Kizungumkuti! - 20
Na Bishop Hiluka
Jacky alifurahi sana na kummwagia Yusuf mabusu mfululizo, kisha kikafuata kitambo kirefu cha kupanga mipango kabambe ya namna ya kufanikisha mambo ya fedha, huku Jacky akitawala mazungumzo. Katikati ya maongezi yao Jacky alishtuka na kuangalia saa yake ya mkononi akapigwa na butwaa.
“Dah, saa tisa usiku!” Jacky alisema na kumshtua sana Yusuf.
“Oh my God, saa tisa! Sijui nitamwambia nini mke wangu! Sijawahi kulala nje hata siku moja na jana nimetoka nyumbani saa kumi na mbili jioni na sijarudi hadi saa hizi! Eeh Mungu nisamehe mja wako,” Yusuf aliwaza huku moyo wake ukijaa hofu…
Endelea...
* * * * *
“
Oh God, help me. What kind of life is this? Why do I live like this?” (Mungu wangu nisaidie. Haya ni maisha gani? Kwa nini ninaishi maisha kama haya?) Jacky alikuwa anawaza huku akilisikilizia tumbo lake lililokuwa dhaifu sana kwa vile usiku uliokuwa umetangulia alikuwa ametia kilevi tumboni na hakuwa amekula chakula.
Ukichanganya na mahaba mazito aliyoyapata kutoka kwa Yusuf usiku kucha yaliyochangiwa na kiu yake ya kutaka kupata taarifa sahihi za mabilioni ya pesa vilikuwa vimemchanganya sana Jacky na kumfanya asahau hata kula.
Kichwa chake kilikuwa kizito sana kutokana na mning’inio (
hang over) uliotokana na uchovu wa pombe kali alizokuwa amekunywa usiku wa siku iliyotangulia. Wakati akiyawaza hayo ilikuwa tayari imeshatimia saa moja ya asubuhi, alikuwa amerudi nyumbani takriban nusu saa tu iliyokuwa imepita.
Alipofika nyumbani asubuhi ile jambo la kwanza alilofanya ilikuwa ni kukimbilia moja kwa moja bafuni kujimwangia maji ya uvuguvugu ili apate nguvu mpya, kwani mwili wote ulikuwa unamuuma kama kidonda kutokana na gwaride la usiku kucha alilokuwa amechezeshwa na Yusuf.
Kiukweli, mwanzoni alikuwa amemchukulia poa Yusuf kwa kudhani asingeweza kumudu dakika tisini za mchezo, kumbe alikosea sana kwani Yusuf aliweza kwenda hadi dakika mia moja na ishirini, na bado walipoingia kwenye matuta hakupatikana mshindi.
Jacky alikuwa amekutana na muziki wa Yusuf usio wa kitoto, kwani Yusuf alijua kucheza ngoma zote, msondo, ndekule, mdundiko, sindimba na nyinginezo pasipo kuomba poo na alikuwa hachoki utadhani alikuwa na mapafu kama ya farasi.
Asubuhi ile Jacky alipomaliza kujimwagia maji alijifunga khanga moja kifuani na taulo kiunoni na kuelekea jikoni ambako alianza kuandaa kifungua kinywa. Wakati alipokuwa mbioni kumaliza zoezi lile la kuandaa kifungua kinywa alishtushwa na mikono ya mtu iliyomshika kiunoni.
Aligeuka haraka nyuma huku moyo wake ukianza kupoteza utulivu, akamuona Carlos akiwa amesimama nyuma yake akitabasamu na hapo tabasamu jepesi likachomoza usoni kwake.
Kumbe muda ule alipokuwa akiandaa kifungua kinywa Carlos alikuwa amenyata taratibu kutoka chumbani alikokuwa amelala na kwenda kusimama nyuma yake bila yeye kujua.
Macho ya Carlos yalikuwa na kila dalili za uchovu na alisimama pale akimtazama Jacky kwa namna ambayo ilimshtua kidogo Jacky. Carlos alimtazama Jacky kwa kitambo kirefu bila kusema neno.
Alikuwa akiitazama hazina matata iliyokuwa imejificha katika umbo matata la Jacky na kujikuta akihisi donge la wivu likimkaba kooni kwake kwa kukubali kumruhusu Jacky kwenda kulala na mwanamume mwingine, eti sababu ya kutafuta pesa.
Kila alipozidi kuutazama kwa makini mwili wa Jacky jinsi ulivyoumbika vyema, ndivyo donge la wivu lilivyozidi kumkaba kooni na kuufanya moyo wake uanze kuumia sana.
“Mbona jana hukurudi nyumbani?” Carlos alijikuta akimuuliza Jacky kwa sauti nzito iliyojaa wivu na hasira. Jacky alimtazama kwa udadisi na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Kazi haikuwa rahisi kama unavyodhani, ilibidi nitumie mbinu ya ziada kumsomesha yule bwana ili anielewe,” Jacky aliongea kwa sauti nyororo yenye kusihi.
“Kwa hiyo baada ya kumaliza kumsomesha ndiyo mkaamua kukesha kabisa! Na usiniambie kuwa uliamua kwenda kavukavu!” Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky kwa wasiwasi.
“Niende kavukavu kwani sijitakii mema!” Jacky aliongea kwa utulivu huku akiruhusu tabasamu lake kuchanua usoni kwake. Kisha alimsogelea Carlos karibu zaidi na kumkumbatia akiizungusha mikono yake kwenye kiuno cha Carlos, akambusu na kugeuka kuendelea na kazi yake ya kuandaa kifungua kinywa.
Carlos alisimama pale kwa kitambo kirefu akimtazama Jacky kwa makini, kisha alilazimisha tabasamu na kuondoka.
Dakika arobaini baadaye Jacky na Carlos walikuwa wameketi kwenye meza ya chakula wakipata kifungua kinywa. Jacky alikuwa mkimya mno wakati wote walipokuwa wakistafustahi asubuhi ile kitendo kilichomshangaza sana Carlos.
Alikuwa akila chakula lakini akili yake haikuonekana kuzama kwenye kile chakula pale mezani badala yake alikuwa akila taratibu kwa kupekua pekua chakula, huku mkono wake mmoja ukiwa shavuni, kuna wakati alikuwa akimtupia macho Carlos na kutabasamu.
Uzoefu wa Carlos kwa Jacky na wasichana warembo wa aina yake ukamwacha njia panda. Alijikuta akishindwa kula na kumtazama Jacky kwa udadisi lakini asielewe ni nini kilichokuwa katika mawazo ya Jacky, mwishowe akashindwa kuvumilia.
“Jacky, kwa nini jana usiku hukurudi, ni nini kilichokufanya ukaamua kukesha na yule bwana hadi asubuhi?” Carlos aliuliza kwa sauti iliyoonesha wazi kuwa sasa wivu kwa Jacky ulikuwa umemtawala.
“Hmm, si nimekwisha kujibu jamani, au kuna kingine? Kama hujapenda ungeniambia, ndiyo maana jana nilikuuliza kama ulikuwa unaona wivu nisiende. Sasa unaponiuliza swali lile lile mara mbili mbili nakuwa sielewi kwa nini ulinituma kufanya kazi ile kama hatuaminiani kiasi hiki!” Jacky alisema kwa utulivu lakini akionekana kukerwa sana na swali la Carlos.
“Siyo hivyo, mpenzi, wewe ni mke wangu tena wa ndoa, ni haki yangu kuhakikisha hupati madhara na unaendelea kuwa usalama, na kama ratiba ilibadilika nilitegemea ungenijulisha kwa simu kuwa hutorudi ili nijue cha kufanya…” Carlos alisema kwa sauti tulivu yenye kusihi.
“Cha kufanya kama kipi! Kwamba na wewe ungetafuta mwanamke mwingine wa kulala naye, siyo?” Jacky alimuuliza Carlos huku akiwa amemtulizia macho.
“Usinielewe vibaya, Jacky…”
“Labda nikwambie ukweli, yule bwana ni mwoga sana japo fedha anazitaka. Hivyo ilibidi nipoteze muda mwingi sana kumsomesha hadi anielewe, nimekuja kushtuka tayari ilikuwa imeshatimia saa tisa usiku, unadhani hapo ningefanyaje?” Jacky alimuuliza Carlos huku akiendelea kumtulizia macho yake.
“Okay nimekuelewa, hebu tuachane na hayo… sasa niambie umemuonaje kakuelewa?” Carlos aliuliza huku akijiegemeza kwenye kiti chake.
“Somo limemuingia sana! Tumeongea mambo mengi na kanipa data zote za kwenye tawi lao na akaunti ambayo tutaweza kuitumia kufanikisha mpango wetu. Kwa kifupi ameonesha ushirikiano mkubwa sana kwa kuwa hata yeye fedha anaitaka.”
“Ni akaunti ipi hiyo aliyokuwa data zake?”
“
The Jacarandah Group…”
“
Wow!” Carlos alijikuta akiruka kwa furaha.
Muda ule Jacky aliinua kikombe chake cha chai ambayo tayari ilikuwa imepoa na kupiga funda kubwa akiimalizia chai yote iliyobaki, kisha alinawa mikono na kufuta midomo wake kwa kitambaa laini.
“Lakini kazi sasa ipo kwenye kuingia pale benki na kutoka na pesa yote hiyo bila kushitukiwa,” Jacky alisema huku akisukumia kando kikombe chake.
“Suala la kutoka na pesa benki wala si kazi, hilo niachie mimi. Mimi ndiye
professional bank robber, nimefuzu mbinu zote za kihalifu na sijawahi kuacha rekodi yoyote ya kuwafanya polisi wanishtukie,” Carlos alisema huku akijipiga piga kifuani katika hali ya kujisifia, kisha akaendelea.
“Kwanza nimefurahi kwa kuwa ni habari muhimu sana kusikia
The Jacarandah Group wanaweka pesa zao kwenye tawi lile, hapo itabidi twende kwa Jasmine tukaongee naye kwa kina sana,” Carlos alisema huku akiinuka kutoka pale kwenye kiti.
“Jasmine yupi?” Jacky aliuliza kwa shauku huku akimkazia macho Carlos.
“Mtoto wa marehemu Kombo, yule rafiki yangu tuliyemzika mwaka jana kule kwenye makaburi ya Vingunguti,” alisema Carlos.
Itaendelea...
Cc
the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater,
Bigjahman moneytalk marybaby,
nipo2,
ram,
kisukari,
Smart911,
Madame S,
carbamazepine,
Astelia,
culture gal ,
Prisoner of hope,
kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes,
Kudo, swahiba92,
ludist,
Toyota escudo,
Clkey,
macson3,
Thad,
boga la kiangazi,
macson3,
Smart911,
Richard irakunda,
skfull,
popie,
Krizy Beat,
hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY@HALELUYA MOSHI
Clkey