Kizungumkuti! - 64
Na Bishop Hiluka
ILIPOISHIA
“
We need to find a quick way to silence Kabwe and Liston before things get worse, and then I’ll find out how to deal with Yusuf in jail,” (Itabidi tutafute njia ya haraka ya kuwanyamazisha Kabwe na Liston kwanza kabla mambo hayajaharibika, halafu nitatafuta namna ya kudili na Yusuf kule kule mahabusu) Carlos alisema huku akiachia tabasamu.
Jacky alishtuka sana na kumkazia macho Carlos kwa hofu kana kwamba alikuwa akitazama kitu cha ajabu sana chenye kutisha.
“
What do you mean to silence them, Carlos?” (Unamaanisha nini kuwanyamazisha, Carlos?) Jacky aliuliza huku akionekana kuanza kuchanganyikiwa.
“
To kill them, like Kisu,” (Wauawe, kama Kisu) Carlos alisistiza huku akiendelea kutabasamu.
“Aah, sasa unataka kutafuta matatizo mengine. Haya bado hayajaisha unataka kuzua mambo mapya!” alisema Jacky kwa huzuni.
Endelea...
“Bila hivyo hatutakuwa salama kabisa, kwanza siamini kabisa kama tangu jana Kabwe na Liston hawajazua balaa lolote huko waliko…
I don't believe at all!” Carlos alisema huku akishusha pumzi.
Jacky alimtazama kwa makini na kutaka kusema neno lakini akasita na kushusha pumzi za ndani kwa ndani kisha akabaki akimtazama Carlos kwa wasiwasi. Alimtazama kwa kitambo kisha akaamua kuvunja ukimya, “
And what about Jasmine?” (Na vipi kuhusu Jasmine?) Jacky aliuliza huku akiwa bado amemtulizia Carlos macho.
“
I want to follow her right now and bring her here, we’ll give her the money belongs to her and ask her to leave the city completely,” (Nataka kumfuata sasa hivi nimlete hapa, tutamkatia anachostahili na kumtaka aondoke kabisa hapa mjini) Carlos alisema na kuinuka kisha akaanza kupiga hatua kutoka, mara akakumbuka jambo na kugeuka kumtazama Jacky.
“
By the way, be careful when you want to get out of here, because I feel like there are people going to be tracking our movements,” (Hata hivyo, kuwa mwangalifu unapotaka kutoka humu ndani, maana nahisi kama kuna watu watakuwa wanafuatilia nyendo zetu) Carlos alimwambia Jacky kisha akatoka kabla Jacky hajasema neno lolote.
Carlos aliingia kwenye gari lake aina ya
BMW X6 xDrive 50i la rangi ya samawati kisha akabofya
remote kufungua lile geti kubwa na kuliondoa gari lake kwa mwendo wa kasi, alichukua uelekeo wa barabara iliyokuwa ikielekea Kinyerezi akiwa hataki kuelekea moja kwa moja Vingunguti ili kuwapoteza watu aliodhani wangeweza kuwa wakifuatilia nyendo zake.
Aliyachunguza magari yaliyokuwa yakija nyuma yake, na kuona magari mawili miongoni mwa magari yaliyokuwa nyuma yake ambayo aliyaanza kutilia shaka.
Magari yale, moja lilikuwa ni gari aina ya
Landcruiser Hardtop la rangi nyeusi na jingine lilikuwa ni gari aina ya
Land Rover 110 jeupe, na yote mawili yalikuwa yakielekea upande ule ule aliokuwa akienda. Katika muda ule barabara ile haikuwa na msongamano mkubwa wa magari, hivyo mwendo wake ulikuwa wa kuridhisha.
Alipoitupia macho saa yake ya mkononi ilimuonesha kuwa ilikuwa ikielekea kutimia saa sita mchana na wakati huo jua lilikuwa limeanza kushamiri huku hali ya hewa ikiwa ya joto kama ilivyokuwa kawaida katika jiji la Dar es Salaam.
Carlos alianza kuteremsha mteremko mkali na baada ya kulivuka gereza la Segerea alikwenda mwendo wa kasi zaidi na mbele kidogo alifika eneo la Mbuyuni Njiapanda.
Hapo aliamua kuiacha ile barabara iliyokuwa ikielekea Kinyerezi na kukata kuelekea upande wa kushoto akiifuata barabara ya Mbuyuni.
Ilikuwa ni barabara ya kawaida yenye kiasi kidogo cha magari na iliyokuwa ikikatisha katikati ya makazi ya watu. Carlos aliendelea mbele na safari yake huku akifanya tathmini nzuri ya barabara ile iliyoonekana kuwa na watu wachache waliokuwa wanatembea kwa miguu.
Baada ya mwendo mfupi wa safari yake akayaona yale magari
Landcruiser Hardtop jeusi na
Land Rover 110 jeupe yakiwa nyuma yake, moyo wake ukapiga kite na kumfanya aongeze mwendo ili kuhakikisha kama yale gari yalikuwa yakimfuata.
Wakati akiendelea na safari yake na akiwa hajui afanye nini mara mbele kidogo upande wake wa kushoto akaiona gereji ya
Wantong, hivyo ili kuhakikisha kama ni kweli alikuwa anafuatwa aliamua kuchepukia upande ule wa kushoto na kuliingiza gari lake kwenye eneo lile la gereji.
Lile gari jeusi
Landcruiser Hardtop lilipunguza mwendo na kuonekana kama vile dereva alikuwa anajishauri kama asimame au lah, lakini akaonekana kuendelea na safari huku lile gari jingine
Land Rover 110 jeupe likipitiliza bila kusimama.
Carlos aliyasindikiza kwa macho yale magari huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani na kujipa matumaini kuwa alikuwa salama. Alisubiri kwa dakika tano kisha akaliondoa gari lake kuendelea na safari yake akiifuata ile barabara.
Alipokwenda mbele zaidi alikipita kituo cha mafuta cha Meru kilichokuwa upande wake wa kushoto na mbele kidogo kulikuwa na kituo kingine cha mafuta cha Anna ATN kilichokuwa upande wa kulia kwenye kona ya ile barabara huku kushoto kwake kukiwa na MTN Bakery.
Carlos alishtuka sana alipoliona lile gari
Landcruiser Hardtop jeusi likiwa limeegeshwa kando ya barabara jirani na Anna ATN Petroleum huku dereva wake akionekana kufungua boneti la gari.
Carlos aliongeza mwendo huku akilitupia jicho lile gari, na baada ya mwendo mfupi mara akamuona yule dereva akifunga haraka boneti na kuingia kwenye gari kisha gari likaingia barabara na kumfuata nyuma.
Hata hivyo, tukio lile bado lisingekuwa kigezo cha kumridhisha Carlos kuwa sasa alikuwa amefungiwa tera, hata hivyo kwa namna nyingine ile ilikuwa ni ishara mojawapo ya kumtahadharisha kuwa alipaswa kuwa makini na nyendo zake.
Hakujua lile gari jingine
Land Rover 110 jeupe lilikuwa wapi muda ule, hivyo mara hii alijikuta akilitazama lile gari
Landcruiser Hardtop jeusi kwa utulivu wa hali ya juu katika namna ya kutafuta hakika kama alikuwa akifuatwa au lah!
Aliongeza mwendo na kuivuka baa ya Darajani White kisha alilivuka daraja katika Mto Msimbazi, na kuzivuka baa nyingine za Ndindindii, Elegant Lodge na baadaye Kilimani Bar huku akifikira kama aingie kwenye mojawapo ya zile baa kujifanya kuwa safari yake ilikuwa inaishia pale.
Lakini akaamua kuendelea mbele na baada ya mwendo mfupi wa safari yake akakifikia Kituo cha Decent na kuiacha barabara ile kisha akachepuka na kuingia upande wa kulia akiifuata barabara finyu ya vumbi iliyokuwa ikielekea Da Prince Lodge.
Aliongeza mwendo na wakati akiifikia Da Prince Lodge, aliliona lile gari jeusi Landcruiser Hardtop nalo likichepuka na kuingia kwenye ile barabara finyu ya vumbi na kufuata uelekeo wa Da Prince Lodge likiwa katika mwendo wa taratibu.
Kitendo kile kikamfanya Carlos ashtuke kidogo baada ya kuridhishwa vizuri na tathmini za hisia zake. Sasa aling’amua kuwa lile gari Landcruiser Hardtop jeusi nyuma yake lilikuwa kazini kumfuata kama alivyokuwa amehisi pale awali.
Hivyo, aliamua kuongeza mwendo bila kujali makorongo katika barabara ile finyu ya vumbi huku kijasho chepesi kikianza kumtoka usoni. Moyo wake nao ulikuwa umeanza kupoteza utulivu, hata hivyo kwa kila hali alijitahidi kupambana kikamilifu na hali ile.
Akili yake ikiwa mbioni kupoteza utulivu sasa alikuwa makini sana kulichunguza lile gari kupitia vile vioo vya ubavuni. Hatimaye akafika mwisho wa ule mtaa na kuchepuka akiingia upande wa kushoto.
Kisha aliongeza mwendo katika barabara ile, hata hivyo hadi alipokuwa mbioni kufikia mwisho wa barabara ile lile gari halikuwa limejitokeza. Carlos hakutaka kuamini kuwa lilikuwa linaishia katika mtaa ule, aliongeza mwendo na kuchepuka tena akiingia upande wa kushoto akiifuata barabara nyingine pana kidogo ya vumbi iliyokuwa inakwenda sambamba na reli ya kati.
Itaendelea...
CC
the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater,
Bigjahman moneytalk marybaby,
nipo2,
ram,
kisukari,
Smart911,
Madame S,
carbamazepine,
Astelia,
culture gal ,
Prisoner of hope,
Mine eyes,
kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes,
Kudo, swahiba92,
ludist,
Toyota escudo,
Clkey,
macson3,
Thad,
boga la kiangazi,
macson3,
LEGE,
Smart911,
Richard irakunda,
skfull,
popie,
Krizy Beat,
hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY