Prisoner of hope
JF-Expert Member
- Aug 9, 2017
- 2,440
- 2,575
Shukrani sana Bishop...much blessing to you ndugu.
Still tupo pamoja.
Sent using Jamii Forums mobile app
Still tupo pamoja.
Kizungumkuti! - 6
Na Bishop Hiluka
“Umelijuaje jina langu?” hatimaye Yusuf aliuliza kwa udadisi huku akizidi kumkazia macho Jacky.
Jacky aliangua tena kicheko hafifu na kunyoosha kidole chake kuonesha beji maalumu iliyokuwa imechomekwa kwenye shati la Yusuf katika kifua chake ikiwa imeandikwa jina lake.
"Si hiyo beji uliyovaa kwenye shati lako. Au wewe siyo Yusuf?" alisema Jacky huku akiwatupia jicho wateja wengine waliokuwa wakihudumiwa kwenye kaunta zingine.
"Hmm, mimi ndiye. Karibu sana, sijui nikusaidie nini, dada…?" alisema Yusuf na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.
Jacky alitoa tena kitambaa chake na kufuta jasho jepesi lililokuwa likimtoka, akageuza shingo yake kuwatazama wateja waliokuwemo ndani ya ile benki kisha akampenyezea Yusuf ile kadi kwa uficho akihakikisha hakuna mtu mwingine zaidi ya Yusuf aliyeona kitendo kile.
Endelea...
Yusuf alimtazama Jacky kwa mshangao na kuipokea ile kadi, aliiangalia kwa makini kwa kitambo kifupi kisha akainua uso wake kumtazama Jacky akiwa na uso wenye maswali.
Jacky aliachia tabasamu kabambe na kujilegeza. "Dont worry, call me anytime when you get chance, there’s something important we need to talk," (Usihofu, nipigie wakati wowote utakapopata nafasi, kuna kitu muhimu tunahitaji kuongea) alisema Jacky kisha akageuka na kuanza kuondoka eneo lile haraka kabla Yusuf hajasema lolote.
Yusuf alitaka kusema neno lakini alisita na kubaki akimkodolea macho Jacky wakati alipokuwa akitembea kwa madaha huku akili ya Yusuf ikijikuta ikipumbazika mno na mtikisiko maridhawa wa mwili wa Jacky.
Yusuf aliendelea kumsindikiza Jacky kwa macho na kwa utulivu hadi pale alipofungua mlango na kutoka nje ya lile jengo la benki, kisha aliitupia tena jicho la haraka ile kadi na kuitumbukiza mfukoni. Akaendelea kupokea hundi za wateja wengine.
Jacky alipotoka nje ya lile jengo la benki alitembea kwa madaha, tembea yake ilikuwa adimu kuipata kwa wasichana wengi ambao pamoja na kujikwatua, bado walishindwa kupata miondoko kama yake. Tembea ya Jacky iliwafanya watu wageuze shingo zao kumtazama alipokuwa akipita huku macho yao yakishindwa kuamini kile walichokuwa wamekiona, ni kama walikuwa wamemuona malaika.
Kila alikopita, wazee kwa vijana walikuwa wakibabaika, na hawakuisha kugeuza vichwa vyao ili kuustaajabia mwili wake jinsi ulivyoumbika! Alikuwa tofauti sana na wasichana wengine wengi ambao walijiona na kujikweza juu ya kila kiumbe duniani, wasiridhike hata kukanyaga ardhi.
Wakati Jacky alipokuwa akivuka barabara ya Lumumba kuelekea lilipokuwa limeegeshwa gari lao, kuna gari moja dogo lilimpita na muda ule dereva alijikuta akimshangaa na kuivamia pikipiki ya magurudumu matatu aina ya Bajaj iliyokuwa imeegeshwa pembezoni mwa barabara, akairusha kule.
Kidogo lizuke vurumai kubwa katika ya yule dereva na wananchi wenye hasira, akiwemo dereva wa Bajaj, vurumai ambalo lingeweza kuigeuza sehemu ile kuwa Mogadishu, badala yake watu wote walisahau kuhusu ile ajali na kujikuta wakigeuza vichwa vyao kuangalia kazi ya Mungu ilivyotendeka vyema katika mwili wa Jacky huku wengine wakipiga mbinja.
“Dah, tuacheni utani jamani, ilikuwa haki ya dereva kupotea njia!” mwanamume mmoja wa makamo alisema kwa sauti ya juu na kuwafanya watu waliokuwa na hasira kuanguka kicheko.
Hata hivyo, Jacky hakujishughulisha nao, aliendelea na safari yake kwani hali kama ile alikwishaizoea, alifika lilipo gari lao na kufungua mlango wa abiria, akaurusha mkoba wake kwenye siti ya nyuma.
Aliminya midomo yake yenye maki na kuachia tabasamu wakati alipokuwa anaingia kwenye gari na kuufunga mlango kisha alifunga mkanda wa siti na kumtazama Carlos kwa tabasamu.
"Let’s go, my love," (Twende, mpenzi) alisema huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
Carlos alimtazama Jacky kwa makini na kuliondoa gari taratibu bila kusema neno. Kisha aliiacha barabara ya Lumumba na kushika uelekeo wa upande wa kulia akiufuata mtaa wa Mkunguni.
Baada ya mwendo mfupi wa safari yao aliyafikia makutano ya mtaa ule wa Mkunguni na barabara ya Bibi Titi Mohammed, mbele ya Soko la Kisutu. Carlos alichepuka na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara ya Bibi Titi Mohammed.
Katika barabara ile ya Bibi Titi Mohammed Carlos alilazimika kupunguza mwendo kutokana na msongamano mkubwa wa magari, alitazama nyuma kupitia kioo cha katikati cha gari kinachoruhusu kuona nyuma ili kuchunguza kama kulikuwa na chochote alichokitilia mashaka au lah!
Alishtuka sana baada ya kuhisi kulikuwa na jambo lisilo la kawaida, alitazama kwa makini na aliweza kuliona gari aina ya Toyota Land Cruiser Pick-up la rangi nyeusi likiwa katika foleni nyuma yao, alikumbuka kuliona gari lile tangu alipotoka barabara ya Lumumba na kuingia katika mtaa wa Mkunguni.
Hata hivyo, hakutaka kumshtua Jacky, aliendesha kimya kimya hadi walipozifikia taa za kuongozea magari barabarani katika makutano ya barabara za Uhuru na Bibi Titi Mohammed. Pale kwenye makutano Carlos walishindwa kuvuka kwa kuzuiwa na taa nyekundu za kuongozea magari barabarani.
Aliitupia macho saa yake ya mkononi na kuminya midomo yake huku akitazama tena nyuma yake kupitia kile kioo cha katikati cha gari kinachoruhusu kuona nyuma, hakuliona lile gari.
Alipogeuza shingo yake kutazama kando akaliona lile gari Toyota Land Cruiser Pick-up jeusi likiwa limesimama sambamba na gari lake upande wao wa kushoto, na sasa aliweza kusoma maandishi makubwa ya POLISI yaliyokuwa yameandikwa ubavuni.
Mbele ya lile gari kulikuwa na dereva na ofisa mmoja wa polisi na nyuma ya lile gari kulikuwa na maofisa watano wa polisi waliokuwa wameketi na walishika bunduki aina ya SMG zilizotundikwa begani na kulalia vifuani.
Wale askari walikuwa wakilitazama lile kwa makini sana. Hapo akili ya Carlos ilianza kupoteza utulivu taratibu kadiri lile gari lilivyoendelea kusimama pale. Jacky alishtuka na kugeuza shingo yake kutazama kule lilikokuwa lile gari la Polisi baada ya kumuona Carlos akioneshwa kubabaika kidogo.
Carlos alikuwa akihisi kijasho chepesi kikimtoka usoni, alitoa kitambaa na kufuta jasho usoni huku akiendelea kuwachunguza wale askari wenye mitutu ya bunduki kwa makini sana huku akijaribu kuyasoma mawazo yao.
Mara taa ya kijani ya kuongozea magari ikawaruhusu kupita, Carlos akashusha pumzi za ndani kwa ndani na kuingiza gia huku akiliondoa gari lake, alizivuka zile taa na kushuhudia lile gari la Polisi likifuatia nyuma yake, alipokwenda mbele kidogo akapunguza mwendo na kukata kona kuingia mtaa wa Sofia Kawawa upande wake wa kushoto ili kuona kama alikuwa anafuatiliwa.
Lile gari la Polisi nalo lilipunguza mwendo na kuingia kufuata uelekeo ule ule japokuwa lilikawia kidogo kuingia. Tukio lile lilimfanya Carlos ahisi kuishiwa nguvu ingawa hakuwa na uhakika kama wale Polisi walikuwa wakimfuata yeye, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini.
Itaendelea...
Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Sent using Jamii Forums mobile app