Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
324
909
Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.

VIJANA🙄
 
Ibada ya mazishi huwa siyo kwa ajili ya marehemu maana maandiko yanasema marehemu hajui neno lolote ibada huwa ni kwa ajili ya waliohai kuwakumbusha kutengeneza njia zao ili nao wakilala walale katika Bwana

Huyo hata angezikwa bila ya ibada hakuna shida historia yake imeshafungwa ktk vitabu vya mbinguni ibada haiongezi wala kumpunguzia chochote ktk hatma yake iliyofungwa
 
Back
Top Bottom