Stori ya kusisimua - Laiti Ningejua!

Stori ya kusisimua - Laiti Ningejua!

Mtunzi Bishop Hiluka
0685 666964


DONDOO

Laiti ningejua kuwa alikuwa na siri nzito namna ile aliyokuwa kaihifadhi kifuani kwake, nisingefanya upuuzi. Ona sasa, macho ya watu yananitazama kwa kunisuta, wapo walio na hasira juu yangu, wapo ambao wananitazama kwa dharau na baadhi kwa huzuni. Hata sijui nifanye nini!

Alikuwa msichana mrembo kwelikweli, mrefu na mweupe wa asili, si ule weupe wa mkorogo bali ule wa asili wenye ung’avu wa kuteleza. Umri wake haukuzidi miaka 25, alikuwa mwembamba lakini mwenye haiba nzuri ya kuvutia.

Kwa mlingano wa macho tu, alitoa tafsiri ya kuwa na ule uzuri usiomithilika ambao ungeweza kumliwaza, kumpumbaza na hata kumlaza kitandani mtu yeyote aliye buheri wa afya, na wapo waliodiriki hata kusema kuwa alikusudiwa kuumbwa malaika, ila akashushwa duniani kimakosa!

Lakini kama tujuavyo kila kizuri alichoumba Mwenyezi Mungu huwa hakikosi kasoro. Hata yeye alikuwa na kasoro au hila moja kubwa sana. Hila yenyewe ni kwamba hakujua kukasirika. Bila shaka pia hakujua umbea ama majungu!

Ili kuyajua yote fuatana nami katika mkasa huu wa kusisimua, kushangaza na kusikitisha…

LAITI NINGEJUA!

Tater, moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, the_legend, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly SUPER EMILY, WISDOM SEEDS nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa SUPER EMILY
Asante sana mpnz kwa kunikumbuka japo nimechelewa kuiona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu the_legend hiyo huitwa VISUALIZATION. Mwandishi makini anatakiwa kuiona picha nzima akilini mwake wakati anaandika hadithi yake, awaone wahusika wake wote, wanafananaje, wamevaaje, sauti zao n.k. Ujuzi wa aina hii ndiyo huitwa “visualization.”

Kwa kawaida uandishi hutegemea sana Ubunifu (Creativity). Ubunifu wa mtu hufanyika kutoka kwenye sehemu mbili za ubongo. Kwanza kuna Ubunifu wa Awali (Primary Creativity) ambao hutokea kwenye sehemu ya ubongo wa kulia, eneo ambalo ndiyo chanzo cha mawazo/mipango na utambuzi. Ni eneo ambalo msukumo wa mwandishi hutokea na kuchangia asilimia 10 tu ya mchakato mzima wa ubunifu.

Kisha, kuna Ubunifu wa Pili (Secondary Creativity), ambao hutokea kwenye sehemu ya kushoto ya ubongo na huchangia asilimia 90, sehemu ambayo hujumuisha uhariri, nidhamu ya kiuandishi, mantiki, muundo, mazoea ya kuandika, taratibu na mpangilio. Ili kuwa mwandishi mbunifu ni kuwa na ujasiri wa kuweza kurudia kumbukumbu zako za utotoni, ambapo ulikuwa huru na hukuwa na msongo wa mawazo au kufikiria sana maisha kama ulivyo sasa.

Unapoanza kuandika, ruhusu upande huo wa ubunifu wa asili kujitokeza kupitia maneno yako bila kuyakosoa au kuyachambua maandiko yako. Kabla hujaanza kupata taswira kichwani mwako (visualization), kwanza ni muhimu sana ufanye taamuli (meditation); fumba macho yako na ujilegeze huku ukivuta pumzi ndefu. Ukipenda unaweza kusikiliza muziki. Endelea kuvuta pumzi hadi unapohisi misuli ya mwili wako inalegea.

Dah, ngoja niishie hapa ingawa hili ni somo zuri sana. Sipendi niharibu uhondo wa hadithi yetu...
Hakika bishop umeiva kwenye sanaa hii. Hongera sana Mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laiti Ningejua! 24

Mtunzi Bishop Hiluka

“Nimefurahi sana kukutana nawe mama… shikamoo!” niliwahi kumsalimia kwa bashasha huku nikiachia tabasamu.

“Marhaba baba, nami nimefurahi sana kukufahamu na pole kwa yote yaliyotokea…” alisema, sauti yake ilikuwa ya upole sana alipoongea nami.

“Nimekwisha poa, mama,” nilijibu kwa unyenyekevu.

“Karibu sana mwanangu, niliambiwa kuwa ulilazwa Sewa Haji pale Muhimbili, lakini tusamehe sana hatukuweza kuja kukuona,” alisema Bi Aisha kwa huzuni huku akifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.

Endelea...

“Usijali mama,” nilijibu huku nikihisi mwili wangu ukinisisimka sana. Mbali na urembo aliokuwa nao yule mama lakini niligundua kitu kingine kikubwa zaidi kilichokamilisha uzuri na mvuto wake, ni upole wake.

Alikuwa ni mpole pindi aongeapo, alionekana mpole atembeapo na pengine hata alipokuwa katika shughuli zingine.

“Maana ule mkasa ulimfanya dada yako kuchanganyikiwa kabisa, wazimu si wazimu basi ni shida tupu, hata hivyo tunamshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea,” aliongea Bi Aisha kwa upole.

“Ni kweli mama, tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo, maana ni mapenzi yake hadi leo tuko hai,” nami nilisema kumuunga mkono yule mama.

Yule mama alirudi kuketi na kukatokea ukimya wa kitambo kifupi, niliwaona Bi Aisha na Rehema wakiwa wamezama kwenye mawazo kila mmoja akiwaza mbali, kisha kama aliyegutuka, Bi Aisha aliitazama saa yake ya mkononi na kuinuka.

“Karibu mwanangu, jisikie huru mimi nipo ndani kuna kitu nafanya,” alisema huku akiondoka.

“Nashukuru, mama,” nilijibu huku nikimsindikiza kwa macho hadi alipopotelea ndani. Kisha niligeuka kumtazama Rehema kwa makini.

“Inaonekana mama yako ni mcheshi sana?” nilimuuliza nikiwa nimekazia macho.

“Sana, kitu kingine mama yangu ni mzungu, siyo mtu wa kufuatilia fuatilia mambo…” alisema Rehema huku akiachia kicheko hafifu. Nikashusha pumzi.

Kinapita tena kitambo kifupi cha ukimya, nikainywa ile juisi yote iliyobakia kwenye bilauri huku nikiwaza namna ya kumuanza Rehema maana pepo mbaya wa ngono alikuwa ananisumbua sana. Rehema alinitazama kwa makini kama aliyehisi kitu.

“Vipi maisha?”

“Maisha ni kama hivi, namshukuru Mungu kwa kuwa nipo hai, vinginevyo…” nikasita kidogo na kubaki kimya. Rehema akanitazama kwa macho ya udadisi.

“Vinginevyo kitu gani mbona huendelei?” aliuliza baada ya kuona siendelei kuongea. Nikajifanya natafakari kidogo kisha nikashusha pumzi ndefu.

“Rehema, naomba nikuulize,” hatimaye nikamwambia Rehema kwa sauti ya utulivu.

“Niulize tu kaka yangu.”

“Je, wewe umeolewa?”

Rehema akaniangalia kwa makini kwa kitambo kirefu kisha akaachia tabasamu huku akitingisha kichwa chake kukataa.

“Ningekuwa nimeolewa nadhani usingenikuta naishi hapa kwa mama yangu. Hii inaonesha kuwa bado sijaolewa!”

“Mchumba je, huna mchumba?”

“Hapana sina mchumba!”

“Boyfriend?”

“Pia sina! Ila kwa sasa Mungu amenipatia friend boy na siyo boyfriend, na si mwingine ni wewe Bilali.”

Nikashusha pumzi za ndani kwa ndani huku nikihisi faraja baada ya kujua kuwa hakuwa ameolewa na wala hakuwa na mchumba, alikuwa tofauti na Jameela ambaye alikuwa mbioni kuolewa. Nikajiegemeza kwenye kochi.

“Kwa hiyo huna mume, huna mchumba, huna boyfriend, je mvulana ambaye labda… unampenda au…”

Rehema akanikazia macho kwa mshangao huku akikunja uso wake. Ni dhahiri alionekana kukerwa na maswali yangu yaliyomjia mfululizo.

“Samahani Bilali, kwani unatakaje! Sipendi kukulazimisha kusema kwa namna ninavyopenda, lakini naona kama nimekwisha jibu vya kutosha maswali yako kuhusu uhusiano wangu na wanaume. Sina uhusiano na mwanaume na wala sijawahi kuwa na uhusiano na wanaume yeyote, sijui unahitaji nini zaidi?”

Maneno yake yakanifanya nibaki kimya kwa muda nikimkodolea macho huku nikijilaumu sana kwa kukosa uvumilivu na kuporomosha maswali mfululizo kana kwamba nilikuwa polisi ninayehitaji taarifa muhimu za kiintelijensia.

“Naomba usinielewe vibaya, Rehema, unakumbuka niliomba tuwe marafiki, ukweli ni kwamba nilikupenda tangu siku ya kwanza tu nilipokuona! Ingawa najua kuna tofauti kubwa ya kipato kati yetu lakini hii hainizuii kukupenda…” sikukata tamaa, nilimchombeza Rehema huku nikizidi kumkazia macho.

Muda huo nilikuwa nahisi msisimko wa aina yake ndani yangu ingawa ukweli kulikuwa na sauti ndani yangu iliyonieleza kuwa sikuwa nampenda kutoka moyoni bali nilimtaka kwa kuwa tu alikuwa mrembo haswa… yaani nilimtamani tu kwa ajili ya ngono… nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu ingeisha na ningeachana naye.

Ndiyo, ningeachana naye kwa sababu nilidhani sikuwa nikihitaji kuishi na mwanamke mrembo wa aina ya Rehema ambaye sikuwa na uhakika kama ningeweza kumuoa na kuishi naye bila kupata ugonjwa wa presha.

“Ni kweli unanipenda?” sauti tulivu ya Rehema ilinizindua kutoka kwenye mawazo yaliyokuwa yakipita kichwani kwangu, nilimtazama nikamuona akinikazia macho, na kabla sijajibu akaendelea, “Kwanza ni upendo wa aina gani huo unaouzungumzia ambao unazuiwa na kipato?”

“Wa mke na mume. Yaani… nahitaji kukuoa Rehema, sijui unasemaje?” nilijikakamua kuzungumza ingawa moyoni niliamini kuwa ule ulikuwa uongo mtupu.

Rehema alishusha pumzi ndefu na kuinamisha uso wake chini, alionekana kufikiria sana.

“Una hakika unanipenda na unataka kunioa, Bilali?” aliniuliza akiwa kanikazia macho.

“Ndiyo, tena niko tayari siku yoyote, na ndiyo maana nilikuwa tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako!” niliongea kwa kujiamini huku nikimtazama Rehema bila kupepesa macho.

Rehema alinitazama kwa makini sana kwa kitambo kirefu, ilikuwa ni kama vile alikuwa akiyasoma mawazo yangu kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu.

“Sijaelewa, mwanzo ulitaka tuwe marafiki lakini sasa unataka kunioa, hivi haya unayoyasema yanatoka wapi, au unataka kunichezea tu umalize haja zako kisha…”

“Najua ni vigumu kuniamini, sijui niseme nini ili uniamini,” nilimkata kauli wakati alipokuwa akiendelea kuongea.

“Okay, naomba nikuulize maswali machache,” Rehema alisema huku akiendelea kunikazia macho.

“Niulize tu,” nilijibu kwa kujiamini.

“Kwa nini unadhani kuwa unanipenda?”

“Kwa sababu nakupenda, penzi halina sababu,” nilijibu kwa kujiamini.

“Una uhakika kuwa hunipendi kwa sababu yoyote ile nyingine?”

“Kama zipo sababu, basi nakupenda kwa sababu unazo sifa zote za mwanamke ninayetaka kumuoa.”

“Asante!” Rehema alisema huku akiachia mguno na baada ya hapo kikapita kitambo kirefu cha ukimya. Nilimuona akiwa anawaza mbali na sikujua alikuwa anawaza nini. Nikawa najiuliza ni wapi nilikotoa ule ujasiri wa kuyatamka yale yote niliyoyatamka kwa Rehema.

“Lakini, hujaniambia bado kama inawezekana au vipi!” nilivunja ukimya baada ya kuona Rehema yupo kimya.

“Unataka kuniambia hujaoa hadi sasa?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi.

“Sijabahatika,” nilimjibu kwa sauti tulivu.

“Kwa nini?”

“Kwa sababu Mungu bado hajanijaalia”

“Na wala huna girlfriend?”

“Ninaye!” nilijibu huku nikimkazia macho Rehema, nikamuona kashtuka kidogo ingawa hakutaka kuuonesha mshtuko wake.

“Sasa… kama una girlfriend nini tatizo hadi uanze kutanga tanga?”

“Wala sijatanga tanga kwani leo ndiyo mara ya kwanza naongea naye na hajui ni kiasi gani nampenda. Girlfriend wangu ni wewe Rehema!”

Haya tena, mambo si mambo... nini kitaendelea? Fuatana nami katika 'Laiti Ningejua'...
Mambo si mambo sasa. Naona Bilalli anatupa ndoano yake.....sijui rehema atanasa kweli?????


Asante sana Bishop

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laiti Ningejua! 25

Mtunzi Bishop Hiluka

“Unataka kuniambia hujaoa hadi sasa?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa udadisi.

“Sijabahatika,” nilimjibu kwa sauti tulivu.

“Kwa nini?”

“Kwa sababu Mungu bado hajanijaalia”

“Na wala huna girlfriend?”

“Ninaye!” nilijibu huku nikimkazia macho Rehema, nikamuona kashtuka kidogo ingawa hakutaka kuuonesha mshtuko wake.

“Sasa… kama una girlfriend nini tatizo hadi uanze kutanga tanga?”

“Wala sijatanga tanga kwani leo ndiyo mara ya kwanza naongea naye na hajui ni kiasi gani nampenda. Girlfriend wangu ni wewe Rehema!”

Endelea...

Rehema akataka kusema neno lakini nikamuona akisita. Aliyakwepa macho yangu yaliyokuwa yakimtazama kwa makini na kuangalia kando, kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Jambo unalohitaji kwangu ni jambo linalohusu maisha… yangu na yako vilevile, kwa hiyo halihitaji uamuzi wa papara,” alisema Rehema na alionekana kumaanisha kile alichokisema na kuendelea.

“Nahitaji muda wa kutafakari zaidi, nahitaji kukufahamu zaidi na kuufahamu ukoo wako kabla sijakubali au kukataa proposal yako. Najua hata wewe hunifahamu vya kutosha…”

“Ni kweli,” nilikubaliana na maneno yake ingawa moyoni sikuona sababu ya kuanza kuchunguzana wakati nilijua kabisa sitaweza kumuoa bali nilitaka kushiriki tendo tu na kumwacha kama wengine.

“Samahani, hivi wewe mwenzangu ni mzaliwa wa wapi?” nilijikuta nikimtupia swali.

“Kigoma.”

“Kigoma?” Nilimaka kwa mshangao huku nikiachia kinywa changu wazi.

“Ndiyo Kigoma… mbona umeshtuka?”

“Wewe ni kabila gani?” Nilimuuliza tena huku nikimkazia macho.

“Mmanyema, kwani vipi?”

“Ni mshtuko wa furaha kwa kuwa imeniongezea sifa nyingine nisiyoitegemea kwako wewe!”

“Sifa gani hiyo?”

“Wewe ni msichana wa kwetu, mimi pia kwetu ni Kigoma, mimi pia ni Mmanyema. Huwezi kujua, nimefurahi mno, Rehema!” nilisema huku nikihisi msisimko na ubaridi ukinitambaa mwilini mwangu.

Rehema alitabasamu tu bila kusema neno. Nikataka kusema neno lakini nikasita baada ya kumuona Bi Aisha akiingia pale sebuleni na kuketi kwenye sofa, kisha kisha mazungumzo ya kawaida ya kufahamiana zaidi yakatawala maongezi yetu.

Niliaga ili niondoke lakini Bi Aisha hakuniruhusu, aliniomba nisubiri chakula nile ndipo niondoke. Kwa kweli yule mama alikuwa mcheshi na mzungumzaji mzuri. Nilipoondoka pale ilikuwa yapata saa kumi za alasiri na moja kwa moja nilirudi nyumbani nikiwa nimefarijika sana.

Zilipita siku tatu tangu siku nilipokwenda nyumbani kwa kina Rehema na kukutana na mama yake, Bi Aisha, katika siku hizo tatu nilikuwa nashughulikia kongamano maalumu la kibiashara ambalo niliamini kuwa niliamini lingetengeneza fedha nyingi ambazo hatimaye zingenipa heshima zaidi mbele ya Rehema.

Siku ya nne nilikutana na Rehema na aliomba anitembelee nyumbani ninapoishi ili apafahamu. Sikupinga, nilimchukua hadi nyumbani na kumkaribisha ndani.

”Hapa ndipo ninapoishi, Rehema,” nilisema mara tu Rehema alipoingia ndani kwangu. “Ni padogo sana, lakini uwezo wangu ndipo ulipoishia.”

“Una maana gani?” Rehema aliniuliza huku kanikazia macho yake. Japokuwa nilishikwa na haya, lakini nilimudu kuunda tabasamu.

“Nyumba hii ni ndogo tofauti na ile ya kwenu, japo ninatamani sana kuishi maisha ya juu lakini siwezi kuishi kama mkurugenzi, ndiyo maana yangu,” nilisema na kushusha pumzi.

“Pia hii ni nyumba ya familia ambayo tumeachiwa mimi na brother wangu ambaye kwa sasa yupo South Africa. Nina hiki chumba kimoja na sebule, vyumba vingine tumepangisha,” nilizidi kujitetea mbele ya Rehema.

“Kupanga ni kuchagua, na sidhani kama huwezi kuishi kama hao wengine wakati wewe pia umesoma na huna kasoro yoyote!” alisema Rehema huku akiniangalia kwa makini.

“Ni kweli,” niliafiki. “Ila itabidi uvumilie tu maana pana joto kidogo, ila kwa huu mji wetu hilo si jambo la kushangaza.”

“Usijali…” alisema huku akiketi juu ya kochi dogo la sofa pale sebuleni kwangu. Kikakipita kimya cha kitambo kifupi.

“Kwani wazazi wako wapo wapi?” Rehema alinishtua kwa swali lake.

“Wapo Kigoma, wanaishi Mwanga mtaa wa Lumumba,” nilimwambia.

Tuliongea mengi sana siku ile na Rehema aliamua kushinda pale kwangu. Aliniuliza maswali mengi kuhusu maisha yangu binafsi na maisha ya familia yangu, nami bila ajizi nilimjibu kila swali alilouliza kwani nilijua alichokuwa akikitafuta.

Pamoja na kuwa na wakati mzuri wa kuongea na kufurahi nilijaribu sana kumuonesha kuwa nilimhitaji kwa ajili ya kushiriki tendo lakini Rehema alionesha msimamo wa kutokuwa tayari, nami niliheshimu msimamo wake kwa kuogopa kuonekana nilikuwa na papara.

Siku ile ukawa ndiyo mwanzo wa kuwa karibu zaidi na Rehema. Baadaye tukawa tukiwasiliana sana kwa simu, lakini siku moja Rehema alikuja tena nyumbani kwangu ingawa safari ile alinishtukiza maana alikuja bila kunitaarifu kama angekuja.

Ilikuwa ni siku ya Jumamosi na alinikuta nikiwa nafanya usafi ndani kwangu. Aliniambia kuwa alikuwa anapita tu akaona si vibaya akishuka kunisalimia, nikamkaribisha ndani kwa bashasha.

Hakuonesha kukaa sana lakini nami sikutaka kuipoteza nafasi ile hivyo tukiwa katikati ya maongezi nikaanzisha tena mazungumzo yaliyohusu uhusiano.

“Unajua Rehema, sifurahii aina ya maisha ninayoishi, ni ajabu kwamba katika maisha ni vitu vichache kati ya unavyovitaka ambavyo unavipata, vingi huvipati!”

“Hebu niambie Bilali, ni vitu gani katika maisha yako ambavyo hujavipata?”

Niliinamisha uso wangu kidogo nikijifanya kutafakari ingawa kimsingi sikuwa natafakari chochote, kisha nikanyanyua uso kumtazama.

“Nashukuru Mungu nimesoma kiasi cha haja, nimehitimu digrii ya Biashara katika Masoko, nimefungua kampuni na kufanikiwa kuajiari watu kadhaa na ninapata mahitaji yangu yote muhimu, lakini bado zipo haja nyingine zilizomo ndani ya nafsi yangu ninashindwa kuzipata!”

Rehema akacheka kidogo. “Kama zipi hizo?”

“Upendo…” nilijibu huku nikimtazama kwa makini.

“Unataka kuniambia kuwa familia yako hawakupendi?” Rehema aliniuliza huku akinitazama kwa mshangao.

“Familia inanipenda, lakini pendo ninalozungumzia hapa, ni lile ambalo ni tofauti na la baba, mama, dada au kaka!” nilisema huku nikiachia kicheko hafifu.

Rehema aliguna na kuangalia kando akijaribu kuyakwepa macho yangu, hata nilipojaribu kumchunguza sikuiona tashwishwi usoni kwake. Kisha nikamuona akiinuka kisha akaaga na kuanza kuondoka.

“Keti kwanza,” nilimwambia Rehema huku nikimzuia asiondoke.

Rehema alinitazama kwa makini kwa kitambo kisha alitii na kurudi kuketi kwenye kochi. Akabaki akinitumbulia macho.

Nilivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku nikiuma midomo yangu, nikajifanya nafikiria kidogo kisha nikamkabili Rehema kwa sauti tulivu.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk, marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
 
Laiti Ningejua! 26

Mtunzi Bishop Hiluka

Rehema aliguna na kuangalia kando akijaribu kuyakwepa macho yangu, hata nilipojaribu kumchunguza sikuiona tashwishwi usoni kwake. Kisha nikamuona akiinuka kisha akaaga na kuanza kuondoka.

“Keti kwanza,” nilimwambia Rehema huku nikimzuia asiondoke.

Rehema alinitazama kwa makini kwa kitambo kisha alitii na kurudi kuketi kwenye kochi. Akabaki akinitumbulia macho.

Nilivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku nikiuma midomo yangu, nikajifanya nafikiria kidogo kisha nikamkabili Rehema kwa sauti tulivu.

Endelea...

“Najua umenisisitiza kuwa na subira, lakini naomba tu nikwambie ukweli, moyo wangu umeshindwa kufanya hivyo ingawa umekuwa mvumilivu mno… Nilihisi kuna wakati pamoja na matendo yangu kwako ningefanikiwa kubadilisha hisia zako lakini naona unazidi kunikatisha tamaa!”

Rehema akaniangalia kwa umakini sana na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Niwie radhi… ninakuthamini, ninakuheshimu na ninakupenda vile vile, lakini siko tayari kwa jambo hilo kwa sasa… huo ni msimamo wangu na sidhani kama unaweza kubadilika,” alisema Rehema kwa sauti yenye utulivu lakini akimaanisha kile alichokisema.

“Lakini…” nilitaka kusema lakini Rehema alinikatiza kwa ishara.

“Suala la kufanya ngono kwa sasa halipo moyoni mwangu na wala halipo akilini mwangu… nasikitika Bilali!”

“Naheshimu msimamo wako, lakini nimeomba jambo ambalo naamini limo ndani ya uwezo wako… nikiamini mimi na wewe ni wachumba! Sasa… bado hujanipa sababu za wewe kukataa!”

Rehema aliinamisha uso wake chini akaonekana kutafakari sana kisha akainua uso wake kunitazama kwa makini. Kulikuwa na huzuni iliyoonekana wazi kwenye macho wake.

“Sababu… sababu zipo, kwanza dini hairuhusu!” alisema huku akiuma mdomo wa chini.

Nikatingisha kichwa changu kukataa. “Hicho ni kisingizio tu. Kwa vyovyote utakuwa na mtu wako, ila mimi unanizuga tu!”

“Sina mwanamume na wala sifikirii kuwa na mwanamume mwingine yeyote. Nimetokea kukupenda wewe tu… wewe ndiye mwanamume wa maisha yangu!” aliniambia. Nikamtazama kwa makini na kuuona ukweli wa maneno yake kwenye macho yake.

Hata hivyo, niliamua kumsogelea karibu zaidi nikamtazama moja kwa moja machoni huku nikimkazia macho.

“Thibitisha kama kuna ukweli katika maneno yako vinginevyo nitaamini vipi?”

Rehema akanitazama kwa makini kwa kitambo kirefu kidogo, kisha akashusha pumzi zake huku akinyanyua mabega yake juu.

“Sioni kwa nini niongope. Kama huniamini sawa, sina namna ya kukufanya ukubaliane na kila kitu nisemacho. Ila ninachojua ni kuwa wewe ndiye mwanamume wa maisha yangu, basi.” Rehema alisema na kuinuka.

“Kwa heri!” alisema na kuondoka akiniacha nimepigwa butwaa.

Donge la hasira lilinikaba kooni, nikarusha mikono yangu hewani kama ishara ya kukata tama kisha nikajibwaga juu ya kochi na kushusha pumzi ndefu huku nikisonya kwa hasira.

“Aende zake asinibabaishe. Kwani yeye nani hadi nimbembeleze sana!” nilijiambia na kusonya kwa hasira.

Japo Rehema alikuwa amenikasirisha lakini ukweli ni kuwa sikuwa mtu sahihi kwake, pamoja na kunihakikishia kuwa alinipenda bado nilimhitaji kwa sababu moja tu… ngono… nilitegemea akinivulia nguo zake tukashiriki tendo hamu yangu ingeisha na ningeachana naye.

Yaani nilitaka kuwa katika uhusiano na Rehema kwa sababu ya ngono tu lakini kilichoniudhi ni yeye kutokutaka kushiriki ngono na mimi. Alinikwepa sana hadi nikajisikia vibaya. Nikahisi huenda alikuwa ana mtu mwingine.

Sasa nikajikuta katika pepo mbaya, nikaamua kumwonesha hadharani kuwa nilikuwa na wanawake wengine. Jioni ya siku ile Rehema alinipigia simu lakini sikupokea, hata alipotuma meseji sikuzijibu, nilitaka kumuonesha kuwa nilikuwa nimechukia kutokana na kitendo chake.

Kitendo cha kutokupokea simu wala kuzijibu meseji zake kilinifanya niwe na uhakika kwamba kingemuumiza sana Rehema na kwa vyovyote kesho yake angekuja nyumbani kwangu, hivyo nilimpigia simu Tausi kumuomba aje nyumbani kwangu.

Tausi hakuwa na pingamizi lolote kwani aliisubiri nafasi ile muda mrefu ndiyo maana hakupinga na bahati nzuri siku ile alikuwa ameanza mapumziko baada ya kumaliza zamu ya usiku.

Tausi alikuwa anafanya kazi ya uuguzi katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), tulifahamiana wakati nilipokuwa nimelazwa pale baada ya ule mkasa uliotokea kule porini Kibiti.

Tausi ndiye mara nyingi aliniuguza nilipokuwa nimelazwa na alijitolea kwa kila hali kunihudumia hata pale alipokuwa hayuko zamu, jambo lililonivutia sana.

Ukawa mwanzo wa kufahamiana zaidi, kisha urafiki ukazaliwa na baadaye tukawa wapenzi. Nilipotoka hospitali tuliendelea kuwasiliana na alikuja nyumbani mara mbili ingawa hatukuwahi kushiriki tendo.

Tausi alikuwa mwanamke wa miaka kati ya ishirini na nane na therathini, alikuwa na umbo kubwa la kuvutia. Alikuwa mweupe kwa asili lakini pamoja na urembo wa asili bado alijiongezea kwa mapambo mengine ya gharama yaliyomfanya kuvutia zaidi.

Hakuwa mwanamke wa kumtizama mara moja tu ukamwacha kwani alivutia sana kutokana na umbo lake lililokuwa na mfano wa umbo la nyigu.

Usiku wa siku ile niliupitisha nikiwa na Tausi nyumbani kwangu na asubuhi ya siku iliyofuata tuliamka kama saa tatu tukiwa hoi.

Tausi aliandaa chai kisha tukaketi sebuleni kwa ajili ya kifungua kinywa, na tulipokuwa tukinywa chai, nilishtushwa na mlio wa gari lililosimama ghafla huko nje. Nikajua tayari mambo yalikwenda kama nilivyopanga.

Tausi alinishtukia akaniuliza, “Vipi baby, kuna nini?”

“Hakuna kitu… Vipi kwani?” Nilimjibu huku nikijaribu kusikilizia vizuri kama ni Rehema au alikuwa mtu mwingine.

“Nimesikia muungurumo wa gari, sitaki wageni saa hizi miye. Tukimaliza kunywa chai tukalale maana bado nina hamu na wewe. Kama kuna mgeni wako umwondoe mapema,” aliniambia Tausi kwa utani.

Nilimtazama nikatabasamu bila kusema neno. Mara nikaisikia sauti ya Rehema akisalimia na wapangaji pale kwenye korido kisha hatua za haraka zilikuja hadi kwenye mlango wangu, kisha zikasimama.

“Nani?” Tausi aliniuliza kwa sauti ndogo huku akifinya macho yake. Nilibetua mabega yangu na sikusema neno japo nilikwisha mjua aliyekuwa kasimama mlangoni.

Taratibu mlango wa pale sebuleni ulifunguliwa. Rehema akiwa amevaa sketi fupi nyeusi yenye miraba myeupe, blauzi ya bluu ya mikono mirefu na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio akaingia.

Itaendelea...
 
Laiti Ningejua! 27

Mtunzi Bishop Hiluka

Nilimtazama nikatabasamu bila kusema neno. Mara nikaisikia sauti ya Rehema akisalimia na wapangaji pale kwenye korido kisha hatua za haraka zilikuja hadi kwenye mlango wangu, kisha zikasimama.

“Nani?” Tausi aliniuliza kwa sauti ndogo huku akifinya macho yake. Nilibetua mabega yangu na sikusema neno japo nilikwisha mjua aliyekuwa kasimama mlangoni.

Taratibu mlango wa pale sebuleni ulifunguliwa. Rehema akiwa amevaa sketi fupi nyeusi yenye miraba myeupe, blauzi ya bluu ya mikono mirefu na viatu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio akaingia.

Endelea...

Mkononi alikuwa amevaa bangili nyingi za pembe na alikuwa amejimwagia mafuta mazuri yaliyosambaa chumba kizima. Alipoingia alisimama akitutazama kwa makini.

“Karibu Rehema,” niliongea huku nikiachia tabasamu. Sauti yangu ilikuwa tulivu sana. “Kutana na best wangu, Tausi…” nilimwambia Rehema kisha nikageuza shingo kumtazama Tausi, “Huyu ni dada yangu mpenzi, Rehema.”

Rehema aliachia tabasamu japo nilihisi halikuwa tabasamu halisi ila lilificha kitu ndani yake, alipiga hatua akaja kuketi kwenye kiti tupu karibu yangu huku akinitazama kwa makini kisha akayahamishia macho yake kwa Tausi.

Tausi akageuza shingo yake kunitazama kwa jicho la kuuliza lakini hakuthubutu kusema chochote. Niliachia tabasamu nikionekana kutobabaika kabisa, kikapita kimya kirefu, huku wanawake wote wawili wakinitazama kwa makini.

“Sijauelewa vizuri utambulisho wako, unaweza kunitambulisha tena huyu ni nani?” Rehema aliniuliza kwa sauti tulivu.

“Mwanamke,” lilikuwa jibu langu.

“Najua kuwa ni mwanamke, lakini nataka kujua yeye ni nani?”

“Nimeshakwambia anaitwa Tausi, hayo mengine wayatakia nini?” niliongea kwa kufoka.

Rehema alinitazama kwa makini, nikayaona machozi yakimlenga lenga kwenye macho yake, hakutaka kuendelea kukaa pale aliinuka na kuondoka haraka, akafungua mlango na kutoka kisha nikasikia muungurumo wa gari yake ilipokuwa ikiondoka na kupotelea mtaani.

Kwa kiasi fulani moyo wangu uliridhika kwa kitendo nilichomfanyia Rehema nikiamini kuwa baada ya siku ile angeniheshimu, maana nilijua kuwa alikuwa ananiona bwege. Moyoni mwangu nikaahidi kuendelea na vimbwanga vya hapa na pale hadi anyooke.

Tausi alinitazama kwa kitambo bila kusema neno, nilijua kuwa alikuwa amejisikia vibaya sana kwa kile kilichotokea kwa mwanamke mwenzake, japo sikujali, nilijitahidi kumsemesha lakini alibaki kimya akinitazama kwa makini. Kisha alishusha pumzi ndefu.

“Bilali, najua wewe ni kijana mtanashati sana na kila mwanamke angependa kuwa na wewe, lakini nimehuzunika sana kwa kuwa sipendi kugombanisha wapendanao, usingefanya uliyofanya, mimi ningeweza kuwapisha badala ya hiki kilichotokea,” Tausi alisema kwa uchungu.

Nilimtoa wasiwasi kuwa Rehema hakuwa mpenzi wangu bali tulizoeana tu kwa kuwa nilimsaidia kwenye lile tukio la kule Kibiti. Nilimsimulia kuhusu tukio zima lilivyokuwa na jinsi nilivyomuokoa Rehema hadi pale polisi walipokuja na mimi kupoteza fahamu.

Tausi aliamua kukubali yaishe lakini hakuonekana kuridhika na maelezo yangu.

Baada ya siku ile ilipita wiki nzima nikiwa sina mawasiliano na Rehema ingawa ukweli sikutaka uhusiano wetu uishie katika hali ile, niliamini kuwa Rehema alikuwa ananipenda ingawa sikujua kwa nini hakuwa tayari kushiriki tendo, bila sababu zozote za msingi.

Japo chozi la Rehema liliniumiza sana siku ile lakini sikujali. Kwa nini alikuwa ananinyima penzi? Nilijiuliza nikakosa majibu. Hatimaye nikafikia uamuzi wa kuachana naye. Lakini tatizo lilikuwa ningeachana naye vipi bila kumjua ladha yake?

Nilijiapia kuwa jambo hilo lisingewezekana hata kidogo, mimi kama mwanamume kamili angenitangaza kwa marafiki zake, kuwa sijawahi kulala naye tukafanya tendo. Ingekuwa aibu kubwa kwangu!

Ndiyo maana ilipopita wiki na Rehema hakuwa amenitafuta niliamua kujishusha, niliacha shughuli zangu na kwenda kwao kumtafuta. Nilipokuwa nakaribia nyumbani kwa kina Rehema mita chache mbele yangu nikawaona wanawake wawili waliokuwa wanatokea upande niliokuwa naelekea.

Nilishtuka kidogo nikiwa siamini macho yangu kuwa niliowaona mbele yangu ni Jameela na mwanamke mwingine wa makamo aliyekuwa na umbo kubwa lililovutia. Mwanamke yule alikuwa mrefu kama alivyokuwa Jameela na alikuwa mwarabu.

Mara moja nikagundua kuwa huyo ndiye yule shangazi yake aliyekuwa akinielezea habari zake. Mwanamke yule alikuwa na macho makubwa mazuri yaliyoambatana na kope nyingi nyeusi ambazo zilizoachia nafasi kwa nyusi ili zipate kujidai, na midomo yake ilikuwa minene yenye kingo nyepesi na mikunjo midogo midogo.

Jameela aliponiona aliongea kitu kwa yule mwanamke kwa sauti ya chini kisha akainua mikono yake kunipokea kwa uchangamfu.

“Wow Bilali,” alisema kwa bashasha huku akinipokea na kuongeza, “habari za nyumbani kwako?”

“Nzuri tu Jameela, sijui nyinyi?”

“Sisi tu wazima… kutana na shangazi yangu, Bi Aisha…” alinitambulisha kwa yule mama kisha alimgeukia, “Shangazi, kutana na Bilali Ibrahim, yulee…” alisema na kuachia kicheko hafifu, wote wakacheka.

Bi Aisha akanyoosha mkono wake na kunisalimia kwa bashasha huku akiachia tabasamu pana usoni kwake.

“Nimefurahi sana kukufahamu, maana kila siku nilikuwa najiuliza huyu Bilali yukoje maana tulikuwa hatuli wala hatulali, kila siku Bilali, Bilali!!” yule mwanamke aliongea kwa sauti ya kishambenga na kuendelea.

“Pole sana kwa mkasa uliokupata.”

“Nimekwisha poa, shikamoo,” nilimwamkia yule mama huku nikiwa na haya usoni kwangu.

“Marhaba… karibu nyumbani kwetu,” aliitikia huku akinikaribisha kwa ukarimu mno na kunionesha kwa kidole ilipo nyumba yao.

Nilishtuka sana maana nyumba aliyonionesha ilikuwa imepakana na nyumba aliyokuwa akiishi Rehema na mama yake mkubwa. Pia nilishtushwa sana kwa kuwa hata yeye pia aliitwa Bi Aisha.

“Twende ukapaone nyumbani kwetu, au kuna sehemu ulikuwa unaelekea?” aliniuliza Jameela baada ya kuona nipo kimya nikiwa nimenywea.

Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani, nikatingisha kichwa. “Kuna mtu ninakwenda kumuona mara moja, ni muhimu sana maana muda wote ananisubiri mimi,” niliamua kuongopa ingawa ukweli nilikuwa nakwenda kwa Rehema.

Waliridhishwa na uongo wangu, lakini Jameela alisema kuwa baadaye angekuja nyumbani kuniona. Niliondoka nikiwa na maswali mengi kichwani, sikuwa nimefikiria kabisa kukutana na Jameela katika mazingira yale, nikawaza sana kuwa kumbe Jameela na Rehema walifahamiana!

Na kweli baadaye Jameela alikuja nyumbani na kuniambia kuwa alikuja kuniaga kwa kuwa harusi yake ilikuwa imekaribia, alisema kuwa alitafuta kila njia ya kuja ili tuagane na alikuja kulala kwangu na kesho yake angerudi Kibiti kwa ajili ya kukaa ndani kama ilivyokuwa desturi yao.

Nilipomuuliza kuhusu shangazi yake Jameela aliniambia kuwa anajua kila kitu na ni msiri wake, hivyo sikutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.

Aliichukua simu yangu na yake akazifungia ndani ya kabati. “Sihitaji simu yoyote saa hizi, leo ni mimi na wewe tu hadi lyamba,” alisema Jamila huku akitoa kila kitu na kubakiwa na nguo ya ndani tu, kisha akajibwaga juu ya kitanda.

Itaendelea...
 
Laiti Ningejua! 28

Mtunzi Bishop Hiluka

Na kweli baadaye Jameela alikuja nyumbani na kuniambia kuwa alikuja kuniaga kwa kuwa harusi yake ilikuwa imekaribia, alisema kuwa alitafuta kila njia ya kuja ili tuagane na alikuja kulala kwangu na kesho yake angerudi Kibiti kwa ajili ya kukaa ndani kama ilivyokuwa desturi yao.

Nilipomuuliza kuhusu shangazi yake Jameela aliniambia kuwa anajua kila kitu na ni msiri wake, hivyo sikutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.

Aliichukua simu yangu na yake akazifungia ndani ya kabati. “Sihitaji simu yoyote saa hizi, leo ni mimi na wewe tu hadi lyamba,” alisema Jamila huku akitoa kila kitu na kubakiwa na nguo ya ndani tu, kisha akajibwaga juu ya kitanda.

Endelea...

Nami nilitoa nguo zangu nikabakiwa na boksa tu kisha nikamfuata pale kitandani. Niliisikia simu yangu ikiita lakini Jameela alinizuia, akanisukumia kitandani kisha alikuja akakaa juu yangu na kuanza kunibusu, nami nikijibu mapigo kwa kumpapasa nyama za mgongo.

Jameela akaanza kutweta kwa ashki huku akionekana kuhisi faraja iliyopenya hadi kwenye mishipa yake ya damu.

Tulichukua muda mrefu tukipapasana na kugusana hapa na pale, na nilimgeuza na kumweka chini kisha nikakaa juu yake na kuendelea kumpapasa, alitulia akiwa amefumba macho yake huku akihema kwa nguvu. Nikapeleka ulimi wangu kwenye sikio lake, Jameela akaonekana kusisimkwa na kuachia kicheko.

Mara nikahisi kama mlango wa sebuleni ukifunguliwa taratibu, nikashtuka na kutulia nikisikiliza kwa makini. Sikusikia chochote maana ukimya ulitawala, nikadhani labda yalikuwa mawazo yangu tu na hakukuwa na chochote.

Nikapeleka tena ulimi wangu kwenye sikio la Jameela, akaonekana kusisimkwa tena na kucheka, muda ule ule mlango wa chumbani kwangu ukagongwa na kukatiza kicheko cha Jameela.

Mimi na Jameela tukashtuka sana na kukodolea macho kwenye ule mlango, kisha Jameela akanitazama katika namna ya kuniuliza kama nilikuwa namjua aliyekuwa anagonga ule mlango. Sikuwa na jibu.

Kwa sekunde kadhaa mle chumbani kukawa na ukimya mzito. Mlango ukagongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi.

“Nani?”

Hakuna aliyejibu. Nikashangaa zaidi na kumtupia jicho Jameela ambaye alibaki kimya akinitazama kwa makini.

“Wewe nani?” niliuliza tena huku hasira zikianza kunipanda.

Lakini mgongaji aliendelea kukaa kimya, kisha nikaona kitasa cha mlango kikinyongwa na mlango ukasukumwa na kufunguka. Bila kusita Rehema akaingia chumbani na kusimama akituangalia pale kitandani, akapigwa butwaa.

Jameela naye alishtuka sana kumuona Rehema, wakabaki wametazamana kwa mshangao kama majogoo yaliyotaka kupigana. Nilimuona Rehema akiwa katika mshtuko mkubwa, midomo yake ilikuwa inamtetemeka.

Kwa nukta chache moyo wangu ulisahahu mapigo yake na yalipoanza tena nilivuta pumzi ndefu, nikazishusha. Nilimtupia jicho Rehema huku nikijaribu kujibaraguza.

“Jameela!” Rehema aliita kwa mshangao mkubwa huku akimkodolea macho Jameela na kubaki mdomo wazi akiwa haamini kumuona pale.

“Rehema!” Jameela naye aliita huku akionesha mshtuko mkubwa sana, kisha akageuza shingo yake kunitazama akionekana kuwa na maswali mengi.

Mimi nilibaki kimya nikiwa nimetahayari sana. Ingawa sikushangaa sana kuona kuwa Rehema na Jameela walikuwa wanafahamiana lakini sikutegemea kuwa wangekutana nyumbani kwangu.

“Unasemaje?” hatimaye nikajikakamua na kuumuliza Rehema.

Rehema alibaki kimya, midomo yake ilikuwa inamtetemeka. Machozi yakaanza kumtiririka mashavuni. Jameela alishindwa kusema chochote na kubaki anashangaa, alitutazama mimi na Rehema kwa zamu akiwa haelewi kilichokuwa kinaendelea, kisha akajiinua na kuketi kitako kitandani huku akiufunika mwili wake kwa shuka.

“Bilali, mbona sielewi, kwani kuna nini kinaendelea hapa? Au…” Alishindwa kumalizia sentensi yake akashusha pumzi akiwa hajui aseme nini.

Nilibaki kimya nikiwa nimetahayari. Rehema akashusha pumzi za ndani kwa ndani, alijaribu kuyazuia machozi yaliyokuwa yanaendelea kumtiririka bila mafanikio. Akajikuta akilia kwa uchungu mbele yangu na Jameela.

“Bilali kwa nini hukuniambia kama wewe na Jameela ni wapenzi, kwa nini siku zote ulikuwa unaniongopea kuwa unanipenda kumbe una mpenzi?”

Niliendelea kuwa kimya nisijue la kufanya. Jameela alinitupia jicho akiwa amekasirika sana, lakini alikuwa akiyakwepa macho ya Rehema.

“Ndiyo maana nakupigia simu hupokei! Ni bora ungenieleza ukweli wala nisingesumbuka hata kuja hapa…”

Rehema alikuwa analia kwa uchungu mbele yangu, kisha aliniambia kwa uchungu kabla hajatoka, “Nakupenda sana Bilali na wewe unajua hilo… wewe ni mwanaume wa maisha yangu, ila kwa hiki ulichonifanyia nashukuru sana na kwa heri.”

Rehema alisema na kugeuka, akatoka taratibu na kuufunga mlango nyuma yake. Chozi lake liliniumiza sana, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilihisi hatia moyoni mwangu lakini sikuweza kuonesha chochote mbele ya Jameela.

Rehema alipotoka tu Jameela akasimama huku akiniangalia kwa hasira na kushika kiuno. “Naomba uniambie ukweli, nini kinaendelea kati yako na Rehema?”

“Sina uhusiano wowote na Rehema. Huyu ni mtu niliyemuokoa siku ile ya mauaji kule Kibiti basi lakini hakuna kinachoendelea, naona anajigonga kwangu hadi kero!”

“Anajigonga? Siyo kwa Rehema ninayemjua! Rehema huwa hana mpango na wanaume, kwanza nimeshangaa kumuona hapa!”

“Kwa hiyo huniamini au vipi, nakwambia sina uhusiano wowote na Rehema…” nilikuwa naongea kwa sauti bila kujua kuwa kumbe Rehema hakuwa ameondoka, alikuwa amesimama sebuleni nje ya mlango.

“Nashukuru sana, kumbe mimi najigonga kwako!” Nikashtushwa na sauti ya Rehema iliyosikika kutokea pale sebuleni. Kisha nikausikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa na kubamizwa kwa nguvu.

Nilijisikia vibaya sana ingawa nafsi nyingine ilinikumbusha kuwa nilikuwa katika uhusiano na wasichana wale kwa sababu moja tu… ngono… na kwa kuwa Rehema hakutaka kushiriki ngono na mimi na alionesha kunikwepa sikuona kwa nini nisiwe na wengine.

Niliinuka na kufungua mlango wa chumbani nikachungulia pale sebuleni lakini nilipotazama sikumuona Rehema kwani alikuwa amekwisha ondoka.

Wakati huo Jameela alisimama nyuma yangu akinitazama kwa hasira huku machozi yakimtoka. Alianza kuvaa nguo zake lakini nikamzuia.

“Jameela, naomba unisikilize basi…”

“Sina haja… mfuate Rehema labda atakusikiliza!”

Nilimsogelea Jameela nikaupeleka mkono wangu wa kulia kwenye uso wake kwa uangalifu huku nikiachia tabasamu la kumlainisha, si kwa kulazimisha. Jameela aliusukuma mkono wangu kwa hasira na kurudi nyuma hatua moja huku aking’aka. “Usiniguse!”

Niliminya midomo yangu huku nikimtazama Jameela kwa uchungu. Jameela alisonya kwa hasira na kuuendea mlango, akaufungua na kutokea sebuleni lakini nikawahi kumzuia asifungue ule mlango wa sebuleni na kutoka nje.

“Sikiliza Jameela,” nilianza kusema huku nimejiegemeza kwenye ule mlango kumzuia Jameela asitoke. Jameela alibaki kimya akinitazama kwa chuki.

“Ukweli ni kwamba, unajua mimi ni bachela na wewe tayari una mtu na siku si nyingi mtafunga ndoa na kwenda kuishi Uarabuni…” nilisema huku nikimkazia macho. Jameela alinitazama kwa makini bila kusema neno.

“Hivi umejiuliza nitaishi vipi bila wewe au unadhani mimi sina wivu? Nimekubali matokeo na sioni sababu ya kuona wivu, kwa nini wewe ufanye hivi? Kumbuka umekuja tuagane, sasa kama kuagana kwenyewe ni kwa staili hii sawa, nakuruhusu uende,” nilisema kwa uchungu huku nikimpisha aondoke.

Jameela alinitazama kwa makini nikauona uso wake ukikunjuka na zile hasira zikaanza kuyeyuka, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kujipweteka juu ya kochi.

Mambo ndiyo yanazidi kunoga, sijui nini kitaendelea?...
 
Ahsante sana Bishop...

Bilal kazingua sana kwa Rehema, kakosa uvumilivu.. Angeenda nae taratibu mwisho wa siku angetunukiwa papuchi..

Nilishawahi kuifuatilia papuchi miaka mitatu, nikiwa nae najidai nauhitaji wa papuchi... Kumbe namchora tuu, pembeni nakula hivo visimi hatari...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom