Suala la nishati ya mafuta nchini lishakuwa janga la Taifa

Sheffer95

Senior Member
Mar 16, 2020
197
460
Habarini za asubuhi, nikiwa na masikitiko makubwa naomba ni address hili suala la mafuta kiukweli limekuwa zaidi ya changamoto

Sikudhani hali ingefikia huku yaani leo nikiwa safarini mkoani nikipita huku maeneo ya Chunya Mbeya mji mzima ni shell moja tu ndio inayouza mafuta

Na hiyo foleni ya magari, pikipiki na vyombo vinginevyo ni kubwa umbali wa mita 400 watu wamepanga foleni kupata mafuta wengine kutokea saa 12 asubuhi

Hivi serikali inaliona hili?
Hivi serikali imeshindwa kutatua hii changamoto?
Inakuwaje serikali haitaki kukubali kwamba nchi ipo kwenye state of emergency? Na wote waliohusika kuleta kadhia hii wakachukuliwa hatua maana ni wahujumu
Huduma hazipatikani, uzalishaji have hauendelei sababu ya hili

Shabiby alisuggest watu binafsi wenye uwezo wapewe ruhusa kuagiza mafuta yao na ewura wabaki kuwa regulators kwann mnashindwa kutoa hivyo vibali mnataka mfumo wenu wa kuagiza bulk

Hakika kwa hili nililolishuhudia leo Chunya, CCM mna kazi sana 2025
 
Serikali ilishasema ambae anaweza Kuagiza mafuta aende Wizarani Apewe kibali hakuna aliyeenda.
 
Uhuru wa kuongea yule dikteta alikuwa anaiendesha nchi Kama family yake. Kuwa huru na kula Uhuru wako,huwezi pata vyote,ngorongoro bye bandari bye, madini yote pamoja na ardhi nzuri yenye rutuba nampatia mjomba wenu ,nyie ongeeni si mlisema kuwa hamtaki vitisho mie siongei
 
Uhuru wa kuongea yule dikteta alikuwa anaiendesha nchi Kama family yake. Kuwa huru na kula Uhuru wako,huwezi pata vyote,ngorongoro bye bandari bye, madini yote pamoja na ardhi nzuri yenye rutuba nampatia mjomba wenu ,nyie ongeeni si mlisema kuwa hamtaki vitisho mie siongei
Daaah yaani inasikitisha Mtu unawahi umepata emergency ufike ila umekwama mahali kisa mambo kama haya ya kijinga,
Ina maana serikali inaongozwa na watu kwenye wizara ambao hawana vision hawawezi forecast au predict mahitaji ya wizara + next shipment ikiwa factors zote considered
 
Wanashindwa kuruhusu installation ya vituo vya kujaza gesi angalau magari madogo yatumie gesi........ndo tatizo la kuchanganya biashara na kazi za umma, wengi wao hawa wana vituo vya mafuta.
 
Back
Top Bottom