Rushwa ndani ya chaguzi za CCM ni janga la Taifa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Chama cha Mapinduzi (CCM), kinaendelea na mchakato wa uchaguzi wa ndani, ambao hivi sasa umefika katika hatua ya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa jumuiya zake za vijana, wazazi na wanawake.

Hata hivyo, uchaguzi uliokamilika wa chama hicho tawala katika ngazi za chini kuanzia matawi, kata, wilaya na mikoa umekumbwa na tuhuma za rushwa, ambazo wadau wa siasa wanaona kwa ukubwa wa chama hicho kinachotawala Serikali, hali hiyo ni kiashiria cha kutamalaki kwa rushwa ndani ya vyama vya siasa, Serikali na jamii kwa jumla.

Tuhuma za rushwa zimekifanya chama hicho, kufuta chaguzi tano za Umoja wa Vijana (UVCCM), huku chaguzi zaidi ya tatu za Umoja wa Wanawake (UWT) zikisimamishwa kwa kukiuka katiba, kanuni na taratibu.

Chama hicho chenye mtandao mpana zaidi nchini, pia kimesimamisha uchaguzi wa wajumbe wa halmashauri kuu mikoa ya Arusha na Mbeya kwa tuhuma hizo hizo.

Hata hivyo, baada ya vitendo hivyo vya rushwa, mapema wiki hii Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni alilieleza gazeti hili wanaendelea na uchunguzi na watakaobainika hatua zitachukuliwa.

“Tayari kuna chunguzi tunaendelea nazo, wao kama chama wametumia taratibu zao na sisi tunaendelea na taratibu zetu kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Hofu kwa wadau

Licha ya hatua zilizochukuliwa na uongozi wa CCM, kuibuka kwa tuhuma za rushwa kwenye uchaguzi kumeibua hoja na hofu kutoka kwa wachambuzi na wadau wa siasa kuhusu uwezo wa chama hicho kukabiliana na janga la rushwa ndani ya Serikali, taasisi zake na siasa kwa jumla.

Suala la rushwa katika chaguzi ni miongoni mwa hoja zilizoibuliwa na viongozi waandamizi serikalini na wastaafu waliofika mbele ya kikosi kazi kilichofanyia kazi masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

Taarifa ya kikosi kazi hicho kilichoongozwa na Profesa Rwekaza Mukandala, ilipendekeza sheria za uchaguzi zirekebishwe kwa kuweka masharti ya mgombea atakayethibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa, kuondolewa sifa ya kugombea katika uchaguzi wowote kwa miaka 10 mfululizo.

Akizungumzia rushwa iliyojitokeza ndani ya uchaguzi wa CCM na kuibua malalamiko kwa makada wake, Wakili wa kujitegemea, Method Kimomogoro alisema: “Wahenga walisema mficha maradhi kifo kitamuumbua. Rushwa siyo tu ni adui wa haki, bali pia maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. CCM ni lazima ionyeshe kivitendo kupambana na rushwa ndani na nje ya chama.

“Viongozi na wagombea wa CCM kujihusisha na rushwa ni janga kwa Taifa, maana chama hiki ndicho kinaunda na kuongoza Serikali,” alisema.

Alisema wakati wa Azimio la Arusha, Tanzania ilidhibiti vitendo vya rushwa kiasi cha kuwa katika orodha ya nchi zenye kiwango kidogo cha rushwa.

‘‘Viongozi hawakuwa na fursa ya kujilimbikizia mali kupitia wao wenyewe wala kwa kuandikisha majina ya wake, watoto na ndugu zao; wote kwa umoja wetu tulipiga vita rushwa tofauti na sasa.”

Aliiomba Serikali kurejesha miiko ya uongozi kwa kuiweka ndani ya Katiba kama ilivyokuwa kwenye rasimu ya katiba ya Tume ya Marekebisho ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

“Wenzetu Kenya viongozi wa umma wanahojiwa na kutaja mali zao hadharani kuwezesha umma kuhoji na kufichua; lakini sisi fomu za mali ya viongozi ni siri ya Tume ya Maadili na viongozi walioorodhesha mali zao. Hakuna fursa ya umma kujua wala kuhoji usahihi wa taarifa hizo,” alisema Wakili Kimomogoro.

Wakili huyo alisema kinachoendelea ndani ya CCM ni kipimo cha uwezo wa chama hicho katika vita dhidi ya rushwa ndani ya vyama vingine na Serikali.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (Saut), Dk Kanaeli Kaale alisema uwepo wa tuhuma za rushwa katika chaguzi za CCM, ni uthibitisho ndani chama hicho wapo watu wenye uroho wa madaraka na ni changamoto kwa chama na Serikali kuboresha eneo la maadili ya uongozi na kanuni za uchaguzi.

“Ni jambo la faraja kuona chama kimeanza kuchukua hatua kwa kufuta matokeo na kuagiza uchunguzi. CCM imeonyesha uimara wa kusimamia Ibara ya 18 (2) ya Katiba yake inayokataza viongozi kupokea rushwa au kushiriki katika mambo yaliyo kinyume na maadili,” alisema Dk Kanaeli ambaye ni mwandishi wa habari kitaaluma.

Akizungumzia uwepo wa madai ya tuhuma za rushwa na hatua za kuchukuliwa, kada mkongwe wa CCM, Mzee Joseph Butiku alisema: “Tusubiri mchakato wa uchaguzi umalizike ndipo tutoe maoni yetu kwa sababu kuzungumza kwa sasa ni kama tunafanya kampeni. Matukio yametokea na watendaji wa chama tayari wamechukua hatua”.

Kada mwingine mkongwe wa CCM, Stephen Wasira yeye alisema; “Katibu Mkuu wa CCM (Daniel Chongolo) na Katibu mwenezi (Shaka Hamdu Shaka) tayari wamezungumza na kutoa mwelekeo wa chama, mimi mjumbe wao wa kamati kuu sina la kusema zaidi ya msimamo huo.”

CCM yafafanua

Akizungumzia tuhuma za rushwa ndani ya CCM, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa uchaguzi umefanyika vizuri kwa zaidi ya asilimia 90.

‘‘Hizi zinazojitokeza ni changamoto ndogo ndogo na tayari tumechukua hatua kwa kufuta matokeo, kuahirisha uchaguzi na kuagiza uchunguzi.”

Alisema chama hicho tawala kitatumia nyenzo tatu ambazo ni katiba, kanuni ya uchaguzi na kanuni ya maadili ya uongozi, kushughulikia changamoto hizo.

“Kila kitu kitaamuliwa kupitia vikao halali vya chama kwa kuzingatia katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2022, kanuni ya maadali na uongozi pamoja na kanuni ya uchaguzi,” alisema Shaka, huku akijinasibu kuwa kasoro hizo ziko ndani ya uwezo wa chama kuzishughulikia.

Zitto Kabwe na kanuni za rushwa

Zitto Kabwe, kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo alisema japo amejiweka pembeni kuzungumzia masuala ya ndani ya vyama vingine vya siasa, msimamo wake kuhusu rushwa ni jambo hilo kuwekewa msingi ndani ya Katiba ya nchi na wahusika kushughulikiwa bila kuonewa muhali.

“Sheria ya vyama vya siasa ifanyiwe marekebisho kuweka sharti la vyama vya siasa kuwaondoa katika mchakato wa uchaguzi wote wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa. Kila chama kiwe na kanuni ya maadili kudhibiti ukiukwaji wa viongozi na wanachama,” alisema Zitto.

Alisema wote wanaothibitika kujihusisha na vitendo vya rushwa pia wanatakiwa kuzuiwa kugombea na kuongoza ofisi ya umma kwa miaka angalau 10.

“Kanuni ziweke utaratibu wa kushughulikia ukiukwaji wa maadili na adhabu, ikiwamo onyo, karipio, faini, kuvuliwa ujumbe wa kikao husika na kusimamishwa au kufutwa uanachama na kuzuiwa kugombea kwa miaka 10 tangu mtu anapopatikana na hatia,’’ alisema.

Maoni kwenye kikosi kazi

Katika maoni ya CCM iliyoyawasilisha mbele ya kikosi kazi kilisema: “Rushwa bado ni tatizo, mbali ya juhudi zilizifanywa kupambana nayo. Bado kuna wanasiasa wanashiriki katika vitendo vya rushwa.”

Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye yeye mbele ya kikosi kazi alisema: “Rushwa katika uchaguzi bado ni tatizo kubwa. Inaonekana kushamiri sana wakati wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa. Kimsingi, nafasi za uongozi wa nchi hii zinanunuliwa.

“Tunapaswa kupiga vita rushwa kwa kuanzia na CCM, vinginevyo tusahau kabisa habari ya demokrasia katika nchi hii,” alisema Sumaye.

MWANANCHI
 
Rushwa imekuwa ni sehemu muhimu kabisa ya maisha ya watanzania wengi. Kwanza wanaifurahia.
 
Bado watu wanashanga Riport za CAG mtu anapoteza muda kuhoji wizi mikataba mibovu ya kidanganyifu hawa ndio ccm bhana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom