Stori gani uliwahi kusimuliwa kuhusu mchezaji wa mpira kumbe 'kamba'?

Wakati Cristiano anatoka Man U kwenda Madrid nliambiwa Man U walikua hawataki kumuuza ko cristiano alipita mashambani hadi akafika kwenye team ya Madrid...we blaza ulienidanganya madako yako
 
Robto Kalosi mashuti yake mabeki wanakwepa sababu makalSana

🤣🤣🤣🤣🤣
Nadhani unamaanisha roberto carlos. huyu jamaa wakiwa wanacheza nadhani kombe la dunia Brazil vs ujerumani ilipatikana faulo nje ya kumi na nane golikipa akiwa oliver kahn.

Wakati akina rivaldo wamejipanga na mabeki wa ujerumani akawa anawaonyesha ishara ya kusogea kwa mkono sasa akina rivaldo wakadhani anawapanga wakawa wanasogea tu.

Ikabidi anyoshe mkono juu ishara ya kuomba refa amvumilie akaenda akamnong'oneza kitu rivaldo nae akamwambia cafu wakatoka mstarinj baada ya kutoka akawaambia wachezaji wa ujerumanj kwa ishara wasogee kuziba huo mwanya.

Jamaa alirudi nyuma kama hatua kumi alipiga shuti usawa wa nyasj za uwanja wakati anapiga wachezaji wa ujerumani wakaruka mpira ukapita chinj ya miguu yao ukamlenga golikipa oliver kahn.

Na akafung sasa muulize oliver kahn mpira ulipitia wapi na ulimlenga.
 
Eti Pele alikuwa na uwezo wa kuuweka mpira kifuani au kichwani na kukimbia nao ukiwa hapo kifuani/kichwani kuanzia mwanzo wa uwanja (golini kwake) au popote atakapokuwa hadi golini kwa wapinzani na kuushusha kisha kupiga shuti la goli.......ndo maana ana magoli mengi vile.
 
kuna mchezaji mmoja alikua bubu kati ya simba, yanga au milambo ya tabora alikua anapiga mashut balaa alishawah kupindisha mwamba wa goli kwa shuti lake pia alisha wahi kutoa mpira nje ya stadium mara kadhaa
 
Fumo felician alikuwa anachana nyavu kwa mashuti
Marehemu gibson sembuli alikuwa akipiga penati kipa lazima akwepe la sivyo anakufa
Rene higuita alikuwa kipa na ndani
Mwameja alikuwa anadaka kama nyani
 
Gibson Sembuli...eti alipiga penati akamwambia kipa ukidaka unakufa au iache ipite ichane nyavu kipa akasema bora nife
Akadaka ikampiga kifuani akafa kipa yule maskini...

Kumbe kamba...Bro wangu alikuwa muongo RIP bro..hiyo ilikua 90 au 91
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom