Kutupilia Mbali.

Jaji: Kuhusiana na Chain of Custody imeelezwa Kwamba Kielelezo Kutoka sehemu Moja kwenda sehemu Nyingine Mahakama lazima itazame sana Endapo Mnyororo Wa Kielelezo Kutoka Sehemu Moja kwenda Sehemu Nyingine Inapokuwa Umevunjika Basi Upande wa Mashtaka Wanakuwa Wamekuwa wameshindwa.

Hakuna Maelezo Yaliyotolewa na Shahidi Namba 08 Kwamba aliwezake Kutoa Kielelezo Hicho kutoka kwa sergeant Johnson.. PGO 229 2(c) PGO Hiyo inasema Kwamba Funguo ya Chumba Cha Vielelezo Inatakiwa itajwe ni nani alikuwa anatunza Kwa Kushindwa Kueleza Hilo wanaona Kwamba Chain of Custody imevunjika.

Jaji: Bwana Kidando Nayeye alitoa Maelezo yake Kwamba Pingamizi hili limekosa Substance Kwamba PGO ya 229 4(a) inavyotakiwa Kidando alieleza Namna ambavyo Shahidi namba 08 aliviepeleka Kwa Sarjent Johnson na Kwenda Kuchukua Tarehe 17 December 2021.

Na Kwamba Shahidi ajahojiwa Kuona ambavyo Ushahidi Wake Unavyotetereka, Akaendelea Kusema Kwa Kina Kuwa Shahidi alieleza kwa Kina namna ambavyo alitunza Kielelezo hicho hapa Mahakamani. Akaomba Mahakama Itumie Sheria Kesi ya IGNATUS MKOKA, Kesi namba 245 ya Mwaka 2013, Pia akaomba Mahakama Itumie sheria Kesi ya KENNEDY SHAYO 84 ya 2017 Ukurasa Wa 31 na 34.

Na Akaendelea Kusema Kwamba Shahidi anaeleza Mahakama Vile Vielelezo ambayo alivi kamata na kuvitunza kwa sergeant Johnson.

Jaji: Upande Wa Utetezi Walisema Kwamba Utunzaji wa Vielelezo Katika Sheria Imetungwa kulinda Vielelezo Visichezewe.. Na Kwamba Sheria inasema Kwamba Polisi anatakiwa kuwa Na Notebook namna ambavyo alikuwa anaviorodhesha.

Na Kwamba Shahidi Hakuonyesha Paper Trade na Vithibitisho Vya paper havikuonyesha kama ambavyo inatakiwa.. Wakaomba kutumia Kesi ya ILUMINATUS MKOKA, Pamoja na Kesi ya MAYALA MBITI 177 ya 2015 Ukurasa wa 6.

Jaji: Kuhusiana na Kesi ya KENNEDY SHAYO wakaomba Kwamba Kesi hiyo I aunga Mkono Hoja za Utetezi, Kwa sababu Bunge liliona kuwa Kielelezo ambacho ni Nguo kuna dalili za kuchezewa. Na Kwamba Mnyororo huo unakuwa Umevunjika.

Na Kuhusiana Kupokelewe kwa Vielelezo hivyo kuwa Vitaathiri Washtakiwa au lah.. Walisema Kuwa Bunge linapotunga Sheria na Sheria hiyo Inapokuwa haifuatwi basi Washtakiwa Wanakuwa wameathirika.

Kwenye suala hili ni seme ni kweli Kwamba suala la Upokelewaji wa Vielelezo Limeelezwa..Na suala Zima La Upokelewaji wa Vielelezo Inategemea Ambavyo Vielelezo vimetunzwa Na Chronological paper Trade inaonyesha namna ambavyo Kielelezo Kilikuwa kimekamatwa Mpaka Kutunzwa.

Jaji: suala Zima La Upokelewaji wa Vielelezo Na Chain of Custody Limeelezwa na Sheria Kwa Kifungu cha 38 cha CPA, Sura ya 322, Sheria Ya Polisi na Polisi Wasaidizi, PGO ya 229 Suala la Kufuatwa kwa Mnyororo Wa Kielelezo Kuna Vipingili Vingi.

Unapokuwa Unaangalia Kipengele Kimoja kikiwa Kimekatika Kimoja basi Mnyororo huo Unakuwa Umekatika.. Katika Kushughulika na Vielelezo Hivyo kuwa Vipo namba ambavyo Vinakatwa Mpaka Vinafika Mahakamani. Siyo Sahihi Shahidi Mmoja tu anapotoka Ushahidi Kueleza Kwa niaba ya wengine Kuhusiana na Mnyororo Kuvunjia au kutovunjika.

Jaji: Kwenye kesi ya CHARLES GAZILABO Mahakama Ilitoa Uamuzi Kwamba Mahakama ya Rufani inaamini uthibishwaji wa Utunzaji wa Mnyororo Hauwezi Kuthibitishwa na Shahidi Mmoja, Kwamba Mahakama Itaweza Kuona baada ya Ushahidi Wote Kutolewa.

Katika Kesi ya CHRISTINA Vs JAMHURI Ukurasa Wa 5 na 7 Kufuatia Mfano huu Mahakama Ya Rufani inasisitiza Kuwa Kama Hakuna Ushahidi Wa Moja Kwa Moja Kwamba Mnyororo Ulichezewa. Na Kwamba Kama Upande Wa Jamhuri hawatoleta Mashahidi Wengine Kuthibitisha Mnyororo huo basi Mahakama Inaweza Kusema Mnyororo huo haujathibitishwa.

Jaji: Kwenye kesi ya ABASI KONDO Vs JAMHURI Kesi 472 ya 2017.. Pia Mahakama Ya Rufani Imetoa Malekezo Kwemye kesi ya ANANIA Vs JAMHURI Mahakama Iliyoketi Dar es Salaam.. Hizo authorities nilizosema hapo Juu ni Authorities ambazo zimetolewa na Mahakama Ya Rufani.

Kwa Maana hiyo Mahakama Ya Chini inapotoa Maamuzi lazima Izingatie Maamuzi hayo ya Juu.. Katika Mazingira hayo basi Kwa Kutizama Shahidi ambaye amekuja Kutoa Ushahidi Hapa Mahakamani Kwamba Vielelezo ambavyo alivikamata hakubaki navyo Bali alimkabidhi sergeant Johnson.

Jaji: Kwakuwa Bado Upande wa Jamhuri hawajashindwa Kumuita sergeant Johnson, bado hajaitwa Mahakamani Kutoa Ushahidi hatuwezi Kusema Kuwa Shahidi aliyepo Mahakamani ameshindwa Kutoa Mnyororo Wa Ushahidi.

Jaji: Kuhusiana na Mwaliko niliopata kutumia Kesi ya MKOKA NA MAYALA MBITI nakubalina na Upande wa Utetezi kuwa Kanuni zilizotumika katika Mashauri hayo ni mazuri lakini Ikumbukwe Maamuzi hayo Yalifanyika baada ya Ushahidi Huo Kutolewa. Naona Hoja za Utetezi Zimeletwa Kabla ya Wakati labda kama ingeletwa wakati wa Final Submission. Kwa sababu hiyo Mahakama haiwezi Kuzingatia na Kwa sababu hiyo Pingamizi hili nalitupilia Mbali.

Jaji: Ikumbukwe Pia Shahidi aliyopo Mahakamani, yeye ndiye aliye fanya Search na alizikamata.. Hoja za Kwamba Shahidi amethibitisha Kwamba Mali ambazo zinatolewa Mahakamani ni Mali ya JWTZ wakati Hakuna Mahala aliyothibitisha Kuwa Vielelezo hivyo ni Mali ya JWTZ na pia hakuna.

Mahali ambapo JWTZ walikuja Kuthibitisha Kuwa ni Mali yao Aliendelea Kusema Wakili JOHN Mallya Kuwa Shahidi alishindwa Kutaja Vizuri Hapa Mahakamani, Ikumbukwe ni Vifaa Vya Kijeshi na Vina Majina yake ya Kijeshi.

Akatoa Mfano Kuwa Shahidi amesema Kuwa Kielelezo ni PONJOL wakati ni Sleeping Bag.. Akaendelea Kuomba Mahakama Kwamba Shahidi ameshindwa Kuvitambua Vielelezo Hivyo Na Kwamba Vielelezo Ambavyo Vilitolewa Hakuna sleeping Bag na akaomba Kwa kusema shahidi hana Knowledge ya kutosha.

Jaji: Shahidi alisema Vielelezo ni Mali ya JWTZ na JKT wakati Shahidi hajawahi Kufanya Kazi JKT wala JWTZ.. Kwa Sababu Vielelezo hivyo ni Vya Jeshi na Shahidi hana Knowledge Basi Mahakama Isipokee Vielelezo hivyo Kwa sababu Shahidi Siyo Competent.

Kwa upande wa Mashtaka walikuja Kusema Kwamba likuwa Kutoa Ushahidi Wa Kile ambacho alikikamata, Na Kwamba Kwa Hatua ya sasa siyo Sawa Kutoa Ushahidi Wa Kitaalamu.. Na Kwamba aliendelea Kusema Kwamba A shahidi alivitambua kwa Alama alizo weka yeye Mwenyewe ambayo ni X /HD.

Shahidi alieleza Kwa Kina Kuwa aliweka alama hiyo baada ya Kuvikamata, Aliomba Mahakama Ione kwamba Shahidi huyo ameweza Kutambua Vielelezo hivyo.. Kwa sasa Mahakama Inatazama kama Vinaweza Kupokelewa na siyo Kuthibitisha Kuwa ni Mali ya Jeshi au siyo Mali ya Jeshi.

Jaji: Mallya hajaonyesha Kuwa yeye alivitambuaje hapa Mahakamani.. Wakasema Kuwa Imeelezwa kwenye kesi ya Jamuhuri Vs CHARLES GAZILABO, Kwamba Mahakama Ishughulike na Kuvipokea. Kuhusu alama aliyoweka aliomba Kusema kwamba Mahakama Ione Vielelezo Hivyo Vilishughulikiwa Vizuri.

Katika Rejoinder Walieleza Upande wa Utetezi Ni kwamba Kwakuwa Shahidi alitaja Kwa Majina Vielelezo Hivyo basi alionyesha kuwa anavitambua.. Maelezo ambayo yameletwa pande zote mbili Kuwa Kukosekana Kwa Uelewa Kuhusu Vielelezo hivyo Inatosha Kum' disqualify.

Jaji: Upande wa Mashtaka Wanasema Kwamba Suala la Utalaam siyo Suala la Sasa.. Katika Kesi ya SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER VS DPP inasema Kwamba Katika Ushahidi Kuna Identification ikifanyika inatosha.. Utambuzi Kwa Kuangalia features pekee.

Kwa Alama ambayo Shahidi ameiweka yeye Mwenyewe, ambayo Nimeweka hapo Juu kuwa Kielelezo Kinaweza Kutambuliwa kwa unique features Features ambayo ni Mabaka inapatikana Katika Vielelezo Vyote Lakini Features ambayo ni X/HD ilikuwa inatosha.

Nafahamu maelezo ambayo yanasema kuwa features X /HD siyo Features ya Kisheria.. Mahakama Inaona Hoja hii itashughulika nayo katika Hoja inayofuata.. Hoja ya Utaalamu tuta shughulika nayo baadae siyo kwa sasa.

Jaji: Hoja ya Kidaftari cha Five star, Kuhusu Kikaratasi ambacho Kilikuwa ndani yake, Kuwa hakikufuata Mchakato wa Sheria Juu ya Kuongeza Kielelezo.. Upande wa Mashtaka hawajafuata Utaratibu Wa Kisheria Kutumia Kifungu cha 289 cha CPA sura ya 20 Juu ya Kutaarifu Mahakama Katika Kuingiza Kielelezo Ambacho hakikukuwa Commited.

Vielelezo ambavyo Havikuwa Commited katika Trial Court.. Kidando Wakati anajibu alieleza Mahakama Kuwa suala Zima La Commital Limeelezwa Katika Kanuni ya 8(2) ya 2019 GN ya 277 Katika Ukurasa Wa 32,33 wa Commital Proceedings, Inaonyesha Kuwa Ilishatajwa.. Katika hali hiyo Waliomba Mahakama Ipokee Kielelezo hicho.. Katika Kesi ya RONJINO walisema Kwamba Haihusiki na urodheshwaji wa Vielelezo.

Jaji: Upande wa Utetezi Wakasema Kuwa Kielelezo ambacho Kinatajwa hakikupokelewa, Wakaomba Mahakama Kuwa katika Certificate of Seizure Kuna Vingine vimetwajwa. Kwa Kuangalia kwa Ujumla naona kuwa ni Kweli Vielelezo vinavyolengwa Kutolewa hapa Mahakamani havikutolewa hapa Mahakamani haviku Orodheshwa wakati wa Commital.

Kifungu cha 246 linataka Kuwa Kielelezo au Ushahidi Wowote unapotakiwa Kupokelewa Mahakamani Unatakiwa uwe Umekuwa Commited Mahakamani.

Jaji: Nikisona Kanuni ya 8(2) ya Mahakama hii inataka Mahakama hii Kusoma Maelezo Kwa Lugha wanayo ufahamu, Kusoma Ushahidi Wanaoshtakiwa nao, Nyaraka za Ushahidi Unaotarajiwa Kutolewa Mbele ya Mahakama. Kinachotakiwa Kufanywa na Mahakama Husika ni Kusoma Mashtaka, Kusoma Ushahidi lakini pia Kusoma Nyaraka zinazo Contain Substance ya Ushahidi unapotakiwa Kusomwa Mahakamani Kinachotakiwa Kufanywa ni Kungaliwa Kama Ni kweli kilisomwa?

Hayo ndiyo Masharti ambayo yapo Kifungu 289 (1) Hakuna Shahidi atakayeitwa kama Ushahidi Wake haukusomwa wakati wa Commital, Shahidi ataitwa endapo Kama Ushahidi Wake Ulisomwa na Ushahidi huo ulienda Upande wa Mashtaka.

Katika Haki hiyo Basi kumbe kinachotakiwa ni Shahidi Kuitwa bila Kutolewa Notisi Upande wa Utetezi, Kama Kuna nia ya Kumuita shahidi huyo na Mahakama Ita angalia Notisi hiyo ni toshelezi au Siyo toshelezi.

Hakuna Takwa la Kisheria Kuwa kuna Takwa la Kuleta Kielelezo ambacho ni physical.. Kwa Maelezo hayo naona Hakuna Sheria ambayo imevunjwa.

Jaji: Na Upande wa Mashtaka Waliomba Kwamba Ili Kusudi tukubali au Kupokea Kielelezo chochote lazima Pawe na Sheria inayokataza.. Kama Hakuna Sheria Wala Sheria Kesi Mahakama Hii itakuwa Inafanya Makosa Kukataa Kielelezo.

Kwa Upande wa Mashtaka Hawalazimishwi Kusoma Kielelezo ambacho ni Physical Vielelezo Vyote ambavyo vinalengwa Kutumika hapa Mahakamani, Hakuna Sheria ambayo imevunjwa. Na Sheria ambayo zimeorodheshwa hazikatazi.. Kwa Maana hiyo Naitupilia Mbali Hoja hii.

