Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Stori ya kusisimua - Kizungumkuti!

Kizungumkuti! - 61

Na Bishop Hiluka

Tangu alipopigiwa simu na Jacky siku iliyokuwa imetangulia na kuelezwa kuhusu maofisa wa polisi kumtilia shaka Kisu kuwa alikuwa mmoja wa walioshiriki katika ule wizi wa mabilioni pale Benki ya Biashara, Carlos hakuweza kulala.

Usiku ule ule alianza harakati za kumtafuta Kisu na bahati mbaya simu yake ilikuwa haipatikani. Alikwenda katika viwanja alivyodhani angeweza kumuona Kisu lakini hakuwepo, hatimaye aliamua kwenda nyumbani kwa Doris, mwanamke aliyewahi kuishi na Kisu na walikuwa na watoto wawili. Hata hivyo Doris alimwambia Carlos kuwa hakuwa ameonana na Kisu kwa takriban wiki tatu, tangu walipoachana Masai Club Kinondoni baada ya kutofautiana.

Endelea...

Carlo alikuwa amerudi nyumbani kwake saa saba usiku akiwa amechoka sana na kumkuta Jacky akiwa amelala kwenye sofa kubwa pale pale sebuleni baada ya kumsubiri kwa kitambo kirefu. Hata hivyo, baada ya kurudi Carlos hakuweza kupata usingizi, usiku wote alikuwa akipanga hili na lile na alfajiri ya siku iliyofuata aliondoka nyumbani ili kwenda kumtafuta Kisu.

Alichukua gari lake aina ya Toyota Landcruiser GX V8 na kuingia barabarani ili kuelekea Sinza Makaburini, alipokuwa akipita jirani na meza moja ya magazeti alimuona yule muuzaji akiwa anapanga magazeti kwenye meza.

Carlos alivutiwa na kichwa kimoja cha gazeti pale macho yake yalipoangukia kwenye maneno makubwa yaliyokuwa yamekolezwa wino mweusi yakiwa na kichwa cha habari: ‘Mfanyakazi benki akamatwa akihusishwa na wizi wa mabilioni, wenzake wasakwa’. Moyo wa Carlos ulipiga mshindo, hata hivyo hakuwa na muda wa kupoteza.

Akaamua kuendelea na safari yake na wakati akiingia katika barabara iliyokuwa inatoka Kinyerezi alimuona mwanamume mmoja, mtu mzima aliyekuwa anapita akiwa na baiskeli iliyobeba madafu akielekea Kariakoo.

Mara Carlos akapata wazo na kumsimamisha yule mtu, alimuuliza bei ya yale madafu na baada ya kuelezwa alimtaka yule mtu amuuzie madafu yote pamoja na ile baiskeli lakini yule mtu alionesha kusita. Lakini alipooneshwa kitita cha fedha shilingi milioni moja alikubali mara moja na kumwachia yale madafu pamoja na baiskeli yake.

Carlos aliipakia ile baiskeli na madafu yake kwenye gari lake kisha alirudi nyumbani kwake na kuvaa kanzu juu ya nguo zake, kichwani akavaa baragashia na miguuni alivaa makubazi, na baada ya hapo safari ya kuelekea Sinza ikaanza.

Jacky alimtazama Carlos kwa wasiwasi, alipotaka kujua alikuwa anaelekea wapi na mavazi yale Carlos alimtaka asubiri angerudi kumpa taarifa na kumtaka asiondoke nyumbani hadi atakapokuwa amerudi.

Carlos alipofika eneo la Sinza Palestina ilikuwa tayari saa moja ya asubuhi, watu walikuwa katika pilika pilika za hapa na pale kuelekea kwenye shughuli zao, Carlos akaamua kuliegesha gari lake jirani na Hospitali ya Sinza Palestina, kisha akaishusha ile baiskeli ya madafu na kuanza kuendesha taratibu.

Kwa yeyote ambaye angemuona Carlos asingeshindwa kumtofautisha na wauzaji wengine wa madafu. Aliendesha hadi alipofika Sinza makaburini na kuiegesha baiskeli yake eneo lile akijifanya kuuza madafu huku macho yake yakiwa makini kufuatilia nyendo zote zilizokuwa zikiendelea eneo lile.

Mara akamuona Kisu akifika kwenye ile nyumba ambayo Carlos alikuwa akiichunguza muda wote na kuegesha pikipiki yake pale nje, kisha aliharakisha kuingia ndani ya ile nyumba akionekana mwenye wasiwasi mkubwa.

Carlos alitaka kumfuata lakini akasita baada ya kuwaona wavulana wawili wa umri wa miaka kumi na kumi na mbili wakisogelea pale kwenye baiskeli yake na kusimamia kando yake huku wakimtazama kwa makini.

“Madafu shilingi ngapi?” mtoto mmoja alimuuliza Carlos huku akimtazama kwa makini.

Carlos alimtazama yule mtoto, akachukua madafu mawili na kuwapa kila mmoja na dafu lake. “Haya, ondokeni!”

Wale watoto waliyapokea yale madafu kwa furaha lakini hawakuondoka. Walibaki wamesimama wakimkodolea macho kwa mshangao, huku wakiwa wameshikilia yake madafu.

Carlos aliwatazama na kutaka kuwafukuza lakini akasita na kuyaondosha macho yake kutoka kwa wale watoto, akayaelekeza kule kwenye ile nyumba. Muda huo Kisu alikuwa anatoka ndani akiwa amebeba begi dogo la mgongoni na kuanza kupiga hatua zake kuifuata piki piki yake.

Muda ule ule Carlos alitoa bastola yake iliyokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti, akamlenga Kisu na kuachia risasi iliyompata Kisu katikati ya paji la uso wake, ikamrusha na kumtupa hatua tatu nyuma yake. Watu wachache waliokuwepo eneo lile karibu na Kisu wakataharuki na kumtazama kwa mshangao wakiwa hawajui alipatwa na nini!

Carlos akateleza taratibu akiiacha ile baiskeli na madafu yake katika eneo lile! Aliingia kichochoroni karibu na duka la mavazi la Kitaani Classic na kutoka mtaa wa Social kisha akazidi kusonga mbele kwa mwendo wa haraka, alipita kwenye kichochoro kimoja kilichokuwa na lundo la takataka, Carlos akaivua ile kanzu na kuitupa pale.

Alipoibuka katika mtaa wa Gandabahari alikuwa tayari amebadilika na kuingia kichochoro kingine kilichokwenda kumfikisha mtaa wa Mjiasali, kisha akaufuata mtaa wa Ramala uliomfikisha nyuma ya majengo ya hospitali ya Sinza Palestina. Wakati akifika alipokuwa ameegesha gari lake aliliona gari moja aina ya Nissan Patrol la rangi nyeusi lililokuwa na maandishi ya POLISI ubavuni likipita pale kwa mwendo wa kasi likielekea Sinza Makaburini.

Carlos aliachia tabasamu huku akiingia ndani ya gari lake na kuliondoa kwa kasi na kuyafanya magurudumu yachimbe ardhi wakati akiliingiza lile gari barabara ya Shekilango.

Alielekea upande ule ule lilikoelekea lile gari la polisi na kulivuka eneo la Sinza Makaburini, alitupa macho yake kutazama upande ule wa kushoto na kuwaona watu wengi wakiwa wamekusanyika eneo lile huku maofisa wa polisi, ASP Komba na Sajenti Mapambano wakionekana kuwahoji baadhi ya watu walioshuhudia tukio lile.

Carlos alishusha pumzi na kuongeza mwendo akilipita eneo la makaburi, akavuka eneo la Sinza Kwa Remi hadi alipofika eneo la Sinza Mori akakunja kuingia kushoto akiifuata barabara ya Mori hadi alipokwenda kutokea katika barabara ya Sam Nujoma jirani na Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, maarufu Kanisa la Kakobe.

Hapo akakunja na kuingia kushoto akiifuata ile barabara ya Sam Nujoma kuelekea eneo la Ubungo.

______

Hazikupita hata saa tatu baada ya tukio la mauaji pale Sinza Makaburi, mwili wa Kisu ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti maarufu kama mochuari katika hospitali ya Sinza Palestina, habari zilizagaa karibu kila mahali jijini kupitia mtandao wa WhatsApp.

Waandishi kadhaa wa habari walikuwa wamefika na kusimama nje ya jengo la Kituo Kikuu cha Polisi wakitaka maelezo ya tukio zima, na nani anayeshukiwa. Waliambiwa kuwa suala lile lilikuwa likishughulikiwa na ASP Komba, ambaye hata hivyo, kutokana na kuchanganyikiwa hakupenda kuongea hata na mmoja wao.

ASP Komba alijilaumu sana kwa kushindwa kumpata Joram Mbezi akiwa hai kwani aliamini kuwa Joram ndiye alikuwa kiungo kikubwa kati ya mtu aliyejiita Belinda Jackson na Yusuf na sasa kazi ilianza kuwa ngumu pasipo Joram.

Alikuwa amebakiwa na kazi moja tu, kumbana Yusuf ili amweleze uhusiano wake na wale watu wawili, Joram Mbezi ambaye sasa alikuwa marehemu na Belinda Jackson, ambaye hawakuwa na taarifa zake hadi muda huo. Alipaswa kupata majibu ya uchunguzi wake haraka iwezekanavyo.

