Prisoner of hope
JF-Expert Member
- Aug 9, 2017
- 2,440
- 2,575
Shukrani sana Bishop...Kizungumkuti! - 56
Na Bishop Hiluka
ILIPOISHIA
“Sijui unatumia kinywaji gani?” Jacob alimwuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.
“Mvinyo mwepesi tafadhali,” Jacky alisema, na hapo Jacob akainuka na kuelekea kwenye jokofu kubwa la vinywaji.na kurudi na chupa ya mvinyo, akamimina katika bilauri mbili, moja akampatia Jacky na nyingine akabaki nayo mwenyewe, kisha waligongesha zile bilauri kutakiana afya njema huku Jacob akiachia tabasamu pana.
Endelea...
Alikunywa kidogo na kuiweka bilauri yake juu ya meza huku akimtazama Jacky katika namna ya kuuajabia uzuri wake. Jacky alikuwa amevaa gauni jepesi jeusi la kata mikono lililokuwa limelichora vyema umbo lake na kuishia juu ya magoti yake na hivyo kuifichua hazina nzuri ya miguu yake. Miguuni alikuwa amevaa viatu vyekundu vyenye visigino virefu.
Kope zake zilikuwa zimekolea wanja mwembamba mfano wa mwezi mwandamo na kuyafanya macho yake makubwa, meupe na legevu yaifanye akili ya Jacob isikinai kumtazama muda wote. Kila wakati tabasamu lake lilizisogeza kingo pana za mdomo wake wa juu na wa chini na hivyo kufanya meno yake meupe yaliyopangika vizuri kuonekana bila kificho.
Alikuwa amevaa hereni nzuri za madini ya tanzanite kwenye masikio yake huku mkufu mwembamba wa dhahabu safi ukiizunguka vyema shingo yake nyembamba na kisha kidani chake kupotelea katikati ya matiti yake.
“When you called me you really confused me a lot, and so far I don’t know what’s exactly the problem can be that makes you want to see me so quickly!” (Uliponipigia simu kwa kweli ulinichanganya sana, na hadi sasa sijajua una tatizo gani kiasi cha kutaka kuniona haraka kiasi hiki!) Jacob alisema huku akipiga funda jingine la mvinyo na kuketi karibu ya Jacky huku akimtazama kwa makini.
“First I must thank you for giving me such great honor to welcome me to your home. A great person like you to invite someone like me is not a small thing,” (Kwanza nakushukuru sana kwa kunipa heshima kubwa kama hii kunikaribisha nyumbani kwako. Mtu mkubwa kama wewe kukubali kunikaribisha mtu kama mimi si jambo dogo) Jacky alisema kwa mzaha huku akilazimisha tabasamu.
“Stop flattering me, here is your home and you don't need to ask to come here, you’re welcome anytime, by the way, I’d not want to miss an angel like you. You don’t know the joy I had after receiving your phone call. After many years of escaping me today I am lucky to be with you, just the two of us, alone, my heart is full of joy,” (Acha kunizingua, hapa ni nyumbani kwako na huna haja ya kuomba kuja, muda wowote unakaribishwa, hata hivyo, nisingeweza kukosa kuonana na malaika kama wewe. Huwezi kujua furaha niliyokuwa nayo baada ya kupokea simu yako. Baada ya miaka mingi ya kunikimbia hatimaye leo hii nimepata bahati ya kuwa na wewe, tukiwa wiwili tu, faragha, moyo wangu umejaa furaha sana) Jacob alisema huku akiupitisha mkono wake mmoja nyuma ya Jacky na kuanza kumpapasa nyama za mgongo.
Jacky alijitahidi kutabasamu lakini uso wake haukuonesha furaha na wala haukuwa na tashwishwi yoyote, alionesha kuwa alikuwa jambo zito lililokuwa likimtatiza sana moyoni, alikuwa na huzuni moyoni iliyojionesha wazi wazi kwenye macho yake ingawa alijitahidi sana kuificha hali ile lakini hakufanikiwa.
Jacob alimtazama Jacky kwa makini na kuhisi uwepo wa jambo lisilo la kawaida, moyo wake ukaingiwa na ganzi huku akijaribu kujiuliza nini kilichokuwa kikimtatiza Jacky?
Jacob alijikuta akiiona siku ile kama siku iliyokuwa imebeba matukio mabaya yenye kumuumiza roho yake, kwanza rafiki yake Yusuf alikuwa mahabusu baada ya kuhusishwa na tukio la wizi wa mabilioni, alikwenda kituo cha polisi mara mbili, mara ya pli akiwa ameongozana na mke wa Yusuf, Mama Jasmine kujaribu kumshawishi ASP Komba ili waweze kumwekea dhamana Yusuf.
Ushawishi wake uligonga mwamba mara mbili, hasa kwa kuwa ilionekana dhamana ile ingeweza kusababisha mchakato wa upelelezi wa kesi ile uwe mgumu zaidi. ASP Komba alimweleza Jacob kuwa kulikuwa na watu wawili wahusika katika wizi ule wa mabilioni, Joram Mbezi na Belinda Jackson waliopaswa kupatikana kwanza…
Jacob aliyakumbuka yote, na sasa alikuwa sebuleni na Jacky, alijikuta akimtazama Jacky machoni kwa udadisi zaidi na kumsogeza zaidi karibu yake huku akimkumbatia, “Ni nani aliyekuudhi mpenzi wangu?” Jacob alimuuliza Jacky, hata hivyo Jacky hakujibu badala yake alikilaza kichwa chake kwenye kifua cha Jacob.
“Niambie mpenzi wangu, nani aliyekuudhi nimshughulikie, you know I don't want to see you so sad!” (…unajua sipendi kukuona ukiwa una huzuni kiasi hiki!) Jacob alisema na kumfanya Jacky ainue uso wake kumtazama Jacob usoni huku macho yake yakionesha kuzingirwa na malenge lenge ya machozi.
“Hakuna aliyeniudhi, mpenzi,” Jacky alisema kwa sauti laini ya chini lakini iliyokuwa imebeba uchungu mwingi.
“Now what makes you so sad?” (Sasa nini kinachokufanya kuhuzunika kiasi hiki?) Jacob aliuliza kwa udadisi.
“It’s you,” (Ni wewe) Jacky alijibu na kumshtua sana Jacob, kitendo kilichomfanya Jacob akamkazie macho kumtazama kama ambaye hakuwa amemsikia vizuri.
“Mimi!” Jacob aliuliza kwa mshangao.
“Ndiyo, ni wewe,” Jacky alisisitiza huku akiendelea kumtazama Jacob kwa huzuni.
“What have I done to you, my love?” (Kwani nimekufanya nini, mpenzi?) Jacob alimuuliza Jacky huku akimtazama kwa makini.
Jacky alivuta pumzi ndefu kisha akazishusha taratibu na kuminya midomo yake huku akimtulizia macho, “To be honest, I began to forget you, but now you’ve come back into my life and hurt the sore that started to heal,” (Kusema ukweli, nilianza kukusahau, lakini sasa umerudi katika maisha yangu na kutonesha kidonda kilichoanza kupona) Jacky alisema huku akijiegemeza kifuani kwa Jacob.
“I’m so sorry for what happened, but the truth is that I still love you very much, I couldn’t stop myself from following you,” (Nasikitika samahani kwa kilichotokea, lakini ukweli ni kwamba bado nakupenda sana, sikuweza kujizuia kukufuatilia) Jacob alimwambia Jacky huku akishusha pumzi za ndani kwa ndani.
Jacky alimtazama Jacob machoni na kutabasamu, “How many of you live here?” (Hivi humu ndani mnaishi wangapi?)
“For now I’m all alone… but I live with my two siblings, a young sister Daisy and a young brother Goodluck, they’ve gone for a short vacation in Songea…” (Kwa sasa niko peke yangu… ila naishi na ndugu zangu wawili, wa kike Daisy Haule na wa kiume Goodluck Haule, ambao wapo Songea kwa likizo fupi…) Jacob alisema huku akimtazama Jacky na kutabasamu.
“What is it?” (Kwani vipi?) kisha Jacob akamuuliza Jacky kwa shauku.
“I’m just curious, you live alone in a big building like this! No wife, no servant to serve you?” (Najiuliza tu, unaishi peke yako kwenye jumba kubwa kama hili! Huna mke, huna hata mtumishi wa kukusaidia kazi?)
Itaendelea...
CC the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman moneytalk marybaby, nipo2, ram, kisukari, Smart911, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, Mine eyes, kuku mweus, Thad, hearly, Shunie, moneytalk,Tumosa, Mine eyes, Kudo, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard irakunda, skfull, popie, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Sent using Jamii Forums mobile app