Jaji: Lakini pia Suala La Mr. Mallya aliomba Mahakama Kuwa Kidaftari ambacho Kilikuwa Commited siyo Kilicho letwa hapa Mahakamani, Mahakama imeombwa Kwenda kwenye Committal Bundle kungalia kama Kielelezo Hicho Kilikuwa Commited.

Mahakama Imeona Kilikuwa Commited na Kiliorodheshwa na Karatasi zimo ambazo zinamichoro Michoro.. Kwa Hoja hiyo ya Malya Pia siyo ya Msingi, Katika Mazingira hayo Basi Mahakama hii Imeona Hoja yake haina Msingi.

Jaji: Mr Mallya ni Kama alitaka Ku' impeachment Kumbukumbu za Mahakama, na Mahakama inaona hoja aliyoleta haina Msingi.

Jaji: Kuhusiana na Kibali cha Kufanya Seizure of certificate Kwamba Baada ya Kukamata Vielelezo hivyo vitakiwa Kupelekwa Kwa Hakimu.. Kuhusiana na Kibali cha Kufanya Seizure of certificate Kwamba Baada ya Kukamata Vielelezo hivyo vilitakiwa Kupelekwa Kwa Hakimu.

Hoja za Kupinga Za Bwana Kidando PGO 226 (2)c Kwamba Afisa wa Upelelezi alikuwa anahusika na Kukamata na Kuhifadhi.

Kesi ya Mbowe Vs DPP ya 420/2018 Mahakama ya Rufani ilisema kwamba kutokutolewa Kwa Taarifa kwa Hakimu haizuii Ushahidi Kupokelewa.

Jaji: Kuhusiana na Kibali cha Kufanya Seizure of certificate Kwamba Baada ya Kukamata Vielelezo hivyo vitakiwa Kupelekwa Kwa Hakimu.. Kuhusiana na Kibali cha Kufanya Seizure of certificate Kwamba Baada ya Kukamata Vielelezo hivyo vilitakiwa Kupelekwa Kwa Hakimu.
Nakumbuka maneno ya mzungu nimemsahau jina Ni mmarekani alisema, hii kesi ni bogus terrorism charges
 
Uzi umedoda,,

Nyumbu wako ccm wanamuunga mkono mama ili kumkomoa Ndugai na marehemu!

Je, mabeberu nao wamemsusa Mwamba? Maana siwaoni hapo.

wanalicheza disco la CCM sasa....leo na week yote hii watamdiscuss Mama, Lukuvi na Kabudi..
Next week na February yote watajadili Spika mteuliwa na Ndugai akiwa kwenye siti za wabunge...

Shangazi yao kule twita naye kapiga U-TURN..
 
Wamfunge haraka sana huyu gaidi..mama usije kuingia kwenye mtego wa kitoto wa Zito kabwe.
Mwisho wa siku utadharaulika na utakuwa umethibitishia ulimwengu yakwamba kesi hii ni yakutengenezwa na umetoa msamaha kwa kushinikizwa na wanaharakati, wanasiasa na vyombi vya habari vyenye mrengo ule wa kisiasa.

Mualivu ni mualivu tu hata Dunia yote ipige kelele...apigwe kitazi mara moja ili iwe fundisho kwa wanasiasa wahuni na kwa vizazi vijavyo
 
Kwa Hiyo Mawakili wa Serikali Wanatumia FANTA
 
Sema hamna mawakili kwa upande wa washitakiwa lakini judge yuko sahihi. Mawakili wa Mbowe wote ni kanyaboya.

SIJUI WAMEHONGWA!!
AU WAMETISHWA!!

NONSENSE
Kina Kibatala wako vizuri sana kwenye mawakilisho yao. Kitu kinacho onekana Jaji yuko kama wakili wa upande wa mashtaka.
Yaani ana wasaidia hata kwenye vitu walivyo visahau.
Kuna shida kubwa sana kwenye hii kesi.
 
Back
Top Bottom