Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,918
- 30,259
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.
Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma na kuandika.
Krapf alikuwa na barua mkononi kutoka Zanzibar kwa Sultan Barghash ikimuomba Chief Kimweri amsaidie Krapf kwani ni "mtu wa Mungu."
Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.
Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.
Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.
Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu "washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.
Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na elimu iliyokuwa imetolewa na madras.
Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.
Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.
Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika.
Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.
Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.
Kati ya mwaka 1888 -1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo na taasisi zake zote katika Afrika ya Mashariki.
Ombwe lililoachwa na madrsa ikajazwa na shule zilizojengwa na Serikali na Kanisa chini ya usimamizi wa wakoloni.
Historia iliyoandikwa inasema kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.
Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.
(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes 1998).
Baada ya karne mbili Rais wa Tanzania kutoka Zanzibar anampa zawadi ya mlango wa Kizanzibari Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani ndani ya Vatican na kumweleza maneno haya:
"This is the door... " - Sultan opened for Christianity..."
Huu ndiyo mlango uliofunguliwa kwa Ukristo kuingia Zanzibar na Afrika ya Mashariki.