Haya, mambo yamezidi kuwa mambo, ni kizungumkuti juu ya kizungumkuti. Je, nini kitaendelea? Endelea kufuatilia stori hii ya kusisimua, KIZUNGUMKUTI...
 
Kizungumkuti! - 59

Na Bishop Hiluka

ILIPOISHIA

“Eti yule malaya ananiletea pozi! Sasa keshokutwa ndiyo atanitambua mimi ni nani labda nisimuone, nitafanya mambo juu ya kaunta…” Liston alisema.

“Umeona eh! Yule bwana si katuahidi kutukatia hamsini zetu! Keshokutwa ndo watajua sisi ni nani, watu tumefanya kweli bladikenge, keshokutwa ndo keshokutwa, hapakaliki hapa,” Kabwe alipaza sauti yake na kurusha mkono wake hewani kitendo kilichomfanya kumpiga mwanamume mmoja aliyekuwa akipita karibu yake.

Wakati yule mwanamume akitaka kuzozana na kabwe mara yule dada aliyemkimbia Liston akarudi mle ndani ya ule ukumbi akiwa ameongozana na Meneja wa ile klabu na kuonekana akinyoosha kidole chake kuelekeza walipokuwa Kabwe na Liston.

Endelea...

Yule Meneja alikuwa mwanaume mfupi mwenye sura ya umbo duara, miwani iliyokuwa imetuama kwenye macho yake makubwa, pua ya kibantu na mdomo wenye kingo pana uliokuwa umezungukwa na ndevu zilizokuwa zimenyolewa vizuri mtindo wa “O”. Alikuwa na kitambi cha ukwasi huku akiwa amevaa suti ya rangi nyeusi, shati la rangi ya kijivu na tai nyekundu shingoni.

Aliwafuata Kabwe na Liston na kuongea nao kwa kitambo kifupi akiwasihi kunywa pombe kistaarabu na kutowabughudhi wateja wengine au kama hawawezi basi waondoke. Kabwe na Liston hawakufurahishwa kupangiwa jinsi ya kutumia fedha zao, walionekana kuchukia sana na kuondoka kwa hasira, lakini waliahidi kurudi tena siku nyingine.

* * * * *

Saa tatu kasoro robo usiku Jacky alikuwa amesimama sebuleni katika nyumba ya Jacob akiwa tayari amekwisha vaa nguo zake akitaka kuondoka. Hiyo ilikuwa ni baada shughuli pevu ya raundi mbili mfululizo kutoka kwa Jacob iliyomuacha hoi.

You are so wonderful Jacky. I swear in heaven and earth, I'll never find a woman who knows how to make love like you. You are so amazing,” (Wewe ni ajabu sana Jacky. Naapa kwa mbingu na ardhi, sitakuja kumpata mwanamke anayeyajua mapenzi kama wewe. Unashangaza sana) Jacob alimwambia Jacky baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika.

Where are you going, come here, darling,” (Unaenda wapi, njoo hapa, mpenzi) Jacob alimwambia Jacky baada ya kumuona akijiinua kutoka pale sakafuni.

I need to call my husband first, I don't want to make him worried,” (Nahitaji kumpigia simu mume wangu kwanza, sitaki kumfanya apate wasiwasi) Jacky alimwambia Jacob huku akichukua simu yake na kuelekea bafuni.

Alijifungia mle bafuni na kumpigia simu Carlos, akamweleza yote aliyoyasikia kutoka kwa Jacob kuhusu Kisu. Alimtaka Carlos afanye kila awezavyo kuwasiliana na Kisu na kumgawo wake ili atoroke nchi kabla polisi hawajamfikia, na alipomaliza kuongea na Carlos alirejea pale sebuleni na kumkuta Jacob akimsubiri kwa hamu.

Hmm! It was not unfortunate, I wanted this to happen. Although I don't like but I needed to do this for a special reason. It has also helped me discover what was hidden inside me, obviously I do love Jacob. I deeply love him and for that I can't argue with my soul…” (Hmm! Haikuwa ni bahati mbaya, nilihitaji kitu kama hiki. Japo sipendi lakini nilihitaji kufanya hivi kwa sababu maalumu. Pia imenisaidia kugundua kilichokuwa kimejificha ndani mwangu, ni wazi bado nampenda Jacob. Nampenda sana na kwa hilo siwezi kubishana na nafsi yangu…) Jacky aliwaza wakati akimfuata Jacob aliyekuwa bado kajilaza pale sakafuni.

Jacob hakusema chochote alimvuta Jacky huku akimtazama kwa macho ya uchu kama fisi aliyeona mfupa na kumkumbatia kwa nguvu huku akimporomoshea mabusu mazito mazito. Jacky alijikuta hajiwezi tena na alihitaji huduma kwa mara nyingine tena.

Jacky alikifahamu alichokihitaji Jacob, hakumkawiza akaanza manjonjo yake na kumpatia huduma, wakaingia katika mzunguko wa pili huku ile sebule ikijazwa na vilio vya mahaba toka kwa Jacky kuashiria raha aliyokuwa akiipata. Walichezeshana gwaride la uhakika na hadi wanamaliza mzunguko wa pili wote walikuwa hoi bin taaban.

Jacky, you are still hot, my love,” (Jacky, hakika bado unadai mno, mpenzi wangu) Jacob alimwambia Jacky huku akitweta baada ya kumaliza ule mzunguko wa pili. Jacob alikuwa amejilaza chali pale sakafuni juu ya zulia nene la manyoya akitiririkwa na jasho jingi. Shughuli aliyoifanya haikuwa ndogo. Jacob alishusha pumzi na kujiinua kutoka pale katika zulia alikokuwa amelala, akajimiminia mvinyo katika bilauri yake na kunywa huku akitweta.

Jacky alichukua nguo zake na kukimbilia bafuni na baada ya muda mfupi alitoka akiwa tayari amekwisha vaa nguo zake zote na kuchukua mkoba wake.

I thought today you would spend the night with me, darling?” (Nilidhani leo ungekesha nami, mpenzi?) Jacob alimuuliza Jacky huku akimtazama kwa makini na kumfanya Jacky anyanyue mkono wake na kuitazama tena saa yake ya mkononi.

It’s quarters to nine, my love, I don't want to upset my husband, see you tomorrow,” (Ni saa tatu kasoro robo, mpenzi, sitaki kumuudhi mume wangu, tutaonana kesho) Jacky aliongea kwa sauti hafifu ya kirafiki na hapo akamuona Jacob akimtazama kwa macho yaliyokuwa yamejaa wivu.

But I thought…” (Lakini nilidhani…) Jacob alisema lakini Jacky akamkatiza.

Another day, darling, please…” (Siku nyingine, mpenzi, tafadhali) Jacky alisema huku akirembua macho yake kisha akaanza kuondoka.

“Jacky…”

“Abee”

I love you so much until I feel confused,” (Nakupenda sana hadi najihisi kuchanganyikiwa) Jacob alisema huku akijiinua pale sakafuni.

Me too,” (Mimi pia) Jacky alisema huku akimtazama Jacob kwa makini.

Please don't let me down, my love, see you tomorrow,” (Tafadhali usiniangushe, mpenzi wangu, kesho tuonane).

Until death separates us,” (Hadi kifo kitakapotutenganisha) Jacky aliongea kwa utulivu huku akiruhusu tabasamu lake kuchanua usoni, kisha alimsogelea Jacob na kumbusu mdomoni.

Taratibu akageuka na kuanza kuondoka akimwacha Jacob anamsindikiza kwa macho huku akiutazama mtikisiko maridhawa wa umbo lake zuri. Jacob alibaki akimkodolea macho jacky huku akihisi nafsi yake ilikuwa imepata utajiri mkubwa wa furaha isiyoelezeka.

Jacky alitoka ndani ya lile jumba la Jacob na kuingia ndani ya gari lake aina ya kisha aliliondoa gari lake aina ya Range Rover Sport L494 la rangi nyeupe taratibu.

Muda ule ile hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam ilikuwa imepoa zaidi, manyunyu hafifu ya mvua yalikuwa yakianguka kutoka angani kulikotanda wingu la mvua kiasi cha kuweza kuizuia nyota. Muda wote alikuwa akiwaza namna ya kujikwamua na lile balaa kutokana na kushiriki katika wizi wa mabilioni pale Benki ya Biashara.

Wakati akiendesha gari macho yake yalikuwa makini kutazama kila mahali katika namna ya kuchunguza kuwa hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia nyendo zake.

Itaendelea...

CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Shukrani sana Bishop, kwa hivi vitamin unavyo share nasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bishop leo it's your day ukipata mda tutupie episode za kutosha tusherehekee birthday [emoji847]
Umesikika Shunie wangu, ngoja niongeze episodes 2...

Kizungumkuti! - 62

Na Bishop Hiluka

ASP Komba alijilaumu sana kwa kushindwa kumpata Joram Mbezi akiwa hai kwani aliamini kuwa Joram ndiye alikuwa kiungo kikubwa kati ya mtu aliyejiita Belinda Jackson na Yusuf na sasa kazi ilianza kuwa ngumu pasipo Joram.

Alikuwa amebakiwa na kazi moja tu, kumbana Yusuf ili amweleze uhusiano wake na wale watu wawili, Joram Mbezi ambaye sasa alikuwa marehemu na Belinda Jackson, ambaye hawakuwa na taarifa zake hadi muda huo. Alipaswa kupata majibu ya uchunguzi wake haraka iwezekanavyo.

Endelea...

ASP Komba alionekana kuchoka sana asubuhi ile alikumbuka kuwa baada ya kurudi tu ofisini mkuu wake wa kazi, Kamanda wa Polisi wa kanda maalumu alimuuliza, “Unadhani kuna haja ya kukuongezea mtu mwingine katika kazi hii?”

“Hapana, afande! Naamini sisi wawili tunatosha. Nikihitaji msaada, nitakujulisha,” ASP Komba alijibu.

Picha ya maiti ya Joram Mbezi iliyokuwa imefumuliwa kichwani iliendelea kumjia ASP Komba akilini mwake, baada ya uchunguzi wa mwili wa Joram Mbezi waliwahoji takriban watu watano, wakiwamo wale watoto wawili waliopewa madafu katika eneo la tukio.

Watu hao watano, watatu wakiwa watu wazima ambao kati yao mmoja alikuwa mwanamume na wawili wanawake, walichukuliwa hadi kituo cha polisi na kuhojiwa na ASP Komba, wote walieleza kuwa walimwona muuza madafu kwa mbali na wala hawakumtilia maanani, hivyo wasingeweza kumtambua endapo wangemuona tena.

Ila wale watoto waliopewa madafu walikiri kumwona kwa ukaribu yule muuza madafu akitumia bastola. Walieleza kuwa waliitambua bastola kwa kuwa waliwahi kuona zikitumika kwenye sinema walizoziangalia kwenye mabanda ya video.

Baada ya mahojiano, wale watu wazima watatu, isipokuwa wale watoto, waliachiwa. ASP Komba na Sajenti Mapambano wakabaki peke yao na wale watoto.

ASP Komba aliwatazama kwa macho ya upole wale watoto. Aliamini kuwa ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushuhudia mauaji na kufikishwa kituo cha polisi kutoa maelezo. ASP Komba alikumbuka kuwa pamoja na mambo mengi aliyowauliza wale watoto lakini alitaka kujua kama wangeweza kumtambua yule mtu aliyewapa madafu endapo wangemuona kwenye picha.

“Mkimwona tena yule baba aliyekupeni madafu mtaweza kumtambua?” ASP Komba aliwauliza wale watoto.

“Sura yake?” aliuliza mtoto mmoja aliyeonekana mjanja zaidi.

”Ndiyo, sura yake”

“Naweza,” yule mtoto alijibu pasipo hata kufikiria mara mbili.

“Hata ukimuona kwenye picha?” ASP Komba alimuuliza kwa upole huku akimkazia macho.

“Ntamjua.”

ASP Komba aliinuka akafungua kabati moja la chuma lililokuwa ukutani na kuvuta droo iliyokuwa ndani yake upande wa kulia, akatoa faili lililokuwa na picha kadhaa za wahalifu, akawawekea mbele wale watoto.

“Angalieni vizuri kama picha ya huyo mtu imo humo. Msifanye haraka,” ASP Komba aliwaeleza kwa sauti ya upole.

Pamoja na kuchukua muda mrefu kufunua na kuziangalia zile picha kwa utulivu mkubwa, wakipitia kila moja kwa msaada lakini hawakuweza kumuona mtu waliyekuwa wakimtafuta. Jambo lile likazidi kumuumiza ASP Komba.

* * * * *

I killed Kisu, he had to die…” (Nimemuua Kisu, alipaswa kufa…) maneno ya Carlos ambayo bado yaliendelea kupita kichwani mwa Jacky na kumsumbua. Baada ya kuambiwa maneno yale Jacky hakusema lolote, alijiondosha pole pole pale alipokuwa amesimama akaketi juu ya sofa.

Uso wake ulionesha mchanganyiko wa huzuni na hasira. Alimtazama Carlos huku akipumua kwa nguvu. Carlos alimtazama Jacky kwa mshangao, akapitisha ulimi wake chini ya midomo yake. Hakuweza kuelewa mara moja ni kipi kilichomkera Jacky.

Carlos alimsogelea Jacky, akaketi karibu yake huku akimtulizia macho yake usoni akimtazama kwa makini.

Why you look so serious?” (Vipi, mbona unaonekana hivyo?) Carlos alimuuliza Jacky huku akiendelea kumkazia macho.

Jacky alimtazama Carlos, akashusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani, “There was no reason to kill Kisu,” (Hapakuwa na sababu ya kumuua Kisu) alisema, uso wake akiwa kaukunja, kisha akaongeza, “We agreed to bring him here, give him his share and then let him leave the country,” (Tulikubaliana kuwa umlete hapa, umkatie chake kisha atoroke nchi).

Carlos alitazama kando akaonekana akiwaza kwa kitambo kifupi kisha akayarudisha macho kwa Jacky, “So, is this what makes you so distressed?” (Kwa hiyo, ndicho kinachokukera sana?)

“Kwani wewe hakikukeri?” Jacky alimuuliza huku aakimtulizia macho.

“Kinikere kwa vipi? Carlos aliongea kwa sauti iliyoanza kuonesha dalili za hasira. “Si alikuwa akisakwa na polisi kwa udi na uvumba, na ilibaki kidogo tu wangemtia mbaroni, sasa weweulitakaje?”

Jacky alibaki kimya akimtazama Carlos kwa makini, kisha alitazama kando, akashusha pumzi za ndani kwa ndani.

I don't understand, what are you trying to tell me, Jacky?” (Sijaelewa, unajaribu kuniambia nini, Jacky?) Carlos alimuuliza Jacky huku akimkazia macho yaliyokuwa yanawaka kwa hasira.

Listen, Carlos. We have everything that man has to have that can buy anything, I didn't see a reason to start killing people who helped us!” (Sikiliza, Carlos. Tuna kila kitu ambacho binadamu anatakiwa kuna nacho ambacho kinaweza kununua chochote, sikuona sababu ya kuanza kufanya mauaji kwa watu waliotusaidia!) Jacky alisema huku akiminya midomo yake.

Carlos aliachia tabasamu la mbali, akatingisha kichwa taratibu, “Jacky,” alisema kwa sauti ya upole. “Hivi tangu lini mwenzangu umeanza kuwa mlokole?”

“Nani mlokole?” Jacky alimuuliza Carlos huku akitoa macho. “Yaani mimi niwe mlokole, are you kidding?

“Kama si mlokole basi ni nini hiki unachomaanisha?” Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky.

”Basi tuyaache hayo, tayari yameshatokea na hakuna namna ya kumrudishia Kisu uhai wake,” Jacky alisema huku akiinuka pale kwenye sofa. Akaingia jikoni. Carlos alimsindikiza kwa macho kisha akainuka na kutoka nje.

Baada ya kuandaa kifungua kinywa, Jacky alitoka na kuelekea sebuleni, hakumkuta Carlos, akaanza kuita akidhani labda Carlos alikuwa chumbani, kimya. Akaamua kuchukua simu yake na kumpigia simu lakini simu ilikuwa inaongea na simu nyingine na baada ya muda alipokea ujumbe mfupi, “Nimetoka kidogo, nitarudi baada ya nusu saa…

Saa tano asubuhi Jacky alikuwa amejipumzisha kwenye kochi kubwa la sofa pale sebuleni, hadi muda huo Carlos hakuwepo nyumbani. Jacky hakuwa na furaha kabisa kama alivyozoea siku zote, alijikuta akiwa na mawazo mengi yaliyokuwa yakizunguka kichwani kwake kiasi cha kutaka kumtia wendawazimu.

Jacky alikwisha anza kuchoshwa aina ile ya maisha waliyokuwa wakiyaishi yeye na mumewe Carlos, alijiona ni mtu mwenye hatia kuishi maisha kama yale, ya kuuza utu wake na hata kuhatarisha maisha kwa sababu ya kutaka kuendelea kupata mabilioni ya fedha.

Alianza kujishangaa, kwa nini aendelee kuishi maisha ya uhalifu wakati tayari walikuwa na fedha nyingi za kutosha kufanya chochote na hata kuishi nchi yoyote!

Nyumba waliyokuwa wakiishi lilikuwa kasri lililokuwa na thamani kubwa ya zaidi ya mabilioni ya fedha na walikuwa na nyumba nyingine tatu jijini Dar es Salaam, zenye thamani ya mabilioni ya fedha na miradi kadhaa iliyokuwa ikiwaingizia fedha nyingi, japo hazikufikia mabilioni. Pia walikuwa na magari kadhaa ya kifahari.

Kila alipofikiria mambo aliyokwisha yafanya na wanaume kadhaa kwa maelekezo ya mume wake Carlos, alianza kuona kinyaa na kujiona mjinga kukubali kutumika kama chambo cha kuingiza mabilioni ya fedha. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akihisi thamani ya utu wake ilikwisha toweka siku nyingi na sasa alikuwa akiishi maisha ya majonzi!

Itaendelea...
 
Kizungumkuti! - 63

Na Bishop Hiluka

Nyumba waliyokuwa wakiishi lilikuwa kasri lililokuwa na thamani kubwa ya zaidi ya mabilioni ya fedha na walikuwa na nyumba nyingine tatu jijini Dar es Salaam, zenye thamani ya mabilioni ya fedha na miradi kadhaa iliyokuwa ikiwaingizia fedha nyingi, japo hazikufikia mabilioni. Pia walikuwa na magari kadhaa ya kifahari.

Kila alipofikiria mambo aliyokwisha yafanya na wanaume kadhaa kwa maelekezo ya mume wake Carlos, alianza kuona kinyaa na kujiona mjinga kukubali kutumika kama chambo cha kuingiza mabilioni ya fedha. Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani huku akihisi thamani ya utu wake ilikwisha toweka siku nyingi na sasa alikuwa akiishi maisha ya majonzi!

Endelea...

Muda ule Jacky alikata shauri kuwa tukio lile la wizi wa fedha katika Benki ya Biashara tawi la barabara ya Lumumba pale Mnazi Mmoja lingekuwa la mwisho, kwani hakutaka kuendelea na maisha kama yale, potelea mbali, kama Carlos angechukia, yeye alikuwa tayari kwa lolote.

Alishusha pumzi ndefu za ndani kwa ndani na kujiegemeza kwenye sofa huku akifumba macho yake.

Hadi muda ule hakuwa ametia chochote tumboni japo alipika na wala hakuwa akihisi njaa, aliamua kuliendea jokofu na kujimiminia juisi ya passion ya boksi iliyokuwa ndani ya lile jokofu, kisha alirejea pale kwenye sofa na kuanza kunywa taratibu huku akiendelea kuwaza hili na lile.

Kando ya lile kochi kulikuwa na meza ndogo na juu ya ile meza kulikuwa na magazeti kadhaa ya siku ile yaliyokuwa yamepitishwa pale na kijana mmoja muuza magazeti ambaye walikuwa wamempa kazi ya kuwapitishia magazeti kila siku asubuhi. Lakini cha ajabu, Jacky aliyapokea na kuyabwaga pale juu ya meza na hakuwa amesoma gazeti lolote hadi muda ule.

Jacky aliyatazama kwa makini na kushusha pumzi za ndani kwa ndani, kisha alijinyanyua na kuchukua gazeti moja akaanza kulipekua akitafuta ukurasa wa mwendelezo wa riwaya moja aliyoipenda sana ya “Hadi Lini!” iliyoandikwa na mtunzi mahili nchini, ambayo ilikuwa ikiendelea kwenye gazeti lile.

Hata hivyo, alisoma paragrafu mbili tu za mwanzo na kulitupa gazeti lile kando akiwa hajisikii kufanya chochote. Muda ule ule alisikia muungurumo wa gari la Carlos wakati lilipokuwa likiingia kwenye uzio wa ile nyumba, kisha mlango mkubwa wa sebuleni ulifunguliwa na Carlos aliingia ndani akionekana mwenye wasiwasi mwingi.

Carlos alisimama akamtazama Jacky kwa kitambo kirefu bila kusema neno kisha kama aliyegutuka alimtupia Jacky gazeti moja alilokuwa amelishika mkononi.

Jacky alimtazama Carlos kwa mshangao na kulitupia jicho lile gazeti lililokuwa limeangukia kwenye mapaja yake, na hapo akapigwa butwaa akiwa haamini macho yake.

Moyo wake ulipiga mshindo pale macho yake yalipoangukia kwenye maneno makubwa yaliyokuwa yamekolezwa wino mweusi yakiwa na kichwa cha habari: ‘Mfanyakazi benki akamatwa akihusishwa na wizi wa mabilioni, wenzake wasakwa’.

Jacky aliinua uso wake kumtazama Carlos kwa wasiwasi, na wakati huo huo Carlos alikuwa akimtazama Jacky kwa makini, wakatazamana kwa kitambo kisha Carlos akatingisha kichwa chake kwa huzuni.

Kwa haraka Jacky aliyarudisha macho yake kwenye lile gazeti na kupitisha macho yake kwenye maandishi ya habari iliyoandikwa chini ya kichwa hicho cha habari, akayatuliza na kuona kuwa jina la Yusuf halikuwa limetajwa kabisa, japo benki aliyofanyia kazi ilitajwa.

Habari ile ilieleza kuwa mfanyakazi mmoja (jina lake kapuni) alikuwa anashikiliwa na polisi kwa kujihusisha na wizi wa mabilioni ya fedha akiwa mfanyakazi wa benki, na kwamba alishirikiana na watu wengine watatu (majina yamehifadhiwa) ambao walikuwa wanatafutwa.

Habari ile iliendelea kueleza kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu alikuwa anawaomba raia wema washirikiane na jeshi la polisi katika kuwafichua wote watakaowatilia shaka.

Jacky aliinua uso wake na kumtazama Carlos, alilifunga lile gazeti na kuketi huku akiendelea kumtazama Carlos, lakini alishangaa kwa kutoiona ile habari mwanzo pale alipokuwa akilipitia lile gazeti lililokuwa na hadithi ya Hadi Lini! ambalo alilitupia pale mezani.

“Kukamatwa kwa Yusuf inaweza isiwe kitu kinachoninyima raha, kwa kuwa hana information nyingi za kuwaeleza polisi… hata kama watambana sana bado hana ufahamu mzuri kuhusu wewe, ila kinachoninyima raha ni kama watambana aeleze wapi mlikutana na wao kufuatilia katika hoteli mlizokutana ili kutafuta picha za video za CCTV…” hatimaye Carlos alisema kwa huzuni akivunja ukimya.

“Ndiyo hapo sasa! Kwa upumbavu wake anaweza kuropoka kila kitu akidhani kuwa anawapunguzia kazi ya upelelezi ili wamsamehe,” Jacky alijibu huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.

Carlos alimtazama Jacky kwa makini na kubetua kichwa chake kukubaliana naye, kisha kilipita kitambo kirefu cha ukimya kila mmoja akionekana kuzama kwenye mawazo.

Carlos alijiinamia akawaza kidogo, kisha akashusha pumzi. Alipoinua macho kumtazama Jacky, akasema, “Now what do you think?” (Sasa una mawazo gani?)

Let us leave the city first, if possible we can leave the country and stay there for several months.” (Tuondoke mjini kwanza, ikiwezekana tuhame nchi tukakae huko kwa miezi kadhaa tukisikilizia).

Where do we go?” (Tuelekee wapi?)

I don't know ... anywhere, we just have to leave. We have enough resources to take us anywhere,” (Sijui… popote pale, mradi tuondoke tu. Tuna mali nyingi za kutosha kutupeleka popote) Jacky alisema huku akishusha pumzi.

Is it really that you’ve reached that decision, Jacky?” (Ni kweli umefikia uamuzi huo, Jacky?)

“Unauonaje, wa kipumbuvu, ee?”

“Sijasema hivyo!”

“Kumbe?”

“Nataka nithibitishe tu kwamba kweli tunataka kuikimbia nchi!”

Carlos, if you would like to stay here, I do not force you to leave,” (Carlos, kama unapenda kuendelea kuishi hapa, sikulazimishi uondoke) Jacky alisema huku sauti yake ikianza kuwa na mikwaruzo ya hasira. “Continue to live here, look for another woman, do…” (Endelea kuishi hapa, tafuta mwanamke mwingine, fanya…)

“Jacky!” Carlos alimkatiza.

What?” (Nini?) Jacky aliuliza huku akimtolea Carlos macho.

“Mbona unataka kuvuka mpaka?” Carlos alisema huku akimkazia macho Jacky.

Wakabaki kimya wakitumbuliana macho. Na wakiwa katika ukimya ule mara Carlos akaonekana kugutuka akionekana kupata wazo na kumkazia macho Jacky.

Oh my God, Jasmine!” Jacob alisema huku midomo yake ikitetemeka kama aliyekuwa amemuona malaika mtoa roho akimjia mbele yake. Jacky alimtazama Carlos kwa mshangao.

Carlos alianza kuranda randa pale sebuleni akiwa ameinamisha kichwa chake chini akitafakari kwa kina. Jacky aliendelea kumtumbulia macho Carlos kwa mshangao bila kusema neno.

I've got an idea,” (Nimepata wazo) Carlos alisema huku akiketi taratibu kwenye sofa. Jacky aliendelea kumtazama kwa makini bila kusema neno lolote.

We need to find a quick way to silence Kabwe and Liston before things get worse, and then I’ll find out how to deal with Yusuf in jail,” (Itabidi tutafute njia ya haraka ya kuwanyamazisha Kabwe na Liston kwanza kabla mambo hayajaharibika, halafu nitatafuta namna ya kudili na Yusuf kule kule mahabusu) Carlos alisema huku akiachia tabasamu.

Jacky alishtuka sana na kumkazia macho Carlos kwa hofu kana kwamba alikuwa akitazama kitu cha ajabu sana chenye kutisha.

What do you mean to silence them, Carlos?” (Unamaanisha nini kuwanyamazisha, Carlos?) Jacky aliuliza huku akionekana kuanza kuchanganyikiwa.

To kill them, like Kisu,” (Wauawe, kama Kisu) Carlos alisistiza huku akiendelea kutabasamu.

“Aah, sasa unataka kutafuta matatizo mengine. Haya bado hayajaisha unataka kuzua mambo mapya!” alisema Jacky kwa huzuni.

Kila kitu sasa kimegeuka kuwa KIZUNGUMKUTI, hata mimi sijui nini kitatokea, tuzidi kufuatilia stori hii ya kusisimua kujionea jinsi hiki KIZINGUMKUTI kinavyoendelea...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom