Bishop tunaomba tena jaman
Clkey nikupe mbinu ya kumleta
Bishop Hiluka..!?
Bishop Hiluka si mtu rahisi kumpata.. Yupo na majukumu mengi sana.. Kuonekana hapa ni mara chache sana..
Ila kama kawaida, hakuna mkate mgumu mbele ya chai.. Kuna njia ya kumleta Bishop hapa tena kwa kasi ya kimbunga hata kama alikua usingizini..
the_legend kuna ndugu yetu
Clkey anahitaji 'kizungumkuti' iendelee, tumpe njia.!??
Hahahaa, kwa kua
Clkey ameonesha nia ya dhati muelekeze tu njia pekee ya kummudu
Bishop Hiluka, njia ambayo imetumiwa na Jacky/
Shunie kwa mafanikio makubwa sana
the Legend☆
😀😀😀 Hahaaaa... yaani
the_legend na
Tater ni wambea nyie sijapata kuona, duh! Hakyanani nimewavulia kofia! Haya ngoja nishushe moja...
Kizungumkuti! - 24
Na Bishop Hiluka
“Kichwa changu kimevurugwa kabisa,
I real need someone to talk to, to comfort me,” aliwaza na mara ya Jacky ikamjia
“
Oh Belinda! I need to talk to her… Dah, sura ya Belinda toka niliponana naye jana asubuhi imeshindwa kabisa kunitoka kichwani. Ninamuwaza kila dakika. Yawezekana ni kutokana na uzuri wake na kasheshe zake za usiku kucha, kwa kweli sikutegemea kama ana uwezo mkubwa kiasi kile na kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimepata mwanamke ambaye amenikimbiza mchaka mchaka kiasi kile… isitoshe ni mtoto mzuri mno. Ameumbwa akaumbika…”
Mawazo ya Yusuf yalikatizwa na sauti kali za breki ya gari lililokuwa likiyumba kumkwepa. Yusuf aliogopa sana akajikunja na kuruka juu huku akitua kando ya ile barabara akiwa amefumba macho yake. Kutokana na kuzidiwa na mawazo alijikuta akivuka barabara ile ya Lumumba pasipo hata kuangalia kulia na kushoto kwake.
Endelea...
Lile gari lilisimama katikati ya barabara na wakati huo huo dereva wa lile gari alishusha kioo cha gari na kumtazama Yusuf huku akionekana kukasirishwa sana. Lilikuwa ni gari la zuri aina ya
Toyota Lexus RX la rangi nyeusi.
“
What’s wrong with you guy, how do you cross the road without looking right and left?” (We bwana una matatizo gani, unavukaje barabara bila kutazama kulia na kushoto kwako?) yule dereva alifoka kwa ukali huku akimkazia macho Yusuf.
Yusuf aligeuza kichwa chake kumtazama yule dereva huku akiwa na uso uliosawajika sana, mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kwa kasi isivyo kawaida kutokana na mshtuko mkubwa alioupata baada ya kunusurika kugongwa.
“
Forgive me, brother, it’s just family problems…” (Niasamehe, kaka, ni matatizo tu ya kifamilia…)
“
Do not bring your family’s problems to the road…” (Matatizo ya familia yako usiyalete barabarani…) yule dereva alimkata kauli Yusuf kwa hasira lakini akaonekana kusita ghafla baada ya kuhisi kumfahamu Yusuf. Akamkazia macho akimwangalia kwa makini.
Yusuf naye alimtazama yule dereva kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kikapita kitambo kifupi kila mmoja akimtazama mwenzake, na kila mmoja alihisi kumfahamu mwingine.
“Yusuf!” yule dereva aliita kwa shauku huku akizidi kumkazia macho Yusuf.
“Jacob!” Yusuf aliita huku akilisogelea lile gari, wakasalimiana kwa furaha.
“
What’s wrong with you, brother?” (Una shida gani, ndugu?) Jacob alimuuliza Yusuf baada ya kumtazama kwa makini na kugundua kuwa hakuwa sawa, japo alijilazimisha tabasamu lakini macho yake hawakuficha huzuni aliyokuwa nayo. Alikuwa akilengwa na machozi.
“
Hmm, just leave as it is. Dunia hii ina mambo, kaka,” Yusuf alisema kwa huzuni huku akishusha pumzi.
Muda ule ule madereva wa magari mengine yaliyokuwa nyuma ya gari la Jacob walianza kupiga honi kumtaka Jacob aondoe gari lake kwani alikuwa amesimamisha gari lake katikati ya barabara na hivyo kusababisha msongamano wa magari nyuma yake.
Jacob alishtuka na kuangalia nyuma yake kupitia kwenye kioo cha gari cha katikati, akayaona yale magari ya nyuma yake yakimuwashia taa kumuashiria aondoe gari lake barabarani. Jacob alishusha pumzi na haraka kutoa
business card na kumpatia Yusuf.
“
If you get a chance, call me my brother, so we can talk,” (Ukipata nafasi nipigie ndugu yangu, ili tuongee) Jacob alisema na kuliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi na kusababisha kelele za msuguano wa magurudumu yalipokuwa yakiserereka barabarani.
Yusuf alibaki amesimama akilisindikiza lile gari kwa macho hadi lilipopotea kwenye macho yake. kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuitazama ile kadi aliyopewa na Jacob na kuanza kuondoka taratibu kuelekea zilipo ofisi zake.
Wakati akitembea mawazo yake yalihamia kwa Jacob, aliwaza kuhusu utofauti wa kipato uliokuwepo kati yake na Jacob, japo walisoma darasa moja na yeye Yusuf alikuwa anamzidi Jacob katika masomo ya darasani.
Jacob Haule na Yusuf walikuwa wamesoma pamoja
Tambaza High School na baadaye wakaenda wote katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam. Walipomaliza Jacob alipata nafasi ya kwenda nchini Uingereza alikosomea shahada ya umahili ya sanaa katika uongozi wa masoko (
Master of Arts in Marketing Management).
Alipomaliza masomo yake alifanya kazi huko huko Uingereza kwa miaka miwili kisha akarudi nchini na kuajiriwa katika kampuni moja kubwa ya simu kama mkurugenzi wa masoko na alikuwa akilipwa mshahara mkubwa mno.
“Dah, sijui na mimi nifanye nini ili nifanikiwe kama Jacob, maana haya si maisha bali inaonekana kama sisi wengine tupo duniani kwa ajili ya kuwasindikiza wenzetu tu…” sasa kichwa cha Yusuf kilionekana kujaa mawazo mengi sana, mara akamkumbuka tena Jacky.
“Hmm! Hapa ndipo ninapoona umuhimu wa Belinda. Nikimtumia yule msichana naweza kutoka… yaani nashindwa kabisa kumtoa mawazoni mwangu na sikujua kama ni msichana mtundu kiasi kile. Sijui kajifunzia wapi yale mambo maana anaonekana ni mtoto wa geti kali,” Yusuf alizidi kuwaza na mara akajikuta akitabasamu.
“
She’s so sweet, I didn't even expect that one day I was going to betray my marriage, for the first time I have failed to be bold in my position before Belinda,” (Mtamu sana, sikutegemea kama siku moja ningeweza kuisaliti ndoa yangu, kwa mara ya kwanza nimeshindwa kuwa jasiri wa msimamo wangu mbele ya Belinda) Yusuf aliendelea kuwaza na muda ule ule akawa amefika ofisini kwake kwenye jengo la Benki ya Biashara tawi la Lumumba.
“
By the way, flies dies on the wound,” (Hata hivyo, nzi hufia kwenye kidonda…” Yusuf alitamka maneno yale na kujikuta akitabasamu huku akiwapita bila kuwasalimia wafanyakazi wenzake walioonekana kuongea na kutaniana wakiwa furaha asubuhi ile.
Wale wafanyakazi wakageuka kumtazama kwa mshangao, walimsalimia lakini alionekana yuko mbali sana kimawazo huku akionekana kuongea peke yake. Wale wafanyakazi wakapigwa na butwaa na kubaki wakitazamana bila kupata jibu.
* * * * *
Saa kumi na mbili jioni ya siku ile iliwakuta Carlos na Jacky wakiwa nyumbani kwa Jasmine katika mtaa wa Butiama eneo la Vingunguti. Jioni ya siku ile hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepoa zaidi kutokana na manyunyu hafifu ya mvua yaliyokuwa yakianguka kutoka angani kulikotanda wingu zito la mvua.
Lakini pamoja na hali ile ya manyunyu bado haikuwazuia watu kurandaranda mitaani huku kila mmoja akiwa kwenye pilika pilika zake.
Jasmine alikuwa akiishi katika nyumba ya kawaida aliyokuwa ameachiwa na baba yake, nyumba ile ilikuwa ya vyumba vinne, sebule, jiko, choo na bafu, na ilikuwa imezungushiwa ua mkubwa.
Alikuwa msichana wa umri wa miaka ishirini na tano, alikuwa mrefu kiasi na mwenye weusi wa kung’aa usiochusha, kichwani alikuwa na nywele nyingi mfano wa mmanga, zilizosukwa kwa mtindo wa yeboyebo na kumwagika mgongoni.
Jioni ile Jasmine alikuwa amevaa gauni fupi la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa
pencil dress na lilionekana kumkaa vizuri sana mwilini huku likiuchora vyema mwili wake matata wenye umbo la kuvutia. Miguuni alikuwa amevaa
sandals ngumu za ngozi zilizokuwa zimeshikilia kwenye miguu yake mizuri kwa kamba.
Jasmine alikuwa na uso wa mviringo na sura ya kitoto isiyoishiwa tabasamu muda wote huku macho yake makubwa na legevu ya kike yakiongezea mvuto wa sura yake. Pua yake ilikuwa ndefu na midomo yake ilikuwa laini yenye kingo pana kiasi zilizopakwa rangi nzuri ya mdomo.
Muda ule Jasmine alikuwa kaketi sebuleni kwake akiwasikiliza wageni wake Jacky na Carlos waliofika kumtembelea katika ugeni ule wa ghafla ambao hakuwa ameutarajia kabisa.
Je, Carlos na Jacky wanataka kumwambia nini Jasmine, na kwa nini wamfuate yeye? Endelea kufuatilia simulizi hii ya aina yake ya kusisimua...