Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Mambo yamekuwa mambo, ni nini kipo nyuma ya sakata hili? Jacky na mumewe Carlos wanapanga kufanya nini? Hakika hiki ni kizungumkuti...
Iko poa sana mkuu. Kama kawaida nimependa sana creativity yako kwenye kuelezea uzuri wa Jacky na alivyopendeza, yani 'visualization' kama ulivyotupa somo siku ile[emoji2]

the Legend☆
 
Kizungumkuti!

Na Bishop Hiluka

“Hii ni trela tu, picha kamili keshokutwa! Hakyamungu keshokutwa hakai mtu hapa… mi naapa! Nitakunywa na nitatembea uchi ukumbi mzima kama mademu wakinimaindi poa tu, au vipi kichaa wangu?” Kabwe alipiga kelele kilevi, wakati huo huo Liston alikuwa analazimisha kumshika matiti dada mmoja aliyepita karibu yake…

Fuatilia stori hii hadi mwisho ya kusisimua kuyajua yote yanayoleta kizungumkuti...

KATIKATI ya jiji la Dar es Salaam hali ya hewa ilikuwa ya joto sana kama kawaida, hata katika majira yale ya saa tano za asubuhi. Asubuhi ile pilika pilika za watu zilikuwa zimeshamiri katikati ya jiji hilo kubwa zaidi Tanzania, na hivyo kulifanya kuchangamka sana kama ilivyokuwa kawaida yake.

Katika eneo la Mnazi Mmoja, barabara ya Lumumba kulionekana msululu mrefu wa magari, zikiwemo daladala zilizokuwa zikizunguka kutokea mtaa wa Uhuru katika kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja na kupita barabara ya Bibi Titi kabla hazijaingia katika mtaa wa Mkunguni na kisha kutokea barabara ya Lumumba.

Katika barabara ile ya Lumumba, gari dogo la kifahari aina ya BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati lililotokea katika barabara ya Morogoro kwa mwendo wa taratibu na kujiunga katika msululu ule, kisha lilichepuka na kwenda kusimama chini ya miti ya kivuli iliyokuwa imepandwa kando ya ile barabara.

Hata hivyo, dereva wa gari lile alionekana kutoridhika na eneo lile, akaanza kutafuta sehemu nzuri zaidi na baadaye alikwenda kuliegesha gari lake kwenye eneo lililokuwa na magari mengine mawili matatu yaliyokuwa yameegeshwa pale, na vijana kadhaa walionekana wakiosha magari.

Vijana wawili waosha magari walimfuata haraka yule dereva wa lile gari na kuonekana kumzonga, kila mmoja alionekana akitaka apewe tenda ya kuosha lile gari lakini yule dereva hakuonekana kuwajali. Alibaki ametulia kimya akiusikilizia muungurumo laini wa lile gari kwa kitambo kirefu.

Ndani ya gari lile kulikuwa na watu wawili tu, mwanamume mmoja ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari na mwanadada mrembo sana ambaye alikuwa ameketi pembeni yake kwenye siti ya abiria.

Yule mwanamume alikadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka arobaini na arobaini na tano. Alikuwa mrefu wa futi sita na ushee, mweusi na shababi kwelikweli aliyekuwa na mwenye mwili uliojengeka kwa misuli.

Macho yake yalikuwa makali na alikuwa amevaa kofia ya rangi ya bluu aina ya kapelo, t-shirt ya pundamilia iliyokuwa na miraba ya bluu na myeupe aina ya form six na suruali ya jeans ya rangi ya bluu. Miguuni alikuwa amevaa buti ngumu za ngozi zilizokuwa na rangi nyeusi.

Mwanamume yule aliitwa Carlos Mwamba na aliendelea kutulia kwenye siti yake nyuma ya usukani akiwa ameibana njiti moja ya kiberiti kwenye pembe ya mdomo wake, huku akiendelea kuusikilizia muungurumo laini wa lile gari.

Kushoto kwa Carlos Mwamba, kwenye ile siti ya mbele ya abiria yule mrembo aliyekuwa ameketi aliitwa Jackline Mgaya na alikuwa mke wa ndoa wa Carlos, wakiwa wameoana takriban miaka mwili iliyokuwa imepita.

Jackline au kama alivyopenda kujulikana kwa kifupi kwa jina la Jacky alikuwa na umri usiozidi miaka therathini, alikuwa mrefu na mweupe mwenye haiba nzuri ya kuvutia sana.

Alikuwa na nywele nyeusi za kibantu alizokuwa amezikata vizuri na kubaki ndogo ndogo na hivyo kumfanya aonekane mzuri wa asili. Alikuwa na sura yake ya duara na macho makubwa ya kike na legevu yaliyokuwa yamezungukwa na kope ndefu na nyeusi.

Pua yake ilikuwa ndogo na iliyochongoka mfano wa pua ya kihabeshi na mdomo yake ilikuwa laini yenye maki na kingo pana kiasi zilizokuwa zimekolezwa kwa lipstick ya rangi ya chocolate pamoja na vishimo vidogo mashavuni mwake vilimfanya azidi kuonekana mrembo zaidi.

Jacky alikuwa na masikio madogo yasiyochusha aliyokuwa ameyatoga na kuyavalisha hereni kubwa za kitamaduni zilizokuwa na umbo la mviringo. Alikuwa amevaa blauzi nyepesi ya arangi ya pinki iliyoyaficha vyema matiti yake imara yenye ukubwa wa wastani yaliyokuwa na chuchu nyeusi imara zilizosimama kikamilifu ndani ya blauzi ile.

Shingoni alikuwa kavaa mkufu mwembamba wa dhahabu uliokuwa umeizunguka ile shingo nyembamba na kidani cha dhahabu kilichokuwa na herufi ya “J” kilikuwa kimepotelea katikati ya uchochoro mdogo wa yale matiti.

Kwenye mkono wake wa kushoto alikuwa amevaa bangili kadhaa za pembe na vidole vyake viwili vya mkono huo alikuwa amevaa pete ndogo za madini ghali ya tanzanite na green tourmaline.

Mkono wake wa kulia alivaa saa ndogo ghali na nzuri ya kike aina ya Cartier La Dona, ambayo bei yake ilikuwa si haba kama angeamua kuibadili kwa pesa za madafu, kwani ilikuwa imemgharimu kiasi cha dola za Marekani 137,000.

Cartier La Dona Watch ilikuwa ni saa ghali sana iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu nyeupe ya Karati 18 ikiwa na kesi imara iliyokuwa na milimita 27 kwa 29 na mkanda wake pia ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu nyeupe, ikiwa na gerentii ya miaka hamsini.

Alikuwa ameinunua nchini Switzerland walipokwenda kwenye fungate muda mfupi tu baada ya ndoa yao iliyoacha gumzo jijini Arusha na kwenye viunga vyake.

Gari ikiwa bado inaunguruma taratibu Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kutazama nje kwa kitambo fulani huku macho yake yakielekea moja kwa moja kwenye jengo la ghorofa la Benki ya Biashara.

Alilitazama lile jengo kwa makini akionekana kama aliyekuwa akijiuliza jambo kuhusiana na lile jengo, kisha aliyashusha macho yake kuutazama mkoba wake mzuri wa kike wa rangi ya pinki uliokuwa umelala juu ya mapaja yake mazuri.

Aliufungua ule mkoba na kutoa humo mkebe mdogo wa duara wa rangi nyekundu kisha aliinua macho yake kujitazama kwa kitambo kifupi kwenye kioo cha lile gari cha katikati kinachotumika kuangalia nyuma huku akigeuza geuza uso wake pembe zote.

Alikunja uso wake huku akiminya midomo yake mizuri yenye maki, na hapo mashavu yake yakapiga misingi, pembe za midomo yake zikafinya, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akigeuka kumtazama Carlos aliyekuwa ametulia tuli kama maji mtungini na kuachia tabasamu bashasha.

Carlos aliendelea kutulia pale nyuma ya usukani akionekana kuwaza mbali sana, alimtupia jicho Jacky mara moja tu, kisha akayahamisha macho yake na kutazama kwenye lile jengo la Benki ya Biashara huku sura yake ikiwa haioneshi tashwishwi yoyote.

Jacky alimtazama Carlos kwa makini kisha akaufungua ule mkebe akatoa vipodozi na kuanza kujiremba akiongezea urembo kwenye sura yake huku akijitazama kwenye kile kioo cha gari cha katikati kinachoonesha nyuma.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Tupo pamoja Bishop....shukrani sana ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Am waiting hiko kizungumkuti....

Sent using Jamii Forums mobile app

Kizungumkuti! - 6

Na Bishop Hiluka

“Umelijuaje jina langu?” hatimaye Yusuf aliuliza kwa udadisi huku akizidi kumkazia macho Jacky.

Jacky aliangua tena kicheko hafifu na kunyoosha kidole chake kuonesha beji maalumu iliyokuwa imechomekwa kwenye shati la Yusuf katika kifua chake ikiwa imeandikwa jina lake.

"Si hiyo beji uliyovaa kwenye shati lako. Au wewe siyo Yusuf?" alisema Jacky huku akiwatupia jicho wateja wengine waliokuwa wakihudumiwa kwenye kaunta zingine.

"Hmm, mimi ndiye. Karibu sana, sijui nikusaidie nini, dada…?" alisema Yusuf na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Jacky alitoa tena kitambaa chake na kufuta jasho jepesi lililokuwa likimtoka, akageuza shingo yake kuwatazama wateja waliokuwemo ndani ya ile benki kisha akampenyezea Yusuf ile kadi kwa uficho akihakikisha hakuna mtu mwingine zaidi ya Yusuf aliyeona kitendo kile.

Endelea...

Yusuf alimtazama Jacky kwa mshangao na kuipokea ile kadi, aliiangalia kwa makini kwa kitambo kifupi kisha akainua uso wake kumtazama Jacky akiwa na uso wenye maswali.

Jacky aliachia tabasamu kabambe na kujilegeza. "Dont worry, call me anytime when you get chance, there’s something important we need to talk," (Usihofu, nipigie wakati wowote utakapopata nafasi, kuna kitu muhimu tunahitaji kuongea) alisema Jacky kisha akageuka na kuanza kuondoka eneo lile haraka kabla Yusuf hajasema lolote.

Yusuf alitaka kusema neno lakini alisita na kubaki akimkodolea macho Jacky wakati alipokuwa akitembea kwa madaha huku akili ya Yusuf ikijikuta ikipumbazika mno na mtikisiko maridhawa wa mwili wa Jacky.

Yusuf aliendelea kumsindikiza Jacky kwa macho na kwa utulivu hadi pale alipofungua mlango na kutoka nje ya lile jengo la benki, kisha aliitupia tena jicho la haraka ile kadi na kuitumbukiza mfukoni. Akaendelea kupokea hundi za wateja wengine.

Jacky alipotoka nje ya lile jengo la benki alitembea kwa madaha, tembea yake ilikuwa adimu kuipata kwa wasichana wengi ambao pamoja na kujikwatua, bado walishindwa kupata miondoko kama yake. Tembea ya Jacky iliwafanya watu wageuze shingo zao kumtazama alipokuwa akipita huku macho yao yakishindwa kuamini kile walichokuwa wamekiona, ni kama walikuwa wamemuona malaika.

Kila alikopita, wazee kwa vijana walikuwa wakibabaika, na hawakuisha kugeuza vichwa vyao ili kuustaajabia mwili wake jinsi ulivyoumbika! Alikuwa tofauti sana na wasichana wengine wengi ambao walijiona na kujikweza juu ya kila kiumbe duniani, wasiridhike hata kukanyaga ardhi.

Wakati Jacky alipokuwa akivuka barabara ya Lumumba kuelekea lilipokuwa limeegeshwa gari lao, kuna gari moja dogo lilimpita na muda ule dereva alijikuta akimshangaa na kuivamia pikipiki ya magurudumu matatu aina ya Bajaj iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara, akairusha kule.

Kidogo lizuke vurumai kubwa katika ya yule dereva na wananchi wenye hasira, akiwemo dereva wa Bajaj, vurumai ambalo lingeweza kuigeuza sehemu ile kuwa Mogadishu, badala yake watu wote walisahau kuhusu ile ajali na kujikuta wakigeuza vichwa vyao kuangalia kazi ya Mungu ilivyotendeka vyema katika mwili wa Jacky huku wengine wakipiga mbinja.

“Dah, tuacheni utani jamani, ilikuwa haki ya dereva kupotea njia!” mwanamume mmoja wa makamo alisema kwa sauti ya juu na kuwafanya watu waliokuwa na hasira kuanguka kicheko.

Hata hivyo, Jacky hakujishughulisha nao, aliendelea na safari yake kwani hali kama ile alikwishaizoea, alifika lilipo gari lao na kufungua mlango wa abiria, akaurusha mkoba wake kwenye siti ya nyuma.

Aliminya midomo yake yenye maki na kuachia tabasamu wakati alipokuwa anaingia kwenye gari na kuufunga mlango kisha alifunga mkanda wa siti na kumtazama Carlos kwa tabasamu.

"Let’s go, my love," (Twende, mpenzi) alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Carlos alimtazama Jacky kwa makini na kuliondoa gari taratibu bila kusema neno. Kisha aliiacha barabara ya Lumumba na kushika uelekeo wa upande wa kulia akiufuata mtaa wa Mkunguni.

Baada ya mwendo mfupi wa safari yao aliyafikia makutano ya mtaa ule wa Mkunguni na barabara ya Bibi Titi Mohammed, mbele ya Soko la Kisutu. Carlos alichepuka na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ya Bibi Titi Mohammed.

Katika barabara ile ya Bibi Titi Mohammed Carlos alilazimika kupunguza mwendo kutokana na msongamano mkubwa wa magari, alitazama nyuma kupitia kioo cha katikati cha gari kinachoruhusu kuona nyuma ili kuchunguza kama kulikuwa na chochote alichokitilia mashaka au lah!

Alishtuka sana baada ya kuhisi kulikuwa na jambo lisilo la kawaida, alitazama kwa makini na aliweza kuliona gari aina ya Toyota Land Cruiser Pick-up la rangi nyeusi likiwa katika foleni nyuma yao, alikumbuka kuliona gari lile tangu alipotoka barabara ya Lumumba na kuingia katika mtaa wa Mkunguni.

Hata hivyo, hakutaka kumshtua Jacky, aliendesha kimya kimya hadi walipozifikia taa za kuongozea magari barabarani katika makutano ya barabara za Uhuru na Bibi Titi Mohammed. Pale kwenye makutano Carlos walishindwa kuvuka kwa kuzuiwa na taa nyekundu za kuongozea magari barabarani.

Aliitupia macho saa yake ya mkononi na kuminya midomo yake huku akitazama tena nyuma yake kupitia kile kioo cha katikati cha gari kinachoruhusu kuona nyuma, hakuliona lile gari.

Alipogeuza shingo yake kutazama kando akaliona lile gari Toyota Land Cruiser Pick-up jeusi likiwa limesimama sambamba na gari lake upande wao wa kushoto, na sasa aliweza kusoma maandishi makubwa ya POLISI yaliyokuwa yameandikwa ubavuni.

Mbele ya lile gari kulikuwa na dereva na ofisa mmoja wa polisi na nyuma ya lile gari kulikuwa na maofisa watano wa polisi waliokuwa wameketi na walishika bunduki aina ya SMG zilizotundikwa begani na kulalia vifuani.

Wale askari walikuwa wakilitazama lile kwa makini sana. Hapo akili ya Carlos ilianza kupoteza utulivu taratibu kadiri lile gari lilivyoendelea kusimama pale. Jacky alishtuka na kugeuza shingo yake kutazama kule lilikokuwa lile gari la Polisi baada ya kumuona Carlos akioneshwa kubabaika kidogo.

Carlos alikuwa akihisi kijasho chepesi kikimtoka usoni, alitoa kitambaa na kufuta jasho usoni huku akiendelea kuwachunguza wale askari wenye mitutu ya bunduki kwa makini sana huku akijaribu kuyasoma mawazo yao.

Mara taa ya kijani ya kuongozea magari ikawaruhusu kupita, Carlos akashusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza gia huku akiliondoa gari lake, alizivuka zile taa na kushuhudia lile gari la Polisi likifuatia nyuma yake, alipokwenda mbele kidogo akapunguza mwendo na kukata kona kuingia mtaa wa Sofia Kawawa upande wake wa kushoto ili kuona kama alikuwa anafuatiliwa.

Lile gari la Polisi nalo lilipunguza mwendo na kuingia kufuata uelekeo ule ule japokuwa lilikawia kidogo kuingia. Tukio lile lilimfanya Carlos ahisi kuishiwa nguvu ingawa hakuwa na uhakika kama wale Polisi walikuwa wakimfuata yeye, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini.

Itaendelea...

Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
 
Kizungumkuti! - 7

Na Bishop Hiluka

Mara taa ya kijani ya kuongozea magari ikawaruhusu kupita, Carlos akashusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza gia huku akiliondoa gari lake, alizivuka zile taa na kushuhudia lile gari la Polisi likifuatia nyuma yake, alipokwenda mbele kidogo akapunguza mwendo na kukata kona kuingia mtaa wa Sofia Kawawa upande wake wa kushoto ili kuona kama alikuwa anafuatiliwa.

Lile gari la Polisi nalo lilipunguza mwendo na kuingia kufuata uelekeo ule ule japokuwa lilikawia kidogo kuingia. Tukio lile lilimfanya Carlos ahisi kuishiwa nguvu ingawa hakuwa na uhakika kama wale Polisi walikuwa wakimfuata yeye, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini.

Endelea...

Aliongeza mwendo hadi alipofika kwenye makutano ya mtaa wa Sofia Kawawa na Indira Ghandi, akaelekea upande wa kulia na kutokea katika Mtaa wa Nkrumah. Kisha aliifuata barabara ya Nkrumah akionekana kurudi kwenda kuungana tena na barabari ya Bibi Titi Mohammed.

Kwa kuwa hakukuwa na msongamano mrefu wa magari katika barabara ile, Carlos aliongeza mwendo hadi alipozifika taa za barabarani za kuongozea magari katika makutano ya barabara za Nkrumah na Bibi Titi Mohammed.

Aligeuza shingo yake kutazama nyuma na kuliona lile gari la Polisi likiingia katika barabara ile ya Nkrumah na kukata kona kuelekea upande wa kushoto likielekea kwenye mzunguko wa barabara katika mnara wa saa maarufu kama Clock Tower.

Hapo Carlos alishusha pumzi za ahueni na kuachia tabasamu huku akigeuza shingo yake kumtazama Jacky. Waliangaliana na kujikuta wakiachia kicheko hafifu.

Haikuchukua muda zile taa za barabarani za kuongozea magari pale Nkrumah na Bibi Titi Mohammed zilimuashiria Carlos kupita. Alipita akiifuata barabara ile ya Nkrumah na mara kwa mara akitupia jicho kwenye kioo cha ubavuni kutazama nyuma yake kama kulikuwa na gari lolote alilolitilia shaka likimfuatilia.

Hakuliona gari la namna hiyo, hivyo aliamini kuwa hali ilikuwa shwari, alizidi kusonga mbele katika barabara ile ya Nkrumah akikatisha katikati ya majengo ya ghorofa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Wakati wakiivuka reli katika eneo la Goldstar Carlos aligeuza shingo yake na kumtazama Jacky ambaye muda wote alikuwa mtulivu sana isivyo kawaida.

How was it? Was it successful?” (Ilikuwaje? Ulifanikiwa?) Carlos alimuuliza Jacky huku akimkazia macho.

Oh C’mon, Carlos! What’s the hurry, my love?” (Oh Carlos, haraka ya nini, mpenzi wangu?) Jacky alijibu kwa sauti tulivu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani na kuegemeza kichwa chake kwenye kioo cha dirisha.

Carlos aliachia tabasamu huku akiyahamisha macho yake kutoka kwa Jacky na kuyaelekeza kutazama barabarani.

Hatimaye walifika kwenye taa za kuongozea magari barabarani katika makutano ya barabara ya Nyerere na mitaa ya Msimbazi, Nkrumah na Gerezani. Gari lake likasimama usawa wa jengo la ofisi za Selous Safari Company.

Eneo lile kulikuwa na askari wa usalama barabarani waliokuwa wametanda wakisimamisha magari. Carlos alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiwatazama wale askari wa usalama barabarani waliotapakaa katika eneo lile.

Askari mmoja ofisa wa ukaguzi wa magari barabarani aliyekuwa na nyota mbili mabegani kwake akiwa amevaa koti refu alipiga hatua zake taratibu kulisogelea gari la Carlos, alifika na kuonekana akilichunguza kwa macho.

Kisha alilizunguka na kwenda nyuma huku akizidi kulichunguza kwa jicho la hadhari, hatimaye alikuja kwa mbele kwenye dirisha la Carlos na kumuashiria Carlos kwa mkono kuwa akaegeshe gari lake mbele kando ya barabara baada ya kuvukaa zile taa.

Carlos aliitazama saa yake ya mkononi na kusonya, kwani siku hiyo alikuwa na mambo mengi ya kushughulikia, hivyo kuegesha gari lake kwa ajili ya ukaguzi ilikuwa ni namna fulani ya kumchelewesha. Wakati huohuo askari wa barabari aliyekuwa akiongoza magari aliyaruhusu magari yaliyotoka Mnazi Mmoja.

Carlos aliliondoa gari lake na kuvuka zile taa kisha akaenda kuliegesha kando ya Barabara ya Nyerere, jirani na jengo zilizopo ofisi za Davis and Shirtliff (T) na Reni International. Na hapo akakuta magari mengine kadhaa yaliyokuwa yamesimamishwa kando ya ile barabara yakikaguliwa na askari wengine wa usalama barabarani.

Carlos alisubiri pale kwa kitambo kifupi huku akionekana kukerwa, hatimaye yule ofisa wa usalama barabarani alifika na kuanza kulizunguka lile gari na kwenda nyuma huku akiwa analichunguza kwa jicho la hadhari, kisha alikwenda moja kwa moja kwenye dirisha la Carlos.

“Naomba leseni yako ya udereva,” alisema yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani huku akiinaama kidogo kumtazama Carlos.

Carlos alimtazama yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani kwa makini huku akionesha kujiamini. “How are you, Officer Lutter?” alimsalimia yule ofisa kwa sauti yake nzito na tulivu huku akitoa leseni yake na kumpa.

Yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani alishtuka kidogo na kumtazama Carlos kwa makini kisha akaachia tabasamu. “Ooh, Mr Mwamba! It’s you, my boss?” alisema huku akijiegemeza kwenye mlango wa dereva.

“Kwa nini hukuniambia kama ni wewe mzee wa mishemishe! Kwema lakini?” aliongeza yule askari mkaguzi wa magari barabarani huku akiangua kicheko hafifu kabla hata Carlos hajajibu.

“Kwema tu, mimi pia sikuwa nimekutambua kabla, nimeshtuka baada ya kusikia sauti yako,” Carlos alisema huku akiachia tabasamu.

Wakati wakiendelea kusalimiana askari mwingine wa usalama barabarani mwenye cheo cha Koplo aliyekuwa ameshika mkononi mashine ndogo ya kielektroniki ya kutolea risiti papo hapo baada ya malipo alisogea.

Alifika na kuanza kulichunguza lile gari kwa jicho la hadhari, kisha alizunguka hadi upande wa pili na kusimama kwenye dirisha la Jacky, alimtazama Jacky na macho yao yakakutana.

Jacky aliachia tabasamu bashasha kumpumbaza yule askari, na kwa kweli hila yake ilifanikiwa, kwani yule askari alionekana kubabaika kidogo, alilamba midomo yake kwa matamanio huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Yule askari aliendelea kumkodolea macho ya tamaa Jacky huku akionekana kuhemukwa na tamaa za kimwili, hata hivyo alinywea kidogo baada ya kumtazama Carlos aliyekuwa akizungumza na bosi wake, Ofisa Lutta walioonekana kufahamiana.

Japo Jacky alikwishayasoma mawazo ya yule askari wa usalama barabarani lakini aliendelea kumtazama kwa namna ambayo ilizidi kumpumbaza zaidi, kisha alijifanya kuyakwepa macho yake na kuangalia chini kwa aibu huku akiachia tabasamu la chati.

Muda ule ule yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani alimruhusu Carlos kuendelea na safari yake huku akimtaka amtafute mwisho wa wiki. Bila ya kupoteza muda Carlos aliachia tabasamu na kumuaga yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani kwa kumpungia mkono kisha aliliondoa gari lake kwa madaha kutoka eneo lile akiifuata barabara ya Nyerere.

Wakati akiondoka alitazama nyuma kupitia vioo vya ubavuni vya gari lake na kuwaona wale maofisa wa usalama barabarani wakiyasimamisha magari mengine huku wengine wakiendelea na ukaguzi wa magari yaliyokuwa eneo lile.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 8

Na Bishop Hiluka

Muda ule ule yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani alimruhusu Carlos kuendelea na safari yake huku akimtaka amtafute mwisho wa wiki. Bila ya kupoteza muda Carlos aliachia tabasamu na kumuaga yule ofisa mkaguzi wa magari barabarani kwa kumpungia mkono kisha aliliondoa gari lake kwa madaha kutoka eneo lile akiifuata barabara ya Nyerere.

Wakati akiondoka alitazama nyuma kupitia vioo vya ubavuni vya gari lake na kuwaona wale maofisa wa usalama barabarani wakiyasimamisha magari mengine huku wengine wakiendelea na ukaguzi wa magari yaliyokuwa eneo lile.

Endelea...

Carlos alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akiongeza mwendo wa gari lake kulipita lori la mafuta lililokuwa mbele yao wakati wingu zito la mvua likianza kutanda angani.

Muda huo Jacky alikuwa ameanza kuchukuliwa na mawazo, alikuwa anawaza kuhusu kazi iliyokuwa mbele yao na jinsi alivyohangaika kupata taarifa za kibenki katika Benki ya Biashara tawi la Lumumba.

alikumbuka siku mbili zilizokuwa zimetangulia kabla hawajaenda pale Benki ya Biashara tawi la Lumumba, yeye na Carlos walikuwa katika chumba fulani nyumbani kwao kilichokuwa kikitumika kama ofisi maalumu na maktaba ya siri ambayo ilikuwa na kila aina ya ulinzi, na ili kuingia mle ndani ilikuwa ni lazima ubofye namba fulani za siri zilizokuwa kwenye kisanduku kidogo chenye namba pembeni ya mlango.

Ndani ya ile ofisi Jacky na mumewe Carlos walikuwa wameketi, Jacky aliketi kwenye kiti kirefu cha ngozi halisi cha kiofisi chenye magurudumu madogo yaliyokiwezesha kusogea na kilikuwa cha kuzunguka, akiwa kazini huku wote wakijipongeza kwa Whisky.

Kwa mtazamo wa kawaida tu ungeweza kudhani ilikuwa ni ofisi ya kawaida tu yenye samani chache za kiofisi ikiwa na kiyoyozi aina ya Singsung kilichokuwa kikisambaza hewa safi.

Ofisi ilikuwa na zulia zuri la rangi nyekundu sakafuni, meza kubwa ya kiofisi ambayo juu yake kulikuwa na kompyuta mbili, IMac Retina 5K ya inchi 27 na PC aina ya Acer i5 yenye kioo cha flat.

Zile kompyuta zilikuwa zimefungwa mfumo maalumu wa udukuzi wa taarifa za kibenki uliokuwa ukifuatilia taarifa mbalimbali za fedha na kuhamisha fedha kutoka akaunti moja na kuzipeleka kwenye akaunti nyingine.

Kwa kutumia mfumo ule Jacky alikuwa ametengeneza kirusi maalumu aina ya Trojans kilichofanya kazi ya kuiba taarifa za kibenki baada ya kutumwa kwenye kompyuta za benki husika kikiwa kama keyloggers na RAT (Remote Administration Tools).

Keylogger ulikuwa ni mfumo uliosimamia keys fulani ambazo kama mtu angebonyeza kwenye keyboard yake angeziingiza kwenye rekodi, na kisha bila kujua angejikuta akituma maelezo kwa wadukuzi.

Na pale ambapo Keyloggers zilionekana kushindwa kufanya kazi ipasavyo ndipo RAT iliweza kupenya kwani ilikuwa ni hatua ya juu ya keylogger iliyosimamia shughuli zote za kiudukuzi. Kwa kutumia RAT, Jacky aliweza kujiunganisha kwenye mfumo wa benki mbalimbali bila kujulikana, wakati wafanyakazi wa benki wakiwa mtandaoni.

Ilikuwa rahisi kwa kwake kufanya mashambulizi ya kimtandao kwa kutumia RAT kwenye mfumo wa intaneti kwa watu waliokuwa wakipakua programu mbalimbali au keygens mtandaoni, ingawa siku hiyo ilikuwa tofauti kidogo.

Akiwa pale kwenye meza ya kiofisi iliyokuwa na kompyuta, pembeni yenye kulikuwa na meza ya kioo ya pembe nne ambayo juu yake kulikuwa na chupa kubwa ya Whisky, na chini ya ile meza kulikuwa na magazeti na majarida kadhaa tofauti ya siku za nyuma yaliyokuwa na taarifa za kifedha. Meza hiyo ilikuwa mbele ya kochi moja kubwa la sofa lililokuwa likitazamana na ile meza ndani.

Kwa ukutani juu ya ile meza ya kioo kulikuwa na shubaka la vitabu lililokuwa na nakala chache za magazeti ya siku za karibuni na majarida machache yaliyopangwa kwa ustadi, na kulikuwa na kidau cha wino, mhuri na kichupa kidogo chenye wino mweupe wa kufutia maandishi.

Upande wa kulia kulikuwa na dirisha pana la kioo lililokuwa limefunikwa kwa mapazia mawili mepesi marefu ya rangi ya samawati, pia kulikuwa na rafu kubwa ya mbao iliyosanifiwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Ndani ya rafu ile kulipangwa vitabu na majarida mengi yaliyohifadhiwa pale kwa muda mrefu na mazingira ya mle ndani yalikuwa nadhifu na yaliyovutia kwa mpangilio wake. Upane wa mbele wa ile ofisi kwa juu ukutani kulikuwa na ramani kubwa ya Tanzania iliyokuwa imetundikwa ikionesha maeneo mbalimbali yenye hazina za madini na mifumo ya kibenki.

Pia kulikuwa na jokofu lenye ukubwa wa wastani aina ya LG ambalo lilikuwa limejaa vinywaji mbalimbali, moto na baridi vilivyoweza kumchangamsha yeyote aliyeingia humo hata kama angekuwa amechoka baada ya kazi ngumu.

Katika muda ule Jacky alikuwa nyuma ya kompyuta yake ya IMac Retina 5K akibonyeza bonyeza kwa kitambo kirefu huku akisoma maelezo yaliyojitokeza kwenye screen na kujaribu kuingiza code number fulani ili ku-log in kwenye SWIFT system ya Benki ya Biashara tawi la Lumumba akijaribu kupata taarifa za kifedha, lakini ujumbe uliokuwa ukitokea kwenye screen uliandikwa 'REMOTE PROCEDURE ERROR'.

Hakukata tamaa akajaribu njia nyingine kwa kutumia Open Source Intelligence (OSINT) akaingia code number fulani na mara maneno 'NOT OPERATING' yakatokea kwenye screen yake, akatweta. Kisha aka-log in kwenye mtandao maalumu wa ‘dark web’, ili kuona kama angeweza kupata taarifa na wadukuzi wengine waliofanikiwa kuvunja ngome za kiulinzi za kibenki.

Maelezo aliyoyapata kutoka katika dark web yakamfanya azidi kuchanganyikiwa, akashusha pumzi za ndani kwa ndani huku akijiegemeza kwenye kiti chake. Muda wote ule Carlos alikuwa ameketi kwenye sofa akimtazama kwa makini.

I think I need to find the latest OSINT program, otherwise we’ve to take the risk by going there physically,” (Nadhani ninahitaji kutafuta programu mpya ya OSINT, vinginevyo tutapaswa kwenda wenyewe) Jacky alisema huku akionekana kuchoka.

What happened?” (Kumetokea nini?) Carlos aliuliza kwa wasiwasi.

It’s not working… tomorrow I’ll know what to do,” (Haifanyi kazi… kesho nitajua nini cha kufanya) alisema Jacky huku akichukua bilauri ya whisky na kupiga funda kubwa la whisky huku akisisimkwa.

What will you do?” (Utafanyaje?)

I think I’ll go to the bank and leave a USB stick preloaded with malware near a teller’s desk with the hopes someone will pick it up and plug it into an internal computer…” (Nadhani nitakwenda benki na kuacha USB yenye virusi kwenye dawati la mhudumu nikitumaini ataichukua na kuifungua kwenye kompyuta za ndani…) alisema Jacky huku akiachia tabasamu bashasha.

If this doesn’t work?” (Kama mbinu hiyo haitafanya kazi?) aliuliza Carlos huku akimkazia macho Jacky.

Hmm… let me think,” (Hmm… ngoja nifikirie) alisema Jacky huku aking’ata mdomo wake wa chini.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 9

Na Bishop Hiluka

I think I’ll go to the bank and leave a USB stick preloaded with malware near a teller’s desk with the hopes someone will pick it up and plug it into an internal computer…” (Nadhani nitakwenda benki na kuacha USB yenye virusi kwenye dawati la mhudumu nikitumaini ataichukua na kuifungua kwenye kompyuta za ndani…) alisema Jacky huku akiachia tabasamu bashasha.

If this doesn’t work?” (Kama mbinu hiyo haitafanya kazi?) aliuliza Carlos huku akimkazia macho Jacky.

Hmm… let me think,” (Hmm… ngoja nifikirie) alisema Jacky huku aking’ata mdomo wake wa chini.

Endelea...

Do like this, I know there’s that handsome guy, go find him and make him fall in love with you…” (Fanya hivi, najua yupo yule kijana mtanashati, kamtafute na uhakikishe anaangukia kwenye penzi lako…) alisema Carlos. Jacky alishusha pumzi za ndani kwa ndani huku akifikiria kuhusu kazi ile.

* * * * *

Jioni ya saa kumi na mbili na nusu katika mtaa mmoja eneo la Tabata Segerea nyumba moja nzuri ya kifahari ya ghorofa mbili iliyokuwa imezungukwa na miti mizuri ya vivuli ilikuwa katika hali ya ukimya sana. Ilikuwa katika eneo la makazi ya kisasa ya watu wenye ukwasi, lenye majumba ya kifahari yaliyozungukwa na miti mirefu na kuta zenye usalama wa uhakika.

Nyumba ile ilikuwa imezungukwa na ukuta mrefu uliofungwa mfumo maalumu wa umeme wa kuzuia wezi juu yake usiomwezesha mtu kuona ndani, na ilikuwa na sehemu za wazi zenye bustani nzuri ya maua na nyasi za kijani kibichi zilizokatwa vizuri.

Ilikuwa na madirisha makubwa ya kisasa na baraza kubwa mbele yake iliyopangwa seti moja ya makochi ya sofa ya rangi nyeusi.

Ndani ya uzio wa ile nyumba upande wa kushoto kulikuwa na banda la wazi la kuegeshea magari na kulikuwa na magari madogo matatu ya kifahari, BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati, Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe na Toyota Landcruiser GX V8 lililokuwa na rangi nyeusi.

Sehemu nyingine ya mandhari ya nyumba ile ilikuwa imezungukwa na miti mirefu na mikubwa ya kivuli. Sehemu ya mbele ya hiyo nyumba ilikuwa imezungukwa na bustani nzuri ya maua ya kupendeza na katikati ya bustani hiyo kulitengenezwa njia nzuri ya kutembea kwa miguu kwa matofali madogo madogo yaliyokuwa yanavutia.

Pia kulitengenezwa njia kubwa ya gari iliyotengenezwa kwa ufundi mkubwa iliyokuwa inaanzia sehemu ya getini hadi mbele ya ile nyumba ili kumruhusu dereva ageuze gari pasipo kurudi nyuma.

Ndani ya ile nyumba kwenye sebule kubwa yenye samani zote muhimu za kisasa, Jacky na Carlos walikuwa wameketi wakiwa na bilauri za whisky mkononi na kwenye meza kulikuwa na chupa kubwa ya Whisky na sahani iliyojaa nyama choma za mbuzi.

Carlos alikuwa amevaa bukta ya khaki na singleti nyeupe na Jacky alivaa nguo nyepesi nyeupe ya kulalia iliyolichora vyema umbo lake la kuvutia na na kuifanya nguo yake ya ndani ya rangi ya bluu ionekane bila kificho.

Sebule ile ilikuwa imepambwa na seti mbili za makochi ya sofa ya kifahari yaliyokuwa yamepangwa katika mtindo wa kuizunguka sebule hiyo. Katikati ya ile sebule kulikuwa na meza nzuri ya kioo yenye umbo la duara.

Pia kulikuwa na mapambo mengine mbalimbali yaliyoifanya ile sebule ivutie sana huku madirisha yake makubwa ya vioo yalikuwa yamefunikwa kwa mapazia marefu.

Jacky alikuwa kimya akitafakari kwa kina, Carlos alimwangalia Jacky kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

But you haven’t answered my question, how do you see the guy?” (Lakini bado hujajibu swali langu, huyo bwana unamwonaje?) Carlos aliuliza huku akimtazama Jacky kwa makini.

How?” (Kivipi?) Jacky aliuliza huku akimtazama Carlos kwa mshangao.

“Yaani… unadhani upo uwezekanao wowote wa kumbana na kupata taarifa muhimu?”

Jacky alimeza funda kubwa la whisky na kuweka bilauri juu ya meza kisha aliachia tabasamu. “Kumpata wala haina wasiwasi, na akishapatikana si ndiyo basi tena! Kwani unadhani kwangu atafurukuta?”

Carlos aliachia tabasamu na kuchukua kipande cha nyama choma huku akimtazama Jacky kwa makini zaidi.

Jacky, don’t take this for granted. You can do anything with him and still get nothing. You do not know, maybe he's got a beautiful wife than you…” (Usilichukulie hili jambo kirahisi rahisi hivyo. Unaweza kufanya naye chochote na bado akafurukuta. Hujui, pengine ana mke mzuri kuliko wewe…) Carlos alisema kwa sauti tulivu.

Jacky alimwangalia Carlos kwa kitambo kirefu na kuachia tabasamu lililokuwa limeficha bezo ndani yake.

So you know that he has a wife?” (Kwa hiyo umeshajua kama ana mke?) aliuliza huku akichukua kipande cha nyama choma na kukitumbukiza mdomoni.

I do not know, but that’s something you should consider more carefully, to know his movements, his habits, his potential talents and his dreams,” (Sijui, lakini hilo ni jambo unalopaswa ulichunguze kwa makini zaidi, uzijue nyendo zake, tabia yake, uwezo wake na ndoto zake) alisisitiza Carlos huku akimeza funda kubwa la pombe na kusisimkwa mwili.

Jacky naye aliinua bilauri ya pombe na kuinywa pombe yote iliyobakia kwenye bilauri huku akisisimkwa mwili, alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani na kuirudisha ile bilauri mezani. Kisha akamtazama Carlos kwa makini.

“Naona sasa unataka kuniongezea kazi zingine nisizoziweza,” alilalamika Jacky huku akijiegemeza kwenye kochi.

Carlos alimkazia macho, akakunja uso wake na kutengeneza matuta madogo madogo usoni kwake. Macho yake yalikuwa yanawaka kwa hasira. “Utoto huo! Kazi zipi usizoziweza?”

“Si kama hizo za kufuatilia nyendo zake, sijui tabia yake na ndoto zake. Basi itabidi nihamie kabisa nyumbani kwake,” alisema Jacky kwa kulalamika huku akipigwa miayo ya uchovu.

“Hamia! Potelea mbali, hamia kwake hata kesho. Tunahitaji pesa, Jacky, tunahitaji bilioni moja na kuendelea! I am ready to take a knife and cut off my mother's curfew for such amount…” (Niko tayari hata kushika kisu na kumkata koromeo mama yangu mzazi kwa fedha kama hiyo…) alisema Carlos huku macho yake yakiwaka kwa ghadhabu.

“Sembuse eti kumruhusu mke wangu ahamie kwa mwanamume nisiyemjua! Hamia hata kesho,” aliendelea kusema huku akionekana kupandwa ghadhabu.

Jacky alitaka kusema neno lakini alipomtazama Carlos kwa makini akasita, alishusha pumzi za ndani kwa ndani na kubaki kimya. Alianza kuhisi hofu na ubaridi fulani wa woga wa aina yake vikimtambaa mwilini, nywele zake pia zilikuwa zimemsimama kichwani kwa hofu.

Carlos aliigundua hofu aliyokuwa nayo Jacky, hivyo aliamua kumsogelea na hapo hapo mikono yake yote miwili ikaanza kufanya ziara ya kwenye mwili wa Jacky, huku mkono wa kulia ukienda moja kwa moja kwenye kifua cha Jacky.

Please forgive me, my love, I did not intend to scare you, you know precisely how much I love you so much and I do not want to see another man navigating to this body,” (Tafadhali nisamehe, mpenzi wangu, sikukusudia kukutisha, unajua kiasi gani nakupenda sana na nisingependa kuona mwanaume mwingine akijivinjari kwenye mwili huu) Carlos alisema kwa namna ya kumbembeleza Jacky.

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 10

Na Bishop Hiluka

Carlos aliigundua hofu aliyokuwa nayo Jacky, hivyo aliamua kumsogelea na hapo hapo mikono yake yote miwili ikaanza kufanya ziara ya kwenye mwili wa Jacky, huku mkono wa kulia ukienda moja kwa moja kwenye kifua cha Jacky.

Please forgive me, my love, I did not intend to scare you, you know precisely how much I love you so much and I do not want to see another man navigating to this body,” (Tafadhali nisamehe, mpenzi wangu, sikukusudia kukutisha, unajua kiasi gani nakupenda sana na nisingependa kuona mwanaume mwingine akijivinjari kwenye mwili huu) Carlos alisema kwa namna ya kumbembeleza Jacky.

Endelea...

Kisha aliupeleka mkono wake kwenye chuchu laini za Jacky zilizosimama kwa utulivu juu ya milima miwili isiyofahamu adha yoyote ya volkano.

But since we need money, I have to let you go to another man, I hope you know precisely what I mean, my darling,” (Lakini kwa kuwa tunahitaji pesa, nalazimika kukuruhusu kwenda kuonana na mwanamume mwingine, natumaini unajua hasa namaanisha nini, mpenzi wangu) Carlos alizidi kusisitiza huku akiachia tabasamu pana.

Jacky hakusema neno bali alibaki kimya huku akimtazama Carlos kwa makini. Hata hivyo, Carlos hakusubiri jibu la Jacky, alipeleka mkono wake kwenye tumbo la Jacky na kuanza kukipapasa kitovu chake laini chenye kishimo kidogo kilichotengeneza ziada nyingine ya uzuri wake.

Kisha mkono wa pili ulikwenda moja kwa moja kiunoni na aliigusa nyonga yake laini iliyokuwa na mifupa miteke iliyopakana na mzigo imara wa makalio yaliyotuama vyema. Wakati akiendelea kumpapasa, Jacky akaamua kuvunja ukimya huku akimtazama Carlos usoni.

“Carlos!” Jacky aliita kwa sauti laini ya mahaba.

Yes, my love,” Carlos aliitikia kwa sauti yake nzito iliyokuwa na kila aina ya kiashiria cha kuhemkwa na tamaa za kimwili.

I’m tired with this life and I need to live a normal life, you don’t know what I’m going through right now…” (Nimechoshwa na maisha haya na ninahitaji kuishi maisha ya kawaida, hujui napitia magumu gani hivi sasa…) Jacky alisema kwa huzuni na kuongeza.

“Hivi kwa nini tusiachane na maisha haya na tuishi maisha huru ya mke na mume? Tuna shida gani, kama ni pesa tayari tunazo nyingi tu…” Jacky alianza kusema kwa utulivu huku akiipitisha mikono yake nyuma ya shingo ya Carlos na kuzifanya chuchu za matiti yake kukitekenya kifua cha Carlos.

Kitendo kile kikafanya joto kali la mwili wa Jacky limfanye Carlos ajisikie faraja ya aina yake. Carlos alimtazama Jacky machoni na kuyaona machozi yakianza kumlenga machoni.

I understand, my love, but nobody ever felt satisfied with money. We still have many things to do so we need money…” (Naelewa, mpenzi, lakini hakuna aliyewahi kutosheka na pesa. Bado tuna mambo mengi ya kufanya hivyo tunahitaji pesa…) alisema Carlos huku kwa kutumia kiganja chake taratibu alianza kumfuta Jacky machozi.

“…so we don’t have time to rest. We need to work day and night to make sure we have more money,” (…hivyo hatuna muda wa kupumzika. Tunahitaji kufanya kazi mchana na usiku kuhakikisha tunapata pesa zaidi) aliongeza Carlos huku akiendelea kuyafuta machozi kwenye macho ya Jacky.

Jacky aliusukuma mkono wa Carlos kutoka machoni mwake kisha akajisogeza nyuma kidogo huku akimtazama Carlos kwa makini.

You depend on me to complete this mission, so you’ll have to listen to me. This is the last mission and after this you’ll never ask me again, promise?” (Unanitegemea kukamilisha mpango huu, kwa hiyo unapaswa kunisikiliza. Huu mpango ni wa mwisho na baada ya hapo hutaniambia tena, unaniahidi hivyo?) Jacky alisema huku machozi yakianza kumtiririka kwenye mashavu yake, hakujua kwa nini alikuwa akisita sana kuifanya ile kazi.

Promise!” (Nakuahidi) Carlos alisema.

“Baada ya mpango huu kukamilika nataka tuachane na hizi kazi. Nataka tuanze aina mpya ya maisha, I’m dreaming to have a good family and be happy,” (Nina ndoto ya kuwa na familia nzuri na maisha ya furaha) Jacky alisema na hapo Jacky akamsogelea na kuvuta karibu zaidi, kisha ndimi zao zikakutana. Kilichofuata baada ya pale ilikuwa ni sauti ya pumzi zao sambamba na miguno isiyoeleweka ya mahaba.

Kama mtu aliyepandwa na wazimu wa mapenzi, Jacky akaanza kumvua Carlos singleti yake na kuitupilia mbali kisha akapeleka mikono yake kifuani kwa Carlos na kuanza kumpapasa kwa pupa. Carlos alitaka kumzuia lakini Jacky akamng’ata mkono.

Don’t stop me, please make my night beautiful,” (Usinizuie, tafadhali ufanye usiku wangu kuwa wa kupendeza) Jacky aliongea kwa hasira kama mwehu huku akiivuta chini bukta ya Carlos kwa pupa.

I thought we still need to talk and plan our things well,” (Nilidhani bado tunahitaji kuongea na kupanga mambo yetu vizuri) Carlos alinong’ona.

No, we’re done. Now I want to spend time with you, I need you so badly,” (Hapana, tumekwisha maliza, sasa nahitaji kujivinjari na wewe, nakuhitaji vibaya sana) Jacky alisema huku akihema kwa nguvu, muda ule ule alimvuta Carlos na ndimi zao zikaingia tena kazini zikitekenyana taratibu mdomoni.

Japokuwa Carlos alikuwa mtu hatari wa kuogopwa aliyekubuhu katika umafia lakini mbele ya mlimbwende yule, hasa wakati kama ule, alikuwa kama mbwa muoga mbele ya chatu mwenye njaa kali.

Jacky aliinuka na kuvua haraka gauni lake na kulitupa kando na hivyo kubakiwa na nguo yake nzuri ya ndani huku harufu nzuri ya manukato yake ikimshawishi Carlos kuendelea na hatua iliyofuata.

Carlos hakuwa na ujasiri tena wa kupingana zaidi na hisia zake, hivyo taratibu aliupeleka mkono wake ndani ya nguo ya ndani ya Jacky na kuanza kuyatomasa makalio yake laini yaliyoshiba minofu.

Jacky aliachia mguno hafifu wakati mkono mwingine wa Carlos ulipokuwa ukiyatomasa matiti yake taratibu. Kisha Carlos alianza kutembeza taratibu ulimi wake shingoni kwa Jacky na hatimaye sikioni na hapo ikasikika sauti hafifu ya Jacky ya mguno wa mahaba.

Jacky hakuweza kuvumilia tena hivyo haraka akaishusha chini nguo yake ya ndani na kuupeleka mkono wake akiichezea ikulu ya Carlos na kumfanya aanze kuhema ovyo.

Muda mfupi uliofuata walikuwa kwenye kochi kubwa la sofa pale pale sebuleni huku kila mmoja akiwa amepandwa na wazimu wa mapenzi. Mara wakajikuta wakiwa kwenye sayari nyingine ya mahaba mazito iliyokuwa kama kisiwa cha raha kwa ajili yao.

Sebule ile ikajazwa na vilio vya mahaba toka kwa Jacky vilivyoashiria raha ya aina yake aliyokuwa akiipata. Jacky alikuwa msichana mtundu sana aliyemudu vyema mitindo mbalimbali kiasi cha kumfanya Carlos ajihisi kama mvulana wa shule ya msingi.

Hiki kweli ni kizungumkuti, je, nini kitaendelea? Fuatana nami katika safari hii ya kusisimua...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom