Stress ni nini?
Desperation ndo vipi?
katika kila kitu tunachokifanya kila siku, hizo terms mbili zinakuwepo tu, kiwango chake ndo mjadala ulipo.
mfano unapenda sana kuwa na aina fulani ya nguo, ile desire yako ndo inakuongezea stress na ukifika kwa muuzaji ile desperation yako ndo itakayokufanya uinunue hata kwa bei kubwa zaidi.
Kwa mantiki hiyo stress na desperation zipo pande zote, na zinatofuatiana kwa mtu na mtu kutokana na Umri, priorities, life style, na mengine mengi tu.
Wenzetu wa jinsia pinzani wana stress/desperation zaidi,
1. kwa maana wao wana deadline kwenye mambo fulani, au tuseme deadline zao zinawahi kidogo.
2. wao siyo waamuzi wa game, yaani yeye hawezi akaamua aolewe mwakani, anasubiria tu aje mtu anayeeleweka kdg (kwa vigezo vyake) na aambiwe, anaweza kudai ila atalazimika kusubiria mipango ya muoaji. wakati mwanaume so hivyo.
3. machaguo mengi ya wanawake hayapo sokoni, yaliyopo kidogo ni ya kugombania na mengi hayako tayari kuanzisha familia. kwa Mwanaume almost 50% ya wanawake anaowasiliana nao anaweza kuwaoa pakinuka.
4. Mwanaume awe ameoa au hajaoa anapanga tu maisha yake, ila wenzetu wengi wanapopanga mambo yao anaishia kwa hapo mbele kdg, akijua baada ya hapo anaingia kwenye mipango ya mwingine. So miaka 30 inapofika anaona anarudi tu nyumbani au anakaa geto tu anachanganyikiwa zaidi. anaanzaje maisha ya kutafuta hata kiwanja ilhali hakuwa kufikiri kama itakuwa hivyo? ila wanaume sisi umri fulani ukifika ni mbele kwa mbele tu tuwe tumeoa au la.
Zipo sababu nyingi sana zinazoongeza zaidi stress upande wa akina dada zetu kuliko kwetu. ila Nakiri hata kwetu stress zipo tu.... hata mimi ninazo
haya ni maoni yangu tu.