Kupanda kwa bei ya mafuta nchini: Wasanii, Madaktari waiangukia Serikali na kuishauri

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
Kupanda kwa bei ya mafuta nchini…

WASANII, MADAKTARI ‘WAIANGUKIA’ SERIKALI, WAISHAURI


JUZI, Serikali kupitia Ewura, imetangaza bei mpya ya mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa ambapo mbali na mikoa mingine, Mkoa wa Dar es Salaam, Lita 1 ya Petroli imekuwa Shilingi 3,400 (ongezeko la Shilingi 300 kutoka kwenye bei ya awali).

Kupanda kwa bei ya mafuta ambako ‘kunatishia’ ongezeko la bidhaa mbalimbali nchini, ikiwemo nauli, kumetajwa kusababishwa na kuzidi kupaa kwa bei ya bidhaa hiyo kwenye Soko la Kimataifa.

Sasa baadhi ya wasanii na madaktari nchini, wameongea jana wakitoa kauli za ‘kuiangukia’ Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakishauri kufunguliwa kwa milango huru kwa wafanyabiashara wote wenye uwezo kuruhusiwa kuagiza na kuingiza bidhaa hiyo nchini wakisema ndiyo njia pekee itakayosababisha udhibiti wa bei.

DAVID MPONJI, msanii wa Bongo Muvi, alisema: “Serikali iache urasimu (utaratibu wa kuendesha kazi za ofisi kulingana na kanuni za utawala), iruhusu kila mfanyabishara mwenye uwezo aagize mafuta, yenyewe (Serikali) isimamie mapato yake tu. Ilimradi waagizaji wasimamiwe kuhusu ubora wa mafuta na kukidhi vigezo.”

JACQUELINE WOLPER: “Kwa nini Serikali isiamue kuruhusu kila mfanyabiashara mwenye uwezo aingize mafuta nchini? Wakiruhusiwa hawa, meli zitakuwa zikipishana bandarini. Hii inapakua mafuta, nyingine imemaliza kupakua na inaondoka kufuata mengine, nyingine iko majini inaleta.

“Endapo itaonekana hakuna mabadiliko basi warudi kwenye utaratibu wa sasa, siyo dhambi mbona. Bei ya mafuta huko duniani inapenda kila siku kwasababuya vita vya Urusi na Ukraine. Kwa hiyo kunatakiwa umakini mkubwa katika uingizaji ili mafuta yasipande zaidi.”

DOKTA CHENI: “Nadhani Serikali ina wasiwasi kwamba, akiachiwa kila mfanyabiashara aagize mafuta atakavyo, wataingiza na uchakachuaji ndani yake. Lakini ushauri wangu Serikali iamue na kusimamia kupitia mamlaka zake ili wasikwepe kodi wala kuchakachua mafuta yenyewe.”

JD: “Duniani kote, mafuta yanapopanda bei hakuna bidhaa inayosalia katika bei ya awali kwa sababu mafuta ndiyo chanzo kikuu cha usafirishaji. Naiomba Serikali itazame hili suala kwa jicho la tatu. Najua Rais wetu hana tatizo na ana nia ya dhati, lakini nadhani baadhi ya wasaidizi wake hawamshauri vizuri mama yetu.”

MADAKTARI;

Baadhi ya madaktari waliyoongea, waliiomba Serikali kuimulika upya sheria ya uagizaji na uingizaji wa mafuta nchini ambapo mpaka sasa, Serikali ndiyo mwingizaji mkuu kupitia utaratibu wa uingizaji wa mafuta kwa wingi nchini, Bulk Procurement System.

John Paul, daktari wa binadamu kwenye hospitali moja ya Serikali alisema: “Sioni sababu kwa nini Serikali isitangaze tenda ya uwazi kwa kila mfanyabiashara mwenye pesa zake za kutosha ajitokeze kuingiza fuel (mafuta), kuliko ilivyo sasa, wafanyabiashara watano sijui sita, hawatoshi.

“Hata huo wasiwasi kwamba, huenda wapo wafanyabiashara watakaoingiza mafuta week (dhaifu), siyo kweli kwani Serikali yenyewe siyo ndiyo inayapokea mafuta na kuyapima hata sasa?! Mfanyabiashara akigundulika kaingiza mafuta yasiyokidhi vigezo afutiwe leseni mara moja.”

Dk. Hassan wa Hospitali yaTaifa, Muhimbili yeye alisema: “Hii hali ya sasa inaashiria bidhaa kupanda. Mimi naiomba Serikali sikivu ya mama yetu, Samia Suluhu Hassan ipange upya huu utaratibu wa kuingiza mafuta nchini.

“Namwomba Waziri wa Nishati, Januari Makamba, asiangalie sura, aje na Plane B (mpango mwingine) wa uingizaji wa mafuta nchini ili kuinusuru hii hali. Hata kama Serikali kwa sasa inatoa Shilingi Bilioni 100 kila mwezi katika ruzuku mwishowe itaonekana pesa hizo ni kidogo. Italazimika kutoa Shilingi Bilioni 200, mwisho wake nini?

“Lakini pia mawazo yangu mengine ni kwamba, ikiwezekana Serikali ijitoe kwenye biashara ya mafuta, waachiwe wafanyabiashara tu, halafu Serikali isimamie kupokea na kuyakagua ubora na kukusanya kodi ya mapato.”

BUNGENI;

Katika kikao cha Bunge la Bajeti kwa mwaka 2022/2023 jijini Dodoma, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby aliishauri Serikali kuruhusu wafanyabiashara wote wenye uwezo kupewa vibali vya kuwaruhusu kuingiza mafuta nchini akisema ndiyo njia pekee ya kushusha bei ya bidhaa hiyo kwa vile kila mfanyabiashara atajua atayapata wapi mafuta na kwa bei gani na kuyatela nchini ili mradi, Serikali iendelee na mamlaka yake ya usimamizi katika kuyapokea chini ya mpango wa Petroleum Bulk Procurement System (PBPS).

Hata hivyo, kufuatia ushauri wa Ahmed Shabiby, Wizara ya Nishati imewapa vibali wafanyabiashara wachache (inadaiwa watano) kuingiza bidhaa hiyo , maamuzi ambayo hayajaonesha tija licha ya Serikali kuingiza ruzuku ya Sh. Bilioni 100 kila mwezi kwa ajili ya bidhaa hiyo.

Nchini Tanzania, uzoefu unaonesha kuwa, kila inapotokea mafuta yamepanda bei, bidhaa nyingi nazo hupanda zikiwemo, mchele, mafuta ya kupikia, unga, vifaa vya ujenzi, nguo, tivii, redio, simu, bila kusahau nauli za ndani na nje ya mikoa. Kisingizio kikubwa cha wapandishaji wa bidhaa ni ‘bei ya petroli imependa.’
 
Nipo kijijin huku naona watu wameanza kutumia zile disko za zamani za kutumia betri la gari,jenereta zimewekwa kando
 
Nipo kijijin huku naona watu wameanza kutumia zile disko za zamani za kutumia betri la gari,jenereta zimewekwa kando
Kuna wizara watu qnatakiwa kuvulumiahwa haraka iwezekanavyo,
1. Fedha na mipango, hapa nikuvulumiasha, mawaziri wote, katibu mkuu, na kwenye idara ya Mipango vyulumiasha wote.

2. Nishati na madini, vulumiasha mawaziri wote, ikiwezekana mpaka katibu mkuu, Wizara ya afya, vulumiasha naibu waziri.
 
Kwa ujumla mafuta yameanza kushuka tangu July kati kuja mwishoni. Na tumeianza nchi nyingi bei kushuka na zinaendekea kushuka!

Tanzania nadhani kuna mahali iko tatizo na hii ni viongozi kutijaki huduma Kwa wananchi.

EWURA na wote mnaohusika tangazeni punguzo haraka sana hii kuendelea kuombwa ombwa hakuwajengei sifa hata kidogo.

Wizi kila Kona! Hata madaktari wamekutwa kuombana Rushwa! Ujinga gani huu!!
 
Kwa ujumla mafuta yameanza kushuka tangu July kati kuja mwishoni. Na tumeianza nchi nyingi bei kushuka na zinaendekea kushuka!.
Tanzania nadhani kuna mahali iko tatizo na hii ni viongozi kutijaki huduma Kwa wananchi.
EWURA na wote mnaohusika tangazeni punguzo haraka sana hii kuendelea kuombwa ombwa hakuwajengei sifa hata kidogo.
Wizi kila Kona! Hata madaktari wamekutwa kuombana Rushwa! Ujinga gani huu!!
Mkuu umeongea vizuri, Kuna majizi lakini pia selikali ijitoe kwenye biashara ya mafuta, ibaki kuratibu na kuahakikisha kodi zinakusanywa vizuri basi,
 
Eti waiamgukia Serikali, ujinga mtupu, nchi imejaaa waoga kama nini pandisha ifike 5000/ ili waendelee kuinagukia Serikali.
 
Watu wanataka uhuru wa kuingiza mafuta ila kuna hatari kubwa kuliko ilivyo sasa..

Chukulia case ya Mbolea, wafanyabiashara waliachiwa wakazingue serikali imerudi kule kule kuagiza yenyewe kwa kumpa mtu kibali na anaweka bond ya pesa..

Point inabakia pale pale kwamba ruzuku haikwepeki kwa sababu ukifuta Kodi zinafika 900 kwa Lita utavuruga sehemu nyingi zaidi so Bora ruzuku iongezwe.
 
Back
Top Bottom