FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,230
- 4,368
STORY: I AM THE ONE WHO KILLED THE PRESIDENT
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
WhatsApp: +255621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UKURASA WA KWANZA
Msafara mkubwa wa gari ishirini na tano ulikuwa barabarani kwa mwendo wa kawaida, ilikuwa ni majira ya jioni muda wa saa kumi na mbili wakati kiza kimeanza kuonekana kwa mbali ila bado mwanga ulikuwa wa kutosha.
Ule msafara ulikuwa umembeba raisi wa Tanzania, raisi alikuwa ametoka kwenye ziara yake hivyo ulikuwa ni muda wa kurudi tena ikulu lakini kabla ya kurudi ikulu kuna sehemu moja ambayo alitakiwa kusimama. Kuna walemavu ambao alikuwa ameahidi kuwapatia msaada hivyo sehemu hiyo alitakiwa kusimama kwa dakika thelathini kisha baada ya hapo ndipo alitakiwa kurudi tena ikulu.
Eneo lile lilikuwa limezungukwa na usalama wa taifa wengi na kitengo maalumu kwa ajili ya ulinzi wa raisi kuhakikisha anakuwa salama na anatoka akiwa mzima. Vyombo vya habari kwa mbali vilikuwepo ila hakuna ambaye aliruhusiwa kumkaribia raisi hivyo alianza kuwasalimia wale walemavu na kutoa zawadi ya shilingi milioni kumi kwa kila mmoja, pesa ambazo aliahidi zingeenda kuwasaidia kufungua biashara za kuendeshea maisha yao. Akiwa amefika kwa mtu wa tano ambaye alikuwa ameketi, alihitaji kusalimiana na raisi kabla ya kupewa pesa, walinzi walitaka kumzuia lakini raisi alitoa ruhusa hiyo jambo hilo liweze kufanyika ndipo bwana yule akaanza kumuuliza raisi maswali.
“Ni heshima kubwa wewe kuwepo hapa kuja kutusaidia mheshimiwa, lakini unajisikiaje kuwa raisi wa taifa kama la Tanzania?” raisi mwenyewe hakuwa amejiandaa kukutana na maswali kwa kutegemea watu hao jambo kubwa ambalo wangelifanya ilikuwa ni kumshukuru kwa msaada wake.
“Tanzania ni sehemu ya ndoto kwa watu wengi hivyo hata mimi najisikia fahari kuwa sehemu kubwa ya historia ya taifa hili, kwa maana hiyo naweza kusema kuwa raisi sio jambo jepesi lakini ni jambo la fahari kuliwakilisha taifa bora kama Tanzania”
“Ni kweli wanasiasa wanaweza hata kuua ili kuweza kuingia madarakani hususani kwenye nafazi kama yako?” mwendelezo wa maswali mazito na magumu kama yale ulimfanya raisi kuanza kupandwa na hasira ila aliigiza kufuahia tu jambo lile.
“Usiamini kila unacho ambiwa lakini pia usipuuze kila ambacho unakiona kwa macho yako” ulikuwa msemo kutoka kwa raisi wakati akiwa anainuka baada ya kumkabidhi bwana yule pesa kwenye mkono wake kutoka kwenye kiti ambacho alikuwa amekalia. Raisi baada ya kuinuka alipohitaji kumgeukia mtu mwingine kumpatia zawadi yake aligeuka baada ya kusikia kauli kutoka kwa bwana yule
“Kuwa makini mheshimiwa, siku hizi kuna watu hawawapendi viongozi wa aina yako” raisi alipandwa na hasira, alimgeukia mlinzi wake na kumpatia ishara ya kichwa ila ndani ya sekunde mbili tu lilitokea jambo la kutisha sehemu ile.
Muda ambao raisi alitumia kumpatia ishara mlinzi wake ni muda ambao yeye alikuwa anahitaji kugeuka aweze kuendelea na zoezi lake la ugawaji wa fedha ila ilionekana damu ikisambaa na kuwarukia walinzi na baadhi ya wahanga ambao walikuwa karibu na raisi, ndani ya sekunde mbili walimuona raisi akiwa anashuka chini jambo ambalo liliwafanya walinzi kuikimbilia kwa kasi ile sehemu ambayo raisi alikuwepo. Waliganda kwa muda huduma ya kwanza wakiwa wanakimbia kwa nguvu zao zote kwenda ile sehemu, raisi alikuwa amepigwa risasi ya paji la uso hali ambayo ilifanya eneo lile kutotulia huku watu wakianza kupiga makelele na kukimbia hovyo huku jeshi la polisi wakijaribu kuwatuliza kwani hawakutakiwa kuondoka sehemu ile.
Walinzi walikuwa wanahaha kujua ni wapi mdunguaji alikuwepo mpaka akapata nafasi ya kuweza kumpiga risasi raisi kwenye sehemu kama ile ila ilikuwa mapema kuweza kupata majibu ya haraka. Daktari alijaribu kila namna lakini ndani ya dakika moja alithibitisha kwa kuangalia saa yake na kutaja muda ambao raisi alikuwa amekufa hivyo kwenye kuusafirisha mwili kwenda hospitali ilikuwa inapelekwa maiti tu raisi hakuwa hai tena.
Eneo lile lilifungwa, hakukuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaruhusiwa kutoka, watu wote ambao walikuwa pale waliwekwa chini ya ulinzi wakiwemo wale vilema ambao raisi alikuwa ameenda kuwasaidia pale. wanaume wawili ambao walikuwa vinara wa sehemu ya ulinzi wa raisi walionekana wakiwa wamepagawa huku wakiongea kwa pamoja
“Hili jambo sio kufukuzwa kazi tu, kuna uwezekano tukahusishwa na kifo cha raisi, sio jambo ambalo wakubwa watalielewa kama tukiwaeleza raisi ameuawa mbele yetu tena kizembe namna hii”
“Darius comon, huu sio muda wa kuwaza kuhusu hatima yetu, naihitaji akili yako kwa sasa kwani tunatakiwa kumpata mhusika wa hili tukio na wewe ndiye unatakiwa kuifanya hii kazi kwakuwa ndiye mwenye uzoefu mkubwa kuliko yeyote hapa hivi sasa. Kwahiyo badala ya kuendelea kujikatia tamaa nadhani ni muda wa kuanza kutekeleza majukumu ambayo yaliifanya nchi kupoteza pesa nyingi kukutengeneza wewe” maneno ya mwenzake yalimpa nguvu kidogo ila alikuwa amekata tamaa na ni kama alikuwa anaiwaza hatima yake kwanza badala ya kazi ambayo ilikuwa inatakiwa kufanyika.
“Upo sahihi Kaini” ni kama alikurupuka kutoka kwenye usingizi, alitembea hatua kadhaa wenzake wakiwa wanamfuata mpaka ile sehemu ambayo raisi alipigiwa risasi, aligeukia ule upande ambao risasi ilionekana kutokea, aiiangalia kwa umakini mkubwa akamgeukia mwenzake
“Kuna watu ambao wametumwa ile sehemu?”
“Ndiyo”
“Muuaji anatakiwa kupatikana haraka, mpaka muda huu atakuwa hajatoka nje ya lile jengo hivyo ulinzi usambazwe kila sehemu na mimi mwenyewe naenda kule muda huu” alivua koti na kubakia na shati yake nyeupe yule bwana, uso wake ulikuwa na wasiwasi, yeye ndiye alikuwa anasimamia ulinzi na usalama wa mhehsimiwa raisi popote ambapo anakuwepo, kufa mbele yake maana yake ule ulikuwa ni msala wake yeye mwenyewe ndiyo maana alikuwa mwingi wa wasiwasi kuliko wenzake wote.
“Darius!!!” alisimama baada ya kusikia sauti ya Kaini
“Nini?” aliuliza kama mtu ambaye alipagawa tena akiwa na jazba kali ndani yake
“Unamkumbuka yule kilema ambaye alikuwa anaongea na raisi hapa?”
“Ndiyo”
“Hayupo”
“Unamaanisha nini kusema hayupo?”
“Kiti chake kipo tupu, wenzake wote wapo chini ya ulinzi ila yeye pekee ndiye hayupo”
“Ni kilema yule, sasa unaniambiaje hayupo? Siku hizi vilema wanakimbia?” wote waliangaliana usoni kisha wakageukia upande wa watu ambao walikuwa wamekalishwa chini kuangalia kama wangemuona bwana yule ila hakukuwa na dalili za uwepo wake.
“Anaweza kukimbia kama tu sio kilema”
“Unataka kuse……”
“Ndiyo Darius, huenda alikuwa sehemu ya mauaji ya raisi ndiyo maana alitumia ule muda kuweza kuongea na raisi na kwa ukaaji wake na namna raisi alivyopigwa risasi inamaanisha alikuwa anamuweka kwenye tageti nzuri”
“Watawanye watu wetu kila sehemu, atafutwe huyu mtu na hawa vilema wengine waanze kuhojiwa haraka ili kama kuna ambaye ana taarifa za yule mtu tuweze kuzijua haraka kwani tunazihitaji. Na hili zoezi nahitaji wewe Kaini ulisimamie mweyewe, mimi naenda kule kwa yule muuaji kumtafuta hivyo hakikisha naporudi hapa ninakutana na majibu” aliongea akiwa hayupo sawa, kusababisha raisi wa nchi kuuawa lile jambo lilikuwa kubwa kuliko hata maisha yake.
MITA MIA MOJA NA HAMSINI KUTOKA ENEO LA TUKIO
Kulikuwa na ghorofa refu ambalo walikuwa wanaishi watu ila kwa wakati huo walihamishwa kwa muda baada ya kuanza kufanyiwa ukarabati upya hivyo hakukuwa na watu ambao walikuwa wanaishi ndani yake na ndiyo ile sehemu ambayo risasi ilionekana kutokea.
Jengo zima lilikuwa limezungukwa na walinzi ambao wengi wao walikuwa wameingia ndani kuweza kukagua kwani waliamini mdunguaji alikuwa mle ndani. Darius naye alifika pale na kuliangalia lile jengo kwa umakini, alikimbia kama amechanganyikiwa kwenda ndani ambapo aliongozwa na walinzi mpaka sehemu ambayo waliamini ndipo alipokuwepo yule muuaji. Ni kweli ile sehemu ilikuwa inaonekana mtu alikaa kwa muda mrefu kidogo na pembeni yake kulikuwa na kipisi cha sigara na harufu yake ikiwa bado ipo ila mhusika hakuwepo. Darius alichukua silaha kubwa na kuilengesha ile sehemu kuelekea kule ambako raisi alikuwepo, ilikuwa ni sehemu sahihi kwa muuaji kuweza kutekeleza adhma yake kwani ni eneo ambalo lilitulia kwa kazi hiyo.
Moyo wake ulipiga kite baada ya kuwaza kwamba ni kwa namna gani alishindwa kupiga hesabu mapema kuhusu uwepo wa sehemu ya hatari kama hiyo? Akatambua ulikuwa ni uzembe mkubwa yeye na wenzake waliufanya, alitazama chini akatambua ilikuwa ni ghorofa ya tano. Kichwa chake kilikuwa na maswali mengi ambayo hakuwa na majibu nayo, muuaji alikuwa na ratiba nzima ya raisi? Aliitolea wapi? Kuhusu raisi kupita na kusimama ile sehemu ilitangazwa siku ile ile, sasa muuaji alitumia muda gani kujipanga mpaka kutambua kulikuwa na sehemu ambayo yeye angeweza kuitumia kutekelezea jambo lake ambalo alikuwa amelipanga? Akiwa anaendelea na maswali yake mengi kutengeneza nadharia ambayo ingemsaidia kuanza upelelezi wa tukio hilo, mwanaume mmoja mwenye suti alimfuata na kumuita pembeni.
“Kiongozi, kuna hatua za mtu kuelekea ukutani na sehemu hiyo ina kamba ambayo imekatwa ila kuna kipisi kimebaki” Hakuzubaa zaidi ya kuhitaji kupelekwa huko, alikutana na kamba ambayo ilionyesha muuaji alitumia kushukia kwenye hilo ghorofa hivyo yeye alijirusha na kudaka floor ya nne, akafanya hivyo mpaka alipotua chini huku walinzi wengine wakibaki wanamshangaa. Alihitaji kufuatilia ule mkasa mzima, alipofika chini aliona kuna hatua zinaelekea ndani ya uchochoro mmoja ambao ulikuwa na vumbi alianza kuufuata kwa kukimbia bastola ikiwa kwenye mkono wake.
Alipofika mbele kabisa ya sehemu ile alikutana na kitambaa kidogo kikiwa kimefungwa kwenye kona ya ukuta, ilikuwa ni ishara ya wapi ambako muuaji alikuwa ameenda ila ilimtisha, sababu ya yeye kutishika ni baada ya kuonekana kama muuaji alikuwa anampatia ishara ya wapi alikuwa anaenda, ile haikuwa hali ya kawaida kwani muuaji alitakiwa kujificha na sio kutoa ishara ya wapi ambapo alikuwepo hivyo yeye akaanza kutembea kwa tahadhari kubwa.
Tumeufungua ukurasa wa kwanza kwenye hili andiko, nakukaribisha ukae na mimi pamoja tuweze kuisoma hii dunia ya kufikirika ya watu wenye uwezo mkubwa pamoja na safari za visasi.
Ni mtu gani ambaye unahisi alikuwa na jeuri ya kumuua raisi wa nchi tena mbele ya halaiki kubwa ya watu kirahisi namna hiyo? Je atakamatwa na Darius na timu ya wenzake? Nini kinaenda kutokea baada ya raisi kuweza kufa? Nchi inaingia kwenye hali ya namna gani? Sina majibu kwa sasa bali andiko hili litatupatia majibu yote.
SIMULIZI HII YOTE UNAIPATA KWA SHILINGI 5000 TU ZA KITANZANIA.
Unaweza kulipia kupitia namba hizi HAPA 👇
0621567672 (HALOPESA)... WhatsApp
0745982347 (M-PESA)
0714581046 (TIGO-PESA)
0689440143 (AIRTEL MONEY)
36316279 (LIPA NAMBA (M-PESA) inapokea mitandao yote)