Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Bishop Hiluka leo utakua umetingwa sana jamani pole Askofu Jacky wako nipo nakusubiri mm

Shunie mwenzio nimekuja mbio baada ya kusikia unaniita. Usikonde Jacky, wangu japo umenisababishia balaa nyumbani, lakini nzi kufia kwenye kidonda ni halali. Ngoja nizimwage halafu niendelee na job...

Kizungumkuti! - 25

Na Bishop Hiluka

Jioni ile Jasmine alikuwa amevaa gauni fupi la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa pencil dress na lilionekana kumkaa vizuri sana mwilini huku likiuchora vyema mwili wake matata wenye umbo la kuvutia. Miguuni alikuwa amevaa sandals ngumu za ngozi zilizokuwa zimeshikilia kwenye miguu yake mizuri kwa kamba.

Jasmine alikuwa na uso wa mviringo na sura ya kitoto isiyoishiwa tabasamu muda wote huku macho yake makubwa na legevu ya kike yakiongezea mvuto wa sura yake. Pua yake ilikuwa ndefu na midomo yake ilikuwa laini yenye kingo pana kiasi zilizopakwa rangi nzuri ya mdomo.

Muda ule Jasmine alikuwa kaketi sebuleni kwake akiwasikiliza wageni wake Jacky na Carlos waliofika kumtembelea katika ugeni ule wa ghafla ambao hakuwa ameutarajia kabisa.

Endelea...

Sebule yake ilikuwa ndogo yenye samani za kawaida zikiwemo seti moja ya makochi yaliyoanza kuchoka foronya na meza ndogo ya chakula iliyozungukwa na viti vinne iliyokuwa upande wa kushoto kwenye sebule ile.

Katikati ya sebule ile kulikuwa na meza nyingine fupi na nzuri ya mbao ya mti wa msonobari iliyokuwa imefunikwa kwa kitambaa cha rangi ya samawati kizuri chenye maua mekundu na kijani ya kufuma kwa mkono.

Upande wa kulia wa ile sebule kulikuwa na kabati dogo lililokuwa na vitabu, DVD mbalimbali za filamu, kisimbuzi cha StarTimes na seti ya televisheni aina ya Hitachi ya inchi 21. Pia kulikuwa na deki ya DVD iliyokuwa na vumbi ikiashiria kuwa haikuwa imetumika kwa muda mrefu.

Sakafu ya mle ndani ilikuwa imefunikwa kwa zulia kuukuu la plastiki lililokuwa na rangi ya bluu na maua yenye rangi nyekundu na njano na kuta za sebule ya nyumba ile zilikuwa nyeupe zikiwa zimetundikwa picha mbili kubwa, moja ilikuwa picha ya Jasmine na picha nyingine ilikuwa ya wazazi wake.

Pia kulikuwa na picha kubwa ya kuchorwa ya wanyama wa mwituni maarufu kama Tingatinga na kalenda ya mwaka huo iliyokuwa imetundikwa ukutani upande mwingine wa ukuta.

Jasmine alikuwa akiishi na dada yake, Zaituni Mungi, mtoto wa mama yake mkubwa, ambaye kwa wakati ule hakuwepo pale nyumbani. Aliishi na zaituni baada ya kufiwa na baba yake mwaka mmoja tu uliokuwa umepita, wakati mama yake alikufa wakati Jasmine alipokuwa na miaka kumi, akiwa darasa la nne.

Katika nyumba ile yenye vyumba vinne Jasmine aliishi kwenye chumba kimoja na dada yake pia alikuwa na chumba kimoja na vyumba vingine viwili vilivyobakia alikuwa amevipangisha na hivyo kila mwezi aliingiza shilingi laki moja kama kodi ya vyumba viwili, na alipoongezea na shilingi laki mbili alizokuwa akilipwa kama mshahara kazini kwake, zilitosha kabisa kumfanya asiukimbie mji.

Jasmine aliwatazama Jacky na Carlos kwa zamu na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani akionekana kutafakari sana. Ilionekana kuwa alikuwa njia panda na alishindwa aamue nini kutokana na maneno aliyoelezwa na wale wageni wake.

Carlos na Jacky walikuwa wametumia zaidi ya dakika ishirini wakijaribu kumshawishi akubaliane na kile walichomweleza katika mpango wao wa kupata mabilioni ya pesa lakini yeye alionekana kutokubaliana kabisa na wazo lile.

Baada ya kuonekana kuwa ameshindwa kushawishika ilimbidi Carlos atafute njia nyingine ya kumfanya akubali, alimtazama kwa makini kisha alimtupia jicho Jacky na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Jasmine, hivi unajua kuwa marehemu baba yako alikuwa rafiki yangu mkubwa na si tu tulisaidiana kwa mambo mengi bali alikuacha mikononi mwangu, kweli si kweli?” aliuliza Carlos akiwa amemkazia macho Jasmine.

“Ni kweli, baba, lakini…” alijibu Jasmine kwa sauti yenye mashaka huku akiangalia chini.

“Aah nisikilize kwanza, Jasmine… najua kuwa baba yako hakukuachia rasilimali yoyote zaidi ya hii nyumba ambayo ni ya kawaida sana. Je, unadhani kwa nyumba hii tu bila mipango mingine utaishi vipi katika karne hii? Kumbuka wewe ni mtoto wa kike na kwa umri wako unahitaji kujirusha, unahitaji kuishi maisha mazuri na pia unahitaji kuvaa vizuri… unadhani vitu vyote hivyo utavipataje?” Carlos alisema huku akizidi kumkazia macho Jasmine.

Jasmin alitaka kusema neno lakini alisita na kubaki kimya akimtumbulia macho Carlos. Carlos alitoa kibunda cha fedha kiasi cha shilingi milioni moja na kumshikisha Jasmine mkononi huku akimlainisha na tabasamu kabambe.

“Sikiliza, fedha hizi si hongo bali ni kwa ajili ya kukusaidia chakula na matatizo madogo madogo tu ya hapa nyumbani kwa hizi siku mbili tatu utakazokuwa unatafakari proposal yangu,” Carlos alisema huku akizidi kuachia tabasamu la kumlainisha.

“Lakini naogopa…” Jasmine alisema kwa wasiwasi huku akitamani kuzikataa zile fedha.

“Jasmin, hivi nikueleze mara ngapi? Hundi moja tu ya katikati itakupa shilingi milioni mia moja ya kuchunga maisha yako ya baadaye!” Carlos alimwambia Jasmine huku sura yake ikiendelea kupambwa na tabasamu.

Jasmin alimtazama Carlos kwa wasiwasi, akaziangalia zile fedha kisha akainua tena sura yake kumtazama Carlos, akataka kusema lakini maneno yakawa hayatoki na hivyo kuishia kufumbua mdomo tu, kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akigeuza tena shingo yake kumtazama Jacky.

Jacky aliachia tabasamu maridhawa ili kumlainisha Jasmine huku akimuonesha ishara ya kumsisitiza akubaliane na proposal ya Carlos. Jasmine alijikuta akichanganyikiwa, aliinamisha kichwa chake na kuanza kutafakari.

Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya wakati Jasmine akiwa amezama kwenye tafakari, muda wote Carlos na Jacky walikuwa wakimwangalia kwa makini huku wakisubiria kusikia jibu lake. Mara Jasmine akainua uso wake kumtazama Carlos huku akilazimisha tabasamu.

“Sawa, nitajaribu,” alisema huku akishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa ametoka kwenye mashindano ya mbio ndefu.

“Usiseme utajaribu, tunachotaka ufanye kweli,” Carlos alimsisitiza kwa sauti tulivu lakini yenye kuamuru.

“Sawa, nitafanya,” Jasmine alisema na kuwafanya Jacky na Carlos watazamane na kutabasamu, kisha wakapeana ishara ya kuondoka. Walisimama wakamuaga Jasmine na kuondoka wakimwacha bado yupo katika hali ya sintofahamu.

Walipotoka nje ya ile nyumba ya Jasmine, Carlos na Jacky waliingia kwenye gari lao la kifahari aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe.

Jacky ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari, aliliondoa kwa utulivu na mara tu baada ya kuyaacha maskani ya Jasmine walishika uelekeo wa barabara ya lami iliyokuwa ikielekea kwenye machinjio ya ng’ombe ya Vingunguti.

Katika barabara ile kulikuwa na magari mengi katika muda ule wa jioni yaliyotokea katikati ya mji, hivyo Jacky alilazimika kuendesha gari lake kwa mwendo wa kawaida, japo alikuwa na haraka.

Wakati wakiwa katika barabara ile macho ya Carlos yalikuwa makini sana kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kama kulikuwa na gari lolote au pikipiki iliyoonesha ishara ya kuwafuatilia nyendo zao. Walivuka daraja la Mto Msimbazi na baada ya mwendo wa dakika chache walifika katika eneo la Barakuda.

Kisha walishika barabara ya kuelekea Segerea na baada ya mwendo mrefu hatimaye safari yao iliwafikisha katika makazi yao ya kisasa katika eneo la watu wenye ukwasi. Lile gari likafunga breki mbele ya geti kubwa jeusi la jumba moja kubwa la ghorofa mbili lililozungukwa na miti mirefu ya kivuli na ukuta mrefu wenye usalama wa uhakika.

Muda ule mvua ya wastani ilikuwa inanyesha, hata hivyo haikuwazuia kuingia ndani ya jumba lao la kifahari.

Jacky alibonyeza remote na mara lile geti jeusi likaanza kufunguka taratibu, kisha gari akaliingiza lile ndani ya uzio mrefu wa lile jumba uliokuwa umefungwa mfumo maalumu ya umeme wa kuzuia wezi juu yake.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 26

Jacky aliliegesha vizuri gari kisha wote wakashuka na kuanza kutembea haraka wakiuendea mlango mkubwa wa lile jumba lao, hata hivyo, Jacky alionekana kuchoka sana. Carlos aligundua na kumwangalia kwa makini.

My love, you seem very tired today!” (Mpenzi, unaonekana umechoka sana leo!) Carlos alimwambia Jacky huku akimtazama kwa makini kisha akafungua mlango wa mbele wa lile jumba.

I really feel tired. I think I need a break,” (Ni kweli ninahisi uchovu mwingi. Nadhani nahitaji mapumziko) Jacky alisema huku akirembua macho yake malegevu na kuingia ndani huku akiufunga mlango nyuma yake.

Kutokana na uchovu alijitupa kwenye sofa pale sebuleni huku akishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani. Hata hivyo, jioni ile ilionekana kuwa usiku tulivu mno, na haukupita muda tangu Carlos na Jacky waingie ndani na kuketi pale sebuleni mvua kubwa ilianza kunyesha.

Darling, are you sure that Jasmine will help us?” (Mpenzi, una uhakika kwamba Jasmine atatusaidia?) Jacky alimuuliza Carlos kwa wasiwasi baada ya kumtazama kwa makini.

Believe me, my love, she will help us, don’t you trust her?” (Niamini mpenzi, atatusaidia, kwani humuamini?) Carlos alimjibu Jacky huku akijiinua kutoka pale kwenye sofa.

I don’t know, but she’s just an innocent girl,” (Hata sijui, lakini ni binti asiye na makuu) Jacky alisema huku akipiga mwayo mrefu wa uchovu.

Jacky, you seem you didn’t get enough sleep last night. Twende ukaoge kwanza uondoe uchovu,” Carlos alimwambia Jacky kwa sauti tulivu ya upole huku akimwangalia kwa makini kisha alimshika mkono na kumuinua kutoka pale kwenye sofa.

Jacky alitii na kuinuka, kisha Carlos akamuongoza hadi kwenye ngazi za kuelekea chumbani kwao kwenye ghorofa ya kwanza kulikokuwa na chumba kikubwa cha kifahari kilichoonekana kuwa na nafasi kubwa ya kutosha.

Katika kile chumba kulikuwa na kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita cha samadari cha mbao ngumu za mninga kilichonakshiwa vizuri na kupendeza, kitanda kile kilikuwa katikati ya chumba na kilikuwa na droo mbili, moja katika kila upande wa kile kitanda, na juu ya droo zile kulikuwa na taa za rangi nyekundu.

Upande wa kulia na wa mbele wa kile chumba kulikuwa na madirisha makubwa mawili yaliyokuwa na vioo, madirisha yale yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu na mepesi. Dirisha moja lilikuwa upande wa mbele ambalo lilikuwa limeungana na mlango mmoja uliokuwa unatokea kwenye kibaraza cha ghorofani, yaani balcony.

Pale dirishani kwenye balcony kulikuwa na ua kubwa na zuri lililokuwa limepandwa kwenye chungu kikubwa cha udongo na kando ya lile ua kulikuwa na kiti kimoja cha kupumzikia kilichokuwa kinatazama nje. Pembeni ya kile kiti kulikuwa na meza ndogo na fupi ya mbao iliyokuwa na droo mbili.

Upande wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na kabati kubwa la nguo la ukutani na kando ya lile kabati kulikuwa na meza nzuri nyeusi ya kioo. Juu ya ile meza kulikuwa na seti moja ya runinga kubwa Flat screen aina ya Samsung iliyokuwa katikati ya spika mbili za sistimu ya muziki maarufu kama Home threatre.

Upande ule ule wa kushoto wa kile chumba kulikuwa na kochi moja la kukaa watu wawili la sofa lililokuwa nadhifu na la kisasa likiwa juu ya zulia zuri la manyoya lenye rangi za ngozi ya Pundamilia.

Mbele ya lile kochi kulikuwa na meza ndogo ya mbao yenye umbo la nusu duara ambayo juu yake kulikuwa na chombo kidogo cha majivu ya sigara, kibiriti cha gesi, paketi mbili za sigara, chupa kubwa ya mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa Navette de Marseille na bilauri ndefu mbili.

Upande wa kulia wa kile chumba kulikuwa na meza nzuri ya vipodozi iliyokuwa na vioo viwili virefu vya kujitazama na pembeni yake kulikuwa na mlango mwingine uliokuwa unaelekea kwenye chumba kikubwa cha maliwato. Ndani ya kile chumba cha maliwato kulikuwa na bafu la kisasa aina ya Jacuzzi. Pia kulikuwa na bomba la mvua kama mtu asingependa kutumia lile Jacuzzi.

Ukutani kulikuwa na picha tatu kubwa na nzuri, mbili zilikuwa ni za kuchorwa zilizokuwa zimetundikwa sehemu mbili tofauti, moja ilikuwa ni picha ya mbuga iliyoonesha wanyama wa porini na picha nyingine ilikuwa ya ua zuri la rangi nyekundu, njano na bluu lililokuwa limechorwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Picha ya tatu ilikuwa ikiwaonesha Carlos na Jacky katika mavazi nadhifu ya harusi huku wakiwa na furaha kubwa katika siku yao ya harusi. Picha zote tatu zilikuwa zimewekwa ndani ya fremu nzuri za kioo na kuzifanya zionekane vizuri katika zile kuta safi zilizokuwa na rangi ya maziwa. Jacky alisimama pale katikati ya chumba huku akiendelea kupiga miayo ya uchovu.

“Dah! Carlos kacheza pele kweli kweli, anajua sana kumchunguza mtu na kuyasoma mawazo yake… hapa nilipo nimechoka sana na ninahitaji kupumzika, maana tangu jana nilipokimbizwa mchakamchaka usiku kucha na Yusuf na asubuhi tena nikakutana na gwaride la nguvu la Carlos sijapata kabisa wasaa wa kupumzika,” Jacky aliwaza huku akivua nguo zake akijiandaa kwenda kujimwagia maji.

Carlos alikuwa amesimama akimtazama Jacky kwa makini kama vile alikuwa akijaribu kuyasoma mawazo yake ili kujua alichokuwa anawaza, kisha akatoka na kuelekea sebuleni akimwacha Jacky anaendelea kutoa nguo zake kabla hajaelekea bafuni kuoga.

Jacky alipotoa nguo alisimama mbele ya kioo kirefu na kujiangalia kwa kitambo huku akiwa mtupu kama alivyozaliwa, alijitazama akionekana kukitathmini kifua chake kilichokuwa kimebeba matiti madogo yenye chuchu ndogo zilizosimama kwa hasira zikiwa tayari kuitoboa blauzi yoyote ambayo angevaa.

Kisha macho yake yalishuka kutazama tumbo lake dogo na kitovu chake kilichotumbukia ndani na kuacha kishimo kidogo tumboni kilichoungana na mstari hafifu ambao ulikuwa umeshuka chini na kupotelea katikati ya mapaja yake huku ukikiacha kiuno chake chembamba na laini kikitanuka kwa namna ya kuvuta hisia za mwanamume yeyote hata angekuwa mgumu.

Kwa kitambo fulani Jacky aliganda pale kwenye kioo akijitazama kwa makini kisha akaachia tabasamu laini akionesha kuridhishwa na muonekano wake mzuri. Kisha aligeuka kutazama pale kwenye ile meza ndogo ya mbao yenye umbo la nusu duara iliyokuwa na chupa kubwa ya mvinyo mwekundu wa Kifaransa wa Navette de Marseille na bilauri ndefu.

Itaendelea...
 
Shunie mwenzio nimekuja mbio baada ya kusikia unaniita. Usikonde Jacky, wangu japo umenisababishia balaa nyumbani, lakini nzi kufia kwenye kidonda ni halali. Ngoja nizimwage halafu niendelee na job...

Hahahahahahahaa...i saw this coming. Ndo maana nlivyoona comment ya Shunie tu kila sekunde nkawa narefresh uzi nkijua fika kua episodes zinashuka soon.
Tater rudi nyumbani ndugu yangu, kushanoga[emoji23][emoji23][emoji23]

the Legend☆
 
Kizungumkuti! - 27

Akapiga hatua zake taratibu akisogea pale kwenye ile meza huku kiuno chake laini kikicheza taratibu kwa kadiri alivyokuwa akipiga zile hatua, alipoifikia ile meza aliinama akanyanyua ile chupa kubwa ya mvinyo kisha akamimina mvinyo kwenye bilauri moja na kugida mafunda kadhaa ya mvinyo huku akiuacha mvinyo ukiteleza taratibu kooni mwake.

Alipiga tena funda jingine la mvinyo huku akionekana kuanza kupata uchangamfu kidogo kisha akaikita ile bilauri juu ya meza na kuingia bafuni ambako alifungulia maji kwenye lile Jacuzzi kisha akaingia ndani yake na kuzama akiacha sehemu ya juu na miguu tu huku sehemu nyingine ya mwili ikiwa ndani ya povu la maji yaliyokuwa yakichemka.

Wakati akiendelea kuoga taratibu ndani ya lile Jacuzzi mara akamuona Carlos akiingia na kusimama, Carlos alikuwa amevaa bukta ya bluu na singleti nyeupe na alikuwa akivuta sigara huku akimtazama Jacky kwa matamanio. Wakatazamana kwa nukta chache huku Carlos akiachia tabasamu la matamanio.

Darling, what are you doing here? Please I’m really tired,” (Mpenzi, unataka kufanya nini? Tafadhali nimechoka kweli kweli) Jacky alimwambia Carlos kwa sauti yenye kukwama kwama.

Relax, darling,” Carlos alisema kwa sauti tulivu huku akiangua kicheko hafifu kisha akaondoka na kueleka chumbani. Baada ya dakika kadhaa za kuoga Jacky alitoka bafuni na kuelekea chumbani na moja kwa moja akaelekea kwenye kabati la ukutani la nguo.

Alipokuwa akitembea kile kiuno chake chembamba kilicheza taratibu sambamba na mtikisiko wa makalio yake laini yaliyopishana taratibu wakati alipokuwa akizitupa hatua zake. Hata hivyo, usoni wake hakuonesha tashwishwi yoyote na alionekana hakuwa na furaha.

Alipofika kwenye lile kabati alisimama mbele ya kioo kikubwa kilichokuwa kwenye kabati la nguo na kujishika kiunoni akijitazama kwa kujizungusha zungusha na baadaye akaanza kujitomasa tomasa matiti yake. Aliendeleaa kusimama pale bila kujua kuwa mle chumbani kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akimwangalia kwa makini.

Carlos alikuwa ameketi kwenye sofa akimtazama Jacky tangu alipotoka bafuni hadi alipokwenda kusimama pale kwenye kabati la nguo, aliendelea kumtazama kwa utulivu muda wote huku akivuta sigara yake taratibu na kuutoa moshi taratibu huku akiuangalia kwa makini.

Japokuwa macho ya Carlos yalikuwa yakimtazama Jacky muda mrefu lakini akili yake ilikuwa imezama zaidi katika ile starehe yake ya kuvuta sigara.

Mara kikamtoka kikohozi kilichomshtua Jacky ambaye aliacha kujitazama kwenye kile kioo na hapo akafungua lile kabati haraka na kuanza kuchagua nguo. Alitoa bikini nyekundu na gauni jepesi la pinkil kulalia na alipoivaa lile gauni lililichora vizuri umbo lake zuri huku likiionesha bikini nyekundu aliyokuwa ameivaa ndani.

Kisha alielekea sebuleni ambako aliandaa meza kwa ajili ya chakula cha jioni na baada ya kumaliza alimwalika Carlos kwa ajili ya chakula. Jacky alikuwa ameandaa kile chakula mapema kabla hawajaondoka kwenda Vingunguti kumuona Jasmine.

Alikuwa amepika wali wa nazi, mchuzi mzito wa kuku ulioungwa kwa nazi pia na mchemsho wa ndizi matoke zilizopikwa kwa ufundi wa hali ya juu huku zikiwa zimechanganywa vizuri na samaki aina ya sato wa Ziwa Victoria.

Pia kulikuwa na juisi ya parachichi iliyochanganywa na passion, bakuli la mboga za majani pembeni, bakuli la saladi na matunda kwenye sinia. Licha ya urembo wake, Jacky alikuwa msichana fundi sana wa kupika na kwa kweli alikuwa amepika chakula kitamu sana.

Carlos alikuja na kujumuika na Jacky pale kwenye meza na wakati wakiwa mezani wanakula chakula taratibu mvua kubwa iliendelea kunyesha huku matone yake yakianguka juu ya paa la nyumba yao.

Jacky hakuwa katika hali yake ya kawaida, bado hakuonesha furaha na muda wote macho yake yalikuwa yakitazama chakula lakini akili yake haikuonekana kuzama kwenye kile chakula pale mezani.

Carlos alimtazama kwa makini na kuguna kitendo kilichomfanya Jacky ainue uso wake kumtazama Carlos, na macho yao yalipokutana Jacky alijitahidi kuumba tabasamu hafifu usoni mwake.

Hata hivyo, hakufanikiwa kwani badala ya kuonesha tabasamu halisi alionekana ni kama mtu aliyekuwa anataka kulia na kucheka kwa wakati mmoja.

Are you okay?” (Uko sawa?) Carlos alimuuliza Jacky huku akiwa amekamkazia macho.

I’m okay, why?” (niko sawa, kwani vipi?) Jacky aliongea kwa utulivu lakini maelezo yake yalikuwa hayaendani kabisa na mwonekano wa sura yake.

Alishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa amekimbia umbali mrefu, kisha aliinamisha tena uso wake na macho yake kuangalia chakula ingawa hakuwa akikitazama kile chakula bali alizama kwenye tafakuri.

Are you hiding something to me, Jacky? You’re not okay, I know you,” (Unanificha kitu Jacky? Hauko sawa, nakufahamu) Carlos alisema huku akitingisha kichwa chake kwa huzuni akionekana kutoridhishwa na jibu la Jacky.

Don’t you trust me, darling? Why do you say that I’m hiding something to you?” (Kwani huniamini mpenzi? Kwa nini unasema kuwa ninakuficha kitu?) Jacky aliuliza huku akimkazia Carlos macho yake yaliyokuwa yamelewa kwa uchovu na usingizi.

Jacky, we have known each other for a long time, almost three years now! Lakini bado umekuwa hueleweki…” Carlos alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Don’t worry, I’m okay… I’m just tired and sleepy, but I'm okay,” (Usiwe na shaka, niko sawa… ni uchovu tu na usingizi, lakini niko sawa) Jacky alisema huku akilazimisha tabasamu, hata hivyo, mwonekano wake usoni ulikuwa na kila dalili za mashaka na wasiwasi ingawa hakutaka kusema ukweli.

Carlos alimtazama kwa makini kisha aliinuka na kwenda kwenye jokofu, akatoa chupa ya mvinyo aina ya Pinot Noir na bilauri mbili kisha akarudi nazo pale mezani.

I think this will make you a little stimulating to remove fatigue,” (Nadhani hii itakuchangamsha kidogo na kukutoa uchovu) Carlos alisema huku akimuonesha Jacky ile chupa ya mvinyo. Waliendelea kula taratibu na waliposhiba wakashushia na matunda.

Kisha wakahamia sebuleni kwenye masofa huku kila mmoja akiwa na kimbaka mdomoni kuondoa masalia ya nyama ya kuku pamoja na masalio mengine kwenye meno.

Moyoni, Carlos alijisifia sana kumpata mke mrembo sana kama Jacky aliyekuwa na sifa nyingine nyingi za ziada, kuanzia mapishi jikoni, utaalamu wa huduma za nyumbani hadi ufundi awapo katika katika uwanja wa futi sita kwa sita.

Kisha Carlos aliifungua ile chupa ya mvinyo na kumimina kwenye zile bilauri halafu moja akampa Jacky. Walishushia ule mvinyo na baada ya dakika kadhaa Jacky alionekana kuchangamka kidogo ingawa aliendelea kupiga miayo ya uchovu.

Baada ya kupiga mafunda kadhaa ya mvinyo Jacky aliinuka na kujikongoja kuelekea chumbani, alipoingia alijitupa kitandani huku akilala kifudifudi. Hakuchukua muda mrefu mara usingizi ukampitia.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 28

Muda ule Carlos alionekana kukumbuka jambo, akachukua simu ya Jacky ambayo alikuwa anawasiliana na Yusuf na kutafuta namba fulani kutoka kwenye orodha ya majina ya watu katika simu yake kisha akabofya ile namba na kuweka simu sikioni, baada ya muda ile simu iliita na kupokelewa. Kwa dakika takriban ishirini carlos alikuwa anaongea mtu, wakipanga na kupangua, hatimaye wakafikia muafaka. Alipokata simu akainuka na kuelekea chumbani.

Kule chumbani alisimama na kumtazama Jacky kwa makini jinsi alivyokuwa amelala kwa uchovu, akatabasamu na kuzima taa za chumbani na kuwasha zile taa za rangi zilizokuwa juu ya droo mbili zilizokuwa kila upande wa kile kitanda, naye akajilaza kitandani kando ya Jacky na kupitiwa usingizi.

* * * * *

Jioni ya siku ile Yusuf alirudi nyumbani kwake Ilala Bungoni mapema mara tu baada ya kufunga ofisi, ilikuwa saa kumi na moja jioni na mvua ya manyunyu ilikuwa inanyesha taratibu wakati akirudi huku akiwa mwenye wasiwasi.

Alipofika nyumbani alimkuta mkewe Mama Jasmine akiwa ameketi kibarazani na jirani yao Mama Shani wakisukana. Yusuf aliwasalimia kwa bashasha zote, Mama Shani aliitikia lakini mkewe hakusema kitu. Yusuf alimsogelea mwanawe Jasmine aliyekuwa akicheza na Shani na kumnyanyua juu huku akimrushia mabegani mwake.

Kisha alimtupia jicho mkewe na kuelekea ndani ambako alivua nguo zake na kuziweka ndani ya tenga la nguo chafu kisha alivaa bukta nyeusi na fulana nyepesi nyeupe na kuketi sebuleni, aliwasha runinga na wakati akitafuta stesheni akajikuta akiweka chaneli iliyoonesha kipindi cha katuni za “Tom and Jerry”, akataka kutoa lakini Jasmine akang’aka huku akimnyang’anya remote, “Baba usitoe.”

Yusuf alitii amri ya mwanawe, hivyo wakawa wanaangalia kile kipindi huku na Jasmine ambaye alikuwa amekaa juu ya kochi la sofa lililoanza kuchoka jirani na baba yake, akijiegemeza na kutulia tuli na mkononi alishikilia ile remote.

Kwa muda mrefu Yusuf aliketi pale sebuleni pasipo kumuona mkewe akiingia ndani kama ilivyokuwa kawaida yake kumpokea mumewe na kumpa pole kwa kazi. Kitendo kile kilimuumiza sana Yusuf japo hakuwa na namna ya kufanya.

Aliendelea kukaa kwa utulivu huku macho yakiwa yameganda kwenye ile runinga japokuwa akili yake haikuwa pale, bali alikuwa akiwaza na kuwazua hili na lile. Mawazo yalimteka na kumrudisha miaka mitano au sita nyuma akakumbuka alivyofahamiana na mkewe Mama Jasmine, ambaye wakati huo alijulikana zaidi kwa jina lake la Zaituni Malocha.

Ilikuwa siku moja wakati Yusuf alipokuwa Msamvu Morogoro akitokea nyumbani kwao Msufini pale pale Morogoro, muda huo alikuwa safarini kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza kazi katika kampuni binafsi ya masoko. Alipita kwenye duka la rafiki yake, Obedi Mkude ili kumuaga, akapishana na mwanadada mmoja aliyetoka pale dukani akiwa na haraka, Yusuf hakuwa amemtilia maanani.

Alisimama pale dukani na kusalimiana na Obedi na wakati wakiagana macho yake yakatua kwenye kitabu kimoja kinachoitwa “The Devil in Love” cha mwandishi Barbara Cartland kilichokuwa kimelala juu ya meza ya bidhaa.

Yusuf alimuuliza Obedi kama kile kitabu kilikuwa chake, lakini Obedi alikana kukifahamu ila alikumbuka kumuona nacho msichana mmoja aliyekuja pale dukani kununua soda ya “take away” akiwa anawahi basi na pengine ndiye aliyekisahau pale.

Yusuf alikifunua kile kitabu akaangalia kurasa mbili tatu, hata hivyo alivutiwa sana na maandishi yaliyoandikwa kwa penseli katika ukurasa wa kwanza tu wa kitabu kwa mwandiko mzuri wa kike yakiwa na ujumbe uliogusa hisia zake.

Chini ya maandishi yale, Yusuf aligundua jina mmiliki wa kile kitabu, “Zaituni Malocha” lililoambatana na anuani ya barua pepe. Yusuf aliamua kuondoka na kile kitabu akiahidi kumtafuta ili amrudishie baada ya kukisoma, kwani alikuwa mpenzi riwaya za watunzi Barbara Cartland na Agatha Christie.

Alipofika Dar es Salaam alimuandikia Zaituni barua pepe akitumia ile anuani aliyoikuta kwenye kile kitabu akijitambulisha kwa jina na mahali alipokuwa akiishi kisha akamweleza kuwa alikuwa na kitabu chake, na mwisho akamuomba urafiki.

“Ni urafiki wa aina gani unaouhitaji, Yusuf?” Zaituni alimwandikia ujumbe Yusuf baada ya kuona kuombwa wawe marafiki.

“Urafiki wa hivi hivi tu, wala usifikirie vibaya.” Yusuf alimjibu.

“Hata mimi ningependa kuwa na rafiki muungwana wa aina yako na ninakubali tuwe marafiki wa hivi hivi tu kama ulivyosema, lakini tafadhali, tafadhali, tusiwe marafiki wa kimapenzi, sawa?” Zaituni aliandika ujumbe ambao Yusuf hakuwa na namna nyingine ya kufanya isipokuwa kukubaliana naye.

Baada ya pale mawasiliano kati yao kupitia barua pepe yaliongezeka kwa kipindi cha mwaka mmoja na miezi miwili, wakati huo Zaituni alikuwa anasoma jijini Mwanza. Kila ujumbe waliotumiana ulikuwa kama mbegu iliyoanguka katika udongo wenye rutuba na taratibu hisia za kimapenzi zikaanza kuchipuka ndani ya mioyo yao.

Yusuf aliomba atumiwe picha lakini Zaituni alikataa akimwambia kuwa kama kweli alimpenda asingejali alikuwa anafananaje, kwani kupenda ni kazi ya moyo na macho hubaki kuwa shahidi tu.

Hatimaye siku ya siku ikawadia, Zaituni alimwandikia Yusuf barua pepe kuwa angefika jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi kwa basi la Shabiby Line akitokea Dodoma ambako wazazi wake walikuwa wamehamishiwa na alitarajia kuingia Dar es Salaam saa 8:00 mchana.

“Fika Ubungo, utanitambua kwa ua waridi jekundu nitakalovaa kifuani kwangu katika titi la kushoto…” Zaituni alimwandikia ujumbe wa kumjulisha.

Hivyo, ilipofika saa 7:30 mchana Yusuf alikuwa amekwishafika katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo akiwa ameshika kile kitabu cha Barbara Cartland akimsubiri msichana mrembo ambaye moyo wake ulimpenda sana, lakini macho yake hayakuwahi kumuona.

Alikaa pale kituoni kwa muda mrefu akisubiri kwa hamu kwani alikwishachoka kuteseka na alikuwa tayari kwa lolote. Aliangaza angaza macho angani kukitazama kile alichokiona mwenyewe “muda” ambao aliuona ukivaa mbawa zake.

“Muda kitu cha ajabu sana!” Yusuf aliwaza baada ya kuitazama saa yake ya mkononi.

“Muda!” alijikuta akiwaza tena, lakini safari hii alitamka kwa sauti kama vile alikuwa akiongea na mtu.

Ni mara ngapi Yusuf alikuwa akiuona “muda” ukipita mbio mbele yake mithili ya duma mwenye kasi! Kuna kipindi aliitamani kuusimamisha ili afurahie maisha bila kuwa na wasiwasi.

Lakini siku hiyo ambayo ilikuwa muhimu sana katika maisha yake “muda” ulionekana kumnyima raha, ulikuwa ukinyiririka taratibu kwa madaha na maringo kama kinyonga. Zaituni ndiye aliyekuwa mchawi wa huo “muda”. Alikuwa na mamlaka ya kuuamuru uwe duma mwenye kasi ama uwe kinyonga.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 29

Yusuf alimuwaza Zaituni muda wote, mbele ya uzuri wa kiumbe huyo aliyeitwa Zaituni, Yusuf alijiona kama limbukeni wa mapenzi. Mawazo yalimpitia na moyo ulimwenda mbio kama mtu aliyekuwa na ugonjwa wa kihelehele. Alijiuliza iwapo hali ile ilikuwa ni matokeo ya kumsubiri Zaituni, ingekuwaje pindi angeingia ndani mwake?

Alijiambia kuwa kama ni mateso yalikuwa yametosha, huo sasa ulikuwa ni muda muafaka wa kumaliza utata. Aliitupia tena jicho saa yake, ilionesha kuwa saa 7:56. Wasiwasi ukazidi kwa kadiri muda ulivyokaribia. Aliendelea kusubiri lakini muda ulivyozidi kusogea ndivyo alivyozidi kuhisi mabadiliko katika akili na mwili wake.

Saa 7:57, Yusuf akaanza kupanga jinsi atakavyompokea Zaituni. Ikamjia picha akilini mwake ya Zaituni akiteremka katika basi la Shabiby na kumfuata lakini akaishiwa nguvu na kuanguka. Picha hiyo haikumpendeza kabisa Yusuf.

Saa 7:58, mwili mzima wa Yusuf ulijaa moto, alihisi joto kali sana likitambaa mwilini kwake kama vile alikuwa amewekwa kwenye tanuru la kuokea mikate. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka!

Saa 7:59, vidole vya mikono yake vilianza kutetemeka kama vile damu ilikuwa ikienda mbio kwenye mishipa. Saa 8:00 alikuwa amebadilika kabisa na yeyote ambaye angemuona kwa wakati huo asingeshindwa kubaini kuwa Yusuf alikuwa katika wakati mgumu sana.

Hata hivyo, alipiga moyo konde na kusubiri ujio wa mrembo wa shani aliyekusudiwa kuumbwa malaika lakini akateremshwa duniani kimakosa. Muda ulianza kuyoyoma na Yusuf hakukata tamaa, aliendelea kumtizamia Zaituni kwa dakika zingine ishirini huku akichungulia kwenye kila gari lililoingia pale Ubungo.

Kichwa chake kilizunguka, na ndani yake mseto wa hamu, hofu na tamaa vilianza kumtambaa taratibu na kuyafanya maungo yake yageuke. Mara akaliona basi la Shabiby kutoka Dodoma likiingia katika Kituo cha mabasi cha Ubungo.

Muda ule Yusuf alikuwa amejiandaa vyema kumkabili Zaituni, alijiandaa kwa kila hali kuanzia kimavazi, namna ambavyo angempokea na kumsalimia kisha angemkaribisha jijini na hata namna ambavyo angemweleza jinsi alivyokuwa akimpenda kwa dhati.

Alisimama kutoka kwenye benchi baada ya kuliona lile basi likisimama na abiria kuanza kushuka, akasogea karibu huku akiweka sawa tai yake shingoni kisha akakaza macho yake kuwatazama kwa makini wale abiria walioshuka kutoka ndani ya basi la Shabiby.

Mara akamuona msichana mrembo aliyeshuka kutoka kwenye lile basi la Shabiby akiwa ameshika begi dogo jeusi la safari na kuanza kupiga hatua zake kwa madaha akielekea upande ule ambao yeye alikuwa amesimama.

Yule msichana ambaye alikiri kuwa hadi wakati huo alikuwa hakuwahi kumuona msichana wa namna ile katika pitapita zake, alikuwa amevaa vazi la kitambaa cha bazee lililoshonwa na kudariziwa vizuri kwa nyuzi za dhahabu na lilikuwa limenasa vyema kwenye kiuno chake chembamba kilichoshikilia mzigo mkubwa wa makalio na minofu ya mapaja yake.

Miguuni alivaa viatu vyekundu vyenye vikanyagio virefu vya mchuchumio na nywele zake nyeusi za kibantu alikuwa amezisuka mtindo wa rasta na kuzifunika kwa kilemba, hivyo kumfanya aonekane mzuri wa asili.

Mkono wake wa kushoto alikuwa amevaa saa nzuri ndogo ya kike iliyotengenezwa kwa namna ya kupendeza na hivyo kuongeza ziada nyingine katika uzuri wake. Begani alikuwa amening’iniza mkoba mzuri mwekundu.

Yusuf akajikuta akipiga hatua zake kumfuata yule mrembo, alisahau kabisa kuwa aliambiwa kuwa atakuwa ameweka ua waridi jekundu katika titi lake la kushoto. Alipokumbuka akasita na kusimama ghafla huku akimkodolea macho ya matamanio, na wakati huo huo yule msichana akampita kwa mwendo wa kasi passipo kumjali na kujichanganya kwenye umati wa watu.

Yusuf alibaki akiwa ameduwaa na alipokuwa bado anashangaa mara akamuona mwanamke mtu mzima aliyezidi miaka 60 akiwa amesimama akiangaza macho yake huku na kule kama vile alikuwa akimtarajia mtu. Yule bibi alikuwa amevaa gauni zuri la kitenge na miguuni alivaa viatu vya flat visivyo na visigino virefu. Yusuf alipomtazama vizuri akaliona ua waridi jekundu katika titi lake la kushoto.

Dah! Alijikuta akiishiwa nguvu, alihisi kana kwamba mwili wake ulikuwa umegawanywa katika mapande mawili, akataka aondoke zake na kumwacha yule bibi kwenye mataa, hata hivyo, hakuona kama ni busara kuondoka bila kuongea naye, hivyo akamfuata na kujitambulisha kwake huku akimuonesha kile kitabu.

"Naitwa Yusuf Akida, nimefurahi sana kukutana na wewe ana kwa ana, Bi Zaituni. Ninaomba kwanza nikupeleke ukapate chakula cha mchana kabla hatujaongea," Yusuf alisema huku akimtazama yule mwanamke kwa tabasamu.

Hata hivyo, alishangazwa sana kuona yule mwanamke hakuwa akimtambua yeye wala kile kitabu alichoshika na alimtazama kwa mshangao mkubwa kana kwamba aliona kitu kigeni cha ajabu kutoka sayari nyingine.

“Kwa kweli vijana mnazidi kunichanganya,” alisema yule bibi, “lakini kuna msichana mmoja alivaa ngyuo ya bazee na kilemba kichwani alielekea huko aliniomba nivae hili ua kwenye kifua changu. Na alisema kama mwanamume yeyote ambaye angenipokea nimuambie kuwa amekwenda kumsubiri katika hoteli ya Landmark. Alisema kuwa hili ni jaribio kuona kama kweli mwanamume huyo ana upendo wa dhati,” alisema yule bibi na kumuacha Yusuf akiwa mdomo wazi.

Haraka sana Yusuf aliondoka na kuelekea Landmark Hotel alikomkuta Zaituni akimsubiri, wakala pamoja chakula cha mchana na huo ndiyo ukawa mwanzo wa mahaba mazito na hatimaye ndoa… Yusuf aliwaza sana na mara akajikuta akipitiwa na usingizi pale pale kwenye kochi…

______

Mama Jasmine aliendelea kukaa kule nje akipiga soga na shoga zake hadi ilipotimia saa moja na ushee ndipo akaamua kuingia ndani na macho yake yakatua kwa mumewe aliyekuwa kauchapa usingizi palepale kwenye kochi, kiganja cha mkono wa kulia kikiwa shavuni.

Macho yake yalihama na kumtazama mwanawe Jasmine ambaye pia alikuwa kauchapa usingizi palepale kwenye kochi. Runinga ilikuwa bado inaonesha vipindi vya katuni.

Mama Jasmine alimfuata mwanawe na kumbeba kisha akaingia naye chumbani na kumlaza kitandani. Akarudi tena sebuleni na kusimama akimtazama mumewe kwa chuki na kuchukua remote kisha akaizima ile runinga.

Yusuf akashtuka na kufumbua macho yake, macho yake yakaanza kutambaa katika mwili wa mkewe, yakianza na mapaja yaliyonona kuelekea juu kisha yakakutana na nyonga zilizofinyangwa barabara.

Macho yake yakatuwama kwa muda katikati ya mapaja ya mkewe, kisha yakafunga safari kuelekea kiunoni yakakutana na kiuno kilichobonyea na kuacha fursa ya nyonga kuchanua zilivyotaka. Kiuno kilirembwa na tumbo dogo ambalo lilikana kuwa wakati fulani lilishabeba kiumbe kwa muda wa miezi tisa.

Hamu haikuishia hapo, macho yalielekea kwenye kifua kilichobeba matiti madogo yaliyokuwa yamesimama kana kwamba hakuwahi kunyonyesha hapo kabla. Hamu ya mapenzi ikamjaa juu ya mkewe.

Macho yake hayakuishia hapo bali yalipanda hadi kwenye uso wa mkewe, akauona uso wa mkewe ukiwa mkavu usio na tashwishwi yoyote. Yusuf akatweta na hamu ya mapenzi ikamuisha mara moja.

Mambo ndo' yanazidi kunoga, endelea kufuatilia stori hii ya kusisimua "Kizungumkuti" ili kuujua mwisho wake...
 
Dah, huo mtego Yusuf aliopewa stendi ni noma. Kuna muda tunafeli vitu vidogo sana. Vijana wa siku hizi wangeona ni bibi ndo kavaa hilo ua wangepotea fasta sana

the Legend☆
 
Shunie mwenzio nimekuja mbio baada ya kusikia unaniita. Usikonde Jacky, wangu japo umenisababishia balaa nyumbani, lakini nzi kufia kwenye kidonda ni halali. Ngoja nizimwage halafu niendelee na job...

Kizungumkuti! - 25

Na Bishop Hiluka

Jioni ile Jasmine alikuwa amevaa gauni fupi la kitenge lililoshonwa kwa mtindo wa pencil dress na lilionekana kumkaa vizuri sana mwilini huku likiuchora vyema mwili wake matata wenye umbo la kuvutia. Miguuni alikuwa amevaa sandals ngumu za ngozi zilizokuwa zimeshikilia kwenye miguu yake mizuri kwa kamba.

Jasmine alikuwa na uso wa mviringo na sura ya kitoto isiyoishiwa tabasamu muda wote huku macho yake makubwa na legevu ya kike yakiongezea mvuto wa sura yake. Pua yake ilikuwa ndefu na midomo yake ilikuwa laini yenye kingo pana kiasi zilizopakwa rangi nzuri ya mdomo.

Muda ule Jasmine alikuwa kaketi sebuleni kwake akiwasikiliza wageni wake Jacky na Carlos waliofika kumtembelea katika ugeni ule wa ghafla ambao hakuwa ameutarajia kabisa.

Endelea...

Sebule yake ilikuwa ndogo yenye samani za kawaida zikiwemo seti moja ya makochi yaliyoanza kuchoka foronya na meza ndogo ya chakula iliyozungukwa na viti vinne iliyokuwa upande wa kushoto kwenye sebule ile.

Katikati ya sebule ile kulikuwa na meza nyingine fupi na nzuri ya mbao ya mti wa msonobari iliyokuwa imefunikwa kwa kitambaa cha rangi ya samawati kizuri chenye maua mekundu na kijani ya kufuma kwa mkono.

Upande wa kulia wa ile sebule kulikuwa na kabati dogo lililokuwa na vitabu, DVD mbalimbali za filamu, kisimbuzi cha StarTimes na seti ya televisheni aina ya Hitachi ya inchi 21. Pia kulikuwa na deki ya DVD iliyokuwa na vumbi ikiashiria kuwa haikuwa imetumika kwa muda mrefu.

Sakafu ya mle ndani ilikuwa imefunikwa kwa zulia kuukuu la plastiki lililokuwa na rangi ya bluu na maua yenye rangi nyekundu na njano na kuta za sebule ya nyumba ile zilikuwa nyeupe zikiwa zimetundikwa picha mbili kubwa, moja ilikuwa picha ya Jasmine na picha nyingine ilikuwa ya wazazi wake.

Pia kulikuwa na picha kubwa ya kuchorwa ya wanyama wa mwituni maarufu kama Tingatinga na kalenda ya mwaka huo iliyokuwa imetundikwa ukutani upande mwingine wa ukuta.

Jasmine alikuwa akiishi na dada yake, Zaituni Mungi, mtoto wa mama yake mkubwa, ambaye kwa wakati ule hakuwepo pale nyumbani. Aliishi na zaituni baada ya kufiwa na baba yake mwaka mmoja tu uliokuwa umepita, wakati mama yake alikufa wakati Jasmine alipokuwa na miaka kumi, akiwa darasa la nne.

Katika nyumba ile yenye vyumba vinne Jasmine aliishi kwenye chumba kimoja na dada yake pia alikuwa na chumba kimoja na vyumba vingine viwili vilivyobakia alikuwa amevipangisha na hivyo kila mwezi aliingiza shilingi laki moja kama kodi ya vyumba viwili, na alipoongezea na shilingi laki mbili alizokuwa akilipwa kama mshahara kazini kwake, zilitosha kabisa kumfanya asiukimbie mji.

Jasmine aliwatazama Jacky na Carlos kwa zamu na kushusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani akionekana kutafakari sana. Ilionekana kuwa alikuwa njia panda na alishindwa aamue nini kutokana na maneno aliyoelezwa na wale wageni wake.

Carlos na Jacky walikuwa wametumia zaidi ya dakika ishirini wakijaribu kumshawishi akubaliane na kile walichomweleza katika mpango wao wa kupata mabilioni ya pesa lakini yeye alionekana kutokubaliana kabisa na wazo lile.

Baada ya kuonekana kuwa ameshindwa kushawishika ilimbidi Carlos atafute njia nyingine ya kumfanya akubali, alimtazama kwa makini kisha alimtupia jicho Jacky na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Jasmine, hivi unajua kuwa marehemu baba yako alikuwa rafiki yangu mkubwa na si tu tulisaidiana kwa mambo mengi bali alikuacha mikononi mwangu, kweli si kweli?” aliuliza Carlos akiwa amemkazia macho Jasmine.

“Ni kweli, baba, lakini…” alijibu Jasmine kwa sauti yenye mashaka huku akiangalia chini.

“Aah nisikilize kwanza, Jasmine… najua kuwa baba yako hakukuachia rasilimali yoyote zaidi ya hii nyumba ambayo ni ya kawaida sana. Je, unadhani kwa nyumba hii tu bila mipango mingine utaishi vipi katika karne hii? Kumbuka wewe ni mtoto wa kike na kwa umri wako unahitaji kujirusha, unahitaji kuishi maisha mazuri na pia unahitaji kuvaa vizuri… unadhani vitu vyote hivyo utavipataje?” Carlos alisema huku akizidi kumkazia macho Jasmine.

Jasmin alitaka kusema neno lakini alisita na kubaki kimya akimtumbulia macho Carlos. Carlos alitoa kibunda cha fedha kiasi cha shilingi milioni moja na kumshikisha Jasmine mkononi huku akimlainisha na tabasamu kabambe.

“Sikiliza, fedha hizi si hongo bali ni kwa ajili ya kukusaidia chakula na matatizo madogo madogo tu ya hapa nyumbani kwa hizi siku mbili tatu utakazokuwa unatafakari proposal yangu,” Carlos alisema huku akizidi kuachia tabasamu la kumlainisha.

“Lakini naogopa…” Jasmine alisema kwa wasiwasi huku akitamani kuzikataa zile fedha.

“Jasmin, hivi nikueleze mara ngapi? Hundi moja tu ya katikati itakupa shilingi milioni mia moja ya kuchunga maisha yako ya baadaye!” Carlos alimwambia Jasmine huku sura yake ikiendelea kupambwa na tabasamu.

Jasmin alimtazama Carlos kwa wasiwasi, akaziangalia zile fedha kisha akainua tena sura yake kumtazama Carlos, akataka kusema lakini maneno yakawa hayatoki na hivyo kuishia kufumbua mdomo tu, kisha alivuta pumzi ndefu na kuzishusha taratibu huku akigeuza tena shingo yake kumtazama Jacky.

Jacky aliachia tabasamu maridhawa ili kumlainisha Jasmine huku akimuonesha ishara ya kumsisitiza akubaliane na proposal ya Carlos. Jasmine alijikuta akichanganyikiwa, aliinamisha kichwa chake na kuanza kutafakari.

Kikatokea kitambo kifupi cha ukimya wakati Jasmine akiwa amezama kwenye tafakari, muda wote Carlos na Jacky walikuwa wakimwangalia kwa makini huku wakisubiria kusikia jibu lake. Mara Jasmine akainua uso wake kumtazama Carlos huku akilazimisha tabasamu.

“Sawa, nitajaribu,” alisema huku akishusha pumzi ndefu kana kwamba alikuwa ametoka kwenye mashindano ya mbio ndefu.

“Usiseme utajaribu, tunachotaka ufanye kweli,” Carlos alimsisitiza kwa sauti tulivu lakini yenye kuamuru.

“Sawa, nitafanya,” Jasmine alisema na kuwafanya Jacky na Carlos watazamane na kutabasamu, kisha wakapeana ishara ya kuondoka. Walisimama wakamuaga Jasmine na kuondoka wakimwacha bado yupo katika hali ya sintofahamu.

Walipotoka nje ya ile nyumba ya Jasmine, Carlos na Jacky waliingia kwenye gari lao la kifahari aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe.

Jacky ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari, aliliondoa kwa utulivu na mara tu baada ya kuyaacha maskani ya Jasmine walishika uelekeo wa barabara ya lami iliyokuwa ikielekea kwenye machinjio ya ng’ombe ya Vingunguti.

Katika barabara ile kulikuwa na magari mengi katika muda ule wa jioni yaliyotokea katikati ya mji, hivyo Jacky alilazimika kuendesha gari lake kwa mwendo wa kawaida, japo alikuwa na haraka.

Wakati wakiwa katika barabara ile macho ya Carlos yalikuwa makini sana kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kama kulikuwa na gari lolote au pikipiki iliyoonesha ishara ya kuwafuatilia nyendo zao. Walivuka daraja la Mto Msimbazi na baada ya mwendo wa dakika chache walifika katika eneo la Barakuda.

Kisha walishika barabara ya kuelekea Segerea na baada ya mwendo mrefu hatimaye safari yao iliwafikisha katika makazi yao ya kisasa katika eneo la watu wenye ukwasi. Lile gari likafunga breki mbele ya geti kubwa jeusi la jumba moja kubwa la ghorofa mbili lililozungukwa na miti mirefu ya kivuli na ukuta mrefu wenye usalama wa uhakika.

Muda ule mvua ya wastani ilikuwa inanyesha, hata hivyo haikuwazuia kuingia ndani ya jumba lao la kifahari.

Jacky alibonyeza remote na mara lile geti jeusi likaanza kufunguka taratibu, kisha gari akaliingiza lile ndani ya uzio mrefu wa lile jumba uliokuwa umefungwa mfumo maalumu ya umeme wa kuzuia wezi juu yake.

Itaendelea...
Hahahahaha Asante Bishop wangu Yusuph na pole mno na kazi
 
Hahahahahahahaa...i saw this coming. Ndo maana nlivyoona comment ya Shunie tu kila sekunde nkawa narefresh uzi nkijua fika kua episodes zinashuka soon.
Tater rudi nyumbani ndugu yangu, kushanoga[emoji23][emoji23][emoji23]

the Legend☆
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom