Stress za kuolewa/kuoa sio kwa wadada tu!

ERoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
55,589
Reaction score
130,956
It's a new day MMU family.

Kwa nini wanaume tunanifariji kuwa wadada pekee ndio wanakuwa na stress za kuolewa? Je, ni kweli kwamba vijana wa kiume hawakumbwi na wimbi la stress hasa wanapofikia "umri sahihi" wa kuoa?

Inasemekana "eti" wadada saa yao inazunguka kuanzia miaka 22--28, baada ya hapo ni stress tupu, kwamba mwanamke akifika miaka 30 anakuwa 'desperate' hadi kufikia kukata tamaa ya kuolewa. Sijui kama ni kweli, wadada waje hapa waseme ukweli wa moyoni

Kwa upande mwingine wa shilingi, hata wanaume wanakumbwa na hii kadhia, tena kwa kiwango kikubwa tu, sema sisi tuna koromeo mengi tunameza bila kusema. Sijui clock hasa kwa wanaume lakini binafsi nilipofika miaka 29 nilianza kuwaza mchumba, nikamuangalia niliyekuwa naye kipindi hicho nikaona nah, huyu hapana "I'm not marrying her", sababu nilizijua mwenyewe, lakini sasa mbona sioni wa kuoa? Ilinichukua mda sana, kuna vigezo vyangu (kama ilivyo kwa kila mtu, huwezi kujibebea tu) lakini nikawa sioni, mda unaenda, kichwa kinauma, sioni popote, sio kanisani, sio kazini, sio mtaani(naona tu wavaa vitait[emoji12] ), lakini mimi nilikuwa na experience ya online dating, hii habari tangu niianze 2007 sijataka kukutana na mtu kanisani tena, it's online and it's very interesting to meet someone online....

Sasa vidume wenzangu, hivi ni kweli hamna stress za kuoa, hasa wale 30+yrs? Imagine upo 35yrs huna hata girlfriend anayeeleweka, hivi hutakuwa na stress kweli, semeni ukweli tumuaibishe shetani leo[emoji12] [emoji1]

NB: Huu uzi ni kwa wale wanaoona umuhimu wa ndoa na wanatamani kuwa kwenye ndoa siku moja. Kumekuwa na tendency ya watu kudharau hii taasisi na kusema Ndoa sio muhimu, wale wanaoona sio muhimu, ni sawa tu na huu uzi utakuwa hauwahusu.

Good morning.
 
Sisi wanawake kuna muda ukomo wa kuzaa unafika nafikiri ndio maana tunakuwa hivyo pindi tufikishapo umri fulani.

Na kuhusu wanaume hawa bhana hata kama anaona umri umesonga stress zake haziwi kati kama za mwanamke.mwanaume hata akiwa na 50+ bado anauwezo wa kuzaa ila si mwanamke

Mfano halis ni Bw.Machache +Klyn=mapacha.

Kwa jicho la tatu naona kuna kalengo kako ndani ya huu uzi.
 
stress zipo kote kaka ila wanaume wanajipa moyo kwa kua wanaweza wakapata mwanamke wa kumgonga hata kila siku akienda kona bar,au kwa wahaya

hiko ndo kinachowapa kibr wanaume
sisi wanawake tunasubiri tufatwe ndo tupunguze ashk zetu
 
Umri mzuri kwa mwanamke kuzaa ni 25-35, wakati mwingine hadi 40 lakini kuna wanawake wamebarikiwa miili mizuri, wengine hata 50 anaenda labor tena sio CS, anajifungua kawaida tu.

Mfano wako wa mzee machache upo irrelevant, yule mzee ana watoto wakubwa, nadhani wengine ni wakubwa kwa K-Lyn, pale anapumzika na uzee wake, hizo ni rare cases. Kwa mtu anayetaka kuanzisha familia na kulea kw uzuri, huwezi kusema at 50yrs aanzishe familia, nah.
 
Niulize kaswali kadogo kuhusu huko kunakoitwa 'kukata tamaa'. Let's say wewe ni graduate umezunguka na bahasha wee umechoka mwisho wa siku ukaona maisha hayapo kwenye kuajiriwa tu ukaamua kuweka vyeti pembeni na kufungua genge lako tuseme umekata tamaa? Hujakata tamaa ila umeangalia upande wa pili wa shilingi na kuona ili mtu uishi maisha mazuri si lazima uajiriwe ukalie lijiofisi hiloo....unaweza kuwa na maisha mazuri hata nje ya kuajiriwa. Wenye kunielewa wamenielewa
 
Sisi wanawake kuna muda ukomo wa kuzaa unafika nafikiri ndio maana tunakuwa hivyo pindi tufikishapo umri fulani.

Na kuhusu wanaume hawa bhana hata kama anaona umri umesonga stress zake haziwi kati kama za mwanamke.mwanaume hata akiwa na 50+ bado anauwezo wa kuzaa ila si mwanamke

Mfano halis ni Bw.Machache +Klyn=mapacha.

Kwa jicho la tatu naona kuna kalengo kako ndani ya huu uzi.
Nadhani wanawake mda muafaka kupata watoto ni 25-35yrs, wenye miili mizuri hadi 50yrs wanaenda labor tena bila SC.

Mfano wa Bw. Machache haupo relevant, yule mzee ana watoto wakubwa kuliko huyo K-Lyn, pale anapumzisha akili na uzee wake kwa mtoto mdogo.

Uzi wangu hauna agenda yoyote, usiutazame kwa jicho la tatu, tumia tu hayo mawili.
 
Stress za mwanaume ni pesa tu maana usipokuwanazo wanawake wengi wanye vgezo unavyohitaj utapishana nao na sis hatuna clock age ya kuoa hata ukiwa na 45+ bado unaezaoa mweny 25. Tofaut na wanawake akishafka 30+ ndoa zinamkimbia kabsa
 
Niulize kaswali kadogo kuhusu huko kunakoitwa 'kukata tamaa'. Let's say wewe ni graduate umezunguka na bahasha wee umechoka mwisho wa siku ukaona maisha hayapo kwenye kuajiriwa tu ukaamua kuweka vyeti pembeni na kufungua genge lako tuseme umekata tamaa? Hujakata tamaa ila umeangalia upande wa pili wa shilingi na kuona ili mtu uishi maisha mazuri si lazima uajiriwe ukalie lijiofisi hiloo....unaweza kuwa na maisha mazuri hata nje ya kuajiriwa. Wenye kunielewa wamenielewa
Khantwe, mfano wako upo sawa kabisa. Kuliko kuzunguka n bahasha miaka mitano, ni heri kuwa na sehemu ukajipatia kipato kidogo, utapunguza soli za viatu kuisha.

The thing is, hiyo ni plan B, baada ya plan A kushindwa, ndio unaona isiwe tabu ngoja niangalie upande huu unakuwa vipi.

Likewise, kama mtu anaona mda unapita, hakuna proposal yoyote ya "ajira" ni heri kujiajiri. Lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa bado mtu angependa kuajiriwa.
 
Stress za kuoa kwa mwanaume ni kwamba una madem kadhaa hujui umwoe yupi kama Side mnyamwezi.. Ila kwa wanawake ni kwamba wanakosa kabisa mwanaume. Kuna tofauti kubwa bro.

Nafukia mashimo niko moto [emoji594][emoji100]
Ukiona mwanamke hana wa kumtoa kutu jua hajataka wanaume wapo kibao
 
Nadhani wanawake mda muafaka kupata watoto ni 25-35yrs, wenye miili mizuri hadi 50yrs wanaenda labor tena bila SC.

Mfano wa Bw. Machache haupo relevant, yule mzee ana watoto wakubwa kuliko huyo K-Lyn, pale anapumzisha akili na uzee wake kwa mtoto mdogo.

Uzi wangu hauna agenda yoyote, usiutazame kwa jicho la tatu, tumia tu hayo mawili.
Kwa bwana machache ni umri niliouangalia mkuu.

Hahahahahaha ngoja nirudishe macho mawili rodini.

Stress za mwanamke ambae umri umepitiliza hana mtoto wa hana mume...we zisikie tu mtu akikupigia story.

Kama anajijua kuwa hawezi kuzaa kabisa inakuwa ni bora.anaishi akijua mimi kwenye hii dunia sitaweza kuacha uzao wangu
 
stress zipo kote kaka ila wanaume wanajipa moyo kwa kua wanaweza wakapata mwanamke wa kumgonga hata kila siku akienda kona bar,au kwa wahaya

hiko ndo kinachowapa kibr wanaume
sisi wanawake tunasubiri tufatwe ndo tupunguze ashk zetu
Kumbe hizi stress huwa zinasababishwa na ashk ya kutaka dushe/papuchi??![emoji15]....Mimi nilikuwa nafikiri kuwa hizi stress huwa zinasababishwa na mtu kuona kuwa anachelewa kuanzisha familia,poor me!!!

Sent from my Armor using JamiiForums mobile app
 
Stress za kuoa kwa mwanaume ni kwamba una madem kadhaa hujui umwoe yupi kama Side mnyamwezi.. Ila kwa wanawake ni kwamba wanakosa kabisa mwanaume. Kuna tofauti kubwa bro.

Nafukia mashimo niko moto [emoji594][emoji100]
Hiyo ipo, "mademu" watano na hakuna anayefit, huoni kuwa wewe utakuwa ndio tatizo. How do you date five girls, with whom there's no match?? Yani wadada watatu lakini hakuna anayefit???
 
Back
Top Bottom