Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Kizungumkuti! - 16

Na Bishop Hiluka

“Kwa nyinyi wenzetu mnaochezea fedha kila siku wala si ghali sana. Ni shilingi laki tatu na elfu hamsini tu kwa usiku mmoja, unapata bia mbili bure na chai ya asubuhi. Unaonaje?” Jacky alisema huku akiachia kicheko hafifu.

Yusuf alitaka kusema neno lakini akasita na kushusha pumzi za ndani kwa ndani huku akitingisha kichwa chake taratibu na kumtupia jicho yule mhudumu wa ile hoteli, ambaye muda wote alikuwa amesimama akiwatazama kwa zamu huku akitabasamu.

Jacky aligundua kuhusu hilo na kubetua mabega yake juu huku akiendelea kutabasamu.

Endelea...

Anyway, what will you drink?” (Hata hivyo, sijui utakunywa nini?) Jacky alimuuliza Yusuf akiwa bado amemkazia macho.

Castle baridi itapendeza,” Yusuf alijibu huku akiketi juu ya kochi mojawapo la sofa.

“Tuletee chupa mbili za castle baridi na chupa kubwa ya whisky,” Jacky alimwambia yule mhudumu aliyekuwa bado amesimama kimya akingoja kupewa oda.

“Vinywaji hivyo vyote vimo ndani ya hilo jokofu, labda kama mnahitaji huduma nyingine kama chakula,” alisema yule mhudumu huku akielekeza kidole chake kwenye lile jokofu dogo.

“Okay, basi tukihitaji chochote nitakupigia simu,” alisema Jacky huku akiachia tabasamu kisha akainuka na kwenda kufungua lile jokofu akatoa chupa mbili za Castle, bilauri mbili na chupa kubwa ya whisky.

Yule mhudumu aliachia tabasamu pana la kirafiki na kuondoka, Yusuf alimtazama Jacky kwa makini na kushusha pumzi zaa ndani kwa ndani. “Niliona nibahatishe kukupigia simu ingalau nisikie sauti yako,” alivunja ukimya.

“Yaani ulitaka usikie sauti tu, basi!” Jacky aliuliza huku akiangua kicheko hafifu kisha akaviweka vile vinywaji juu ya ile meza ndogo fupi ya mbao. Yusuf alitabasamu tu bila kujibu kisha akainamisha kichwa chake akionekana kufikiria mbali, huku akionekana kumtupia jicho la wizi Jacky kwa matamanio.

“Haya sauti yangu tayari umeshaisikia na mimi mwenyewe ndiyo niko hapa hapa mbele yako, tena tukiwa peke yetu, unasemaje?” Jacky alisema na kuangua tena kicheko hafifu.

“Kwani ninalo tena!” lilikuwa jibu fupi la Yusuf lililomaanisha kuwa alikuwa amesalimu amri huku akiinamisha sura yake kutazama chini kwa aibu.

Hata hivyo, Yusuf alikuwa akihisi joto kali la mwili lililosababisha kijasho jembamba kianze kumtoka licha ya kuwa mle ndani kulikuwa na kiyoyozi kilichokuwa kikitoa ubaridi mkali. Alianza kuhisi mapigo ya moyo wake yakibadili mwendo wake na kwenda mbio isivyo kawaida!

Aliilamba midomo yake iliyoanza kukauka huku akianza kuhisi pumzi zake zikimpaa na kuanza kuhema kwa nguvu kama mtu aliyekosa hewa safi ya oksijeni, alifungua vifungo vya shati lake na kubaki kifua wazi. Muda wote huo Jacky alikuwa akimtazama kwa makini kisha akaachia tabasamu.

“Kama unahisi jasho livue kabisa halafu njoo uketi hapa kitandani,” Jacky alimwambia Yusuf huku akimuonesha kwa mkono sehemu ya kukaa karibu yake.

Yusuf hakupinga alilivua lile shati na kulitupia juu ya kochi jingine la sofa kisha akainuka na kwenda kuketi pale kitandani sehemu aliyooneshwa na Jacky.

Jacky alifungua zile chupa za bia, akamimina pombe kwenye bilauri zote mbili, kisha bilauri moja alimpa Yusuf na nyingine aliishika mkononi. Akanyoosha mkono wake kumwelekea Yusuf, wakagongesha zile bilauri.

Cheers!” walisema kwa pamoja wakitakiana heri na kuangua kicheko hafifu.

Yusuf aliinua ile bilauri akapiga funda moja kubwa la bia na kusisimkwa mwili wake. Alipoishusha ile bilauri alimtazama Jacky kwa tabasamu.

“Hivi una muda gani wa kazi pale benki?” Jacky alimuuliza Yusuf huku akipiga funda la bia na kuiweka ile bilauri juu ya meza.

“Nina miaka minne,” Yusuf alisema huku akiinua tena bilauri ya bia. Jacky alimtazama kwa makini kwa kitambo kifupi kisha akaitazama pete ya harusi iliyokuwa kidoleni kwake na kuachia tabasamu.

Are you married? I can see you have a wedding ring,” (Umeoa? Naona una pete ya harusi) Jacky alisema huku akiangua kicheko hafifu.

To be honest… I have a wife and a kid. Kwani vipi?” (Kusema kweli… nina mke na mtoto) aliuliza Yusuf huku akimkazia macho Jacky.

“Aah, napenda tu kujua nipo na mwanamume wa aina gani, mbona wewe kwenye simu uliniuliza kama nimeolewa!” Jacky alijibu kwa madaha huku akijipinda kumtazama Yusuf kwa mahaba. Walibaki wametazamana kwa kitambo fulani na kujikuta wote wakiachia tabasamu lililozaa kicheko.

“Hivi umepanga au unaishi katika nyumba yako?” Jacky aliuliza tena baada ya kile kicheko kukoma huku akimkazia macho Yusuf.

“Sijafanikiwa kujenga, pesa ngumu sana siku hizi, si unajua tena awamu hii ya hapa kazi tu jinsi inavyokaba kila kona…” Yusuf alisema na kuangua kicheko hafifu.

“Najua, ila kila kitu kinataka mipangilio. Je, una gari?” Jacky aliuliza tena lakini kabla Yusuf hajajibu, simu yake ya mkononi ilianza kuita.

Yusuf alishtuka na kuitazama kwa makini, akaonesha kusita kidogo huku akimtupia jicho Jacky. Hata hivyo Jacky alimuashiria kuwa aipokee tu, Yusuf aliichukua na kubofya kitufe cha kupokelea na akuiweka kwenye sikio.

“Eh mama Jasmine!” Yusuf alisema mara tu alipoiweka ile simu kwenye sikio.

“Uko wapi, baba Jasmine? Huku Jasmine ananisumbua sana!” sauti ya mke wake ilisikika ikilalamika kutoka upande wa pili wa simu.

“Kwani homa imemrudia tena?” Yusuf aliuliza kwa wasiwasi huku akimtupia jicho Jacky.

“Wala hana homa, ila hataki kulala mpaka akuone,” sauti ya mke wake ilisikika tena ikilalamika.

Okay, nipo sehemu nina kikao kidogo na rafiki zangu, nitarudi mara tu nikishamaliza kikao, kama nusu saa hivi inayokuja,” Yusuf alisema na kukata simu kisha alimtupia jicho Jacky huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Is that your wife?” (Ni mkeo huyo?) Jacky alimuuliza Yusuf huku akionekana kutabasamu.

Yusuf alikubali kwa kubetua kichwa kisha akanyanyua bilauri yake ya bia na kuinywa bia yote iliyokuwemo kwenye ile bilauri huku akishusha pumzi ndefu. Jacky alimtazama kwa madaha na kummiminia bia nyingine.

But you have not yet answered my question…” (Lakini bado hujajibu swali langu…) Jacky alimwambia Yusuf huku akimkazia macho.

What question?” (Swali gani?) Yusuf aliuliza huku akimtazama Jacky kwa mshangao.

I asked if you had a car.” (Niliuliza kama una gari).

I do not have a car,” (Sina gari) Yusuf alisema huku akiweka msisitizo kwa kutingisha kichwa chake kukataa.

“Hata kagari kadogo dogo tu?” Jacky aliuliza tena huku akiachia tabasamu.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 17

“Kwani hako kadogo dogo kanapatikana bure? Napenda kujenga, napenda kumiliki gari… tena Mercedes Benz au hata Toyota Landcruiser GX V8 kama lako, lakini tatizo ni fedha,” Yusuf alisema kwa huzuni.

“Si utani tatizo ni fedha, lakini nyie watu wa benki fedha kwenu siyo tatizo kabisa,” Jacky alichombeza huku akiachia kicheko hafifu.

“Aah wapi, kakwambia nani?” Yusuf alisema huku akimwangalia Jacky kwa mshangao na kukunja sura yake, kisha alishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Kila siku si mnachezea fedha? Mnahesabu mamilioni kwa mamilioni ya fedha, sema tu nyie wenyewe mmezubaa!” Jacky alizidi kumchombeza Yusuf huku akiachia kicheko hafifu.

Yusuf ambaye muda ule alikuwa ameshika bilauri ya bia akitaka kunywa alionekana kusita kidogo na kumtazama Jacky kwa mshangao.

“Tumezubaa, ki vipi?” Yusuf alimuuliza Jacky huku akiendelea kumtazama kwa mshangao kana kwamba alikuwa ameambiwa habari ya kushangaza sana ambayo hajawahi kuisikia kabisa maishani mwake.

“We mwenyewe si unaona? Mwaka wa nne uko benki unawahesabia watu fedha zao… mamilioni kwa mabilioni lakini wewe unapata nini? Pengine mshahara wako haufiki hata shilingi milioni moja kwa mwezi…” Jacky alisema kwa uchungu huku akibetua midomo yake na kunyanyua juu mabega yake.

Imagine, less than one million shillings per month is the salary for a guy like you? When will you build your child's future? And when will you own your own car or build a house?” (Hebu fikiria chini ya shilingi milioni moja kwa mwezi ni mshahara wa kulipwa kijana kama wewe? Utajenga lini maisha ya baadaye ya mwanao? Na utamiliki lini gari yako mwenyewe au kujenga nyumba?) Jacky alisema huku akishika tama.

Yusuf alimtazama Jacky kana kwamba alikuwa kiumbe wa ajabu kutoka sayari ya mbali, alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akijaribu kuyachuja yale maneno ya Jacky.

“Ukweli ni kwamba, chini ya shilingi milioni moja kwa mwezi si mshahara, mpenzi wangu, it's only an allowance. Tena posho yenyewe shombo tupu! Amka Yusuf, muda unapita,” Jacky alisema huku akijiegemeza kwenye kifua cha Yusuf.

Yusuf aliinamisha uso wake kwa kitambo kirefu akionekana kuguswa sana na yale maneno ya Jacky, aliwaza sana na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. Alipoinua uso wake kumtazama Jacky kwa makini alihisi machozi kumlenga lenga. Akanyanyua bilauri yake ya bia na kuinywa bia yote iliyokuwemo.

“Hebu niwekee whisky naona bia haipandi,” Yusuf alisema huku akimpa Jacky ile bilauri. Jacky aliichukua ile bilauri na kuiweka juu ya ile meza.

Kisha akaifungua ile chupa ya whisky kisha akaijaza pombe bilauri ya Yusuf kwa whisky na kuishika ile bilauri, akaipeleka kwenye mdomo wa Yusuf kutaka kumnywesha kwa mahaba lakini Yusuf alimnyang’anya na kuishika mwenyewe, akaigida pombe yote kama maji kisha akaikita ile bilauri juu ya meza.

Jacky aliijaza tena pombe ile bilauri ya Yusuf na kumpa, Yusuf akaiangalia kwa makini kisha akayahamisha macho yake kumwangalia Jacky kwa uchungu na kufinya jicho moja.

I love you so much, Belinda, where were you all this time?” (Nakupenda sana, Belinda, hivi ulikuwa wapi siku zote?) Yusuf alisema huku akizungusha mkono wake kumshika Jacky kiunoni bila ruhusa yake, hata hivyo hakukutana na upinzani wowote.

Jacky alimtazama Yusuf machoni kisha tabasamu maridhawa likachomoza usoni mwake na hatimaye aliachia kicheko hafifu.

Do not laugh, Belinda, I'm not drunk yet, I’m fit… okay explain well to me about money matters,” (Usicheke Belinda, sijalewa bado, niko fiti… haya hebu nielezee vizuri kuhusu mambo ya fedha) Yusuf alisema kwa uchungu huku akionekana kuanza kulewa.

Money matters, uh? It's like that. You really have to be awake,” (Mambo ya fedha, eh? Ndiyo kama hivyo. Inabidi uchangamke kweli kweli) Jacky aliongea kwa utulivu huku akijigeuza na kuipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Yusuf na hapo akasababisha chuchu za matiti yake kukitekenya kifua cha Yusuf.

Kitendo cha chuchu za Jacky kukitekenya kifua cha Yusuf kilimfanya Yusuf ajisikie faraja ya aina yake na alipomtazama Jacky machoni akaliona tabasamu pana likiwa limechanua usoni kwake.

Well, I real need the money, ila huko kuchangamka ndiyo sijajua sawa sawa, nichangamke vipi?” aliuliza Yusuf huku akianza kuhema kwa nguvu kutokana na ashki iliyoanza kumpanda.

“Lakini kwanza kabla ya yote, ninataka unihakikishie kwamba ni kweli hauna uhusiano na mwanaume mwingine yeyote yule? Kama unaye naomba uniambie ukweli ili nijue kwamba ninaingia katika uhusiano na mtu ambaye ana mahusiano na mwanaume mwingine,” Yusuf alisema huku akianza kumpapasa Jacky mgongoni.

Jacky alijilegeza na kufumba macho yake huku akionekana kuhema kwa nguvu kisha akaupeleka mkono wake kwenye shavu la Yusuf na kumbusu huku akimtazama kwa makini.

Why do you insist on that? Don’t you trust me when I told you that I’m not married?” (Kwa nini unasisitiza kutaka kufahamu jambo hilo? Kwani huamini nilipokwambia kwamba sijaolewa?) Jacky alimuuliza Yusuf huku mkono wake ukishuka hadi kifuani kwa Yusuf, akaanza kumpapasa chuchu zake.

Because I need you so badly, Belinda. I want to spend more time with you,” (Kwa sababu nakuhitaji sana, Belinda. Nataka kuwa na wewe kwa muda mrefu) Yusuf alisema huku akionekana kuhema kwa nguvu kutokana na ashki.

I’m all alone. That’s all I can say,” (Niko peke yangu. Hicho ndicho ninachoweza kusema) Jacky alisema huku akijilegeza kifuani kwa Yusuf.

Thank you for reassuring me about that,” (Nashukuru kwa kunihakikishia kuhusu hilo) Yusuf alisema huku akimwangalia Jacky kwa matamanio.

Jacky aliachia tabasamu huku akizidi kujilegeza huku akimchezea Yusuf maeneo nyeti ambayo yalianza kufura kwa hasira kali. Yusuf akaanza kutoa mguno wa ashki kwa msisimko huku akimkumbatia Jacky kwa nguvu na kuanza kumpapasa maungoni kwa pupa.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 18

Na Bishop Hiluka

I’m all alone. That’s all I can say,” (Niko peke yangu. Hicho ndicho ninachoweza kusema) Jacky alisema huku akijilegeza kifuani kwa Yusuf.

Thank you for reassuring me about that,” (Nashukuru kwa kunihakikishia kuhusu hilo) Yusuf alisema huku akimwangalia Jacky kwa matamanio.

Jacky aliachia tabasamu huku akizidi kujilegeza huku akimchezea Yusuf maeneo nyeti ambayo yanafura kwa hasira kali. Yusuf anaanza kutoa mguno wa ashki kwa msisimko huku akimkumbatia Jacky kwa nguvu na kuanza kumpapasa maungoni kwa pupa.

Endelea...

Kwa utundu Jacky aliipeleka ncha ya ulimi wake katika sikio la Yusuf na kumfanya azidi kutoa mguno kwa msisimko alioupata. Yusuf alishindwa kuvumilia na kumuinua Jacky kwa nguvu kisha alimtupa juu ya kitanda na kuanza kuvua suruali yake haraka na kuitupa kule.

Oh c’mon Yusuf, not so fast my love, I’m ready to give you what you want, but we need to talk first,” (Oh subiri Yusuf, usiwe na haraka mpenzi wangu. Niko tayari kukupa unachohitaji, lakini tunahitaji kwanza kuongea) Jacky alisema huku akijiinua kutoka pale kitandani kisha akamvuta Yusuf na kumbusu huku akimpapasa sehemu mbalimbali za mwili wake akizidi kumtia wazimu wa mapenzi.

Talk about what?” (Kuzungumze kuhusu nini?) Yusuf aliongea huku akihisi pumzi zinampaa.

About money matters,” (Kuhusu mambo ya fedha) Jacky alisema na kumtulizia macho Yusuf. Yusuf alimkodolea macho Jacky pasipo kusema neno, alionesha wazi kuwa alikwishapandwa na mzuka wa mapenzi.

“Ni hivi, kama tukishirikiana tutafanikiwa. Kwa kweli hakuna asiyehitaji pesa. Walionazo wanataka kujilimbikizia, wasionazo wanataka wawe nazo… kikubwa hapa ni ushirikiano tu, fedha mbona zipo!” Jacky alisema kwa sauti tulivu huku akimkazia macho Yusuf.

“Zipo wapi?” aliuliza Yusuf kwa shauku huku akiketi juu ya kitanda.

“Zipo benki. Wewe unafikiri wapi penye fedha ya mkupuo?” Jacky aliendelea kusema kwa utulivu huku akiendelea kumkazia macho Yusuf.

“Fedha ya benki tutaipataje?” Yusuf aliuliza tena huku akimtazama Jacky kwa mshangao.

“Usinichekeshe Yusuf, mbona watu wanachukua pesa kiulaini kabisa tena kwenye benki za kimataifa, itakuwa hizi za hapa Bongo? Ni kwamba tukishirikiana wala haitapita wiki tutakuwa mamilionea,” Jacky alisema kwa sauti tulivu yenye msisitizo.

Yusuf alimtazama Jacky kwa kitambo kirefu bila kusema neno, kila alivyomtazama hakuona mzaha kwenye uso wa Jacky. Kikapita kimya cha kitambo kirefu wakiwa wanatazamana.

Okay, nakusikiliza Belinda, hebu nielezee vizuri,” hatimaye Yusuf alisema na kuvunja ule ukimya ulioanza kutawala mle ndani.

Jacky aliachia tabasamu na kuanza kuishusha chini boksa ya Yusuf kisha akaivua kabisa na kutupa kule, baada ya hapo akaupeleka mkono wake katika ikulu ya Yusuf, akaanza kuzichezea malighafi zake, kitendo kile kilimfanya Yusuf aanze kutoa mguno kutokana na msisimko huku akihema ovyo.

Alimtazama Yusuf kwa makini na kujiinua kidogo akalipandisha juu gauni lake, taratibu akaanza kuishusha nguo yake ya ndani na kuiweka pembeni huku akirembua macho yake. Muda ule ule akamvuta Yusuf karibu yake na kummwagia mabusu mfululizo yaliyomchanganya.

Yusuf alionekana kuzidi kuchanganyikiwa huku akihisi pumzi zake zikimpaa na kuanza kuhema kwa nguvu kama mtu aliyekosa hewa safi ya oksijeni. Alijikuta akishindwa kabisa kuvumilia na hakuwa tena na ujasiri wa kupingana na hisia zake, muda huo alikwisha pandisha mori na kutaka kumwangusha Jacky kitandani lakini Jacky alimzuia tena.

“Ngoja kwanza…” Jacky alisema huku akijiinua na kusimama. Yusuf alimtazama kwa matamanio.

“Hebu nieleze ni akaunti gani pale kwenye tawi lenu yenye fedha nyingi?” Jacky alimuuliza Yusuf kwa sauti ya utulivu huku akirembua macho yake.

“Zipo kamaa… n…nne hivi!” Yusuf alijibu kwa kubabaika kidogo baada ya kufikiria.

“Nitajie mojawapo.”

The Jacarandah Group,” Yusuf alijikuta akiongea bila hata kufikiri.

“Ooh, kumbe wanaweka pesa zao pale!” Jacky alionesha kushangaa kidogo.

“Ndiyo, kwani unawafahamu?”

“Sana, nasikia wana hela hao jamaa hakuna mfano, hao ndiyo wa kula nao sahani moja…” Jacky alisema huku na kumsogelea Yusuf, akamvutia kifuani kwake na kuzidi kuzitomasa malighafi zake kwa ufundi wa hali ya juu, kitendo kilichomfanya Yusuf aropoke kila alichoulizwa.

“Unakumbuka mfumo wao wa kuweka na kutoa pesa?” Jacky aliuliza kwa sauti ya kunong’ona.

“Wanaweka pesa zao kila Alhamisi, lakini hawana ratiba maalumu ya kutoa,” Yusuf alisema huku akimkodolea Jacky macho ya uchu kama fisi aliyeona mzoga.

Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akaachia tabasamu pana, “Unaweza kuniambia, ni kiasi gani cha pesa hutoa benki wanapoamua kutoa?”

It’s between six million and one billion shillings, sometimes they withdraw up to two billions,” (Ni kati ya shilingi milioni mia sita hadi bilioni moja, wakati mwingine wanatoa hata bilioni mbili) Yusuf aliongea kwa sauti hafifu ya kirafiki.

I see! Do they withraw such a huge amount of money?” (Kumbe wanatoa kiasi kikubwa vile cha pesa?) Jacky aliuliza huku akishindwa kuficha mshangao wake.

“Wale jamaa achana nao kabisa! Kuna tetesi kuwa hata yule tajiri mkubwa duniani, Bill Gate ana hisa kwenye kampuni hiyo, ndiyo maana huwa hakosi kuja Tanzania mara kwa mara,” alisisitiza Yusuf.

“Unadhani lini watatoa tena fedha?”

“Kati ya kesho ama keshokutwa.”

“Safi sana, sasa itabidi unitafutie saini za waidhinishaji wa fedha za kampuni hiyo,” Jacky alisema kwa sauti hafifu huku akiachia tabasamu lake maridhawa.

“Ki vipi?” Yusuf aliuliza kwa mshangao huku akimkodolea macho Jacky.

Hapo Jacky alijigeuza na kumkabili Yusuf, kisha aliipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Yusuf na kuanza kumbusu mfululizo.

“Usijali, sasa nenda kazime taa nikupe kwanza ile kitu roho inataka, mambo mengine nitakueleza vizuri baadaye,” Jacky alisema huku akilitoa gauni lake na kulitupa kando.

Yusuf aliinuka haraka na kwenda kuzima taa akionekana hakuwa tayari kucheleweshewa mambo kutokana na uchu wa ngono uliokuwa umemnasa vilivyo, huku macho yake yakiwa yamemwiva kwa ashki.

Mambo si mambo, Yusuf keshaingia kichwakichwa na sasa yupo mikononi mwa Jacky. Je, nini kitaendelea?...
 
Tatizo la huyu mtunzi akifika katikati anasepa zake anawaacha hewani, bora kutomsoma tu kabisa
 
Bishop watu kama hao usihangaike kuwajibu bwana ebu tuwekee hata kaepisode kamoja jamani
Poa poa Shunie kwa kuwa umeongea kwa sauti ya upole, nami sina budi kufanya utakacho, mimi kwako ni kama Yusuf kwa Jacky tu...😀😀😀

Kizungumkuti! - 19

Na Bishop Hiluka

Hapo Jacky alijigeuza na kumkabili Yusuf, kisha aliipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Yusuf na kuanza kumbusu mfululizo.

“Usijali, sasa nenda kazime taa nikupe kwanza ile kitu roho inataka, mambo mengine nitakueleza vizuri baadaye,” Jacky alisema huku akilitoa gauni lake na kulitupa kando.

Yusuf aliinuka haraka na kwenda kuzima taa akionekana hakuwa tayari kucheleweshewa mambo kutokana na uchu wa ngono uliokuwa umemnasa vilivyo, huku macho yake yakiwa yamemwiva kwa ashki.

Endelea...

Ilionesha wazi kuwa alikuwa akiisubiri nafasi ile kwa muda mrefu. Alikuwa katika hali mbaya sana na hakuweza tena kuvumilia. Wakaingia mchezoni na muda mfupi uliofuata walikuwa kwenye dunia nyingine kabisa ya mapenzi yenye kila aina ya kionjo cha kumtoa nyoka pangoni.

Pale kwenye uwanja wa seremala mambo yalikuwa si mambo, mapenzi yalinoga kwa namna yake, sarakasi za kila aina na miguno ya mahaba ikahanikiza kila mahali mle chumbani. Jacky alikuwa akilia kilio kilichokosa kabisa tafsiri inayokubalika kwa haraka.

Wakati Yusuf akikaribia kumaliza safari yake ya kufika kileleni, alianza kutapatapa kama mtu aliyekuwa akitaka kukata roho, jambo lile likamfanya Jacky kupitisha vidole vyake laini kwenye masikio ya Yusuf. Kitendo kile kikamfanya Yusuf kuvunja dafu huku akilia kama mtoto mdogo.

Thank you, darling. Thank you very much,” (Asante, mpenzi. Asante sana) Jacky alisema huku akimbusu Yusuf kwenye paji la uso baada ya kumaliza ngwe ile.

Yusuf aliinuka pale kitandani na kuketi kwenye kona ya kile kitanda akionekana kuwa mbali sana kimawazo, alijiinamia huku akitweta, kwa kweli alionekana kuwa na mawazo mengi.

Sasa alianza kuhisi hatia kubwa ikimkaba kooni, kitendo kile cha kuzini na Jacky kikaufanya moyo wake uumie sana na kupoteza utulivu huku nafsi yake ikianza kumsimanga katika namna ya kumlaumu kuwa alikuwa amefanya maamuzi yasiyokuwa sahihi kukubali kumsaliti mkewe.

What is wrong, my love?” (Kuna tatizo gani, mpenzi?) Jacky alimuuliza baada ya kumuona akiwa kajiinamia kwa huzuni.

I’ve betrayed my wife, you know this is my first time to cheat on my marriage,” (Nimemsaliti mke wangu, unajua hii ni mara yangu ya kwanza kuisaliti ndoa yangu) Yusuf alisema kwa huzuni huku machozi yakimlenga.

C’mon darling, you have no reason to worry! I know you wanted to enjoy, right?” (Oh mpenzi, huna sababu ya kusikitika! Najua ulihitaji kufurahi, siyo?) Jacky alimwambia Yusuf huku akimsogelea na kuanza kumpapasa kifuani. Yusuf hakujibu kitu bali alibaki akiwa ameduwaa.

Don’t let me down, I’m all yours, darling. I want you now so badly. Please hold me tight in your hands,” (Usiniangushe, mimi ni wako, mpenzi. Nakuhitaji mno. Tafadhali nikumbatie mikononi mwako) Jacky alisema kwa sauti nyororo ya chini iliyoshawishi huku akianza tena utundu wake.

Yusuf alijikuta akisahau ghafla kuhusu mawazo ya kumsaliti mkewe na kujikuta akiwa katika hali mbaya kwa mara nyingine, hakuweza tena kuvumilia. Wakaingia tena mchezoni kwa ngwe nyingine.

Baada ya ngwe ile ya pili kumalizika wote walikuwa hoi na hakuna aliyetaka tena waendelee kwani walikuwa hoi wakiwa wanatweta kwa uchovu. Muda ule Yusuf alishindwa hata kumwangalia Jacky kutokana na aibu.

Belinda you are wonderful lady. Nashindwa kuelewa unatumia uchawi gani, maana nina mke wa ndoa na mtoto mmoja, nawapenda sana ila sielewi ni kitu gani kimenitokea kujikuta nikivutiwa sana na wewe. Nilipokuona mara ya kwanza pale benki moyo wangu ulivutwa kwako kama sumaku. Japo nimekuwa na msimamo mkali katika kuilinda ndoa yangu lakini kwako nimeshindwa kabisa kuwa na msimamo na kwa mara ya kwanza nimeisaliti ndoa yangu,” Yusuf alisema kwa huzuni huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Nakupenda sana Belinda, nakuahidi nipo tayari kufanya kila linalowezekana kuhakikisha unafanikiwa katika mpango wako wa kupata mabilioni na unakuwa na maisha mazuri zaidi na yenye furaha. I promise you, my love, I’m ready for anything,” Yusuf alizidi kubwabwaja baada ya kuonekana amepagawishwa na Jacky.

Jacky aliachia tabasamu laini na kumbusu Yusuf kwenye paji la uso. “Thank you very much, my love. I need someone like you. You are a person who knows how to love and care. I promise I will give you all kinds of pleasures of this world and I will not need anything from you beyond your love,” (Asante sana, mpenzi wangu. Namhitaji mtu kama wewe. Wewe ni mtu mwelewa unayejua kupenda na unayejali. Nakuahidi nitakupa kila aina ya vionjo na raha za dunia hii na wala sitahitaji kitu chochote toka kwako zaidi ya penzi lako tu) Jacky alichombeza huku akimpapasa Yusuf kwa mahaba.

I promise, anytime you need me just call me and I’ll be right there. For you I feel the wonderful joy I’ve missed for many years,” (Nakuahidi, muda wowte utakaonihitaji nipigie tu nami nitakuwa hapo mara moja. Kwako ninahisi furaha ya ajabu niliyoikosa kwa miaka mingi) Yusuf alisema huku akimeza funda la mate kutowesha koo lake lililokuwa limekauka.

Jacky alifurahi sana na kummwagia Yusuf mabusu mfululizo, kisha kikafuata kitambo kirefu cha kupanga mipango kabambe ya namna ya kufanikisha mambo ya fedha, huku Jacky akitawala mazungumzo. Katikati ya maongezi yao Jacky alishtuka na kuangalia saa yake ya mkononi akapigwa na butwaa.

“Dah, saa tisa usiku!” Jacky alisema na kumshtua sana Yusuf.

“Oh my God, saa tisa! Sijui nitamwambia nini mke wangu! Sijawahi kulala nje hata siku moja na jana nimetoka nyumbani saa kumi na mbili jioni na sijarudi hadi saa hizi! Eeh Mungu nisamehe mja wako,” Yusuf aliwaza huku moyo wake ukijaa hofu…

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart Super EMILYHALELUYA MOSHI Clkey
 
Hahahaha Bishop umenifurahisha sana Asante mno jamani ubarikiwe sana [emoji120][emoji120]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom