Simulizi: For You

Elton Tonny

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
262
1,877
Story na Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa
Rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA KWANZA

★★★★★★★★★★★★★


"Kulikuwa na demu mmoja aliyekuwa anasumbua kitaa fulani hivi, yaani kwa uzuri, shepu na maringo hakukamatika. Alikuwa wa kishua, mdingi wake alikuwa hataki aguswe na yeyote yule. Nyumba yao ilikuwa na ghorofa tatu; ya chini alikaa mshua wake, ya pili maza wa demu, af' ya tatu ndo' dodo alikuwa anakaa, yaani yale maisha ya usiniguse, usinitachi, salamu iwe kwa miguu. Basi wasela nini kitaa wakawa wanajikuta wanaweka mipango eti kumnasa, lakini hamna yeyote aliyefanikiwa. Ndo jamaa mmoja akajitoa akili na kuwaambia ndani ya siku 7 tu angekuwa ashakula huyo demu..."

"Ahahahah... enhe..." akasema Ramla.

"Wakambishia na kumwambia hangeweza na kwamba anajidanganya tu, kwo' mshkaji akasema angerekodi na video kabisa awaonyeshe. Basi siku iliyofuata jamaa akajipeleka kwa ile nyumba na kuomba kazi kama house boy... akaongea maneno mazuri mpaka mshua yule akamkubali. Alipomuuliza jina, jamaa akasema 'mimi kwa jina naitwa B(..).' Dah! Mshua akacheka sana na kumwambia apande juu ili aongee na mke wake. Alipofika kwa maza, akamwambia 'mimi kwa jina naitwa K(...). Huyo maza akacheka kifala na kumwambia apande juu kwa binti kisura ili akajitambulishe na huko..."

"Dah! Na wenyewe wanakubali majina ya matusi kabisa, si muhuni huyo! Hapo msela kashaweza mishe, an atateleza kiulainiii..." akasema Mecky.

"Tulia sasa story bado haijaisha..."

"Eti! Yaani Mecky naye! Em' endelea Xander..." akasema Ramla.

"Alipofika kwa mtoto akakubali sana maana kweli demu alivutia. Lakini alikuwa na nyodo nyingi mno. Alipouliza jina lake, jamaa akasema anaitwa 'kiazi na mchuzi.' Mtoto akafurahia sana na kuanza kuongea naye zaidi, na hapo ndo' akaona jamaa alikuwa mcheshi. Akaongea kwa sauti ya juu kuwaambia wazazi wake wamuajiri maana alimpenda. Basi siku mbili tatu jamaa akaendelea kazi. Alionyesha kujituma kinoma, lengo lake akiwa hajasahau lakini..."

"Enhe..." akasema Ramla.

"Ndo' siku ya siku akaandaa msosi ili kumpelekea demu. Sikuzote kabla ya kupeleka chakula juu ilikuwa lazima kipite kwa maza kwanza, kwo' alipokiangalia akashangaa kidogo. Jamaa alikuwa ametengeneza kiazi na mchuzi wa nyama, na mazeli alijua binti yake asingekula. Lakini jamaa akasisitiza akisema atavipenda, kwo' akamwachia ampelekee. Alipofika chumbani kwa mrembo, akaviweka pembeni af' akamfata kitandani pale alikuwa amejilaza huku ana-chat. Akapanda juu yake af' akaanza kumtekenya. Demu akaanza 'kiazi na mchuzi me sitaki buana... kiazi na mchuzi sitakiii.' Sa' si maza'ake akasikia, akapayuka, 'kama hutaki kiazi na mchuzi mpe K(...) ale!"

Marafiki wa kijana huyu waliokuwa wanamsikiliza wakacheka sana.

"Dah! Jamaa akamwambia mtoto, 'umesikia mama alichosema? Unipe nini nile?' Mh! Mtoto akatulia kwanza, af' akamuuliza maza'ake kwa sauti 'nimpe nini...?' Maza akajibu, 'mpe K(...) ale!' Msela akaanza kushughulika fasta! Ilibidi demu atulie tu... jamaa akapiga show ya kibabe huku anachukua mkanda mzima..."

"Ahahah... ahahahah... hizo fujo zote wazazi wake hawakuzisikia?" Ramla akauliza.

"Mama'ake alikuwa anasikia binti yake anasema, 'kiazi na mchuzi, tamu! Tamu jamani!' Akasema kwa sauti na yeye, 'sasa ulikuwa unalalamika nini kama ni vitamu?' Bila kujua mtoto wake analiwa!"

Wote wakacheka.

"Kwo' ikawaje?" akauliza Benjamin.

"Si ndo' maza'ake akaanza kuhisi kama na miguno inatoka huko juu. Ajabu! Akapanda kwenda kuona utamu wa hivyo viazi na mchuzi, kukuta mtoto wake anabenjuliwa kiaina..."

"Jamani... endelea..." akasema Ramla.

"Huyo maza akapiga kelele eti 'pervert! pervert!' jamaa akasanuka fasta na kuvaa bukta yake, af' alivyo mkuda akamgonga denda ya kumuaga mtoto... hapo dodo limeshalegea kinyama! Akatoka nduki mpaka kule chini, ma-bodyguard wakawa wanamkimbiza. Sa' si mzee akawa anawaambia 'kamateni b(..)! kamateni b(..)!' wakashindwa kuelewa wafanye nini, kwa hiyo wakasimama na kuyashika madude yao eti! Aheheheh... ai kudadeki!"

Marafiki wa kijana huyu walimpenda sana kwa kuwa alikuwa na vituko kupita maelezo. Wote walicheka sana baada ya yeye kuwa amewasimulia hadithi hii ya kubuni, na kuanza kuizungumzia utafikiri kilikuwa kisa cha kweli. Kijana huyu aliitwa Alexander, au kama wengi walivyomfahamu na kumwita, Xander. Hapa alikuwa chuoni, pamoja na rafiki zake watatu aliopenda kuwa nao mara nyingi, yaani Mecky, Benjamin, na binti mrembo aliyeitwa Ramla, ijapokuwa alikuwa na marafiki wengi. Ramla pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pamoja na Xander.

Pamoja na ujanja wake mwingi hasa kwenye maneno lakini Xander alikuwa kijana mwerevu sana. Alifahamika kuwa mchezaji mahiri wa timu kuu ya mpira wa miguu ya chuo hiki walichosomea kwa kuwa tegemeo la ufungaji, naye alikuwa na umri wa miaka 21 tu. Pamoja na umri wake kuwa mdogo lakini kimwili alikuwa ngangali haswa, na sura yake ilikuwa nzuri pia na kufanya Ramla awe mwenye ushindani na wasichana wengine chuoni walioitaka nafasi yake; na ndiyo sababu aliringa sana.

Hapa alikuwa na rafiki zake hao baada ya kutoka kwenye kipindi cha somo fulani na kuketi nao sehemu ya nje ya uzio wa jengo la chuo hiki, wakifurahia maongezi ya hapa na pale. Walikuwa wamekaa chini ya mti mfupi wenye kivuli, uliozungukwa na nyasi zilizokatwa vizuri chini na kufanya eneo hilo lipendeze; kukiwa na baadhi ya wanachuo sehemu za pembeni pia. Xander alikuwa amelalia mgongo wake huku kichwa chake akikilaza kwenye mapaja ya Ramla, kama wapendanao wafanyavyo.

"Uliitolea wapi hiyo story?" Benjamin akamuuliza Xander.

"Alinisimuliaga mshkaji wangu mmoja hivi anaitwa Ishmael... nimemkumbuka sana..." Xander akajibu.

"Wa wapi?" akauliza Ramla.

"Kigoma. Nilikutanaga naye sekondari Mwanza, alikuwa poa sana..."

"Eeh afu' nyie mmesikia kuhusu lile kundi la majambazi, sijui majambazi, waliovamia ile shule ya kule Kigoma?" akauliza Benjamin.

"Eeh Ujiji. Nimeona kwenye habari eti wanajikuta magaidi na wenyewe wanajiita Demba Group sijui... Lakini hamna hata mmoja aliyekamatwa na waliwaumiza walimu na wanafunzi wengi," akasema Ramla.

"Mafala tu hao. Siku mbili utasikia wameshakamatwa wote... sijui huwa wanajipelekaga kwa mapolisi?" akasema Xander.

"Ahahah... ni shida," akasema Ramla.

"Dah! Communication sasa hivi, tuwahi class maana patajaa sitaki kuhangaika kutafuta viti," akasema Mecky huku ananyanyuka.

Wote wakanyanyuka na kuanza kuelekea ndani ili kuwahi kipindi. Xander sikuzote alivalia kwa njia yenye mpangilio mzuri sana; yaani ni kama alitaka kujionyesha lakini kihalisi haikuwa hivyo. Alitupia pamba kali mara nyingi na alinukia vizuri sana. Nywele zake alizitengeneza kwa mtindo wa kiduku, nazo zilikuwa laini zenye kuviringika kutokana na yeye kuwa na asili ya uarabu fulani hivi; ijapokuwa hakuonekana hivyo usoni. Yaani alikuwa mwenye sura na ngozi nyeupe, lakini haikupita kiasi sana kama wazungu, na macho yake hayakuwa makubwa.

Ramla alikuwa msichana kutokea Tanga, mwenye miaka 22, naye alikuwa na asili ya uarabu pia (shombe shombe) ijapokuwa hakuwa mweupe sana. Alikuwa mfupi kiasi kumfikia Xander begani, na alibeba hips nene kiasi zilizotokeza kalio lake kwa nyuma vizuri. Alijivunia mwonekano wake, na hasa kuwa mtu wa Xander pia. Mara nyingi alipokuwa naye alipenda kutembea karibu yake au akiwa amemshika mikono, ili kuonyesha wadada wengine kwamba chake kilikuwa chake hivyo wachote vyao kwingine.


★★★


"Kwa hiyo Sandra una mpango gani?"

"Kuhusu?"

"Kuhusu Danny..."

"Sophia... mimi na Danny hatuendani. Sijui nikwambie mara ngapi uelewe..."

"Mpe nafasi tu jamani... mimi sioni ikiwa wewe na Raymond mko vizuri. Kwanza anakuzingua-zingua tu, mara yupo, mara hayupo... kwa nini usiangalie mtu anayeku-feel kama Danny, eh? Mzuri, ana hela..."

"Best, kama hela ingekuwa inanunua kila kitu basi trust me... ningekuwa na mabwana kumi na tano sasa hivi!"

"Sijamaanisha kwamba anataka kukununua. Danny anakupenda sana Sandra... yaani huwa ananieleza jinsi anavyoumia sana kutoweza kuwa nawe. Kwa nini umemng'ang'ania tu Raymond wakati hana hata...."

"Nini? Pesa? Ndiyo unachojali tu hicho maishani mwako Sophie?"

"Sasa siku hizi baby bila pesa unafikiri itakuwaje? Unataka wewe ndo' uje uwe unamlisha?"

"Ahahah... sikia. Mimi siangalii pesa. Kama pesa ninayo, kwa hiyo naangalia vitu zaidi ya pesa. Danny simjui vizuri, lakini ninaweza tu kukisia anachokitaka kutoka kwangu kama ilivyo kwa wasichana wengine. Na kiukweli Sophia mimi sipendi anavyokutumia wewe rafiki yangu kuniandama namna hii. Nilishamkataa. Naomba umwambie aelewe hilo... na aliheshimu. Vinginevyo, atakuwa anatafuta matatizo."

"Utafanyaje... utamwambia baba'ako?"

"Ahahahah... sikufikiria hilo ila ikifikia hatua hiyo atajuta..."

"Mh... haya bwana. Kaka wa watu anaumia sana... Fikiria tena maana siku hizi huwezi kujua mara paap majambazi wakaja kukuteka halafu yeye ndo' akakuokoa!"

"Ahahaaa... kama Demba Group? Ajibebe tu kwa kweli, me hapana... Twende tuwahi class ni Communication sa'hivi..."

Haya yalikuwa ni maongezi baina ya marafiki wa karibu sana; Sophia, na Alexandra. Ni ndani ya chuo hiki hiki, na hapa wawili hawa walikuwa wakijiandaa kuelekea kwenye kipindi cha somo la Communication walipoanza kuongelea mambo hayo. Sophia alikuwa akijaribu kwa siku kadhaa sasa kumshawishi Alexandra amkubali mwanaume fulani aliyeitwa Daniel, ambaye alikuwa ndiye mkuu ndani ya chuo hiki (principal). Pamoja na kwamba Sophia alikuwa mwenye uvutano wenye nguvu sana kwa Alexandra, lilipokuja kwenye suala hilo, binti alikataa katakata kuafikiana nalo.

Alexandra alikuwa binti mrembo sana. Chuoni hapo alikuwa anafahamika kama Waziri wa Afya, kwa sababu ya cheo chake kwenye masuala ya kuongoza na kushughulika na mambo yaliyohusiana na afya za wanachuo. Hii ilikuwa kawaida kwa wanachuo fulani pekee kupewa vyeo vya uongozi wa masuala mbalimbali kwenye chuo hiki, kukiwa na raisi, makamu wake, mawaziri mbalimbali, na wengine kwenye vitengo tofauti. Yaani mambo yaliendeshwa kwa njia fulani rasmi kama ilivyo serikalini. Lakini pia Alexandra na Sophia walikuwa kwenye timu ya mchezo wa kuogelea ya chuo hiki, na hilo lilifanya wajulikane na wengi hasa kwa kuwa wote walikuwa wenye ustadi sana kwenye mchezo huu.

Principal Daniel alikuwa amejaribu kumfanya Alexandra awe ndiyo raisi wa wanachuo eti ili awe juu. Lakini binti alielewa hiyo ilikuwa ni moja ya njia za kutaka kumlaghai ili awe pamoja naye kwa sababu kuna vifaida ambavyo angepata kutokana na cheo hicho. Alichaguliwa kuwa Waziri wa Afya na wanachuo wengine walioona anastahili hilo, na hiyo kwake ilitosha; hakutaka kupewa vitu ili naye arudishe vitu fulani vya faida kwa yeyote.

Alexandra alikuwa msichana mwenye miaka 21. Alikuwa mweupe sana, mwenye sura yenye kuvutia iliyomfanya aonekane kama mwanamitindo, mrefu kiasi, na mwenye umbo la wastani; siyo mwembamba, siyo mnene. Hips zake zilijichora vyema lakini hakuwa na kalio kubwa mno; la wastani lililotokeza kwa kadiri kwa kuwa alikuwa mtu wa mazoezi pia. Nywele zake nyeusi na laini zilikuwa ndefu kufikia mabegani, naye alipendelea sana kuvaa suruali za jeans zilizochanikia magotini na hata mapajani kiasi. Alikuwa binti mwerevu na aliyependa sana masomo yake.

Alexandra alikuwa na mpenzi wake aliyeitwa Raymond, ambaye alikuwa kijana mstaarabu aliyefahamiana naye tokea sekondari. Walikuwa marafiki tu zamani, lakini walipokuja kukutana tena chuoni hapo walianzisha uhusiano. Alimpenda kwa sababu alikuwa kijana mpole asiye na makuu kabisa. Lakini ni watu wachache mno waliojua kuhusu uhusiano wao kwa sababu hawakujionyesha kwa watu.

Raymond alimpenda sana Alexandra pia, naye ijapokuwa aliishi maisha ya familia isiyokuwa na uwezo mkubwa kifedha lakini alinwonyesha binti huyu upendo kwa njia zozote zile alizoweza hata kama kwa wengine ingeonekana ni kidogo. Mama yake alikuwa kwenye mkoa mwingine toka yeye alipofika kwenye huu ili kuanza chuo. Alikuwa na ndugu wengi wa kiukoo ambao hawakumjali sana mama yake wala yeye, hivyo walisaidizana tu kutegemezana kimaisha huku akiendelea kusoma. Naye pia alisoma kwa bidii.

Kufikia hapa ni rahisi kukisia kuwa hadithi hii inawahusu hasa vijana hawa wawili; Alexander, na Alexandra.

Alexander ni Alexandra, na Alexandra ni Alexander. Vijana hawa ni mapacha, na ijapokuwa ni mapacha wa jinsia tofauti, wanafanana sana. Wote wanachukua kozi za masomo yanayohusiana na Tehama (technology), nao wanapenda sana kozi hii na kutazamia kuja kufanya kazi zinazohusiana nayo. Huu ni mwaka wao wa tatu wakiwa kwenye chuo hiki tokea walipojiunga nacho wakiwa na miaka 19. Wamebakiza mwaka mmoja kumaliza diploma, na wanatazamia kuendelea mbele zaidi hata kufikia masters; ijapokuwa hilo ni jambo ambalo ni wazazi wao ndiyo wamewapangia.

Alexandra ni mtaratibu sana, mwelewa, na mwenye msimamo imara. Kwa wengi anafahamika kama Sandra. Yeye hufanya mambo mengi kwa kutumia busara, na ndiyo sababu akapewa cheo cha Waziri wa Afya hasa kutokana na kiwango chake cha juu cha usafi. Lakini Alexander ni mwongeaji, jasiri, na mtukutu kupita kiasi. Anapendwa hasa kwa sababu sikuzote ana njia fulani kwenye maneno inayowapendeza wengi. Pamoja na ujanja wake lakini anampenda sana dada yake. Yaani kwa mambo mengi anaweza kutenda kijeuri na kwa kuongozwa na hisia badala ya hekima, lakini inapokuja kwenye suala la dada yake sikuzote huwa anaonyesha kumjali sana.

★★

Wote wakawa wameingia kwenye darasa moja pamoja na wanachuo wengine, wakimsubiria mwalimu wa somo la Communication Skills. Wanachuo wa kozi mbalimbali husoma somo hilo pia, hivyo mara nyingi darasa hujaa sana. Alexander kama kawaida aliketi upande walioketi wanaume zaidi, naye Alexandra upande waliojaa wasichana. Baada ya mwalimu kuingia, utulivu ukaanza kutawala maana walikuwa wakipiga makelele mno.

Sikuzote mwalimu huyu alipoingia, ukimya ulitawala haraka hasa kwa sababu alipendwa na kuheshimiwa na wengi. Jina lake lilikuwa ni Valentina, na wengi walizoea kumwita madam V. Alikuwa mwanamke anayevutia, mwenye urefu wa wastani. Alipenda kusuka nywele ndefu za rasta na mitindo mingine tofauti-tofauti. Leo alikuwa amesuka mtindo wa nywele nyingi zilizokuwa kama mawimbi-mawimbi na kuziachia zimwagikie mpaka mabegani. Hakuwa mweusi tii, bali kama watu wanavyosema, rangi ya maji ya kunde. Mwili wake ulikuwa mwembamba kiasi lakini kutokea kwenye kiuno chake chembamba kufikia mapajani alikuwa amenawiri vyema kuwaonyesha wengine kwamba 'hips' zake zilinona kwa kadiri fulani. Siku hii alikuwa amevalia T-shirt nyeusi yenye mikono mifupi iliyobana, na sketi ya rangi ya maziwa (cream) iliyobana pia na kuishia magotini mwake.

Umbo lake pia lilichangiwa na yeye kuwa mtu wa mazoezi. Alifundisha somo hili, lakini pia alikuwa ndiye kama mwalimu na kocha wa timu ile ya kuogelea ya wasichana ambayo Alexandra na Sophia walishiriki pia. Ijapokuwa alikuwa mkubwa kiumri, bado mwonekano wake ulimfanya awe kama binti mdogo. Alikuwa mstaarabu sana pia, na maisha yake ya ndani sikuzote hakuwa na kawaida ya kuyaweka wazi kwa yeyote; isipokuwa labda iwe ni kwa mtu aliyemwamini sana. Kwa hiyo wengi hawakuwa wanafahamu maisha yake binafsi yalikuwa vipi.

Siku hii alikuwa akifundisha kuhusu jinsi mawasiliano yanavyoweza kutumika vizuri sehemu kadha wa kadha. Alikuwa akiwaelezea wanafunzi wake kuwa ili waweze kuboresha njia za kuwasiliana vizuri na watu wa maeneo na hali mbalimbali, wanahitaji kujua jinsi ya kujielezea vizuri kuanzia kwenye maongezi mpaka kwenye uandishi. Akaandika pointi kadhaa kwa ufupi huku akizielezea, kisha akaomba waulize maswali kuhusiana na mada hii. Wengi, hasa wanaume vijana humo, walipenda sana kumuuliza maswali kwa kuwa angewapa majibu kwa njia nzuri sana, na pia ili wamfanye aendelee tu kuwepo darasani kwa muda mrefu zaidi.

"...na ijapokuwa mawasiliano ya namna hii wakati mwingine yanaweza kuwa yenye challenge, hasa ikitegemea na sehemu tuseme labda... kwenye vyumba vya wagonjwa, njia ya therapy ya kuwasiliana nao ndiyo inakuwa yenye faida zaidi kwao, na hata kwa familia zao pia..." akaendelea kuelezea.

"Kwa hiyo kumbe njia hiyo hata ICU inaweza kutumika?" akauliza mwanachuo mmoja.

"Ndiyo, tena hasa wagonjwa wa ICU. Kwenye vyumba vya ICU kwa mfano, communication ambayo itategemea huruma ya kutoka moyoni na... experience nzuri ya muuguzi, au mtu wa karibu na mgonjwa, ni jambo la muhimu linalowasaidia sana wagonjwa waweze hata kuona mambo wanayopitia kwa njia positive, badala ya kupoteza matumaini kabisa..." akaeleza madam Valentina.

"Dah, mwanangu huyu ticha anaongeaga vizuri! Yaani kila neno analotamka ni maua tu..." Mecky akamsemesha Xander kwa sauti ya chini.

Xander akatikisa kichwa na kutazama simu yake. Alikuwa ametumiwa ujumbe na Ramla kuwa baadae amtoe "lunch."

"Kuna swali lingine?" madam Valentina akauliza.

Ilionekana hakukuwa mtu mwingine aliyetaka kuuliza swali, na kwa kuwa Mecky hakutaka madam aondoke haraka, akaona tu aulize chochote.

"Okay, kuna kazi hapa nataka... ndiyo una swali?" madam Valentina akasitisha alichokuwa anataka kusema baada ya kumwona Mecky amenyoosha mkono.

"Aaaa... eti kirefu cha ICU ni nini?" Mecky akauliza.

Minong'ono ikaanza kusikika hapo. Watu walikuwa wanajiuliza alikuwa anafikiria nini kuuliza swali hilo.

Valentina akatabasamu kwa mbali, kisha akasema, "Msaidieni. Eti kirefu cha ICU ni nini?"

"Ingia Chumbani Ufe!" Xander akajibu kiutani bila kutazama mbele.

Wanachuo wenzake wakacheka kwa sauti sana, hasa wasichana.

"Ni Intensive Care Unit bwana," akasema Sandra.

"Eeeh? Waziri wa Afya huyo!" Xander akamwambia dada yake na kumwonyesha ishara ya vidole kumpiga kwa bastola.

"Asante. Alexander, ulipojibu vile ulikuwa ukitania siyo?" Valentina akamuuliza Xander.

"Ndiyo ni joke kutoka FB," akajibu Xander.

"Kwa nini unaingiza utani?" Valentina akamuuliza tena.

"Nilifikiri ungetambua kiurahisi nia ya Mecky kukuuliza hilo swali lakini kwa sababu umeuliza... ni ili nifurahishe watu, maana wameboeka," Xander akamjibu hivyo.

Valentina akatabasamu kidogo, kisha akamwambia, "Simama."

Darasa likatulia. Hali ilikuwa imegeuka kuwa nzito ghafla. Xander akasimama na kumtazama "madam" kwa umakini.

"Somo la Communication Skills ni required kwa wote mlio humu. Wengine huwa wanaliona kama la kupoteza muda tu, lakini ni somo la muhimu sana. Hii semester nataka kila mmoja wenu anionyeshe kwamba anaweza kuandika vizuri, na itakuwa inaburudisha sana ikiwa hamtaona kwamba inachosha..." Valentina akasema.

"Nahisi kama inachosha kusimama, nikae?" Xander akasema kwa kejeli.

Wenzake wakacheka.

"Nawapa assignment. Nataka mwandike essay, plain nne. Elezeeni kitu fulani mlichoona nyie wenyewe kipindi fulani cha nyuma. Mnatakiwa kuelezea vizuri sana na kwa ufasaha ili kunifanya mimi kama msomaji niweze kuona mambo jinsi nyie mlivyoyaona. Onyesheni mlichohisi kuwa sehemu hiyo, na jinsi ilivyowaathiri kwa ujumla. Kesho CR kusanya kazi saa 5. Marks mnajua ni za muhimu so get to work. Na wewe..." Valentina akahamishia umakini wake kwa Xander baada ya kumaliza kuwaambia wengine hayo.

Xander akabaki kumwangalia tu. Valentina akaanza kumfata mpaka aliposimama na kumtazama machoni kwa ukaribu.

"Wewe assignment yako ni hiyo hiyo, lakini nataka uiandike leo leo na umpe CR aniletee ofisini kabla ya muda wa kuondoka," Valentina akasema.

"Leo?" Xander akashangaa.

"Leo," Valentina akajibu.

"Kwa hiyo nisiende lunch?" akamuuliza.

"Ndiyo maana yake," Valentina akajibu.

"Kwo' unanipa adhabu kwa sababu..."

"Ndiyo," Valentina akamkatisha na kurudi mbele.

Watu hapo wakaanza kumcheka Xander. Akaishiwa pozi kabisa.

Baada ya madam Valentina kuondoka, wengi wakamfata Xander na kumtania kuwa madam kweli leo alimweza. Ijapokuwa ilimkera kiasi lakini alijua ikiwa angeacha kuifanya hiyo kazi basi kungekuwa na shida, hivyo akaamua angeondoka kuelekea kufata karatasi nne nyeupe ili aanze kuandika haraka.

"Una kiherehere mno, shavu limekushuka," Sandra akapita karibu yake na kumwambia hivyo, kisha akamsukuma kichwa kwa kidole na kuondoka huku anacheka.

"Kwa hiyo hatuwezi kwenda lunch wote baby?" Ramla akamuuliza Xander.

"Hapana. Nenda tu na wengine, me naenda library kuandikia huko," Xander akajibu.

"Haya poa baadae," Ramla akamwambia.

Binti akaenda upande mwingine na kumwacha Xander anaelekea maktaba. Hakuona sababu muhimu iliyofanya mpaka madam Valentina achukue hatua hiyo kwa sababu alikuwa akitania tu. Akawaza labda yeye kusema kwamba madam hakujua nia ya Mecky kumuuliza swali lile ndiyo kulimuudhi, lakini akaona huo ni kama utoto. Kwa vyovyote vile hakuwa na jinsi ila kwenda kuianza tu kazi ili amalize haraka.

Xander akaandika kuhusu wakati fulani alipokuwa na miaka tisa. Yeye, mama yake, pamoja na dada yake walikuwa sehemu fulani ya kujistarehesha wakati wa matembezi siku za likizo. Wakati walipokuwa wamekaa kuzunguka swimming pool, aliona mvulana fulani wa miaka minne au mitano hivi akiwa ndani ya maji hayo. Mvulana huyo alianza kutapatapa, akipiga-piga mikono yake na miguu juu chini ndani ya maji, akiwa anajitahidi kuelea vizuri kwa juu. Mwanzoni watu walifikiri labda alikuwa anatania tu, lakini vilio vyake vilipoanza kuzibwa na maji, msichana fulani wa kama miaka kumi na kitu akaingia upesi ndani ya maji na kumwokoa mtoto huyo. Ni kitu ambacho Xander pia angefanya kama msichana huyo asingemwahi mapema.

Xander alikiandika kisa hiki vizuri na kwa ubunifu sana, naye akampelekea CR (Class Representative) ili aifikishe kazi yake kwa Valentina. Baada ya Valentina kuipokea, akaipitia kwa umakini sana, kisha akaiwekea alama alizoona zinafaa.

★★

Wakati fulani wakiwa wamemaliza vipindi vyao, Xander akafatwa na CR, aliyemwambia kwamba madam Valentina alitaka kumwona ofisini kwake. Xander akaanza kujitapa kwa marafiki zake kuwa alikuwa ameua hiyo kazi na hapo bila shaka madam alikuwa anamwita kumpongeza. Wakampa sifa kama jinsi ambavyo vijana wahuni hufanya, naye akaondoka na kuelekea mpaka ofisini kwa Valentina, na baada ya kuingia akamkuta akiwa ameketi kwenye kiti upande wa pili wa meza yake kutokea aliposimama Xander.

"Vipi Alexander, uko poa?" Valentina akamsalimu.

"Kama kawa," Xander akajibu kwa kujiamini.

"Sawa. Nilikuwa nataka tuongee. Nikuulize kitu fulani?"

"Uliza tu."

"Unalionaje somo la Communication Skills?"

"Nalipenda."

"Unalipenda? Hivyo tu? Tafadhali elezea zaidi hiyo kauli."

"Napenda nywele zako pia. Nakwambia kwa kuwa unastahili kujua," Xander akatania.

Midomo ya Valentina ikaonyesha tabasamu hafifu, kisha akasema, "Asante. Lakini nilikuwa namaanisha uelezee kile unachofikiria kuhusu hili somo."

"Ndiyo... kiukweli... ni darasa zuri. Tokea nilipoanza kusoma hivi vitu kwangu havijawahi kuwa vigumu sana... ijapokuwa siyo mara zote najua jinsi mambo yatakavyokuwa. Unafundisha vizuri sana tokea tulipoanza kusoma. Angalau wewe ni mwalimu unayejali kwamba siyo wanafunzi wote watakuelewa ukitumia English mwanzo mwisho kila unapofundisha," Xander akaeleza.

Valentina akacheka kidogo.

"Sawa. Hii hapa kazi yako," akampatia karatasi zake.

"Kwa hiyo ulikuwa unataka nikueleze... 2? Nimepata 2 ya 5?!!" Xander akashangaa.

"Ndiyo. Umeandika vizuri, na unajua kujieleza, lakini hukueleza jinsi ambavyo kisa hicho kiliku-affect WEWE. Nataka nione ni nini kilichokuchochea zaidi kutokana na yote uliyoona, yaani... Passion," Valentina akaeleza.

"Aisee!" Xander akaonyesha kuvunjika moyo.

"Najua inaonekana kuwa unfair..."

"Sana!"

"Ahahah... okay. Vipi nikikupa assignment nyingine?"

"Kwa nini unafanya hivi madam V?" Xander akauliza.

"Sitakuficha. Unaandika vizuri sana. Nataka tu uzame zaidi kwenye core muhimu za uandishi ili uone jinsi inavyoburudisha, na hivyo hautakuwa unaboeka sana class," akajibu.

"Kwa hiyo unakiri kwamba hujanitendea haki?" Xander akauliza.

Valentina akashindwa kujizuia kucheka. Kwa sababu fulani, Xander alipenda sana kuona jinsi mwalimu wake huyu alivyopendeza sana alipocheka. Akabaki kumwangalia kwa makini.

"Fanya hii assignment uni-impress, ndiyo utaona haki ikitendeka," Valentina akamwambia kiurafiki.

"Nambie..."

"Kaandike essay ya biography, ya mtu yeyote halisi unayempenda au unayemkubali sana. Elezea vitu vinavyokufurahisha au kukukwaza kumhusu kwa utaratibu mzuri sana. Plain tatu tu zinatosha... au ni nyingi?"

Xander alikuwa anamwangalia sana mwanamke huyu, kama anamtathmini kupita kiasi, mpaka Valentina akajishtukia.

"Alexander? Vipi?"

"Oh... fresh. Nita... nitaishughulikia. Unaitaka lini?"

"Kesho."

"Ai... nahisi nitapasua kichwa leo."

Valentina akatabasamu tena, kisha akamruhusu kijana huyu aondoke.

Xander alitoka nje akitafakari jambo fulani kwa kina, na baada ya akili yake kulisawazisha vyema, akaachia tabasamu la hila akipanga kufanya kitu ambacho alijua kingemkomesha mwalimu huyo.



★★★★★★★★★★★★
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TATU

★★★★★★★★★★★★★


MWANZA


Tukio fulani lenye kushtua sana linatokea katikati ya jiji hili. Kikundi cha watu wanaojiita "Demba Group" wanavamia jengo kubwa la ofisi za PPF wakiwa na silaha nzito za mikononi aina ya AK-47, nao wanawafyatua risasi watumishi wa serikali pamoja na walinzi wa jengo hilo. Eneo zima linalozunguka hapo linapatwa na msukosuko mkubwa kwa kuwa watu wengi wanaanza kukimbia ovyo ovyo na shughuli nyingi zinaachwa ili kuokoa maisha yao.

Washiriki wa kikundi hiki wanaharibu vitu vingi hapo, na hakuna yeyote anayeweza kuwatambua kwa sura kwa sababu wanavaa viziba uso vinavyofunika mpaka vichwa vyao na kuacha macho na mdomo wazi kidogo. Hawaibi chochote, bali wanafanya tu vurugu hizo na kuua watu kadhaa hapo, kisha wanatokomea kusikojulikana. Mapolisi kama kawaida wanafika hapo kwa kuchelewa na kuingia jengoni, wakitaka kuhakikisha usalama, lakini bomu linalipuka kutokea ndani ya jengo hilo na kusababisha vifo vya mapolisi wote waliokuwa ndani.

Hali ya hewa inachafuka sana katikati ya jiji hili kwa kuwa sasa ni wazi kwamba hakuna usalama. Hii inakuwa mara ya pili kwa kundi hili kujitokeza na kufanya vurugu namna hii. Mara ya kwanza ilikuwa ni kule Kigoma kwenye shule ya sekondari. Waliua walimu na wanafunzi wachache tu na kufanya vurugu, lakini hii ya Mwanza ndiyo ikawa mbaya zaidi kuliko ile ya huko. Eneo likabaki bila mtu hata mmoja aliyethubutu kusogea, maana walihofia kuna bomu lingine lingelipuka.

Baada ya tukio lile la kwanza kule Kigoma, serikali, kupitia jeshi la polisi, ilikuwa imeahidi kwamba watu hao wangetafutwa na kukamatwa, lakini ahadi hiyo ikawa deni kubwa sasa lisiloweza kulipwa. Haya yaliyotokea jijini Mwanza yalitokea mchana kweupe, lakini hamna hata mtu mmoja wa kundi hilo aliyenaswa.

Muda fulani baadae, vyombo vya usalama vya serikali vilifika hapo na "kupiga kambi" ya muda. Maaskari wengi kutokea idara mbalimbali walifika na kuzuia shughuli yoyote ile isiendelee upande huo. Waandishi wa habari kutoka vituo mbalimbali vya runinga walifika pia, na baadhi wakaweza kuongea na Kamanda wa Polisi wa mkoa kuhusiana na matukio haya. Akaeleza ni wazi sasa kuwa kundi hili ni hatari sana, nao wangefanya kila njia kuhakikisha kwamba wale wote wanaohusika wanakamatwa na kuadhibiwa, hivyo kokote walipo, wajiandae.

Jiji likawa kwenye tafaruku kubwa kwa kupoteza watu 38 siku hiyo; 16 wakiwa mapolisi. Lakini jambo lingine likatokea. Kuna video ikaanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwaonyesha watu kadhaa, wakiwa wamefunika sura zao kabisa huku wameshikilia bunduki mikononi. Mmoja wao alikuwa anasema kwamba yeye ndiyo kiongozi wa Demba Group, na nia yao ni kupindua utawala wa Raisi kwa sababu anaongoza nchi kimabavu. Akatoa kiapo kwamba mambo haya yote mabaya hayataacha kutokea mpaka Raisi ajiondoe kutoka madarakani.

Ilikuwa ni video fupi tu yenye dakika moja na nusu. Ilisambaa kwa uharaka sana mpaka kwenye kampuni za vyombo vya habari, lakini vikapigwa marufuku kuionyesha kwenye runinga zao. Hilo halikuwazuia watu kuiona kwa kuwa wengi tayari waliipata kwa njia ya simu, hivyo hofu iliyoanza kujengwa na kundi hili ikazidi kuongezeka. Midomoni mwa watu wengi siku hii mada ilikuwa ni hiyo. Siyo kwamba wote nchini walipata kujua upesi, ila habari hazingechelewa kuwafikia.


★★★


JENGO LA KITUO CHA USALAMA WA TAIFA

Mkutano wa dharura uliitishwa haraka isivyo kawaida. Walifika baadhi ya viongozi wa vikosi vya ulinzi nchini ili kujadili matukio haya mawili yaliyotokea ndani ya wiki moja tu bila kupatiwa suluhisho la haraka. Aliyeitisha mkutano huu alikuwa ni Jenerali (General) mkuu wa jeshi la nchi (wanajeshi), ambaye aliitwa Jenerali Pingu Senganya. Waliokuwepo walikuwa na vyeo vilivyofuata kutoka kwake; Luteni Jenerali (Liutenant General) aliyeitwa Geneya Oyayu, Brigedia Jenerali (Brigadier General) aliyeitwa Sebastian Tambwe, Kanali (Colonel) aliyeitwa Jacob Rweyemamu, na Luteni Kanali (Lieutenant Colonel) aliyeitwa Oswald Deule.

Hao walikuwa ni baadhi ya viongozi wa jeshi la nchi. Pia, Inspekta Jenerali wa jeshi la polisi (IGP) Donald Ngassa na Kamishna wa jeshi la polisi (CP) Osman Hamisi walifika upesi, na aliyekuwa msimamizi msaidizi wa kitengo cha huduma za ulinzi nchini (Ministry of Defence), mwanamama shupavu Emiliana Ngoyi, alikuwepo pia. Jenerali Pingu alitaka kuwataarifu IGP Donald Ngasa na CP Osman Hamisi kwamba hali hii ilianza kuwa mbaya kupita maelezo, na hivyo angefanya mpango wa kuingiza wanajeshi kwenye msako wa kuwakamata Demba Group.

"Inawezekanaje... inawezekanaje watu 7 wanaingia kwenye jengo lenye ulinzi na kufanya mambo kama vile ni kwao na kuondoka tu? Askari wanakufa, watu wanakufa, halafu wanapotea tu? Halafu wanapost na video kabisa inayosambaa bila sisi kujua chanzo kimetokea wapi, watu wa tech wanafanya nini? Wiki nzima imeisha na sasa ya pili bado hatujawakamata, kwa nini?" Jenerali Pingu akaongea kwa mkazo sana.

"General, hili suala wangetupatia sisi ili tushughulike nalo, maana wanafanya nchi inaonekana ya kizembe," akasema Brigedia Sebastian, akimaanisha wanajeshi waingizwe badala ya mapolisi.

"Tunajua mambo yamekuwa magumu, lakini General, tunafanya kila kitu na wakati huu hawataweza ...." IGP Donald Ngasa akawa anajaribu kutoa maoni.

"Vitendo, matokeo. Ndiyo tunachotaka. Wiki nzima imeisha mmetoa ahadi ambayo imevunjwa na tukio la leo. Hawa watu wanataka kuipindua serikali, na wanaua ovyo tu kama kuwaonyesha wanaweza na hamtawafanya lolote. Tukio la leo linathibitisha kwamba hamjui mnachokifanya, wote ni ubweche tu!" Jenerali Pingu akafoka.

"Mheshimiwa, sisi hatuko chini ya jeshi, na tunaheshimu sehemu yenu kubwa hapa nchini. Ila hili suala tumepewa tushughulike nalo, na ninajua ndani ya siku chache watu hao watakamatwa. Kuna vitu tumeshaanza kufuatilia, na tuna uhakika tutawapata. Jeshi likiingia watu wengi wataumia, kwa sababu brute force mnayotumia huwa ni...."

IGP Donald alipokuwa anasema hayo, akakatishwa na Kanali Jacob Rweyemamu, aliyenyanyua kidole chake juu kumzuia asiendelee kuongea.

"Kwa hiyo ni bora zaidi kuwaacha nyie mwendelee kusinzia, hawa washenzi waendelee kujitawaza mbele ya chakula chetu, halafu tukae tu kuwaangalia? Unajua kwamba sisi hatuko chini ya yeyote ila Raisi, kwa hiyo tunaweza kufanya LOLOTE lile tunalotaka. Hatujali ikiwa kuna mtu yeyote ataumia mpaka tuhakikishe wanatoweka. Mnahesabu kwamba wako 7, kwa sababu mnataka kuonyesha wako 7 tu, lakini hawa wapuuzi wanaweza kuwa nchi nzima. Tumia akili IGP kutambua kwamba wanapotokeza tukio moja sehemu fulani, tukio la pili wanalifanya kwa njia itakayohakikisha wale waliokuwa kwenye lile la kwanza wanatoka huko kirahisi. Ndani ya siku mbili utasikia ni Arusha, Lindi, Nzega, na labda hata nyumbani kwako," Kanali Jacob akasema kwa uzito sana.

"Raisi atatoa tamko kuhusiana na tukio la leo litakalorushwa moja kwa moja kwenye Televisheni. Baada ya video hiyo kusambaa kwenye mitandao, imekuwa wazi kwamba hawa watu siyo wahuni tu. Wana lengo, na mipango yao inafanikiwa kwa njia ambayo inaonyesha wako makini. Bomu la leo liliwalenga mapolisi. Walikuwa wameshaondoka, kwa hiyo inamaanisha walipiga mahesabu kujua mapolisi wangeingia pale muda gani, na kwa utaratibu gani, ili watege muda gani kwenye bomu hilo. Ni wazi wana mafunzo. Kwa hiyo, kwa heshima yote General, ninahitaji kujua nini kitafanywa ili Raisi atoe kibali kwenu," akasema Secretary Emiliana Ngoyi.

"Hakuna cha kufikiria. Raisi ahidhinishe tu ruksa kwetu kuingiza vijana wetu na hili suala halitasikika tena. Kila kitu tutamaliza sisi. Watu hao, tunaowaona kuwa wachache sasa hivi, watasababisha vita. Ni muhimu tuwakalishe kabla hawajaianzisha," akasema Luteni Jenerali Geneya Oyayu.

"Na jeshi la polisi?" akauliza CP Osman Hamisi.

"Nyie fanyeni yenu. Tambeni kwenye vyombo vya habari. Imbeni, imbeni, imbeni... watu wote wasikie kwamba mtawashughulikia. Ndiyo mnachowezea hicho," akasema Jenerali Pingu.

"Lakini General, huu siyo aina ya ushirikiano..."

"Ushirikiano? Tuliwasumbua lini sisi tokea tukio la kwanza? Si mlisema mngewakamata? Raisi anafanya mengi kwa ajili ya hii nchi halafu sasa hivi, out of nowhere kunguni fulani waanze kumsumbua huku nyie mkiwa mmesinzia? Wewe unaweza ukawa na motivation lakini watu wenu wengi wamesinzia mno. Hatutaki mchezo na nchi yetu. Kapigeni domo, kazi tuachieni sisi," Jenerali Pingu akasema.

"Askari 16 wamekufa leo. Next watafata 30, 40, 50. Hatukai kuangalia hiyo pumba aisee," akasema Brigedia Sebastian.

"Tekeleza unayohitaji kufanya," Jenerali Pingu akamwambia Emiliana.

Secretary Emiliana Ngoyi akanyanyuka na kuwaaga wote kwa heshima, kisha akaondoka. IGP Donald Ngasa na CP Osman Hamisi pia wakanyanyuka na kupiga saluti, kisha nao wakaondoka zao.

"Lieutenant Colonel..." Jenerali Pingu akaita.

"Ndiyo..." Luteni Kanali Oswald Deule akaitika.

"Tuma taarifa kwa Meja mpakani kuhusiana na hili. Nataka Meja achague vijana finest walio makini zaidi ili order ikitoka waanze kutembea," Jenerali Pingu akamwambia.

"Sawa mkuu," Luteni Kanali Oswald Deule akakubali.

"Samahani General, naomba hiyo kazi uniachie mimi. Ninajua vijana wazoefu zaidi hasa kwa sababu niko juu ya Meja. Na..."

"Hapana," Jenerali Pingu akamkatisha Kanali Jacob.

Wote wakamtazama.

"Nataka Meja ndiyo achague na yeye ndiyo atawapanga. Anajua tactic nyingi vizuri na anawafunza vizuri vijana wake. Hatutakuwa na shida sana upande wetu akilishughulikia hili. Naamini atalipatia ufumbuzi haraka sana. Deule, zifike haraka," Jenerali Pingu akatoa amri.

Wote wakanyanyuka na kupiga saluti, kisha wakatoka ndani ya chumba cha ofisi hiyo.

Luteni Kanali Oswald akafanya kama alivyoagizwa. Akamtafuta upesi Meja (Major) wa jeshi la nchi, ambaye hakuwa mwingine ila Casmir Eliakim Sona. Ndiyo. Huyu ndiyo baba wa mapacha wale, Alexander na Alexandra. Luteni Kanali akampatia ujumbe wa muhimu kutoka kwa Jenerali Pingu, na bila kusita Meja Casmir akamhakikishia kuwa mambo yote waliyotaka angeanza kuyafanyia kazi haraka sana na hivyo ambacho angesubiri ni amri tu.


★★★


"Kwa nini umekubali?"

"Ningefanyaje sasa, ningekataa?" akauliza Meja Casmir.

"Lakini hili suala si angeshugulika nalo Kanali, kwa nini wakupe wewe?"

"Sijui Kendrick, lakini ni amri kutoka kwa Jenerali Pingu. Ni lazima nitekeleze," akasema Casmir.

Haya yalikuwa maongezi baina ya Meja Casmir Sona na Kapteni (Captain) Kendrick Jabari wa jeshi pia. Kapteni Kendrick alikuwa akimfuata Meja Casmir kwa cheo, lakini wawili hawa walikuwa marafiki wa karibu sana. Walishirikiana kwa mambo mengi sana tokea walipokutana mara ya kwanza kwenye kambi ya mafunzo ya jeshi na kutumikia pamoja kwa muda mrefu mpaka kufikia vyeo hivi. Hapa walikuwa kwenye ofisi zao ndogo za mpakani, wakiwa pamoja wakati Luteni Kanali Oswald alipompa Casmir taarifa ya Jenerali Pingu.

"Vipi kuhusu birthday ya Alice sasa? Na hii utaikosa tena," Kapteni Kendrick akamwambia.

"Ah... yaani sijui. Na nilikuwa nimemwahidi ningekuwepo," akasema Casmir kwa huzuni kiasi.

"Unajua siyo watu wengi wanaopata mwanamke kama wako Casmir. Ni muda mrefu sana unapita haumwonyeshi hata sura yako..."

"Kila siku nampigia video call..."

"Kwa hiyo unafikiri hiyo inatosha?"

"Najua haitoshi..."

"Kwa hiyo?"

"Lakini nitafanyaje? Jambo kama hili ni dharura... sikutegemea..."

"Sizungumzii kuhusu leo tu Casmir..."

"Dah, kaka na wewe umeanza kusound kama mama yangu..."

"Nakwambia ukweli. Wewe ni Meja kaka. Una mke na watoto wazuri... perfect. Wape time. Likizo zote au wakati wa kupumzika wewe unautumia kukaza misuli ya nchi. Maisha ni mafupi, usisahau hilo," Kendrick akamwambia.

"Yeah. Hawa Demba Group wakinisababishia nikakosa event za mke na binti yangu, nawanyoa vipara makalioni," akasema Casmir.

"Tako ni kipara," Kendrick akamwambia kiutani.

Wote wakacheka kidogo.

"Unamwonea sana Alice. Utamwambia kuhusu hili?" Kendrick akamuuliza.

"Ngoja kwanza tuone itakavyokuwa..."

"Birthday yake iko kwenye kona tu hapo..."

"Najua. Lakini sitaki kumvunja moyo. Najua pia nisipomwambia halafu... ikafika tu ndiyo niseme ataumia hata zaidi. Na Sandra, Azra..."

"Bila kumsahau mzee wa fujo," akasema Kendrick, akimaanisha Xander.

"Yaani! Uko sahihi sana Ken. Nimeionea familia yangu kwa kipindi kirefu," akasema Casmir kwa hisia.

"Haina haja ya kuvunjika namna hiyo. Unakumbuka wakati ule tumejikuta chini ya shida? Ilionekana kama mimi na wewe hatungeokoka lakini mara puuf! Mungu akatuonyesha handaki lile lililookoa uhai wetu. Nachotaka kusema ni kwamba, usikate tamaa. Lazima itakuja njia tu. Lakini jambo la muhimu kwa Alice siyo birthday moja tu... ni wewe Casmir. Anahitaji uwepo wako karibu naye. Tafakari. Kuna mambo ni ya muhimu kutanguliza kwanza hata kama una wajibu mwingine. Familia Casmir. Familia kwanza. Hizi vita zipo tu. Kumbuka umesoma siasa na vita ili wanao wapate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa," Kendrick akatoa ushauri.

"Dah, kaka inabidi huo upuuzi wa John Adams uuweke pembeni!" Casmir akasema, nao wote wakacheka.

"Ahheheheh... jamaa alikuwa anajua anachokiongea bwana. Ila sikwambii hivi kwa kuwa labda nataka ukiache cheo chako..."

"Ahahahah... usijali naelewa. Nina mambo mengi sana ya kufanya," Casmir akasema.

"Niko pamoja nawe kamanda," Kendrick akamwambia.

Kisha wakaunganisha viganja vyao kwa nguvu kwa njia ya kirafiki, naye Kendrick akatoka hapo.

Casmir alikuwa mwanaume mtu mzima, mwenye miaka 50, mrefu na mwenye mwili mpana wa mazoezi. Alikuwa mwenye utu wa kujali na mkarimu, lakini thabiti sana aliyefuata viwango vya juu vya maadili. Alimpenda sana mke wake na watoto, na kwa kipindi kirefu alijichukia sana kwa kuwanyima muda wake mwingi kwa sababu aliutumia kuimarisha ulinzi wa mipaka ya taifa. Sasa alitakiwa kufikiria kwa kina angefanya nini ili kuirudia familia yake tena na kuepuka kuwavunja moyo.

Kendrick alikuwa mwanaume mwenye nguvu pia, mkali, imara, na mwenye akili sana. Yeye ndiye aliwapa mafunzo na kuwaongoza wanajeshi wengi katika mazoezi ya kila siku ili kuwaimarisha, na hata mara nyingine kuhakikisha vifaa vya kivita vinakuwa sehemu maalumu kwa ajili ya matumizi. Yeye pia alijuana na familia ya Casmir, akiwaona mapacha wale walipozaliwa mpaka wanakua na kucheza nao. Watoto wa Casmir walizoea kumwita "Uncle Kendrick," kwa sababu ukaribu wake kwa baba yao ulifanya ionekane kama ni ndugu yake.

Yeye Kendrick hakuwa na familia yake mwenyewe wakati huu. Kipindi cha nyuma alioa mwanamke fulani lakini akapatwa na ugonjwa uliosababisha kifo chake, hivyo Kendrick aliamua kujiunga tu na jeshi na kutojihusisha na mahusiano kwa muda mrefu sana kwa sababu alisikitishwa mno na kifo cha mke wake. Mara kwa mara ingetokea mahusiano ya "gusa nikuache" na wanawake kadhaa aliokutana nao, lakini hakuweka umakini wake wote kwa yeyote kati ya hao kwa sababu hakutaka kupenda tena kupitiliza. Labda kama ni mwanamke mmoja aliyeitwa Margaret, ndiye aliyempenda sana Kendrick kipindi fulani cha nyuma. Lakini aliondoka nchini kwenda kufanyia kazi Ghana.

Kendrick alikuwa na nyumba moja kwenye jiji lile lile ilipokuwepo familia ya Casmir pia, na hapo walikuwepo mama yake mzazi, pamoja na wadada wengine wawili ambao walikuwa ni ndugu wa kiukoo. Kwa kuwa umri wa mama yake ulikuwa umesonga, wanawake hao walikuwa pale kumsaidia wakati ambao Kendrick aliutumia kazini. Alimpenda na kumheshimu sana Casmir. Alimsikiliza kwa vitu vingi, na hata yeye pia alimshauri kwa mambo mengi kama alivyofanya wakati huu. Kendrick alikuwa na miaka 49.

Bila kuchelewa, Meja Casmir akaanza kujipanga kwa mambo ambayo angehitaji kufanya kwa ajili ya kazi mpya aliyopewa. Alianza kuangalia ni wanajeshi gani wangefaa kwa ajili ya kazi iliyohitajika kufanywa, na ni mbinu zipi wangetumia upesi ili kuhakikisha wanafanikiwa kuwafatilia na kuwakamata waasi wale. Hakuweza kujizuia kutulia kidogo na kuitafakari familia yake na yale Kendrick aliyomwambia, lakini akaendelea tu kufanya mipango ya mambo hayo aliyokabidhiwa.


★★★


UPANDE WA MAPACHA (SIKU HIYO HIYO)

Alexandra, au Sandra, alikuwa ameondoka nyumbani kwao mida ya saa 10 jioni ili kwenda kuonana na mpenzi wake, Raymond. Xander alikuwa ameondoka kabla yake kuelekea uwanjani kwa ajili ya mechi baada ya kumfikisha kwao kutokea chuoni muda mfupi nyuma. Ijapokuwa Sandra alivaa kwa njia ya kawaida tu, alipendezea sana. Alivaa T-shirt nyeupe na suruali ya jeans yenye kubana kiasi, iliyochanikia magotini kama kawaida. Kuwa mtoto wa kishua hakukumfanya ajidodeke mavitu mengi sana mwilini yasiyo na ulazima, kwa kuwa mwonekano wa kawaida ndiyo ulikuwa mtindo wake sikuzote.

Raymond aliishi mtaa mwingine jijini hapo, akiwa amepanga chumba kwenye nyumba ya kulipia. Alikuwa msafi na nadhifu sana, naye alijitahidi kuishi na wapangaji wengi wa pale kwa amani. Leo yeye ndiye alimwambia Sandra kwamba angemtoa "out" kwenye sehemu nzuri sana, hivyo binti alikuwa na hamu kubwa kwa kuwa hakuonana naye kwa siku chache za nyuma kutokana na yeye kuondoka jijini hapo. Alikuwa ndiyo amerejea sasa, na kitu cha kwanza alichotaka ilikuwa ni kumwona mpenzi wake.

Sandra alikwenda mpaka maeneo fulani ya jiji kwa kutumia usafiri. Alimkuta Raymond anasubiri sehemu waliyotumia mara nyingi kukutana, nao wakakumbatiana kwa furaha. Raymond alimzidi urefu kidogo, naye alikuwa mweusi kiasi, mwenye mwili imara wa mazoezi uliofanya T-shirt nyingi alizovalia zimbane na kuchoresha kifua chake vizuri. Hakuwa mtu mwenye makuu kabisa. Alikuwa mwelewa, mstaarabu, na mwenye heshima sana. Kipindi fulani cha nyuma kabla hajakutana tena na Sandra, aliumwa sana kwa muda mrefu, hivyo alihitaji uangalizi wa hali ya juu na mazoezi yaliyomjenga kimwili kufikia namna hii wakati huu.

Wawili hawa wakafanya matembezi kidogo huku wakifurahia maongezi, na baada ya dakika kadhaa Raymond akamwomba Sandra waelekee kule alipokuwa ameandaa "kiburudisho" chao. Baada ya kufika, Sandra akashangaa kujua kwamba ilikuwa ni kwenye hoteli moja kubwa sana na ya kifahari jijini hapo. Raymond alimwambia alitaka kumfanya ashangae namna hiyo, lakini uhondo haukuishia hapo. Uhondo ulikuwa kule ndani. Wakaelekea ndani ya hoteli hiyo mpaka kwenye chumba kimoja juu kwenye ghorofa ya 7, ambacho Raymond alikuwa ameshalipia.

Walipoingia, Sandra aliachia tabasamu baada ya kukuta meza iliyowekewa viti viwili kwa pande zake, huku katikati kukiwa na vyakula na vileo (wine) kwenye glasi. Chumba kilikuwa kipana, chenye masofa, kitanda kikubwa upande wa pili, choo na bafu la kisasa, vifaa vya kuwekea vinywaji na kuingiza hewa safi chumbani, na TV kubwa ukutani. Alistaajabu sana kwa kuwa alijua gharama ya hapa ilikuwa ni kubwa sana. Alijua pia kwa Raymond haingekuwa rahisi kugharamia sehemu hii, labda kama angekuwa ameanza kazi au amekopa pesa sehemu. Mara zote walizotoka kipindi cha nyuma, ilikuwa ni kufanya mambo yenye kufurahisha kwenye sehemu za kawaida tu, na alipenda sana mambo "simple." Hivyo jambo hili kutoka kwa Raymond lilikuwa jipya kwake.

Akamgeukia na kumuuliza, "What is all this?"

"Ni... zawadi ndogo tu... yaani... outing ndogo nilipanga nikufanyie. Umeipenda?" Raymond akasema.

"Lakini Raymond, nilishakwambia kwamba mimi sijali sana vitu fancy. Nafurahia zaidi unapokuwa unanitendea kwa njia yako... kawaida tu," akasema Sandra.

"Ndiyo najua. Lakini leo nilitaka kujaribu hivi pia. Wewe ni malkia kwo' lazima utendewe kama malkia kweli," Raymond akasema.

"Ray..."

"Nmekumiss sana yaani. Nikafikiria niweke na njonjo kidogo kwa leo. Ila kama hujapenda hii, basi..."

"No, siyo kama sijapenda. Nimeshangaa tu. Umemfungia nani ndiyo ukamwibia chumba chake?"

"Ahahahah... najijua me masikini sana kwa hiyo sehemu kama hizi hautegemei nitakupeleka..."

"Ahahah... sijamaanisha hivyo..."

"I know love... natania tu. Nime... nimeachiwa sehemu fulani ya urithi na babu yangu," akasema Raymond.

"Babu yako? Si ndiyo huyo uliyekuwa umeenda kumwona?"

"Ndiyo. Amekufa hiyo juzi..."

"Ooh, pole sana Ray. Pole."

"Usiwaze..."

"Ila, si alikuwa mzima... ndiyo ulienda kumsalimu?"

"Ndiyo. Alituita mimi na mama yangu kwa sababu alikuwa anaumwa sana. Ndiyo zilikuwa dakika za mwisho..."

"Jamani Raymond, mbona hata hukuniambia?"

"Naah, mzee mwenyewe hakutaka wengi wajue kwamba alikuwa anakwenda..."

"Acha utani huo Raymond..."

"Ahah... well, sisi wenyewe hatukutarajia. Hakuwahi kuweka ukaribu wowote na sisi, lakini mwishoni ndiyo akaweka wazi kwamba anampenda sana mama na mimi. Mali zake amejitahidi kuzigawa kwa wanae wengi na mama, na mimi pia akanipa chenji kidogo. Ndiyo maana unaona nimekuja na mng'ao mpya," Raymond akasema.

"Ahahahah... samahani, sidhani kama ni sahihi kucheka kwa hilo..." Sandra akamwambia.

"Usihofu. I want us to enjoy this moment," Raymond akamwambia huku akiweka mikono yake kiunoni kwa Sandra.

"Me too. I really missed you," Sandra akamwambia huku naye akizungushia mikono yake kichwani kwa Raymond.

Wawili hawa wakaanza kupeana busu ya upendo. Sikuzote kilichomfurahisha Alexandra kuhusu Raymond ni kwamba alikuwa na mapenzi yasiyotaka papara. Alipeleka mambo taratibu na kistaarabu, hivyo alimpa binti muda mwingi wa kufurahia kile alichompatia. Busu hii ikawa denda kadiri walivyoendelea, na sasa mifyonzo ya midomo yao ikawa inasikika vyema. Kisha, taratibu Raymond akajitoa mdomoni mwake. Sandra akawa anamwangalia kwa hamu.

"Plan A ilikuwa... tuje, niwashe muziki wa soul kidogo, tukae kwenye hiyo romantic dinner table; kuna msosi wa ukweli hapo..."

Raymond akawa anasema na kumfanya Sandra acheke kidogo.

"Lakini kufikia hapa nadhani tukianza na plan B ndiyo itafaa zaidi, au siyo?" Raymond akauliza.

"Na hiyo plan B ndiyo ipi?" Sandra akauliza huku anatabasamu.

"Wacha nikuonyeshe..."

Raymond akasema hivyo na kuirudia midomo ya binti tena. Walipiga busu kwa huba nzito sana, huku Raymond akitembea taratibu pamoja naye kuelekea upande uliokuwa na kitanda. Jinsi Raymond alivyotembeza viganja vyake kwenye mwili wa Sandra, ilimpa binti hisia nyingi nzuri ajabu. Alihisi ni kama mtikisiko mkubwa wa ardhi unautetemesha mwili wake kwa jinsi alivyosisimka, kwa kuwa Raymond alifanya mambo kwa njia yenye ufundi sana; hapo bado hajamvua nguo. Na hili ndiyo lililompa mrembo hamu ya kutaka mengi zaidi.

Wakiendelea na mahaba yao ya kuvuruga kitanda, ilifikia hatua Sandra akawa anamwomba jamaa aongeze kasi na nguvu zaidi. Raymond akatii na kuushika mkono wake mmoja. Sandra alihisi kama anataka kupasuka, huku mara kwa mara Raymond akiuliza ikiwa alitakiwa kuacha, lakini binti akaomba aendelee tu kwa mtindo huo huo. Alikunwa kwa nguvu mpaka alipoanza kuhisi kitu ndani yake kikimtetemesha kwa nguvu ndani ya mwili wake wote, naye akapiga kelele zaidi na kuanza kutetemeka mapaja kwa nguvu.

Raymond akajitoa kwa binti na kumshikilia Sandra tumboni alipokuwa anaendelea kushtuka-shtuka kwa nguvu sana. Akawa anatoa miguno iliyoenda sambamba na kila mshtuko uliotokea kiunoni kwake, huku akiwa amekilaza kichwa chake kitandani kilegevu. Jasho lilimjaa Raymond mwilini, huku jasho la mwili wa Sandra likionekana kiasi na kufanya kama kuing'arisha ngozi yake.

Kisha binti akajilegeza na kujilaza chali kitandani, akiwa amefumba macho huku ameweka mkono wake mmoja juu ya kichwa. Raymond alimwangalia kimaswali sana. Hakujua ni nini kilikuwa kimempata mpenzi wake ghafla.



★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!


★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA NNE

★★★★★★★★★★★★★


Raymond akalala pembeni ya mpenzi wake akiwa bado anajiuliza alipatwa na nini. Sikuzote Alexandra alipenda kupewa mapenzi kwa njia ya kistaarabu, kwa hiyo jambo hilo lililotokea lilikuwa jipya kwake. Akashika tumbo lake taratibu, naye Sandra akashtuka kidogo na kumtazama usoni. Raymond akawa anamwangalia kwa kujali sana, naye Sandra akamsogelea mdomoni na kumbusu kidogo. Kisha akajilaza kifuani kwake na kutembeza kiganja chake kwenye mwili wa Raymond, naye jamaa akawa anafanya hivyo hivyo pia.

"My... uko sawa?" Raymond akauliza kwa sauti ya chini.

"Yeah. Asante Ray," akasema Sandra.

"Unajua... nahisi labda nisingefata ulivyoniambia..."

"Kwa nini?"

"Nilikuwa nahofia nakuumiza, lakini wewe ukataka niendelee tu..."

"Hapana haujaniumiza..."

"Usinidanganye Alexandra. Najua ulikuwa unaumia. Lakini... nahitaji uniambie ni kwa nini ulikuwa unataka kuumia..." akasema Raymond.

Sandra akabaki kimya.

"Kuna tatizo. I know you. Pamoja na kwamba una umri mdogo lakini mambo mengi huwa unayafanya kwa njia mature sana. Sikuzote. Ila leo, umenifanya nihisi ni kama vile ulihitaji nikuadhibu... na sijui sababu ni nini. Tafadhali niambie..." Raymond akamwomba.

Sandra akaanza kulia kwa sauti ya chini. Raymond akawa anamfuta machozi kwa upendo.

"Shida ni nini mpenzi wangu?" Raymond akauliza.

"I'm sorry. Nimekuwa... nimekuwa tu na wakati mgumu kihisia," akasema Sandra.

"Nini kimetokea? You know unaweza kuniambia lolote..."

"Hakuna kitu wala. Labda... labda ni mimi ndiyo najiendekeza tu..."

"Kwa nini unafikiri hivyo?"

"Kwa muda mrefu sasa... nimejitahidi sana kuonyesha kwamba namwelewa baba yangu. Hata nimemtetea mara kwa mara kwa wengine... hasa Xander. Ila sasa hivi sijui tu Ray yaani... nahisi kama vile... ndani yangu... kuna sehemu inayotaka kunisukuma...." akaishia hapo.

"Kumchukia?" Raymond akauliza.

"Haionekani kuwa fair. I mean... kuna watoto wengine wengi ambao hawapati kuwa hata na wazazi wote kama sisi, kwa hiyo ninapaswa kuwa na shukrani, si ndiyo? Yaani, kwa nini baba kuwa mbali inanifanya.... yaani aah..."

"Basi Alexandra... basi," Raymond akambembeleza.

"Aisee! Yaani ni kama sijitambui tena, huwa siko hivi. Ila zamu hii suala hili limekuwa zito sana kwangu. Nimejitahidi kuonyesha niko sawa lakini kiukweli naumia sana," akasema Sandra huku akilia.

"Pole Alexandra. Najua siyo rahisi, hasa kwa sababu hata mimi ninaweza kuelewa inavyokuwa kwa kuwa baba yangu alinitelekeza nikiwa mdogo. Siujui sana upendo wa baba, ila kwa sababu wewe umeujua... naweza kusema anawaonea kwa kadiri kubwa..." Raymond akamwambia.

"Umeona eeh?" Sandra akaongezea.

"Ndiyo. Hafanyi vizuri kukaa mbali kisa kazi..."

"Huwa natamani sana kufanya kitu kubadili haya yote lakini nashindwa. Baba anafanya ionekane kama hatujali, lakini najua anatupenda. Sasa tatizo sisi kwa jinsi tulivyolelewa... inakuwa ngumu sana kuacha kufikiria ni mambo gani yanayomzuia kuwa pamoja na sisi... mwisho wa siku... aah am sorry Ray... nisamehe..."

"No usijali. Naelewa..."

"Hapana... hii ilitakiwa kuwa siku nzuri kwetu, hatujaonana kwa muda sasa, halafu mimi nimeharibu..."

"Ahahahah... umeharibu kwa kunipa penzi la kibabe ambalo sijawahi kupewa maishani mwangu?

Sandra akacheka kidogo.

"Hapana Alexandra, nakuelewa. Nimesema kwamba baba yenu hawafanyii fair... hilo ni kweli. Ila... nafikiri najua kwa nini anashindwa ku-rectify mambo haraka..." Raymond akasema.

"Why?"

"Nafikiri baba yako anaogopa. Anaogopa kwamba... atakuja, mtafurahi, then atapaswa kuondoka tena. Anatafuta njia ya kurudi kwa mtindo utakaoonekana kuwa wa moja kwa moja, lakini anaikosa. Na inaonekana anaipenda kazi yake pia, sasa... ukichanganya na upendo alionao kwenu na majukumu yake... hiyo njia haiwi rahisi kuonekana..." Raymond akasema kwa busara.

Sandra akayatilia maanani maneno yake.

"Kwa hiyo usijichukie kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wako. Yeye ni mtu mzima, anapaswa kujua lililo sahihi kufanya au kuacha, na kuchukua hatua anayoona itafaa. Wewe tu... mpende. Mwonyeshe kwamba mnampenda sana. I think kila kitu kitajipa..." Raymond akasema.

"Asante Ray. Nilihitaji sana maneno yako mazuri. Unajua kunifanya nihisi vizuri. Sijui hata nilikutoa wapi..." akasema Sandra.

"Ahahah... me mwenyewe huwa nikikaa nawazaga hivi nilifanyaje kweli mpaka nikabarikiwa kukupata..."

Sandra akaulalia mwili wa Raymond kwa juu na kumbusu mdomoni. Wakaendelea na denda hii, kisha Raymond akauliza, "Vipi kuhusu hiyo dinner?"

"Achana nayo. Me nataka tuendelee na hii tamu zaidi..." akajibu Sandra.

"Hapo umeongea!" Raymond akasema kwa furaha.

Wawili hawa wakaanzisha tena penzi lao hapo kitandani, na zamu hii Sandra akajitahidi kuongoza mambo vizuri zaidi. Baada ya muda, kasi na ufundi kutoka kwao wote vikaongezwa, na mahaba yao yakaendelea mpaka usiku ulipoingia.


★★★


Ilifika mida ya saa mbili usiku; siku hiyo hiyo. Xander alikuwa ametoka kwenye mechi muda mfupi nyuma, akiwa na furaha baada ya upande aliochezea, yaani timu yao ya chuo, kufunga magoli manne kwa sifuri dhidi ya timu pinzani. Alichangia goli moja pia kwenye mchezo huu, na sasa alikuwa pamoja na Ramla baada ya kujisafisha vizuri na kuondoka kutoka huko uwanjani. Ramla alikuwa amemsisitizia amtoe "out" ili ajisikie vizuri kwa sababu alihitaji sana kuwa karibu naye.

Ramla aliishi kwenye mabweni (hostel) ya chuo, na walikuwa na sheria iliyowapaswa wanachuo walioishi hostel kuwa ndani kabla ya mida ya saa 4 kamili usiku, la sivyo geti lingefungwa nao wangepewa aina fulani za adhabu kwa sababu ingeonwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Kwa hiyo Xander akaamua kumridhisha mtoto.

Kihalisi Ramla alikuwa anataka sana kupeana mahaba na Xander siku hii, lakini jamaa akamwambia muda uligoma kwa kuwa Ramla alihitaji kufika hostel mapema. Hii ilikuwa ni kwa sababu alijua kama angefanya naye mapenzi basi angetumia muda mwingi sana, na hivyo angemchelewesha binti. Kwa hiyo kumtoa out ikawa suluhusho kwa leo, halafu hilo lingine akamwahidi kumpa kesho. Alimpeleka kwenye sehemu nzuri sana ya starehe, kama mgahawa, nao wakapata chakula kizuri hapo kama wapendanao wafanyavyo. Binti alipenda sana mambo haya hasa kwa kuwa alijua pesa kwa Xander haikuwa changamoto.

Wakawa wanafurahia na maongezi huku wanashushia na vinywaji. Baada ya dakika kadhaa, Alice akampigia simu Xander kumuuliza alikuwa wapi, naye akamjulisha kwamba alitoka na rafiki kujipongeza baada ya kumaliza mechi kwa ushindi. Akamwambia mama yake wasimsubiri kwa ajili ya chakula, kwa kuwa yeye angefika nyumbani akiwa ameshiba. Alice alizoea kula na wanae wote mara nyingi, ndiyo maana alitaka kujua ikiwa angewahi au kuchelewa. Wakaagana, kisha Xander akamwambia Ramla ajiweke tayari ili amrudishe chuoni.

Baada ya kunyanyuka ili waelekee nje, Xander alitazama upande mwingine wa sehemu hiyo na kumwona madam Valentina akiwa ameketi, kwenye meza moja akiwa peke yake, na kwa haraka akakumbuka alichokifanya kuhusiana na kazi aliyompatia. Akatabasamu kidogo, na ndipo hapo Ramla akamshika mkono ili waondoke. Yeye Ramla hakuwa amemwona, lakini Xander kumwona kulimfanya akumbuke mambo aliyoandika kumhusu, na ukweli wa kwamba ni kama leo hakumwona kabisa chuoni.

Walipanda kwenye pikipiki na mpenzi wake, kisha akaanza kumrejesha chuoni. Alisimulia story za kumchekesha sana Ramla, mpaka wanafika kule, binti alikuwa amechangamka mno. Wakati akishuka na kumuaga mpenzi wake, Ramla akampa denda nzuri sana kumwonyesha jinsi alivyompenda, kisha akaelekea kule ndani. Xander alimfurahia Ramla, na alithamini jinsi ambavyo binti alionyesha upendo mwingi kwake ijapokuwa mara kwa mara na yeye alikuwa mwenye kuudhi. Akageuza pikipiki yake na kuanza kuelekea nyumbani.

Alipokuwa bado barabarani kuelekea huko, aliipita tena sehemu ile waliyotoka na Ramla muda mfupi uliopita, naye akakumbuka kwamba alimwona madam wake akiwa hapo. Akaingiwa na hisia fulani ya kutaka kumwona na hata kuongea naye kuhusiana na kazi aliyoifanya, ili ajue alihisije. Hakuwa mwoga hata kidogo kwenye mambo kama haya. Akaiegesha pikipiki nje na kurudi tena pale ndani, akifurahi kuona kwamba bado madam alikuwepo.

Alifika usawa wa meza yake na kusimama hapo, akikuta kuna glass ya wine mezani na nyama choma zilizotengenezwa vizuri sana kwa kuwekewa "roast" pia. Akajifanya kama anakohoa ili auteke umakini wa mwanamke huyu, ambaye alikuwa amezama kusoma jambo fulani kwenye simu yake, naye akanyanyua uso wake na kumtazama mkohoaji.


"Hey... madam Valentina... niaje?" Xander akamsalimu.

"Safi," Valentina akajibu kibaridi.

"Naweza kujiunga nawe? Au kuna mtu unamsubiri?" Xander akauliza.

"Hapana. Hakuna mtu namsubiri. Nilifikiri labda unajua hilo tayari maana unafahamu mengi kuhusu maisha ya watu," Valentina akasema bila kumwangalia.

"Ohohooo... there it is. Nilitarajia bango. Bila shaka umenizungushia yai la adabu kwenye paper..."

Valentina akamwangalia na kutabasamu kidogo, kisha akasema, "Hapana. Umeistahili A wakati huu."

"Kweli?"

"Yeah."

"Okay... asante kwa A. Sasa hivi kweli umenitendea haki," akasema Xander.

"Sawa. Hongera. Unaandika vizuri sana," akasema Valentina na kunywa wine yake.

Xander akatambua kwamba hakuwa sawa.

"Una hasira na mimi?" akamuuliza.

"Kwa nini niwe na hasira na wewe?"

"Well... haujasema lolote kuhusu nilichoandika. Na hapa umekaa unaniambia tu hongera huku unapiga booze... sihitaji kuhofia kujikuta mtoni bila nguo asubuhi?" Xander akasema kiutani.

Valentina akashindwa kujizuia kucheka.

"Hapana sijakukasirikia. Kazi yako ilinishangaza, lakini nimekuwekea A kwa sababu umeiandika vizuri na kwa usahihi..."

"Lakini..."

"Lakini sijapendezwa nayo kwa kweli. Ilinifanya nihisi kama vile nachokonolewa sehemu nisiyotaka ichokonolewe," Valentina akafunguka.

"Sehemu gani hiyo?" Xander akasema kwa sauti ya chini kimasihara.

"Nini?"

"Namaanisha... samahani kwa kukufanya uhisi hivyo. Ila ulisema niandike kitu kwa passion kubwa. Mimi ndiyo nilichokifanya," Xander akamwambia.

"Tokea lini ulianza kuwa passionate kwangu mimi Xander?"

"Tokea... nilipoona jinsi unavyopendeza ukitabasamu," Xander akaongea kwa sauti yenye hisia.

Valentina akamwangalia kidogo, kisha akapiga ulimi wake kwa njia ya kusikitika na kutikisa kichwa.

"Ulitolea wapi mambo yale yote?" Valentina akauliza.

"Mimi ni mwana-IT... tuna njia zetu," Xander akasema.

"Kwa hiyo unataka kuniambia vitu vyote kuhusu maisha yangu vipo kwenye intaneti?"

"Ahahah... hapana. Kiukweli mimi nina njia yangu tu ya ku-hack kwenye maisha ya mtu nikiamua. Ni kipaji tokea udogoni."

"Kuna watu hawapendi, na wanaweza hata wakakuchukulia hatua ukijulikana..."

"Najua. Lakini si unaona bado niko hapa? Sijachukuliwa hatua. Hiyo ni kwa sababu sifanyagi hivyo ovyo ovyo, na niko makini..."

Valentina akanywa kinywaji chake kidogo tena.

"Usi-mind sana madam. Nitajitahidi kuandika kilicho bora zaidi wakati mwingine, ili nistahili marks za juu zaidi," Xander akasema.

"Alama za juu kuipita A? Ni zipi hizo?"

"Uuuh... madam nilifikiri wine imekukolea, kumbe kichwa chako bado kizima!"

"Sijakasirika Xander. Nime... niliaibika tu kusema kweli. Sikufikiria kuna mtu angewahi kuyaandika maisha yangu namna hiyo," akasema Valentina kwa hisia.

Xander akamsogelea karibu zaidi. Valentina akamwangalia kimshangao kiasi.

"Usione aibu. Story yako inagusa sana. Ni inspiration kubwa kwangu, hilo sitakudanganya. Any time ukijihisi kuwa down, just remember kuna kijana mmoja anayekukubali sana... na huyo ni Xander," akamwambia kwa ustaarabu.

Nyuso zao zilikuwa zimekaribiana sana, naye Valentina akawa anaona ni kama anaongea na mtu fulani aliyezijua hisia zake vizuri sana. Akatambua kuwa Xander alikuwa kijana jasiri na aliyejua kujieleza sana. Akashindwa hata aseme nini na kubaki amemwangalia tu, kisha Xander akarudi nyuma kidogo na kumwambia angeondoka sasa, hivyo wangeonana kesho yake. Akamwacha madam wake akifikiria kuhusu alichomwambia, naye akaingia barabarani kurudi nyumbani.


★★★


Sandra anafika kwao kwenye mida ya saa tatu na nusu usiku baada ya kutumia muda pamoja na mpenzi wake kule hotelini. Anawakuta mama yake, Azra, pamoja na Salome wakiwa pamoja wanaangalia TV. Anawasalimu na kuelekea chumbani kwake kubadili mavazi, kwa kuwa alioga pamoja na Raymond kule kule hotelini, hivyo hahitaji kurudia hilo tena. Akatoka chumbani kwake baada ya muda mfupi ili kwenda kukaa na wengine huko chini.

Mama yao hakuwa na shida yoyote ile watoto wake hawa kuja nyumbani usiku, isipokuwa kama hawakutoa taarifa. Sandra alikuwa ameshamwambia mapema mama yake kuwa angeenda kutembea na rafiki, hivyo uwezekano wa kuchelewa ulikuwepo. Na tena siyo kwamba labda saa tatu ni kuchelewa sana, sema kwa familia hii iliyokuwa na baba mjeshi, sheria-sheria nyingi zilikuwepo, ijapokuwa hazikuwabana sana. Wengine walikuwa wakitazama kipindi cha kiingereza chenye kuchekesha kwenye chaneli pendwa ya Azra; Nickelodeon.

"Ulienda kutembelea wapi?" Alice akamuuliza Sandra.

"Town tu. Nimeenda na rafiki yangu CBD," akasema Sandra.

"CBD? Mlienda kufanya nini kwenye hiyo hoteli?" Alice akamuuliza kiudadisi.

"Kujifurahisha tu," akajibu.

"Gharama ya hapo najua ni kubwa..." Alice akasema.

"Yeah. Rafiki yangu ana tuhela-hela kwa hiyo haikuwa na noma," akasema Sandra kwa njia ya kificho.

"Huyo rafiki yako ni nani?" Alice akamuuliza.

"Nitakuja naye siku moja umwone," Sandra akasema huku anaibana midomo yake kiutundu.

Alice akamtazama kwa macho ya kudadisi, naye Sandra akachekea kwa chini.

"Azra... nani huyo?" akauliza Sandra.

"Yupi?" Azra akauliza.

"Huy... huyo... mwenye nywele nyeupe," akamwonyesha.

"Anaitwa Kendall. Hao wengine ni marafiki zake... wanaimbaga naye," akasema Azra.

"Aaaa... sawa," akasema Sandra.

"Azra anawapenda! Yaani lazima awaangalie kila siku," akasema Salome.

Ni wakati huu wote wakasikia geti la nje likifunguliwa, na pikipiki ikaonekana inaingia.

"Xander huyo," akasema Azra.

"Mbona umemuuliza Azra huyo ni nani?" Alice akamuuliza Sandra.

"Nimemuona siku fulani nyuma kwenye mtandao... sijui kwenye simu ya mtu... kama vile ameimba na Snoop Dogg..." Sandra akataarifu.

"Eee wameimba wote! Wote yeye na kundi lake hawa Big Time Rush wameimba na Snoop Dogg... remix wimbo wa Boyfriend," Azra akasema kwa shauku.

"Hee! Unawajua hivyo?" Alice akamuuliza.

"Wote! Huyo hapo James... Kendall... Logan... na Carlos. Nampenda zaidi James..." Azra akasema.

"Kwa sababu ni handsome kuliko wote kama sikosei?" akasema Sandra.

"Man of my dreams!" Azra akasema akijishika moyoni.

Wote wakacheka kidogo.

"Siyo hata mzuri sana," akasema Salome.

"Eeeh kwanza pua yake imekaaje sijui... ki-flamingo flamingo yaani..." Sandra akawa anatania.

"Acheni wivu nyie. Hata mseme nini nimeshakufa na kuoza," Azra akasema kwa uhakika.

Wanawake wote wakacheka kwa sauti sana. Xander akawa ameingia hapo na kuwafuata wote. Azra akanyanyuka na kumkimbilia ili amkumbatie.

"Xander!" akasema kwa shauku.

"Azra... naona mnaangalia BTR," Xander akasema.

"Umeniletea?" Azra akamuuliza kwa njia ya deko.

"Pff... nisahau tena? Chukua mtoto mzuri," akasema Xander huku anampatia boksi la chocolate.

Azra akafurahi na kumshukuru, kisha akarudi kukaa kwenye sofa ili aanze kula.

"Za mechi dork?" Sandra akamuuliza.

"Nne mtungi! Dadeki! Achana na sisi kabisa," Xander akajisifu.

"Mbona haunuki jasho, nani amekuogesha?" Sandra akamuuliza kiutani.

"Bomba la mvua," akajibu Xander.

Sandra akatabasamu.

"Nafurahi kujua kwamba leo mlitoka kujifurahisha ila mnapaswa kuwa makini sana sasa hivi. Matukio mengi yanayotokea ni mabaya, anytime, anyplace..." Alice akawaambia mapacha.

"Unaongelea kuhusu Demba Group?" Sandra akauliza.

"Ndiyo," akasema Alice.

"Heee! Hao jamaa ni hatari. Wanapiga watu risasi ovyo. Yaani eti watu 28 wamekufa leo. Watu hao siyo kuku!" akasema Azra.

"Oh, nakuhakikishia mdogo wangu, walikuwa 60. Ila taarifa za habari kwa kufinya mambo hazijambo," Xander akasema kimasihara.

"Mm... hamna bwana..." Azra na Salome wakakataa.

"Anatania tu. Mmeiona ile video?" Sandra akauliza.

"Nimeiona. Hawamtaki Raisi eti. Hawa watu wanatoka hapa, wanakwenda pale, muda wowote, sehemu yoyote... ni hatari sana," Alice akasema.

"Lakini Raisi ametangaza kwenye habari kwamba watawakamata ndani ya siku chache. Ameyasema yote kwa uhakika kweli, kwa hiyo ngoja tuone," akasema Salome.

"Ndiyo... tutaona," akasema Alice.

"Itakuwa vizuri wakitangaza vyuo kufungwa tupumzike kidogo," akasema Xander.

"Hiyo haitasaidia. Inabidi tu wawakamate haraka maana tumeshaanza kuingiwa na wasiwasi na hofu kubwa mno," Alice akasema kwa uzito.

"Mambo yamezidi kuchacha. Lakini kama ni njia ya kuweka kisingizio kipya cha kukosa mambo ya muhimu... hii itakuwa happy hour kwake," Xander akasema.

Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake.

Alice na Sandra waliangaliana kwa sekunde kadhaa, wakiwa wameelewa alichosema Xander kwa njia ya fumbo. Alikuwa anamaanisha baba yake. Kwamba kwa sababu ya matukio haya yenye kushtua yaliyokuwa yameanza kutokea, ingekuwa ni sababu nyingine mpya ya kisingizio kwa Casmir kutoweza kujiunga nao kama familia; hasa kwa pindi muhimu za sherehe ya Alice na shindano la kuogelea la Alexandra.

Wanawake hawa wawili hawakuweza kuzizuia hisia za kuvunjwa moyo kwa sababu walijua kuna ukweli kwenye maneno ya Alexander. Lakini wakajitahidi tu kuliweka hilo pembeni na kuendelea kuwa na imani.


★★★


Siku iliyofuata, mapacha wakawa wamefika chuoni kama kawaida. Sasa ilikuwa ni asubuhi ya saa 3 kwenye kipindi cha somo la Communication. CR wa madam Valentina alikuwa akizigawa karatasi za kazi aliyokuwa amewapatia kufanya juzi. Madam Valentina alikuwepo pia, akiwaelezea kwamba wengi walijitahidi na walihitaji kuongeza bidii katika suala hilo la uandishi mzuri. Alisifia zaidi kazi ya Benjamin, dada mwingine aliyeitwa Salima, na Alexandra pia, akisema waliandika kwa mtiririko mzuri sana unaostahili pongezi kubwa.

Xander alikuwa akimtazama kwa makini madam Valentina karibia muda wote. Mwalimu huyu hakuweza kujizuia kumwangalia Xander mara kwa mara na kukuta akimtazama sana, naye angekwepesha macho yake na kukazana kuwafundisha wanachuo humo darasani. Njia ya Valentina ya kumwangalia Xander ilikuwa yenye mkazo sana, kama hakutaka masihara kabisa, naye Xander alijua hiyo ni kutokana na yeye kuandika vitu vya maisha ya mwalimu huyo bila idhini yake.

Baada ya kipindi kumalizika, wanachuo wakatawanyika kila mtu kwenda mahali alikojua yeye mpaka wakati mwingine wa vipindi siku hiyo. Ramla akamwambia Xander kupitia ujumbe kuwa alihitaji sana kuwa naye leo ili wapeane mapenzi motomoto. Alikuwa anasisitiza waondoke hapo haraka kwenda hoteli yoyote ile maadamu tu alipate penzi la Xander haraka, kwa kuwa hamu ilimzidia na ilikuwa inakaribia kuisha wiki nzima tokea walipofanya mara ya mwisho.

Xander akamwambia alipaswa kuwa na subira kidogo kwa kuwa bado alihitajika chuoni, lakini Ramla akawa analazimisha waondoke la sivyo angejisikia vibaya. Jamaa akajitahidi kueleza kwamba pindi tu ambapo vipindi vingekwisha ndiyo angekwenda pamoja naye, tena sehemu nzuri sana, lakini Ramla akaacha kutuma tena sms kwa kuudhika. Yeye pia alikuwa na hamu ya kutoka na Ramla, lakini alijua kuna mambo mengine yalihitajika kufanywa kwanza, hivyo akambembeleza (kupitia ujumbe) kuwa angempa raha nyingi leo baada ya kutoka hapo chuo.



Basi, baada ya hapo Xander akawa pamoja na rafiki zake sehemu fulani za nje ya chuo wakipiga story zenye kufurahisha. Alikuwa na rafiki yake mwingine aliyeitwa Lucas, naye akiwa pamoja nao. Lucas alitambua kwamba yule "dogo," yaani Isiminzile, alikuwa amekaa sehemu fulani peke yake huku akiwaangalia sana. Akamtania Mecky kwamba dogo alikuwa anataka kuziruka naye bado kama njia ya kisasi, lakini Mecky akampuuzia tu na kuendelea na mambo yao hapo. Hazikupita dakika nyingi nao wadada wazuri Alexandra na Sophia wakawa wamefika sehemu hiyo.

Kama kawaida ya vijana wa kiume, walianza kuwasifia sana, lakini Xander akatambua kwamba kuna jambo halikuwa sawa. Sophia alionekana kama alikuwa analia, lakini akasema tu kuwa macho yalimuuma tokea alipoamka. Sandra akamwomba Xander waende pembeni ili waongee kidogo, naye akakubali upesi na kwenda pamoja nao mpaka usawa wa mti fulani mkubwa. Sophia akawa kama anamzuia Sandra asimwambie Xander jambo fulani, lakini Sandra akamwambia asijali kwa kuwa angeweza kumwamini Xander. Xander naye bila hata kujua shida ilikuwa nini, akasisitiza wamwambie tu ili aweze kusaidia.

Sandra akamwomba Xander amsaidie Sophia kwa kiasi fulani cha pesa kwa kuwa mama yake aliumwa sana kule mkoani kwao Singida, na alilazwa hospitalini tokea jana. Sophia alikuwa amepokea taarifa hizo muda mfupi nyuma, na zilikuwa taarifa nzito kwa sababu mama yake alihitaji tiba fulani haraka sana la sivyo... angekufa. Muda haungekuwa rafiki kwao, na kiwango cha pesa kilikuwa kikubwa sana. Baadhi ya ndugu zake waliokuwa huko walikuwa wanajichanga, lakini Sophia pia alihitaji kusaidia ijapokuwa hakuwa akifanya kazi.

Sandra yeye alikuwa ametumia sehemu kubwa ya pesa zake wiki chache nyuma, na mama yao hakuwa bado amemwekea kwenye akaunti yake. Kiasi alichoweza kutoa haraka wakati huu kilikuwa ni shilingi laki moja na nusu, lakini alihitaji Xander asaidie pia ili kiongezeke.

Xander akamuuliza gharama yote ya matibabu ya mama yake ilikuwa shilingi ngapi, naye Sophia akasema kwenye laki nne. Hapo Xander akamwambia asiwaze kwa kusema kiutani kuwa alikuwa amebakiza chenji ambayo ingetosha. Lakini angehitaji kwenda kutoa kiasi cha laki tatu ATM, hivyo amsubiri hapo ili yeye aende maeneo ya mjini kumtolea na kumletea. Lakini Sandra akafikiria hivi; kwa nini wasiende pamoja huko ili aweze kuunganisha na laki moja aliyompa Sophia na kuituma pesa yote moja kwa moja? Akamwambia Sophia awataarifu ndugu zake kwamba angetuma pesa hiyo, hivyo wajiandae kuipokea na kuanza taratibu za kumtibu mama yake.

Lilikuwa ni wazo zuri, na kwa kuwa bado walikuwa na kama saa moja hivi kabla ya kipindi kingine kufuata, Xander akamwambia Sophia waondoke haraka kwenye pikipiki yake ili kwenda kukamilisha zoezi hilo. Sophia akawashukuru sana mapacha hawa kwa ukarimu wao na hata kuahidi angewalipa, naye Xander akamtania kwa kusema ole wake aache. Sophia akawa anatoa machozi ya furaha, naye Sandra akamkumbatia.

Kisha Xander na Sophia wakaondoka ili kuifata pikipiki ya jamaa. Xander alimshika mkono wake na kutembea naye kwa ukaribu kama kumpa kitulizo cha kirafiki, huku akijaribu kumwambia mambo yenye kumfurahisha. Wakaifikia pikipiki na kupanda, Sophia akiwa nyuma ya jamaa huku amezungushia mikono yake kiunoni kwake, kisha Xander akaiondoa pikipiki hapo kuelekea katikati ya jiji.

Hawakuwa wametambua kwamba kuanzia walipoanza kutembea pamoja mpaka kupanda pikipiki na kuondoka, Ramla alikuwa akiwatazama.


★★★


Xander na Sophia walikamilisha kutuma kiasi cha laki nne na nusu kwa familia ya binti. Xander alimpatia Sophia laki moja ya matumizi yake mwenyewe, huku dada huyo akishangaa alikuwa akitoa wapi pesa zote wakati hakufanya kazi. Ndiyo hapo Xander alimwelezea kwamba wazazi wake yeye na Sandra walikuwa na kawaida ya kuwawekea pesa kwenye akaunti zao kila mwezi; hasa mama yao.

Jambo hili la kuwekewa pesa lilianza zamani sana tokea wakiwa sekondari, hivyo mara nyingi walikuwa wanakuta pesa zimeshaongezwa tu bila kuambiwa lolote. Lakini Xander hakuwa na matumizi mengi sana ya pesa, kwa hiyo kwenye akaunti yake zilikuwemo nyingi. Sophia akaweka wazi kwamba alipenda sana aina yao ya maisha na kutamani angewahi kuishi namna hiyo, hivyo Xander akamtania kwamba asiwaze kwa sababu angemwoa wakimaliza chuo.

Kabla ya kurudi naye chuo baada ya kutoka benki, Xander akaamua kumpitisha Sophia kwenye mgahawa mzuri ili wapate chai nzuri ya haraka. Alitaka sana kumfanya rafiki ya dada yake ajisikie vizuri, na mambo haya yalimtia sana moyo Sophia. Akapendezwa hata zaidi na Xander sasa kuliko ilivyokuwa mwanzoni, kwa sababu kipindi cha nyuma alimwona kama mtu asiyejali sana. Walipomaliza mlo wao mfupi, wakarudi chuoni hatimaye.



Vipindi vichache vilivyofuata viliisha saa 9 alasiri. Marafiki wa Xander walikuwa wanamshawishi kwenda pamoja naye sehemu fulani yenye fukwe ya starehe (beach) ili kujifurahisha, lakini yeye akasema alikuwa na mipango mingine kwa siku hiyo, hivyo angejiunga nao wakati mwingine. Mipango aliyosemea ilikuwa ni kumtoa "out" Ramla ili baada ya hapo atimize ahadi yake ya kupeana naye mahaba aliyokuwa anayalilia sana. Lakini kwa sababu asizozijua, Ramla hakuwa akijibu SMS wala kupokea simu yake alipompigia.

Xander akawaza labda bado alikuwa amenuna, na alijua njia rahisi ya kusuluhisha hili ilikuwa ni kumbembeleza kwa maneno mazuri, hivyo hakukata tamaa kumtafuta. Akajaribu kumuulizia kwa rafiki zake kwenye simu, na mmoja wao akamwambia kwamba Ramla alikuwa kwenye mgahawa fulani siyo mbali sana na chuo akipata chakula. Hivyo Xander akaona aelekee huko ili kuongea naye. Alizoea Ramla kuwa aina ya msichana mwenye kutaka sana "attention," hivyo kumpatia haikuwa jambo gumu sana kwake hata kama iliboa.

Baada ya kufika pale, alimkuta Ramla pamoja na rafiki yake mmoja wakiwa ndiyo wamemaliza kula ugali nyama. Huyo rafiki aliyekuwa amekaa naye, Xander alikuwa amempigia muda ule pia kumuuliza Ramla alipo, lakini akasema hajui. Sasa kuwakuta wote hapa ilimaanisha alimdanganya, lakini akaliweka hilo pembeni kwanza. Akaenda walipokaa na kuketi karibu na Ramla, kisha akazungushia mkono wake begani kwa binti.

"Mbona umenunaaa...." Xander akaigiliza wimbo fulani wa taarabu kiutani.

Ramla hata hakumwangalia, hakuonyesha itikio lolote, akautoa mkono wake begani kwake na kuanza kunyanyuka ili aondoke na rafiki yake bila kusema lolote.

"Aaaa... ndo' nini sasa? Eti jamani mama Ashura, ndo' nini?" Xander akasema huku akiongea na mama mmoja aliyefanya kazi hapo.

"Inaonekana umemuudhi," mama Ashura akasema.

"Ana mambo mengi ya kufanya. Mimi wa kazi gani?" Ramla akamwambia mama Ashura kwa kukerwa na kuanza kuondoka.

Xander akatabasamu na kumfuata nje.

"Ramla subiri..." akamwita na kumshika mkono.

Lakini Ramla akautoa mkono wake kwa nguvu sana, kitu kilichomshangaza Xander kiasi.

"Ramla usiwe hivyo. Nimekuja sasa. Ndiyo nataka nikutoe..." akamwambia kwa kubembeleza.

"Sihitaji," Ramla akasema na kuanza kuondoka tena.

Xander akakerwa kidogo. Akamfata na kusimama mbele yake.

"Mbona unakuwa hivyo? Kwani kungekuwa na utofauti gani hata kama tungetoka muda ule na siyo sasa hivi?" Xander akamuuliza.

"Sijui," Ramla akajibu kwa njia ya kejeli.

"Badala ufurahi utapata mambo mengi kwa muda mrefu, we..."

"Kwani uliyatunza wiki nzima kwa ajili yangu au huyo malaya wako?" Ramla akamkatisha.

"What?" Xander akashangaa.

"Ukikaa eti ooh... subiri kwanza, utachelewa kurudi hostel, kuna vipindi, visa visa tu vya uwongo kumbe unakisugua hicho kimlingoti kingine!" Ramla akasema kwa ukali.

"Unaongelea nini?" Xander akawa haelewi.

"Acha kujishaua Xander. Tumekuona unaondoka na yule rafiki ya dada yako," akasema rafiki ya Ramla.

"Sophia? Ahahahah... kwa hiyo mkafanya team up ya kunizingua kwa sababu mmeniona naondoka naye? Unajua nilikuwa nampeleka wapi?" Xander akamuuliza Ramla.

"Utajua mwenyewe," Ramla akasema na kutaka kuondoka, lakini Xander akamzuia.

"Ramla sikia, tuache utoto..."

"Mtoto mwenyewe!" Ramla akasema.

"Kwa hiyo mimi kuondoka na Sophia ndiyo kumekukasirisha? Kuna jambo la muhimu nilikuwa nimeenda..."

"Si ndiyo ulikuwa umeenda naye maana yeye ni wa muhimu sana! Mimi nilipokwambia mapema tuondoke, ukasingizia vipindi. Lakini nusu saa baadae vipindi vikawa siyo vya muhimu tena, except kwa mtu mwingine ambaye alikubana kiunoni vizuri sana wakati mmepanda pikipiki," Ramla akatoa madai yake.

"Ndiyo unahitaji kunisikiliza kwanza. Usikurupuke bwana. Sophia..."

"Hajakurupuka, anakwambia ukweli," rafiki yake Ramla akamkatisha.

"Aisee, we demu nitakuzingua. Hayakuhusu haya, kwo' ondoka hapa," Xander akamwambia kwa hisia kali akiwa amemnyooshea kidole.

"Hamna haja ya jazba baba. Ukweli sikuzote unauma," rafiki huyu akamwambia hivyo Xander.

"Unasemaje? Nitakukata kofi sasa hivi na hayo ma-make up yako kama mavi ya bata usoni! Toka hapa!" Xander akamfokea.

Kakaendelea kujisimamisha kwa kiburi. Ramla sasa akaona Xander alikuwa amekasirika, na sikuzote alijua akikasirika hilo halingekuwa jambo zuri. Lakini akaendelea kujifanya yuko sahihi sana.

"Umpige kwa nini? Kama unataka kupiga mtu nipige mimi," Ramla akasema.

Mama Ashura pamoja na wengine kutoka mgahawani kwake wakawa wamesogea hapo kujua nini kiliendelea.

"Xander kijana wangu, nini tatizo?" mama Ashura akauliza.

"Hakuna tatizo wala," rafiki ya Ramla akajibu.

"Nimekuuliza wewe?" mama Ashura akamwambia.

"Samahani mama. Hakuna shida kubwa. Kazi njema," Xander akamwambia mama Ashura na kuanza kuondoka akiwa ameudhika.

Ramla kuona hivyo, akaanza kumkimbilia na kumsimamisha.

"Kwa hiyo unaenda wapi? Unarudi kwa mtu wako siyo?" Ramla akaendelea kumkasirisha tu.

"Unataka kuamini unachoamini, amini hicho hicho. I don't care anymore," Xander akamwambia na kuanza kuondoka.

"Xander... Xander!" Ramla akaita kwa sauti, lakini jamaa hakugeuka hata mara moja.

Sasa binti akabaki tu kujiuliza nini kingefuata. Kihalisi alikuwa anajaribu kuonyesha umuhimu wake kwa mwanaume aliyempenda, lakini njia hii ikawa imemponza. Alishindwa kuelewa kama ni Xander ndiyo mwenye makosa au ni yeye. Lakini bado alimpenda na hangetaka waachane kabisa, kwa hiyo kwa kiasi kikubwa akaanza kujilaumu moyoni.

Xander aliudhika kwelikweli. Alirudi mpaka pikipiki yake ilipokuwa na kuondoka chuoni hapo upesi sana. Alikuwa anawaza jinsi huyo msichana alivyomtendea kwa dharau, naye hakupenda hata kidogo. Tatizo la wanawake kama yeye ni kwamba wanajali zaidi maoni yao kuliko kusikiliza maoni ya wengine, na ndiyo maana wanapoelewa jambo kwa njia tofauti na ukweli halisi, inakuwa ngumu kuwaelewesha kwa sababu HAWASIKILIZI. Akapata wazo la kuwapigia rafiki zake kuwauliza ikiwa walikuwa wameshakwenda kule "beach," hivyo akasimama sehemu na kumpigia Lucas.

Baada ya rafiki yake huyo kumwambia walikuwa ndiyo wanaelekea huko, Xander pia akasema angefika huko muda si mrefu, kwa kuwa alitaka kwenda nyumbani kwanza kubadili mavazi. Akarudi mwendoni tena baada ya kumaliza kuongea na Lucas.


★★★


Sandra alikuwa ameshafika nyumbani kwao kutokea chuo muda fulani nyuma. Alikuwa ameamua kurudi na kukaa tu nyumbani kwa leo, kwa sababu alihisi uchovu baada ya kutumia muda fulani kufanya mazoezi ya kuogelea kule chuoni. Sasa alikuwa sebuleni ameketi huku ana-chat na Raymond. Ndani alikuwepo Salome tu, kwa kuwa Azra alibaki shuleni kwa ajili ya masomo ya ziada mpaka saa 11 (kama tuition), na mama yao alikuwa kazini bado.

Baada ya muda mfupi akaona geti likifunguliwa na pikipiki ya Xander ikiingia. Akaendelea kuchat na mpenzi wake, akimsubiri kaka yake afike ndani. Baada ya Xander kufika, Sandra akamwomba aende mpaka alipo ili waongee.

"Nambie Sandra, sina muda mrefu... naingia beach," Xander akamwambia.

"Unaenda na nani?" Sandra akauliza.

"Na washkaji..."

"Kupekenyua bikini za wake wa watu au siyo?"

"Ebwana ndiyo..."

"Ahahahah... haya sawa. Nilikuwa nataka kukushukuru tena kwa kumsaidia Sophia leo," Sandra akamwambia.

"Si mmeshanishukuru, inatosha..."

"Hapana Xander, niko serious. Ulichokifanya leo... kimenigusa moyo sana. Nashukuru kwa kumsaidia rafiki yangu. Nimeona ni kama umenisaidia mimi..." Sandra akasema kwa hisia.

"Usijali sister. Nimefurahi kusaidia pia," Xander akamwambia.

Sandra akatabasamu. Xander akashusha pumzi kwa njia iliyomwambia Sandra kwamba kuna tatizo.

"What's wrong?" akamuuliza.

"Aagh... nahitaji ku-clear kichwa changu kidogo. Huu mchana haukwenda vizuri kama nilivyotarajia," akasema Xander.

"Kwa nini? Nani amemzingua my baby brother?" Sandra akasema kiutani.

"Ahahah... ni Ramla. Ameniudhi sana..."

"Kisa?"

"Sophia..."

"Nini? Sophia amemfanyaje?"

"Hmm... muda ule... tulivyoondoka alituona. Anafikiri ninatoka naye eti..."

"Ish! Girlfriend wako ana matatizo gani?"

"Yaani hata sielewi. Af' njia aliyotumia kuongea na mimi sikuipenda yaani imenifanya nihisi kama vile ananidharau kweli. Na kale karafiki kake kanajifanya kana nyodo! Amenikata deep sana leo..." Xander akasema.

"Ulimwambia kilichokufanya uende Benki na Sophie?"

"Mwanzoni nilikuwa kidogo nimwambie, ila baadae sikuona haja maana alinidis sana. Halafu sidhani kama ingekuwa sahihi kuongelea maisha ya Sophia na kila mtu, kwa hiyo nafurahi sikumwambia..."

"Pole mwaya..."

"Usiwaze..."

"Kwa hiyo... ndiyo mmezinguana kabisaaa?"

"Agh yaani hata sielewi. Nataka nipotezee hilo kabisa leo..."

"Mh... hmmm. Ramla anajua sana kukera. Anyway najua mtayanyoosha tu mambo yenu. Asante sana kwa leo Xander," Sandra akarudia kutoa shukrani kwa mara nyingine.

"Ondoa shaka Sandirito..."

"Ahahah... Sandi-nini? Unaharibu jina langu bwana..."

"Ahahahah... kama Condorito!"

"Sitaki uniite hivyo tena... ever!"

"Ahahahah... bado huwa najiuliza ilikuwaje kifupi cha jina lako kuwa Sandra badala ya Xandra... ili iendane na Xander," Xander akamwambia.

"Watu walizoea tu hivyo I guess. Kwanza Xandra isingependeza. Me nilikuwa napenda sana mnifupishie jina langu kuwa Lexi, lakini mazoea yameshawapa tabu," Sandra akasema.

"Lexi wa TVD eeh?" Xander akauliza.

"Nampenda huyo dada!" Sandra akasema.

"Ahahahah... haya bwana. Ngoja me niende. Ushanipotezea nusu saa nzima," Xander akasema na kupanda kuelekea juu.

Sandra alibaki kwenye sofa akicheza na simu yake viganjani mpaka Xander alipotoka huko na kumuaga kuwa anaelekea beach. Akasema ikiwa mama yao angefika kabla hajarudi, basi amwambie kwa niaba yake alikokuwa. Sandra hakuwa na kipingamizi na kumwacha pacha mtu aende kujifurahisha.


★★★


UPANDE WAKE CASMIR

Meja Casmir Eliakim Sona, baba ya mapacha hao wawili, alikuwa amezama kwenye tafiti mbalimbali kuhusiana na mambo yaliyotokea Mwanza na Kigoma kwa kusababishwa na kundi la Demba Group. Alikuwa akisoma njia walizotumia kutoroka kwa umakini sana, na kuna jambo likaonekana kama haliko sawa. Kila jambo walilofanya watu wa kundi hili halikuwa sawa, lakini kilichomsumbua ni JINSI walivyoyafanya.

Kwa kusaidiana na Kapteni Kendrick, rafiki yake wa karibu, walifikia mkataa kwamba kundi hili lilikuwa na watu wenye mafunzo ya hali ya juu, kwa sababu walijua vizuri jinsi ya kuingia sehemu, jinsi ya kutoka, njia za kutumia, muda waliopaswa kutumia, na hata kuwachengua maaskari na kuwafanya waonekane duni sana. Kwa hiyo kama walikuwa wanatakiwa kuwakamata watu hawa, walipaswa kwenda na njia bora zaidi ya kuwachengua vizuri na wao, siyo kichwa kichwa kwa sababu tu walikuwa wanajeshi.

Walipangilia mbinu mbalimbali za kuweza kuwasaidia kufanikisha hili, kisha wakachagua wanajeshi wenye ustadi wa hali ya juu kuweza kufanya kama upelelezi wa ndani zaidi kwenye baadhi ya maeneo waliyoona huenda yangepatwa na janga lingine kama Mwanza na Kigoma. Kwa kuwa bado hawakuwa wameambiwa kuanza kazi moja kwa moja, walifanya hivi kisiri ili kutosubiri amri ambayo huenda ingechelewa, na hili ndilo lililomfanya Casmir awe mahiri sana kwa sababu alichukua hatua za muhimu kuhakikisha mipango inafanikiwa hata kama hakupewa amri za moja kwa moja.



Baada ya muda fulani, wawili hawa wakapokea taarifa kuhusu magari sita ya kijeshi yenye masanduku ya silaha, zilizokuwa zinaelekea kwa wanajeshi mkoani Arusha. Kapteni Kendrick ndiye ambaye sikuzote alitoa kama kibali kuruhusu yapite kwenye sehemu ambazo yangesimamishwa ili kuangalia kila kitu kiko sawa. Wakati akitaka kutoa ruhusa, kuna jambo likaingia kwenye akili ya Casmir. Akamzuia kwanza Kendrick, kisha akarudi kuangalia aina za risasi ambazo zilitumiwa na kundi la Demba Group kuwaua maaskari na watu wale wengine kule Mwanza.

Baada ya kuthibitisha, akamwomba Kendrick waongozane pamoja kuelekea huko ili aangalie jambo fulani. Hii ilimshangaza Kapteni Kendrick kidogo kwa sababu hakujua nia ya Meja wake kufanya hivi ilikuwa ni nini, lakini akatii na kutuma ujumbe kuwa magari hayo yasimamishwe kwanza ili yeye afike kwanza hapo. Kwa kuwa hawakuwa mbali sana na eneo hilo, ingewachukua kama dakika 30 za kuendesha gari upesi ili kufika.

Wakiwa njiani, Kendrick alimuuliza Casmir alikuwa anataka kuangalia nini, naye akajibu kwamba kuna kitu fulani aliwaza ambacho hakuwa na uhakika nacho sana, na huko wanakoenda ni kwenda kuhakiki.



Walipofika maeneo hayo, waliyakuta magari hayo makubwa yakiwa yameegeshwa kwa kufuatana pembeni ya barabara kwenye kiwanja kidogo kisichokuwa na makazi. Mbele ya magari hayo kulikuwa na gari nyingine ya kijeshi, na hapo palikuwa na wanajeshi wengine 9; wakionekana kusubiria wakuu hawa wafike. Baada ya Kendrick na Casmir kuegesha gari lao sehemu hiyo, wakashuka pamoja na kusalimiwa kwa saluti za heshima na wanaume hao; walioonekana kuwa makini ndani ya sare zao za kijeshi.

Watatu kati ya hao 9 ndiyo walikuwa wakiongoza msafara huu wa silaha, hivyo wakawaambia Meja na Kapteni kuwa kila jambo lilikuwa sawa kabisa, na hakutokea shida yoyote. Meja Casmir akasema kwamba alitaka kuangalia masanduku ya silaha hizo, hivyo wakamwongoza kuelekea nyuma ya gari moja na kufungua sanduku kubwa lililotengenezwa kwa mbao nzito. Casmir aliweza kuona bunduki za kivita na mabomu ya kurusha humo, na mjeshi mmoja aliyeongoza msafara huu akamwambia kwamba kwenye kila sanduku kulikuwa na silaha nyingi tofauti-tofauti zilizopangwa vizuri kama hivyo.

Casmir akaulizia kama aina ya bunduki ambazo zilibeba risasi za aina ile waliyouliwa wale watu zilikuwepo, lakini bila kuwaambia moja kwa moja kuhusiana na jambo hilo. Wakamwambia kuwa zipo; kwenye gari la mwisho. Akawaomba waende kumwonyesha, nao wakatii. Lakini wakati walipokuwa wanalielekea, gari nyingine ambayo waliweza kuitambua kwa urahisi kuwa ya kijeshi ikafika hapo pia na kuegeshwa. Wakaiangalia kwa umakini sana, kisha akashuka mwanaume mtu mzima ambaye hakuwa mgeni machoni mwao.

Huyu alikuwa ni Luteni Weisiko (Lieutenant). Mwanaume mwenye mwili mkubwa wa mazoezi, mwenye sura isiyotaka mchezo hata kidogo. Cheo chake kilifata cha Kapteni Kendrick; yaani kwa vyeo vikubwa kutoka kwa Jenerali mpaka kwa Luteni Kanali, alifata Meja, Kapteni, halafu ndiyo huyu Luteni. Wote hawakuwa wameutarajia ujio wake hapo, hivyo wakabaki kumtazama alipoanza kuwaelekea pamoja na wanajeshi wengine wawili waliokuwa pamoja naye.

Wale wanajeshi wa msafara wakamsalimu Luteni Weisiko kwa saluti, naye pia akawasalimu kwa saluti ya heshima, hasa kuwaelekea Meja Casmir na Kapteni Kendrick.

"Luteni... habari za muda?" Casmir akamuuliza.

"Ni nzuri Meja," Luteni Weisiko akajibu kirafiki.

"Ulikuwa unaelekea wapi?" Kendrick akamuuliza.

"Oh... nowhere in particular. Nimewaona tu hapa ikanibidi nisogee kusalimu," Weisiko akasema.

"Naona bado kimombo unapenda kukitwanga vizuri," Kendrick akasema kiutani.

Yeye na Weisiko wakacheka kidogo. Lakini Casmir alikuwa anamtazama kiudadisi.

"Aam... kwa ajili ya batalioni hizo eeh? Zinaelekea wapi?" Weisiko akauliza.

"Ni masanduku tu yanaingia Arusha, hakuna mizinga hahah... Tumeona kuja na sisi kuwasalimu vijana hawa mara moja," Kendrick akamwambia.

"Aaa inspection kidogo," Weisiko akatamka.

"Yeah, kidogo," Kendrick akamjibu.

"Bila shaka vijana wamehakikisha kila kitu kiko poa. Au kuna shida boys?" Weisiko akauliza wanajeshi wa msafara wa silaha.

"Hapana mkuu. Kila kitu kiko sawa," akajibu mmoja.

"Inaonekana hakuna haja ya ku-check. Me pia nilihakikisha mambo yote yanakuwa swadakta. Vipi mkijiunga na sisi? Tulikuwa tunaelekea kupata nyama choma. Kapteni nakumbuka unapenda mbuzi nyama choma. Nakununulia nzima upige yote," Weisiko akasema.

"Ahahahah... ni muda mrefu umepita kijana wangu. Itakuwa jambo zuri sana," Kendrick akamwambia.

"Meja... unaonaje?" Weisiko akamuuliza Casmir.

"Ni sawa. Lakini ngoja kwanza," Casmir akasema.

Kisha akageuka na kutoa ishara kwa mwanajeshi wa msafara kuwa afungue moja ya masanduku yale aliyosema kuna aina zile za bunduki. Baada ya mwanaume huyo kulifungua sanduku hilo kubwa, wote wakashangaa sana baada ya kukuta sanduku hilo liko tupu! Mwanajeshi huyo alionekana kuchanganyikiwa, naye akaanza kuwauliza wenzake silaha zilizokuwa humo zimekwenda wapi. Wenzake wakaanza kupekua na masanduku mengine, lakini yote yalikuwa na silaha ndani yake.

Kapteni Kendrick aliwauliza kwa ukali silaha hizo zilikuwa wapi, nao wakasema labda kuna tatizo lilitokea kwenye upakiaji huko nyuma, kwa hiyo huenda sanduku hilo lilikuwa tupu tokea mwanzo nalo likachanganywa pamoja na mengine pia. Wakaomba radhi kwa hitilafu hiyo na kuahidi kuwa makini zaidi, naye Kapteni Kendrick akawaamuru waondoke eneo hilo haraka sana.

"Ah... yaani vijana hawa! Wanakosa kuwa makini kwa vitu vya namna hii halafu wanajiona wako juu kweli. Samahani sana Meja kwa hilo," Kendrick akamwambia Casmir.

"Hapana usijali. Kama walivyosema... inaonekana ilikuwa hitilafu," Casmir akaongea hivyo na kumwangalia Luteni Weisiko.

"Okay wakuu. Kwa hiyo... mtajiunga nasi?" Luteni Weisiko akawauliza tena.

"Hapana. Kuna sehemu tunaelekea kwanza. Na... jitahidi kutotumia muda mwingi kwenye starehe Luteni. Hatari ziko nyingi... popote pale," Casmir akamwambia.

Luteni Weisiko akamtazama kwa sekunde kadhaa, kisha akapiga saluti ya heshima pamoja na wenzake wawili, nao wakaaga na kuondoka hapo. Sasa wakawa wamebaki Casmir na Kendrick peke yao.

"Cas, kuna tatizo gani? Nimetambua ulikuwa serious sana, na... hatuna mpango wa kwenda popote. Unafikiria nini?" Kendrick akamuuliza.

"Kuna kitu fulani chenye utata kinaendelea Ken. Aina ya silaha walizotumia Demba Group kuua watu Kigoma na Mwanza ndiyo aina ya silaha ambazo hazikuwepo kwenye hilo sanduku. Hizo tu," Casmir akasema.

"Kwa hiyo... unataka kusema kwamba Demba Group wameziiba hizo silaha? Hiyo hai-make sense. Wangeiba masanduku mengi, siyo moja tu," Kendrick akasema.

"Ndiyo hai-make sense. Lakini umeshawaza kuwa labda... wamepewa?" Casmir akauliza.

"Nini? Na nani?"

"Nitajuaje Ken? Siku chache baadae utasikia tena watu Arusha au Singida au kokote wameuliwa na hawa watu, na kama sikosei, silaha zitakuwa ni za aina hiyo hiyo. Sisemi kwamba nina uhakika kuna mtu anawapa ila..."

"Ni jambo linalo-make sense," Kendrick akamalizia.

"Yeah."

"Kwa hiyo inawezekana kuna mtu kutoka jeshini anashirikiana nao. Na kuchagua aina moja ya silaha ambazo watatumia... wanakuwa makini sana. Kila mara mzunguko wa silaha ukifanywa, wanapokea silaha hizo ambazo zinafikiriwa kuwa hazikuwekwa. Meja... wanatengeneza kikundi cha kivita!" Kendrick akamwambia kwa hisia za mshtuko.

"Ken, Ken, tulia... hatuna uhakika. Ni assumption tu ambayo..."

"Inaweza kuwa ya kweli! Vipi kama ni mmoja wa hao wanajeshi tuliowaacha waondoke sasa hivi?" Kendrick akauliza.

"Hapana Ken. Siyo wenyewe. Walikuwa tayari kutuonyesha bila kusita kabisa. Lakini..."

"Lakini?"

"Luteni Weisiko..."

"Nini kuhusu Weisiko?"

"Ametokea tu out of nowhere, all of a sudden anataka tukale nyama choma. Sijui sana lakini... sijapenda hiyo hali," Casmir akasema ukweli.

"Lakini kijana ni mwaminifu sana huyo. Namjua kwa sababu na mimi nilisaidia kumkocha... unafikiri anaweza kuwa anahusika na hili?"

"Sina uhakika Kendrick. Kama nilivyokwambia ni assumption tu. Kufika kwake hapa ghafla kumewasha taa nyekundu kichwani kwangu. Fikiria alivyojikanyaga kwa kuuliza msafara unaenda wapi, halafu tena akasema amehakikisha mambo yamekwenda swadakta. Ni kama alikuwa hataki nilifungue hilo sanduku," Casmir akasema kwa mkazo.

Kendrick akabaki kimya akitafakari mambo hayo.

"Hii ishu ya Demba Group iko deep. Tunahitaji kuwa werevu sana juu ya hili," Casmir akasema.

"Unafikiria tumwambie General Pingu?" Kendrick akauliza.

"Hapana, bado kwanza. Tuchunguze mambo haya kisiri zaidi ili tuthibitishe. Then tujajua ikiwa kweli Demba Group ni kundi la waasi washenzi, au waasi wenye akili... na aliye nyuma yao ni nani," Casmir akasema kwa uzito.

Wawili hawa wakarejea kwenye gari lao na kuanza safari ya kurudi kule walikotoka baada ya mambo hayo yaliyotokea.


★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★

Usikose mwendelezo wa hadithi hii yenye kusisimua.

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA TANO

★★★★★★★★★★★★★


Xander anaanza kurejea nyumbani kwenye mida ya saa 2 usiku baada ya kutoka kujifurahisha na rafiki zake. Angalau kufikia wakati huu alikuwa amechangamka zaidi na kutomwaza Ramla hata kidogo baada ya kitendo alichokuwa amemfanyia mchana huo. Mpaka wakati huu, bado mwanadada huyo hakuwa amemtafuta, naye Xander ndiyo kwanza hakuwa na habari naye.

Wakati alipofika maeneo ya mgahawa ule wa kifahari ambao alimpeleka Ramla siku chache nyuma, aliweza kuliona gari aina ya IST yenye rangi ya silver hapo nje, na upesi akafikiria kwamba huenda lilikuwa ni la madam Valentina. Alijua mwalimu wake huyo alipenda kuja hapo, hivyo akaona ahakikishe kama gari lilikuwa ni lenyewe ili ikiwezekana akamsalimu huko ndani. Hawakuzungumza kabisa leo chuoni kwa kuwa ilionekana ni kama madam bado hakujisikia vizuri kuhusu jambo alilomfanyia kwenye kazi ile; hata kama alipata A.

Baada ya kufika na pikipiki nyuma ya IST hiyo, akawa amehakiki kuwa ndiyo yenyewe kwa kuangalia namba za usajili, kisha akaiegesha pikipiki yake karibu na hapo pia, naye akaelekea kule ndani. Kama kawaida, alimkuta madam Valentina akiwa kwenye meza yake ile ile ambayo alikuwa amekaa siku ile. Alikuwa mwenyewe tu hapo, huku sehemu zingine zikiwa na watu mbalimbali waliofurahia milo na vinywaji. Akaelekea mpaka hapo na kumshika begani akiwa nyuma yake.

Valentina akageuka na kuachia tabasamu hafifu la kirafiki. Hii ikamfanya Xander ajihisi ahueni kwa sababu sasa haikuonekana kama madam wake ana kinyongo naye.

"Alexander... unafanya nini hapa?" akamuuliza.

"Nilikuwa napita nikakuona... nikaona nije nikusalimie," Xander akajibu.

"Ooh... nilifikiri ulikuja na girlfriend wako," Valentina akasema.

"Hapana. Mh? Kumbe siku ile ulimwona?" Xander akauliza.

"Siku gani?"

"Kwani ni nini kimekufanya uniulize hivyo?"

"Aam... nimekuona leo pamoja naye. Mlikuwa kama mnagombana sijui au vipi... kwa hiyo' nikafikiri umemleta hapa..."

"Aaaa... ulikuwa wapi wakati huo?"

"Pembeni tu..." Valentina akasema kimkato, kisha akanywa 'wine' yake kwenye glass.

Xander akamtazama kwa sekunde kadhaa, kisha akauliza, "Naweza kukaa na wewe?"

"Ndiyo. Karibu. Lakini ni lazima uagize kitu ule," Valentina akasema.

"Sawa. Niagizie," Xander akasema huku akiketi.

"Huwa unapenda nini?"

"Nyama."

"Mhm... haya," Valentina akasema na kuita mhudumu.

Xander alikuwa anamwangalia tu kwa umakini sana. Valentina akamwagizia nyama nusu ya kukaangwa na kinywaji, kisha mhudumu akaondoka.

"Ulikuwa unatokea wapi?" Valentina akauliza.

"Beach."

"Aaaa... okay."

"Na wewe... ulikuwa unatokea wapi?" Xander akauliza.

"Sina sehemu maalumu nayokuwa. Mimi ni mvivu kupika. Kwa hiyo hii sehemu ndiyo jikoni kwangu napokuja kupata msosi..."

"Ahahah... sawa. Nimekorofishana na girlfriend wangu leo kwa hiyo nahitaji kujifurahisha angalau. Sipendi stress," Xander akamwambia.

"Kupata stress inamaanisha unampenda sana..."

"Ah! Siyo kivilee. Ana miosho na swaga ambazo mara nyingi huwa zinanikera, lakini ananielewa sana ndiyo maana bado niko naye. Ila... hata kama angesema azingue uzi wetu, ningeichomoa sindano fasta," Xander akasema kiutani, naye Valentina akacheka.

"Una maneno wewe! Kama tu kwenye uandishi wako," Valentina akamwambia.

"Asante. Nilikuwa nahofia labda bado ulikasirishwa, sorry... hukupendezwa saana na kazi ile... kupita maelezo yaani..."

"Hapana wala usiwaze. Nilipenda. Ilinigusa. Ilikuwa ni kama ulitegesha camera ndani ya maisha yangu yote," Valentina akamwambia.

"Ila najua nilienda mbali sana. Kiukweli, nilikuwa najaribu kukufanya uone kwamba ninajua vitu vingi... lakini sasa hivi natambua hiyo haikuwa adabu wala heshima. Sikutakiwa kufanya vile. Samahani kwa hilo..." Xander akamwambia kwa hisia.

"Ahah... sawa. Haina shida. Unajua... labda ni kweli. Labda nilikasirika. Ila unajua ni kwa nini? Ni kwa sababu katika mambo yote ambayo uliandika... kuna jambo fulani hukuliweka. Ulifanya hivyo makusudi si ndiyo?" Valentina akauliza.

"Madam V..."

"Nataka uniambie. Niambie sasa hivi..."

"M..madam V sidhani kama..."

"Please... tell me. Please..."

Xander akaangalia chini kihuzuni kidogo, kisha akashusha pumzi kidogo.

"Ulikuwa... ulikuwa na mtoto. Alikufa siku hiyo hiyo uliyojifungua," Xander akamwambia bila kumtazama.

Valentina akanywa wine yote ya kwenye glasi kwa kishindo. Alikuwa akijikaza asitoe machozi.

"Hivi ulifanya nini mpaka ukajua mambo haya yote?" akamuuliza kwa sauti ya chini.

Xander akamwangalia. "Nilitafuta kupitia kwenye website zenye bio za faculty member wa chuo kwa somo lako, social media pia... nikapata taarifa nyingi kuhusu maisha yako ya zamani na marafiki, umri wako, unakoishi..."

"Hadi tattoo yangu," Valentina akamkatisha.

Xander akatazama pembeni.

"Lakini ukaacha kuandika kuhusu hili lingine. Kwa nini? Ulifikiri kwamba nitaumia sana? Au kwamba nilikuwa najaribu kusahau kila kitu kibaya kilichonipata maishani? Kwamba unaweza kuyaandika maisha yangu kwa njia ambayo WEWE unataka yawe?" Valentina akasema kwa hisia.

"Siyo hivyo. Madam V... nilikuwa tu najaribu ku..."

Xander akakatishwa na mhudumu aliyefika hapo akiwa na sahani liyojaa nyama na kinywaji kwa ajili ya Xander. Xander aliweza kumwona Valentina akijifuta chozi kwa uharaka, naye akamwonea huruma sana. Kisha ghafla Valentina akanyanyuka na kubeba mkoba wake. Akamwambia Xander kwamba yeye angeondoka sasa, hivyo kijana abaki kufurahia msosi wake. Lakini alipotaka kupiga hatua kuondoka, akayumba nusu kuanguka, ila mhudumu pamoja Xander wakawahi kumshika mwili wake.

"Madam V uko sawa?" Xander akamuuliza kwa kujali.

"Ndiyo niko sawa. Rudi ukae..." akajibu huku akijisawazisha.

Xander akatambua kwamba ile wine aliyokunywa kwa kishindo ilimgonga kichwani vibaya. Valentina akaanza kuondoka hapo taratibu, akitembea kwa umakini ili asianguke. Xander alijua kuwa hapo lazima shida ingetokea kwa sababu Valentina alihitaji kuendesha gari, na hali hii aliyokuwa nayo haikufaa. Akamwambia mhudumu amfungie mboga yake vizuri ili aondoke nayo, naye akampatia pesa bila kujali chenji. Alimwomba aharakishe ili aweze kumwahi Valentina, na mhudumu huyu akafanya upesi.

Baada ya kuchukua chakula chake akatoka haraka na kufika mpaka sehemu ambayo Valentina aliegesha gari lake. Akamkuta akiwa amesimama kando ya mlango akitaka kuufungua. Akamwahi na kumshika mkono.

"Madam V... huwezi kuendesha. Nafikiri wine imekuingia vibaya..." akamwambia.

"Niko sawa Alexander. Usiku mwema," Valentina akasema na kuanza kuweka funguo sehemu ya kufungulia mlango.

Xander akaona jinsi alivyohangaika kuiingiza kiusahihi, na ni wazi alikuwa anaona vitu mara mbili-mbili.

"Madam V... utaanguka. Huwezi kuendesha. Na mimi siwezi kukuruhusu," Xander akamwambia.

"Wewe kama nani?" Valentina akamuuliza.

Xander akabaki kumwangalia tu jinsi alivyomtazama kwa mkazo. Aliona sasa mwanamke huyu alikuwa na hisia nyingi sana zilizovurugika. Lakini pamoja na hayo yote, asingeweza kumwacha tu afanye jambo hili ambalo huenda lingemsababishia matatizo. Valentina akafanikiwa kuufungua mlango, lakini Xander akazikwapua funguo kutoka kiganjani mwake na kuanza kumvuta mkono kuelekea upande wa pili wa gari. Valentina alikuwa anajivuta na kumfokea kuwa amwachie, lakini Xander alimzidi nguvu na kufungua mlango wa pembeni wa mbele, kisha akamwingiza kwa lazima akae.

Mambo haya yote yalimuudhi sana Valentina kwa sababu aliona ni kama kijana huyu anavuka mipaka. Xander akaufunga mlango na kuzunguka mpaka upande wa usukani na kuingia hapo, kisha akai-lock milango yote baada ya kuwasha gari bila hata kumwangalia madam wake usoni. Valentina alikuwa anamtazama kwa ukali, naye akamwambia alizime haraka sana la sivyo angemshtaki. Lakini kijana akaweka wazi kuwa hiyo ingekuwa hasara kwake kwa sababu ni yeye ndiye aliyetaka kuendesha gari huku akiwa amelewa.

"Sijalewa!" Valentina akakanusha.

"Okay... umelewa-lewa kwa mbali," Xander akamwambia.

"Unanipeleka wapi? Kwangu unapajua?"

"Ndiyo. Baada ya ile research yote, najua hadi namba yako ya nyumba..."

"Acha upuuzi Alexander, nitakuja kusema kuhusu huu ujinga kwa wazazi wako!" Valentina akamtishia.

Xander akamwangalia na kusema, "Sawa tu. Tutawaambia nilikuteka."

Valentina akakunja uso wake kimshangao.

Xander akaligeuza gari kutoka hapo na kuingia barabarani, akiwa ameiacha pikipiki yake nje ya eneo lile la mgahawa.


★★★


Mida hiyo hiyo, Meja Casmir, akiwa sehemu yake ya kupumzikia, anapigiwa simu na Kanali Jacob Rweyemamu, ambaye anamtaarifu kuwa anapaswa kwenda kwenye jengo la ofisi za kijeshi siku ya kesho; yeye pamoja na Kapteni Kendrick. Jambo hili linamshangaza kiasi, naye anauliza kuna jambo gani huko, lakini Kanali anamwambia tu Meja kwamba anapaswa kufika kesho pamoja na Kapteni, yote watayajua huko huko.

Casmir akaonyesha heshima na kutii agizo hilo. Kanali Jacob akamwambia kwamba amtaarifu Kapteni Kendrick mapema ili kesho kufikia mida ya mchana wawe wamefika huko. Casmir akamtafuta Kendrick kwa simu na kumwambia kuhusu hilo. Hata na yeye pia alishangaa kwa sababu walitakiwa kuacha sehemu zao za kazi ghafla tu na kwenda huko. Lakini akamwambia haikuwa na shida, naye angeanza matayarisho mapema ili kesho asubuhi waweze kuondoka mapema kwa pamoja.


★★★


Xander alimwendesha Valentina na kumfikisha mpaka nje ya nyumba yake. Tokea walipoondoka kule, hawakusemeshana lolote lile ndani ya gari hili. Xander akamtazama usoni madam wake, akiwa anataka kumuuliza ikiwa itakuwa sawa kwenda kumfungulia geti lake na kuingiza gari ndani. Lakini akahisi hilo lingekuwa swali la kipuuzi, maana hakuhitaji ruhusa kumlazimisha kuja pamoja naye. Ni kwamba alikuwa tu anataka kumsemesha lakini akakosa la kusema.

Hivyo, akauchukua mkoba wa madam wake na kuupekua, akitafuta funguo zingine. Alipata tano zilizounganishwa sehemu moja, naye akatoka na kuelekea getini. Valentina alikuwa anamtazama kwa makini sana, akiwa ameudhika pia, lakini akamwacha tu kwa kuwa Xander alijiona kuwa mjuaji sana. Xander akafanikiwa kufungua mlango mdogo wa geti na kuingia kwa ndani, kisha akalifungua geti lote pia. Akarejea kwenye gari na kuliingiza mpaka ndani, na baada ya kushuka akarudi kulifunga geti tena.

Nyumba aliyoishi Valentina ilikuwa ya kupanga, yaani nyumba yote aliilipia ili aishi hapo. Ilikuwa kubwa na pana kiasi, iliyozungushiwa uzio uliokaribiana na kuta za nyumba yenyewe. Ndani ya uzio wa nyumba, kulikuwa na sehemu ndogo ya kuegeshea gari lake kabla ya kuingia kule ndani kabisa. Ndani kabisa, kulikuwa na mpangilio maridadi wa vitu; mlango wa kuingilia kwenye sebule pana kiasi iliyokuwa na meza kubwa nyeusi katikati, huku pembeni kukiwa na masofa marefu ya aina moja yaliyozunguka kona zote za sehemu hiyo, na ukutani TV kubwa ya flat screen. Sehemu ya jikoni iliyotunza vyombo pia ilikuwa kwa mbele, na korido fupi upande mwingine lililoelekea kwenye vyumba vitano; chake, viwili kwa ajili ya wageni, kimoja kilichogawanywa kuwa bafu kubwa na choo, na kingine alichotumia kama ofisi yake ndogo iliyojaa vitabu na vifaa vyake vingi. Sakafu lote lilikuwa la vigae, na palikuwa pasafi sana. Alikuwa akiishi na msichana wake wa kazi hapo kipindi fulani nyuma, lakini baadae akamwachia aondoke kwa kuwa alitaka kubaki peke yake tu.

Akiwa ameanza kurudi alipoegeshea gari, akakuta Valentina akiwa ndiyo anatoka ili aelekee ndani. Xander akamwambia kwamba yeye angerudi tu nyumbani sasa, lakini hakujibiwa. Valentina akaelekea mpaka kwenye mlango wa kuingilia ndani ya nyumba na kuufungua, na ni hapa Xander akakumbuka nyama ile aliyotoka nayo kule mgahawani. Akaiwahi kwenye gari na kuitoa, kisha akamfata na kumwambia aichukue. Lakini Valentina akawa kama hamsikii vile, naye akaingia tu ndani bila kumjali kijana huyu.

Xander akahisi hatia kiasi kwa sababu alikuwa ametoka kumwomba samahani usiku huo huo kwa sababu ya kutenda bila adabu kumwelekea, lakini tena sasa ikaonekana ni kama amerudia yale yale. Ijapokuwa hakukosea sana zamu hii, alijua Valentina alikuwa tu amevurugika, hivyo lolote ambalo kijana angefanya lingekuwa baya tu machoni pa mwanamke huyu.

Kutoka hapo aliposimama baada ya Valentina kuingia ndani sekunde chache tu, Xander akasikia sauti kama ya kilio, na kwa haraka akatambua ilikuwa ni Valentina. Akakimbia ndani upesi na kumkuta sehemu ya korido lile fupi, akiwa kama amekaa chini kwa kupiga magoti, huku akijishika mguuni. Usiku huu alikuwa amevalia gauni nyeupe na nyepesi tu ya maua-maua, na chini vilikuwa viatu virefu. Xander akatambua kwamba alikuwa ameanguka, naye akawahi hapo chini kumsaidia.

Valentina alikuwa amekunja sura kiasi kwa kuwa mguu wake uliteguka kidogo baada ya kiatu alichovaa kusababisha aanguke, lakini hasa kwa sababu alihisi kizunguzungu kwa mbali. Xander akamsadia kunyanyuka na kumpeleka sehemu ile ya sebule, kisha akamkalisha kwenye sofa na kuanza kuinyoosha sehemu ya mguu wake iliyoteguka. Mwanzoni Valentina alikuwa akitoa sauti za maumivu, lakini baada ya muda fulani akaacha kwa sababu Xander alimpa "massage" nzuri sana.

"Bado unauma sana? Tutumie dawa ya kuchua. Una dawa ya kuchua humu ndani?"

Xander akauliza hivyo bila kumtazama huku akiendelea kuugeuza-geuza mguu taratibu. Valentina hakumjibu, bali akawa anamtazama tu kwa umakini. Xander aliponyanyua uso wake kumwangalia na kukuta anatazamwa namna hiyo, naye akabaki kumwangalia tu machoni mwanamke huyu mwenye sura ya kuvutia. Utizami ambao Valentina alimpa Xander, ulimfanya kijana huyu apoteze mawazo mengine yote na kukaza akili yake yote kwa mwanamke huyu tu.

Bila hata kutambua haraka aliingiliwa na nini, Xander akajinyanyua taratibu na kuketi karibu naye kwenye sofa, na sasa wakawa wanaangaliana kwa ukaribu sana. Kwenye akili ya Valentina, alijua moja kwa moja jambo hilo lilikuwa linaelekea wapi, lakini ni kama akaamua kuacha aone ikiwa lingefika huko.

Xander alikuwa amepandwa na hisia kali sana kumwelekea mwanamke huyu, naye akamshika usoni kwa kiganja chake, wakiwa wanatazamana kwa njia fulani kama vile ni watu ambao hawajuani, kisha akaifata midomo ya madam bila kusita na kuibusu kwa juu. Ilimchukua ujasiri fulani kufanya hivyo, kwa sababu kichwani kwake alikuwa ameshajiwekea wazo la kwamba huenda madam angemzingua, lakini bado akafanya hivyo.

Busu yake ya kwanza kwa mwanamke huyu ilikuwa kavu tu, kisha akambusu tena mara mbili huku madam Valentina akiwa kama anajirudisha nyuma. Lakini Xander akaendelea kulazimisha tu, na sasa Valentina akailegeza midomo yake kidogo na kuruhusu Xander aanze kumbusu kimahaba sana. Pumzi za Valentina zilikuwa nzito na miguno ya mbali ikaanza kusikika, lakini akawa kama amerudiwa na ufahamu na kumsukuma Xander kidogo.

Xander akawa anamwangalia kwa hamu sana huku wote wakitoa pumzi zenye presha kubwa. Valentina alikuwa anamwangalia kwa njia iliyoonyesha kama hakupendezwa na hilo.

"Alexander... nafikiri itakuwa vyema ukiondoka..." akamwambia.

"Lakini... madam V..."

"No! Tafadhali ondoka..." Valentina akasema kwa uthabiti.

Kisha akanyanyuka na kuanza kutembea akichechemea kuuelekea mlango. Xander hakutaka kukubali kwamba huu ndiyo ungekuwa mwisho, kwa sababu kuna vitu aliweza kuhisi wakati anambusu mwanamke huyu. Alihisi uhitaji wake mkubwa wa kupewa kitulizo, lakini alikuwa anajaribu kujizuia. Akanyanyuka haraka na kumwahi pale tu Valentina alipokuwa ameufikia mlango na kushika sehemu ya kuuvutia. Akafika nyuma yake, karibu sana, kisha akaushika mkono huo kama kumzuia.

Valentina akashtuka kidogo. Akamhisi vyema Xander nyuma yake, jinsi alivyoigusanisha miili yao.

"Alexander... unafanya nini?" akauliza kwa wasiwasi.

"Shhhh... relax madam V. Just... relax," Xander akasema kwa sauti ya kunong'oneza.

Hapo hapo Valentina akahisi shingo yake ikipewa busu laini kwa midomo ya Xander. Akasisimka sana na kutaka kugeuka kwa nguvu, lakini Xander akamdhibiti.

"Alex... Alexander sst... stoop... no..."

Valentina akawa anaendelea kukataa huku Xander akiendelea kumbusu shingoni mwake. Xander alitumia mkono wake mmoja kuubana vyema mwili wa Valentina kwake, huku mwingine akiutembeza kuanzia tumboni kuelekea mpaka usoni kwa mwanamke huyu. Valentina alianza kupata hisia za juu sana, na pumzi zake zikawa zikitoka kwa njia iliyothibitisha hilo.

Mambo yakazidi kupamba moto pale Xander alipoanza kushika sehemu zenye kukoleza hisia hizo hata zaidi kwenye mwili wa mwanamke huyu. Vizuizi alivyokuwa ameanza kutoa vikapungua, na sasa akawa amefumba macho tu akimwacha Xander amtawale, akitoa miguno ya juu juu ya pumzi. Kisha Xander akapeleka mchezo huu hatua nyingine wakiwa bado mlangoni hapo. Alipenda sana jinsi madam alivyoonyesha kufurahia kile alichopata, naye akaona aongeze manjonjo hata zaidi.

Akaanza kutembea kuelekea kwenye masofa akiwa amembeba, kisha akaendelea kumpatia penzi kisawasawa mwanamke huyu. Valentina alikuwa amenyanyua miguu hewani kama mbuzi aliyetoka kuchinjwa, akitoa vilio vya raha huku ameubana mgongo wa Xander kwa nguvu sana. Madam akalegea kupita maelezo, akawa anaongea maneno yasiyoeleweka na hata kumpiga vibao Xander kwa nguvu, lakini kijana akakazana tu. Kisha baada ya dakika kadhaa wote wakawa wameridhishana na kutulia kwenye sofa hilo.

Hiki ni kitu ambacho Xander alikuwa akihitaji sana leo, na alifikiri angekipata kwa Ramla, lakini akamzingua. Ila hakutegemea kama angeweza kukipata kwa mwanamke huyu, aliyemzidi umri, na ambaye hakujua ikiwa angeweza kuja kurudia naye jambo hilo tena kwa sababu mambo yote yaliyotokea hapa yalifanikishwa na msaada kidogo wa wine aliyokunywa madam. Akabaki akipumua kiuchovu kiasi, huku madam Valentina akiwa amefumba macho na kupumua kilegevu pia.

Xander akashindwa afanye nini. Alibaki kumtazama tu, kisha akajinyanyua na kuchukua boxer yake pale chini, naye akaitumia kumfuta Valentina. Alipomtazama tena, akatambua kwamba Valentina alikuwa amesinzia. Akawaza huenda alihisi uchovu sana; jumuisha na wine aliyokunywa. Akasogea mpaka karibu na uso wake, kisha akambusu kidogo mdomoni. Akamnyanyua kwa nguvu na kumbeba mikononi mwake, kisha akatoka sebuleni hapo kuelekea vyumbani; akitafuta kimoja ambacho angetambua ni cha kwake.

Hii ilikuwa ngumu kidogo kwa sababu Valentina alikuwa na uzito kiasi ijapokuwa hakuwa mnene, na kuzunguka naye mikononi kulichosha, lakini kijana akajikaza. Baada ya kuingia kwenye chumba cha madam, akamlaza kitandani, kisha akamfunika kwa shuka na kuondoka. Alikuwa bado hajavaa suruali kwa chini, hivyo akarudi sebuleni kule na kuivaa bila boxer, na baada ya kuangalia simu yake, akakuta missed call kadhaa kutoka kwa mama yake.

Akamtumia ujumbe mfupi mama yake kumjulisha kwamba alikuwa njiani kurudi nyumbani, hivyo akaharakisha kuondoka hapo ikiwa ni saa 6 usiku sasa. Aliamua kuchukua funguo ya ziada ya geti la nyumba hii ili aufunge mlango mdogo wa geti kwa nje, naye akaacha ujumbe kwenye simu ya madam Valentina kumwambia kwamba amefanya hivyo, kwa hiyo yeye angetumia funguo nyingine akitaka kuondoka asubuhi (Valentina), halafu kesho Xander angempatia hii huko chuoni.



Ilimchukua kama nusu saa kufika kwao, kwa sababu alipotoka kwa madam Valentina alihangaika sana kutafuta usafiri, na baada ya kuupata akaenda mpaka kwenye sehemu ile aliyoacha pikipiki yake na kuikuta bado iko pale, kisha ndiyo akaenda nyumbani. Alimkuta mama yake akiwa bado hajalala, naye alimuuliza sana sababu ya yeye kutomwambia alipokuwa mpaka usiku hivyo. Haingekuwa na tatizo kutoka hata kama angeenda kulala na rafiki zake, lakini sikuzote Alice alipenda kupewa taarifa.

Xander akamwomba samahani na kumwahidi kwamba haitajitokeza tena, sema kwa siku hii alijisahau. Baada ya Alice kumwambia waliweke suala hili pembeni, Xander akamuuliza maandalizi ya sherehe yake ya siku ya kuzaliwa yalikwendaje, naye Alice akasema mambo yalikuwa yanakwenda vizuri.
Xander akasema alihisi uchovu sana, hivyo Alice akamwacha aende kupumzika, naye angeenda kulala baadae.

Xander alifika chumbani kwake na kujitupia kitandani, akianza kuyarudia kichwani mambo yaliyotokea nyumbani kwa Valentina. Alianza kuikumbukia sura yake, mwili wake, miguno yake, jinsi alivyomng'ang'ania sana wakati alipokuwa akimpa penzi murua, naye hakuweza kujizuia kutabasamu kwa kuhisi raha sana.

Muda haukupita mwingi sana na usingizi ukamjia hapo hapo.


★★★


Asubuhi na mapema sana, Meja Casmir pamoja na Kapteni Kendrick waliondoka kutoka sehemu zao za kikazi kwa kuelekea kwenye jengo la ofisi za kijeshi kwenye kambi yao baada ya kupewa mwito huo wa ghafla na Kanali Jacob Rweyemamu. Ofisi hizo zilikuwa kwenye jiji lile lile ambalo familia ya Casmir na Kendrick zilikuwa pia, hivyo Kendrick aligusia uwezekano wa wawili hawa kwenda kwa familia zao kutoa salamu pia. Lakini Casmir akamwambia walipaswa kwanza kujua walichoitiwa ni nini, ndiyo mambo mengine yangefuata.

Walikuja kufika jijini hapo kwenye mida ya saa 6 mchana na moja kwa moja kuelekea kwenye kambi ile yenye jengo la ofisi za wanajeshi. Nyumbani kwa Casmir kulikuwa upande tofauti na maeneo hayo kwa umbali mrefu kiasi. Walikuwa wamekuja pamoja kwa kutumia gari la Casmir, wakiwa wamefikiri kwamba wangerudi kule walikotoka pamoja tena.

Baada ya kufika nje ya kuta zilizozunguka jengo lile kubwa na pana, walikaribishwa na baadhi ya wanajeshi wenye vyeo vya chini yao kwa heshima kubwa, kisha wakaambiwa kwamba Kanali Jacob Rweyemamu alikuwa akiwasubiri ndani ya ofisi yake kuu. Bila kukawia wakaanza kuelekea huko huku wakiangalia na mazingira ya eneo hilo. Kulikuwa na uwanja mpana eneo la nje lenye sehemu mbalimbali ambazo walitambua zilitumiwa kwa ajili ya mazoezi. Pia kulikuwa na majengo madogo madogo kwa ajili ya wanajeshi waliokuwa hapo, na sehemu za pembeni za kuta zilizozungukia majengo haya kulikuwa na wanajeshi wenye silaha wakilinda.

Ndani ya jengo baada ya kuwa wamefika, waliweza kuona jinsi lilivyopangiliwa vizuri kwa kuta imara na vyumba kadhaa ambavyo bila shaka vilikuwa na matumizi maalumu hapo ya kiofisi; yaliyoshughulika na masuala ya usalama wa taifa. Walifika mpaka kwenye mlango wa ofisi ya Kanali, na baada ya Kanali Jacob kutaarifiwa kwa simu kuwa wamefika, akaomba waingie upesi. Wawili hawa wakaingia kwenye ofisi yake na kukuta akiwa ameketi kwenye kiti chake mbele ya meza yenye makablasha kadhaa, nao wakatoa heshima kwa kupiga saluti.

"Meja... Kapteniii! Aah... ni muda sana hatujaonana!" Kanali Jacob akasema kwa shauku kubwa.

Wawili hao wakashusha mikono yao kutoka kichwani na kumtazama pia. Kendrick alikuwa anatabasamu kwa furaha baada ya kumwona Kanali amewaonyesha shauku ya urafiki, ikimaanisha hakukuwa na shida; naye Casmir akawa anamtazama kwa njia ya kawaida tu.

"Kanali Jacob... ni kitambo," akasema Kapteni Kendrick.

"Ah sana! Naona sasa hivi hadi una kitambi!" Kanali Jacob akamwambia Kendrick.

"Ahahahah... siyo kama chako," Kendrick akasema.

"Hahahah... and look at you... Major Casmir! Ah, jina lina nguvu sana hilo," Kanali akamsifia.

Casmir akatoa tabasamu hafifu na kusema, "Asante Kanali."

"Bila shaka mnajiuliza ni kwa nini nimewaita ghafla. Kuna jambo ninataka kuongea nanyi vijana wangu," akasema Kanali.

"Kanali, niite tu mimi kijana. Nywele nyeusi za Meja zisikudanganye ameficha mvi kwa chini," Kendrick akatania.

Kanali Jacob akacheka na kuuliza, "Kwa hiyo hastahili kuitwa kijana?"

"Haswaa!" Kendrick akasema.

Casmir akatabasamu na kumwangalia Kendrick huku akitikisa kichwa.

"Sawa sawa. Nina... nafahamu mmepewa mission ku-deal na Demba Group muda si mrefu sana," Kanali akasema.

Wote wakasema ndiyo.

"Na bila shaka mmeshaanza kusaka mambo mengi kuwahusu, kwa kuwa najua vizuri Meja ni mtekelezaji wa mambo kama haya discretely sana. Nilikuwa nahitaji kujua mmefikia wapi wakati huu," Kanali akawaambia.

Kendrick akamtazama Casmir, naye Casmir akamwangalia pia.

"Kuna jambo lolote zito linaendelea?" Kanali akawauliza.

"Aam... kwa heshima yote mkuu, ni kwamba nilipatiwa kazi hii moja kwa moja kutoka kwa Jenerali...."

"Jenerali Pingu. Ndiyo najua. Na najua unachotaka kusema ni kwamba taarifa unatakiwa kumpatia yeye kupitia njia aliyokuagizia utumie. Well, hiyo ndiyo sababu nimewaita hapa. Ni kuwataarifu kwamba kuanzia sasa mimi ndiyo nitakuwa nampatia taarifa hizo Jenerali, kwa hiyo mambo yote ambayo mnayapata yanapaswa kupita kwangu ili niyawasilishe kwake," Kanali Jacob akawaambia.

Wawili hawa wakatazamana kwa kifupi, kisha wakamwangalia tena Kanali.

"Kwa hiyo mambo tuliyoyapata tunatakiwa kukuambia kwanza si ndiyo?" Kendrick akauliza.

"Ndiyo," Kanali Jacob akajibu.

"Mbona mambo yamebadilika haraka? Taarifa tungetakiwa kumpa Luteni Kanali, halafu azifikishe kwa..."

"Ndiyo, lakini sasa hivi zitakuwa zikipita kwangu. Oswald amepata mgawo mpya, hiyo ndiyo sababu," Kanali akaeleza.

"Aaaa..." Kendrick akaonyesha kuelewa.

"Yeah. Kwa hiyo, mmefikia wapi?" Kanali Jacob akauliza kwa mara nyingine tena.

"Well... Meja ameongoza operesheni ya kuanza kuwasaka kisiri watu hao, na mpaka sasa tumepata vigezo kadhaa ambavyo vinaweza kutuongoza kuwatambua haraka. Tunajua bado amri haikuwa imetolewa lakini... tuliona ni bora kuanza mapema," akasema Kendrick.

"Haina shida. Ni kwenye mikoa gani?" Kanali akauliza.

"Hatuna uhakika sana, lakini macho yetu hasa yako mikoa ya Arusha, Singida na Dodoma. Ila tunajitahidi kuongeza force na maeneo mengine," akajibu tena Kendrick.

Kanali Jacob akatikisa kichwa kuonyesha ameelewa, naye Casmir akawa anamtazama kwa makini sana. Akili yake aliijua yeye mwenyewe.

"Okay sawa. Hakuna jambo lingine lolote ambalo nahitaji kujua?" Kanali akauliza.

"Well... jana kuna jambo fulani lilitokea..."

"Siyo muhimu sana," Casmir akamkatisha Kendrick.

Wote wakamtazama.

"Nimetoka kusema kwamba natakiwa kujua kila kitu. Kwa hiyo MIMI ndiyo nitaamua kama ni muhimu au siyo muhimu sana. Kendrick... sema," Kanali akaongea kwa mkazo.

"Jana kuna silaha hazikukutwa kwenye sanduku moja kati ya mengi wakati zinaelekea Arusha, na zilikuwemo bunduki na mabomu yaliyofanana na zile ambazo Demba Group walitumia. Tulifikiri tu ni ajabu kidogo..." akasema Kendrick.

"Mmmm. Wewe Meja unalionaje hili?" Kanali akauliza.

Casmir akatulia kidogo, kisha akasema, "Kama nilivyosema, siyo muhimu sana kwa sababu inawezekana tu hilo sanduku walisahau kuliwekea silaha."

Kendrick akamtazama Casmir kimaswali kidogo.

"Kwa hiyo hakuna jambo lolote mnalohisi haliko sawa na tukio hilo?" Kanali akawauliza.

Casmir akawa wa kwanza kukanusha, naye Kendrick akaona akanushe pia.

"Basi sawa. Hiyo haina haja ya kufika popote kwa kuwa kama ulivyosema, siyo muhimu. Ninawahamishia post zenu sasa. Mtakuwa huku badala ya kule kwa wiki nzima," Kanali Jacob akasema.

Wote wakashangaa.

"Unamaanisha nini Kanali?" Kendrick akauliza.

"Ohoo usijali Kapteni. Namaanisha nawapatia ofisi maalumu hapa kwa wakati huu ambao ni wa muhimu kwa Meja Casmir. Kwa hiyo mnaweza kuendelea kufanyia utafiti wenu mkiwa hapa na kutuma maagizo mnakohitaji," akasema Kanali Jacob.

"Wakati wa muhimu? Sijaelewa kikamili Kanali," akasema Casmir.

"Ninafanya hivi kwa ajili yako Meja. Ninafahamu kutakuwa na birthday ya mke wako wiki hii, tena siku mbili tu zimebaki. Naelewa haujawa na muda mwingi ku-spend na familia yako, na baada ya kuona ni jinsi gani hii mission ingekubana, nikaamua nikusogeze huku ili uweze kuhudhuria. Hakutakuwa na haja ya kuhamahama... wewe na Kapteni mtakuwa na ofisi zenu hapa, then baadae mwaweza rudi kule... kama mtachagua kufanya hivyo. Au mnaonaje?" Kanali Jacob akawaambia.

Kendrick alimtazama Casmir akiwa anatabasamu kwa furaha, naye Casmir alikuwa akishangaa na kutabasamu kwa wakati ule ule.

"Lakini... lakini..." Casmir akashindwa kuendelea.

"Kanali, hilo pigia mstari. Tuko tayari kuhamia huku. Nashukuru sana kwa ufikirio huu," akasema Kendrick.

"Haina shida. Ni muhimu kujali hali za ma-comrade wenzangu. Lakini nina ushauri kwako Casmir..." akasema Kanali Jacob.

"Ndiyo Kanali..." akajibu Casmir.

"Vipi uki...fanya kama surprise? Bila shaka mke wako atafurahi sana. Usimwambie kwamba upo huku tayari, ili ufike tu siku hiyo paap! Atarukaruka eeh..." akasema Kanali.

Wote wakacheka kwa pamoja, huku Casmir akihisi furaha mpya moyoni mwake.

"Sijui niseme nini Kanali..." Casmir akanena.

"Asante tu itatosha," Kanali Jacob akasema.

"Ahah... asante sana. Ninakuahidi nitakupatia Demba Group kama zawadi," akasema Casmir huku akipiga saluti.

Kendrick pia akapiga saluti.

"Sawa kabisa. Kumbukeni, mambo yote tunayafanya kisiri ili kuwapata hawa jamaa kabla hawajaufikisha mwiba mbali sana kwenye koo zetu. Nina imani tutashinda," Kanali akasema.

"Ndiyo Kanali. Tutashinda," akajibu Kendrick.

"Okay. Sasa mnaweza kwenda. Mtaonyeshwa ofisi zenu ambazo ziko tayari. Karibuni sana," Kanali akawaambia na kuwapigia saluti huku akiwa ameketi.

Wawili hawa wakapiga saluti pia kwa mara nyingine tena, kisha wakatoka kwenye ofisi hiyo.

Kanali Jacob Rweyemamu, akiwa ameweka sura yenye umakini sana baada ya wawili hawa kuondoka, akachukua simu yake na kupigia namba fulani, kisha akaanza kwa kusema, "Hallo... ndiyo... mnaweza kuendelea..."


★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA SITA

★★★★★★★★★★★★★


Meja Casmir pamoja na Kapteni Kendrick walipotoka ofisini humo, Kendrick alikumbuka kwamba kidogo kwenye maongezi yao mule ndani ni kama Casmir alikwepesha mambo kuhusiana na silaha zile kuibiwa. Akaona amuulize ni kwa nini hakumwambia Kanali yale aliyoyafikiria jana.

"Sikuona umuhimu tena. Labda nilifikiria mambo mengi kupita kiasi," akasema Casmir.

"Hapana bwana, ile ilikuwa ni discovery muhimu sana. Hatuwezi kuupuuza uwezekano wa yale yote kuwa kweli. Vipi kama kuna mtu jeshini anawasaidia hawa nyoko group kupata silaha? Tunapaswa kumwambia Kanali kuhusu hilo," akasema Kendrick.

"Lakini ndiyo hivyo Captain, hatujui ni nani hata kama ingekuwa kweli. Vipi kama ni Kanali mwenyewe halafu unamwambia hayo?" Casmir akasema.

"Aaaaa Meja..."

"Nime-assume tu. Namaanisha hatuwezi kuwa na uhakika sana, ndiyo maana inabidi tuchimbe zaidi..."

"Okay nimekuelewa. Lakini najua umerukaruka kwa furaha moyoni kwa sababu sasa unaweza kwenda nyumbani tena... kwa uhakika zaidi..."

"Ahahahah... yeah. Unajua... hii yote bado inanishangaza. Jenerali Pingu huwa... habadiliki-badiliki namna hii. Halafu... Kanali amejuaje kuhusu birthday ya mke wangu?" Casmir akaanza kudadisi.

"Umeona sasa? Umeshaanza kuwaza mbali kama kawaida yako. Hapo utaacha kuwafatilia nyoko group ili ujue ikiwa Kanali anamnyemelea Alice," Kendrick akamtania.

"Ahahahah... siyo hivyo bwana. Imenishangaza, that's all. Yaani..."

"Umefurahi sana, I get that. Kwa hiyo utamficha Alice kuhusu wewe kuwa huku mpaka birthday kama Kanali alivyo-suggest?"

"Hapana. Hapana Kendrick yaani, siwezi kusubiri. Nahitaji kumwambia mke wangu aisee..."

"Ila ngoja. Unajua ukimwambia kwamba uko huku tayari anaweza akakulazimisha uache masuala ya huku ili uende kuonana naye kwanza. Na najua jinsi anavyokuwaga akidekadeka, lazima utasahau na mission ili tu ukale tunda ohooo..."

"Ahahahah... dah! Kiukweli nimemiss sana hizo deko zake. Uko sahihi lakini. Nahitaji kuchagua wakati mzuri."

"Yeah. Mimi pia nitakuwepo. Natamani Margaret angekuja pia," akasema Kendrick.

"Iih! Hivi kumbe bado... huwa unawasiliana na huyo mwanamke wa Ghana? Si uliniambia uliachana na habari zake?" Casmir akauliza.

"Ndiyo, mwanzoni ilikuwa kama hit and run..."

Casmir akacheka.

"Lakini baadae akaja kuniambia kwamba alinipenda sana. Sema... mimi na mambo yangu mengi, na umbali pia kutoka huko aliko toka alivyoondoka... lakini huwa ananiambia hajanisahau na anatamani sana tuwe pamoja... akanifanya nianze kuwaza labda yeye ndiyo ananifaa zaidi, kama wewe na Alice... nikafikiria..."

"Basi, basi... inatosha. Nimeelewa. Umempenda, lakini wewe bado ni Playboy," Casmir akasema.

"Mimi siyo Playboy!" Kendrick akakanusha.

"Ahahahah... sawa. Ila... mambo mengine pembeni kwanza... tunahitaji kwenda kuendelea na mission. Wacha tuone layer zetu mpya hapa..." Casmir akasema.

Kendrick akakubali, kisha wote wakaelekea sehemu ambayo wangepata mtu wa kuwaelekeza mpaka kwenye vyumba vya ofisi zao mpya.


★★★


CHUONI

Ikiwa ni mida ya saa 7 mchana, ukawa ni wakati wa Xander pamoja na rafiki zake kusubiri kipindi kingine cha somo ambalo lingefuata mida ya saa 8. Akiwa ameketi kwenye mabenchi yale pamoja nao kama kawaida, akamwona Isiminzile akiwa amesimama chini ya kivuli cha mti mwembamba tu wa ua fulani pembezoni mwa kuta za uzio wa kuzunguka jengo la chuo. Alikuwa peke yake, akiwatazama yeye na rafiki zake hapo. Benjamin akamtania Mecky kwamba "dogo" bado anam-mind, hivyo ajiandae maana muziki wake angeusikilizia puani. Mecky akasema "dogo" hana lolote huyo na huwa anamkera sana, hivyo kama ni kumwalika hapo ili aje amkarabati vizuri, basi wamwite.

Xander akanyoosha mkono wake kumwelekea Isiminzile na kumwonyesha kwa ishara kuwa aende hapo. Mwanzoni, kijana huyo alionekana kutoamini kwamba Xander alimwita yeye, lakini baada ya Xander kusisitiza, akaanza kwenda walipokuwa. Mecky akamuuliza alikuwa na maana gani kufanya hivyo, naye akamwambia ndiyo alikuwa anamwita ili aone kama atampiga kweli. Akamwonya kuhusu kumtendea kijana wa watu bila heshima, naye Isiminzile akawa amefika.

Bernard, Benjamin, Hussein, Lucas, na Xander, wote walimsalimu kirafiki kijana huyu, naye akawasalimu pia. Xander akamwambia aketi pamoja nao ili wajuane vizuri. Isiminzile alijihisi utofauti sana kwa sababu hiki ni kitu ambacho hakuwa ametarajia kabisa. Marafiki wa Xander wakawa wanamuuliza maswali na kumfanya azungumzie kuhusu mambo aliyojua, nao wakatambua kwamba alikuwa na ujuzi sana.

"Yaani uko course ya Human Resources lakini masuala ya magari na mapikipiki ndo' unajua hivyo?" akauliza Lucas.

"Ndiyo. Ninapenda kusoma mambo mengi kuhusiana na magari... motor vehicles yaani..." akajibu Isiminzile.

"Si ungesomea uinjinia wa magari?" akauliza Benjamin.

"Nilitamani sana ila... haikuwezekana..." akajibu huku anaangalia chini.

Xander akaona abadili mada.

"Okay. Tuambie hapa chuoni ni demu gani unayemkubali kuliko wote," akasema Xander.

Wenzake wakacheka huku wakimwambia Isiminzile aseme. Mwanzoni alikuwa akiona aibu, ila baada ya kusisitizwa sana akafunguka.

"Yupo hivi... mweupe... mrefu mfupi kiasi, ila siyo sana... huwa ni mwislamu anavaaga ushungi..." akawa anawaambia.

"Anaitwa nani?" Hussein akamuuliza.

"Ramla Jabir..." akajibu.

Wote wakaanza kucheka, kasoro Isiminzile. Alikuwa anashangaa kwa nini wanacheka.

"Oya oya kaa ukijua starehe gharama..." Mecky akaanza kutania.

"Ahahah... mtoto Ramla? Unamkubali kinoma eeh?" Bernard akamuuliza Isiminzile.

Isiminzile akaangalia chini tu.

"Dah mwanangu competition hii hapa... kazi kwako..." Lucas akamwambia Xander.

"Ahahah... unampenda Ramla? Si mko wote Human Resources?" Xander akamuuliza Isiminzile.

"Ndiyo... ila yule dada hawezi kutoka na mtu kama mimi..." Isiminzile akasema.

"Kwa nini asitoke na wewe?" Hussein akamuuliza.

"Kwanza ananizidi umri na... anaonekana wa pesa sana halafu..."

"Mmmm wewe... nani kasema? Yule demu anaweza kutoka na yeyote yule. Haangaliagi pesa, demu wa hivyo anaangalia kama unajua show vizuri na swagger... basi. Hupaswi kuwa mnyonge hivyo, yule unakula mbona!" Lucas akamwambia.

"Kweli?" Isiminzile akauliza.

"Kabisaaa!" Bernard akapigia mstari.

Xander alikuwa kimya tu anawaangalia rafiki zake walivyomfanya kijana wa watu aonekane kama mjinga.

"Sasa sikia. Huyo demu atakuja hapa muda siyo mrefu. Akifika tu tunakuunganisha kwake, sawa?" Lucas akamwambia.

Isiminzile akaanza kusema hapana maana alimwogopa.

"Wewe tulia, yule ni rafiki yetu. Tena rafiki wa Xander. Atakuunganisha kwake. Au siyo jembe?" Lucas akazidisha chumvi.

"Haya, mchumba kafika..." Mecky akasema.

Wote wakatazama pembeni na kumwona Ramla akiwa anakuja na rafiki zake wengine wanne. Wawili walikuwa ni wapenzi wa Benjamin na Hussein pia. Xander alihisi kama kuishiwa pozi kwa kuwa bado alikumbuka jinsi Ramla alivyomrushia maneno bila kuwa na uhakika wa madai yake siku ya jana. Lakini bado mtoto alimwelewa sana jamaa, naye hakutaka kumpoteza hata kama angehitaji kumpigia magoti mbele ya wengine. Na hapa alikuwa amekuja kuthibitisha kwamba bado alimpenda sana.

"Ramla huyooo..." Lucas akamsifia alipofika.

Wadada hawa wakasalimiana na washkaji kisha story zikaanza.

"Mnamwona huyu? Huyu ndiyo pedeshee mpya hapa... mpeni respect!" akasema Lucas kwa mabinti.

"Eeh jamani Isiminzile... vipi?" mmoja akamsalimu.

"Safi," Isiminzile akajibu kwa haya.

"Nampendaga huyu kaka, mpole kweli," akasema dada mwingine huku akimshika Isiminzile begani.

"Unaona unavyopendwa?" Lucas akamwambia Isiminzile.

Ramla alikuwa anampa jicho la wiziwizi Xander ili kuona kama bado alikuwa na hasira naye. Alitarajia hata angemwangalia na kutabasamu lakini hakufanya hivyo. Kisha....

"Ramla mtoto mzuri, tuna jambo letu dogo hapa... hapana, ni kubwa sana tunataka kukuambia," akasema Bernard.

"Ropoka," Ramla akasema.

"Tumepata pedeshee mwingine zaidi ya yule mwenye sura ya mbuzi anayekukubali kinoma sana," Lucas akamwambia.

Xander akachekea kwa chini.

"Nani tena?" akauliza Ramla.

Isiminzile alikuwa anataka kukimbia kwa kuwa aliogopa sana, lakini akajitahidi kuzuia hisia zake na kujikakamaza hapo hapo alipokaa.

"Ila mshenga aliyetumwa ni Xander, kwa hiyo yeye ndo' atakwambia kuhusu pedeshee wetu," akasema Benjamin.

Ramla tayari aliweza kukisia maongezi haya yangeelekezwa kwa Isiminzile, lakini hakujali kumhusu; yeye alitaka kuona ikiwa Xander angemsemesha. Tokea walipogombana hawakutumiana ujumbe hata mara moja.

"Xander, mwambie..." Benjamin akasema.

Xander akamwangalia Ramla kwa ufupi, kisha akazungushia mkono wake begani kwa Isiminzile na kusema, "Isiminzile anakupenda sana Ramla. Toka alipojiunga na darasa lenu, hakuna mwanamke yeyote ambaye ametaka kuwa naye ila wewe. Mpe moyo wako."

Rafiki zake wote wakacheka sana. Isiminzile bado hakuelewa kilichowachekesha hasa kilikuwa ni nini, lakini Ramla hangechelewesha kumpatia jibu. Akatoka alipokuwa amesimama na kwenda mpaka alipoketi Xander, kisha akamkalia na kumpiga denda bila aibu yoyote. Wenzake wakaanza kuguna, huku Isiminzile akishangaa sana.

"Mmmm jamani... siyo vizuri hivyo Ramla," akasema rafiki yake.

"Nimeshanasa hii sehemu, sing'oki. Dogo akapambane na hali yake," Ramla akawaambia huku akiwa bado amemshika Xander.

Isiminzile akakaa kwa kutulia tu, akiigiza kwamba hilo lilikuwa ni kawaida. Wengine wakaendelea kuwatania Xander na Ramla kwamba waliyafanya mapenzi yao kuwa ya hadharani sana mpaka ilikera. Kihalisi Xander hakufurahishwa na kitendo ambacho Ramla alifanya, hasa kwa sababu ni kama hamu yote kumwelekea ilimwishia, lakini aliona afanye tu ustaarabu wa kutomwaibisha mbele ya rafiki zake. Benjamin akamweka wazi sasa Isiminzile kuwa Ramla alikuwa mpenzi wa Xander, hivyo walikuwa wakimtania tu, na alipaswa kumwona kama rafiki yake pia.

"Usimkalie muda mrefu, Oprah akija hapa... ehee..." rafiki yake Ramla akamwambia, akimaanisha mwalimu wa nidhamu.

Ramla akasimama tena, zamu hii akiwa nyuma ya Xander huku ameweka mikono yake begani kwa jamaa. Alifanya ionekane ni kama hawakuwa na tatizo lolote kabisa. Isiminzile alijisikia vibaya sana. Wengine wakaendelea na story, lakini yeye akawa kimya tu kwa sababu hawakujua kihalisi kwamba jambo hilo lilimuumiza. Wenyewe walichukulia kuwa limeshasahaulika, ila kichwani kwake Isiminzile likaendelea kuzunguka.

Wakiwa bado wanaendelea na maongezi ya hapa na pale, akafika binti mwingine ambaye alifahamiana nao.

"Xander... teacher wa Com anakuita," akamwambia na hapo hapo kuanza kuondoka.

"Aaaa sasa mbona haraka hivyo... hujaachiwa matumizi nini? Njoo me nikupe," Lucas akawa anamtania huku binti huyo akiondoka.

"Basi Xander kupiga A plus nafikiri ndo' atakuwa CR wa madam V sa'hivi," akasema Benjamin.

"Ngoja nikamsikilize," Xander akasema na kunyanyuka.

Ramla alikuwa anamwangalia kwa matumaini kwamba angemwambia hata jambo fulani dogo, lakini jamaa akaondoka tu kuelekea ofisi za chuo. Wengine hawakujua kuhusu tatizo lao, labda rafiki zake Ramla tu kwa kuwa aliwaambia, hivyo hawakuweza kuhisi kwamba walizinguana. Isiminzile akaendelea kukaa hapo na "rafiki" zake wapya, akijitahidi kuchangia maongezi pia mara kwa mara. Ramla aliketi sehemu ambayo Xander alikuwa hivyo Isiminzile alimwangalia kwa ukaribu, akivutiwa sana na uzuri wake, lakini pia akisikitika moyoni kwamba haingekuwa rahisi kumpata.



Xander hakujua atarajie nini kwenye mwito huu na madam Valentina, ila mapigo yake ya moyo yalikimbia kwa kasi kutokana na kuwa na hamu ya kutaka kujua alichoitiwa. Alijua kilichotokea nyumbani kwa mwanamke huyu usiku wa jana kilimfanya apambane na akili yake mwenyewe na labda kuhisi yuko ndani ya wakati mgumu, hasa kwa sababu kijana alisukuma sana mpaka mambo yote yaliyotokea kutokea. Hivyo alitaka kuona sasa haya yote yangeishia wapi, na kuitwa kwake kukawa mwanzo mzuri kwa kuwa toka alipofika chuoni siku hii hakuwa ameonana naye.

Alipofika ofisini kwa madam Valentina, Xander alikuta mlango ukiwa wazi kiasi na kumwona madam akiwa amesimama usawa wa kabati lenye mafaili; akionekana kuangalia jambo fulani. Akaugonga mlango kidogo, naye Valentina akageuka na kumwona akiwa anachungulia. Akamwambia aingie na kuufunga mlango, naye Xander akatii. Ofisi yake ilikuwa pana kiasi yenye madirisha makubwa yaliyowekwa mapazia marefu sana, nayo ilipendeza kwa mwonekano safi na mpangilio mzuri wa vitu.

Siku ya leo Valentina alivalia gauni ya rangi ya samawati (blue) iliyoishia magotini, ambayo iliubana mwili wake kiasi. Nywele zake za mawimbi-mawimbi alikuwa amezibana kwa nyuma, naye Xander alipenda jinsi mkufu wa Valentina ulivyong'aa na kuipendezesha shingo yake. Aliposogea karibu na alipokuwa amesimama, akatambua kwamba Valentina hakuwa amevaa sidiria ndani, kwa kuwa sehemu za kifua chake zilijichora kwa mbali juu ya nguo aliyovaa.

"Madam V... Nimekuja," Xander akasema.

Valentina alikuwa anamwangalia sana machoni, kisha akashusha pumzi kama mtu aliyevunjika moyo.

"Alexander..."

"Niite tu Xander," akamkatisha.

"Sawa," Valentina akajibu na kuangalia chini.

"Vipi mguu?" Xander akauliza.

"Niko sawa," Valentina akajibu.

"Umependeza..."

"Asante."

"Huo mkufu ni dhahabu?" Xander akauliza.

"Ndiyo."

"Ni mzuri, umekupendezea..."

Valentina akaona ni kama Xander alikuwa hataki asikie kile alichomwitia, hivyo akaona akatishe maongezi hayo ambayo hayakuwa na mwelekeo wowote mzuri.

"Okay, inatosha. Nashukuru. Nimekuita ili tuongee kuhusiana na jambo la muhimu. Wewe Xander... ni kijana mzuri na... una akili, ni mwerevu, una kipaji kizuri cha kuandika..."

"Na ni handsome... ila nilikuwa tu nakazia maana tayari ulisema me mzuri," Xander akatania.

"Ni sawa. Jana... kilichotokea kati yetu... ni kitu ambacho kimeniweka kwenye wakati mgumu sana. Mambo hayakupaswa kuwa vile..."

"Lakini ulifurahia sana..."

"Nisikilize usinikatishe."

Xander akatulia baada ya kuona jinsi Valentina alivyokuwa "serious."

"Kuna mipaka. Mipaka ambayo haipaswi kuvukwa. Jana ilikuwa too much. Mimi na wewe hatuna connection yoyote zaidi tu ya uhusiano wetu kama mwalimu na mwanafunzi. Nataka ibaki kuwa hivyo... kwa sababu singependa uingie kwenye shida yoyote kisa mimi. Unanielewa?" Valentina akasema.

"Ndiyo..." Xander akajibu kiupole.

"Ni vizuri. Hii siyo rahisi kwangu. Kitu tulichofanya... mambo yote... hata kama ni wazazi... au girlfriend wako akijua hangefurahi. Na pia mimi ni mkubwa sana kwako... nataka tu..."

Xander akamkatisha kwa kumsogelea karibu zaidi. Valentina akabaki kumwangalia kimshangao.

"Hata mimi siyo rahisi kwangu. Lakini nitafanyaje? I can't help it. I'm into you..." akasema kwa sauti yenye kubembeleza.

"Xander!" Valentina akashangaa.

"Ni kweli madam. Nimekuelewa sana yaani. Haitakuwa rahisi kwangu kusahau kila kitu; macho yako, pumzi zako, miguno yako, ngozi yako laini... kila mguso wako usiku wa jana... busu zako..."

Xander alikuwa anaongea maneno haya yenye kuamsha hisia huku akitembeza vidole vyake kwenye viganja vya Valentina. Ni kama yote ambayo mwanamke huyu aliyasema hakuwa ameyasikia kabisa. Valentina alisisimka sana, huku Xander akimsogelea mdomoni.

"Xander unafanya nini? Hapa ni ofisi... chuoni," Valentina akasema kwa sauti ya chini.

"Najua ulifurahia sana jana. Nataka sana kukuona ukifurahia vile tena... mbali na stress zako zote..." Xander akamwambia.

Valentina akarudi nyuma kidogo, lakini Xander akamsogelea tena na kuvishika viganja vyake.

"Nataka nikufanye uzisahau. Mimi ni mdogo ndiyo, lakini kukupa unachostahili ninaweza..." Xander akasema kwa kujiamini.

Alianza kupandisha viganja vyake mpaka juu ya mikono ya Valentina, huku mwanamke huyu akimwangalia tu, kisha akaifata midomo yake na kumbusu. Valentina aliangalia usawa wa mlango kwa uharaka, akihofia kuna mtu angeweza kuingia, lakini Xander akataka kumsahaulisha hilo na kuushika uso wake ili ampe denda kiusahihi. Sasa mwanamke huyu akalegea zaidi baada ya Xander kuanza kumbusu kimahaba. Ilikuwa busu nzito iliyomfanya afumbe mpaka na macho, akisahau kabisa yote aliyokuwa amemwambia muda mfupi nyuma.

Wawili hawa wakaendelea kudendeshana huku mikono yake Xander ikimbana zaidi madam wake kwenye mwili wake. Valentina aliweza kuhisi jinsi Xander alivyopandisha hisia, na ijapokuwa alitaka kumwambia waache, hamu ikamzidia nguvu na kumruhusu kijana huyu aendelee kumpa busu hiyo; wakisahau kabisa kuwa wako ofisini. Kisha mara ghafla Xander akajitoa kwenye mdomo wa Valentina na upesi kuyapiga mafaili yaliyokuwa mezani kwa mkono wake, kitu kilichofanya yaangukie chini na kuzagaa.

Xander akainama kuanza kuyaokota. Valentina alishangazwa na jambo hilo, na hapo hapo mlango wa kuingilia ofisini kwake ukafunguliwa. Akashtuka kiasi kwa kutokutarajia hilo, na aliyeingia hakuwa mwingine ila mkuu wa chuo mwenyewe, Mr. Daniel. Akamtazama Valentina kimaswali na kumwangalia Xander akiwa anaokota makaratasi hapo chini, bila kumtambua kwa sababu alimpa mgongo.

"Valentina vipi?" Daniel akamsalimu.

"Aa... safi tu. Nambie..." Valentina akaficha wasiwasi wake.

"Huyu vipi? Wewe unafanya nini?" Daniel akauliza.

Mpaka kufikia sasa Xander hakuwa amemgeukia kwa sababu alificha mwonekano wa suruali yake kwa mbele iliyokuwa imetuna haswa na kujichora. Hivyo, akageuza shingo na kumwangalia mkuu machoni.

"Ah... Alexander kumbe! Umefanyaje?" Daniel akauliza.

"Nimemwangushia madam mafaili ndo' nayaokota hapa," Xander akajibu.

Daniel akaingia mpaka ndani na kusimama karibu na Valentina. Akaanza kuongea naye kuhusu masuala fulani ya kitaaluma, huku Xander akiendelea kujiokotelesha makaratasi taratibu ili msuli wake usinyae. Daniel akamaliza kuongea na Valentina na kuwaacha humo. Alimjua vizuri Xander hasa kwa kuwa kijana alichezea timu yao ya chuo, na pia Daniel alikuwa anamfukuzia pacha wake. Hivyo hakuwa na noma naye hata kidogo. Baada ya kutoka, Xander akawa amemaliza kuyakusanya makaratasi na kusimama.

"Sorry! Nilifanya hivi ili..."

"Usijali nimeelewa. Yaweke tu hapo," Valentina akamkatisha.

Xander akayaweka mezani, kisha alipomgeukia akamshika kiunoni na moja kwa moja kumpiga busu mdomoni.

"Xander..." Valentina akajitoa kwenye mikono yake.

"Hiyo ilikuwa tamu madam V. Nitaipata tena..." Xander akamwambia kichokozi.

"Lakini wewe!" Valentina akasema.

Xander akachekea tu kwa chini na kuanza kuelekea mlangoni. Kisha akamgeukia alipokuwa anataka kutoka nje na kumwonyesha kwa ishara ya vidole kuwa angemtafuta kwa simu, na baada ya hapo akatoka. Valentina akabaki hapo akimtafakari kijana wake huyo machachari. Hakuweza kujizuia kupendezwa sana na jinsi Xander alivyomwonyesha ujasiri wa mapenzi na kumfanya aonekane kama mtu aliyemzidi umri. Lakini bado kuna sehemu fulani ya moyo wake ambayo ilimwambia hakupaswa kujiachia sana kwake; ijapokuwa tayari alionyesha kushindwa dakika chache nyuma.

Xander yeye akatoka hapo akijihisi kama mshindi mkubwa mno. Alijisifu sana moyoni na kujiahidi kuwa ni lazima angemlegeza zaidi madam wake mpaka anyong'onyee kwenye penzi lake ambalo alijua alilipenda na alilitaka tena. Hakutaka fikira za Ramla wala nini zimwondolee uhondo huu mpya ambao aliufurahia sana moyoni. Akaelekea zake darasani ili kusubiri kipindi.


★★★


Baada ya kipindi kumalizika, Xander akatoka darasani pamoja na Lucas na Bernard na kwenda usawa wa kingo za chuma zilizozungukia ghorofa ya juu waliyokuwepo. Wawili hawa wakamwambia walitaka kwenda kupata msosi pamoja kwa kuwa rafiki zao wengine walitangulia, lakini Xander akasema waende tu kwa kuwa yeye hakuhisi njaa bado. Wakamshangaa kiasi kwa sababu hakuwa amekula kutokea asubuhi, na baada ya utani utani kidogo, wakawa wamemwacha peke yake.

Akawa anaangalia kwenye simu yake mambo kadhaa, zikiwemo jumbe za Ramla za kuomba samahani kwa jinsi alivyomfanyia jana. Lakini Xander hakujibu hata moja, naye akaamua kumtumia ujumbe madam Valentina. Alimuuliza kama alikuwa ameshakula, na kwa kushangaza, Valentina akajibu kwa kusema bado. Alitarajia labda hata asingejibiwa, hivyo jambo hilo likamfurahisha. Akaanza kuingiza maneno mafupi ya hapa na pale, na muda si muda, wawili hawa wakawa wana-chat.

Xander alifurahi sana, naye alijitahidi kumtumia meseji ambazo alitumaini zingemfanya Valentina atabasamu. Jambo hili lilianza kuonekana kuwa zuri sana kati yao ijapokuwa mwanamke alionyesha kama hataki mwanzoni, naye Xander akataka lisonge mbele hata zaidi. Wakati akiwa anasubiri SMS yake moja ijibiwe, akafika Isiminzile hapo na kumsalimu Xander. Alikuwa ameshikilia glasi mbili mikononi mwake.

"Bado mna vipindi?" Xander akamuuliza.

"Hapana. Wengi wa HR wameshaondoka," akasema Isiminzile.

"Na wewe?"

"Ah... me nilibaki kunywa soda kidogo. Nimekuona hapa nikaona nikuletee na wewe kidogo," akasema Isiminzile.

Akampatia glasi moja, iliyokuwa na soda kidogo ya Fanta Orange. Xander akatabasamu na kuipokea, akijua ni jinsi gani kijana huyu alivyokuwa mwenye kujishusha na kuhitaji marafiki.

"Asante," akasema Xander na kuinywa kidogo.

"Unamsubiri nani?" Isiminzile akamuuliza.

"Simsubiri mtu. Nilikuwa nazingua tu hapa," Xander akajibu huku akituma ujumbe kwa Valentina.

"Kwa hiyo... ngoja niulize... hivi... Ramla huwa anapenda mambo gani?" Isiminzile akauliza.

Lakini Xander hakumtilia maanani sana. Alikuwa ametoka kutuma ujumbe kwa Valentina akimwambia kwamba alisahau kitu fulani muhimu sana kwake usiku wa jana, hivyo alitaka kukichukua. Valentina akawa ameuliza ni nini ili amletee kesho, lakini Xander akasema ni boxer yake; kiuchokozi tu ijapokuwa ilikuwa kweli. Valentina akajibu kwamba kwa kitu kama hicho, angepaswa kukifata yeye mwenyewe, na jambo hili likamfanya Xander afurahi sana. Hakujua ni kwa nini lakini ilionekana ni kama Valentina alikuwa anampa mwaliko usio wa moja kwa moja. Akabaki anatabasamu tu.

"Eti Xander... Ramla huwa anapenda mambo gani? Kama movie labda... muziki... au mkiwaga wote huwa... huwa..." Isiminzile akawa anaendelea kumsemesha.

"Kwa nini? Uliongea naye muda ule? Mmepanga date?" Xander akauliza bila kumtazama.

"Aa... hapana... nilikuwa tu..."

Kabla Isiminzile hajamaliza kuongea, Xander akaachia tabasamu pana sana huku akiwa anaangalia simu yake. Valentina alikuwa amemwambia kwamba, muda siyo mrefu angeondoka, hivyo kama alitaka kwenda akaichukue boxer yake, basi aambatane naye kwenye gari lake. Hii ilikuwa ni sehemu ya ushindi kwa Xander ambao haukuwa umekamilika bado. Alianza kuona ni kama madam Valentina amemwelewa pia, na furaha aliyohisi ikapitiliza sana.

Kwa kuingiwa na hamu kubwa, akainywa soda yote haraka na kuiweka glasi pembeni, kisha akamwangalia Isiminzile.

"Oy... pole mwanangu sitaweza kuongea, kuna sehemu nawahi mara moja. Asante kwa..."

Kabla hajamaliza kuongea, akashtushwa na sauti ya Sandra ikimwita.

"Alexander!"

Yeye pamoja na Isiminzile wakatazama upande wa nyuma yake na kumwona Sandra akiwa pamoja na Sophia, huku akija kwa njia iliyoonyesha amekasirika. Xander akiwa anajua vizuri alichokifanya, akaigiza kujificha nyuma ya Isiminzile ili dada yake asimpige. Sophia alikuwa anacheka tu. Sandra akafika hapo akiwa amekunja sura na kutaka kumshika Xander, lakini jamaa akawa anamkwepa kwa kuizungusha miili yake yeye na Isiminzile.

"Umefanya ujinga gani huu?" Sandra akamwambia.

"Mdoli sikiliza..." Xander akawa anasema huku akicheka.

"Nilikwambia usiniite tena lile jina... Xander nitakukaanga uwe mweusi!" Sandra akalalamika.

"Kwani amefanyaje jamani?" Sophia akauliza.

"Me mwenyewe nashangaa!" Xander akasema.

"Kapost... amepost picha yetu ya wakati tuna miaka 10. Kaipost FB, hii hapa... eti limeandika Throw back nikiwa na cute baby Sandirito!" Sandra akalalamika.

Sophia akacheka.

"Ahahahah... sasa shida iko wapi? Kukuita cute baby ni vibaya?" Xander akauliza.

"Nitakutafuna Xander, ifute! Nimekwambia usiniite hilo lijina tena. Yaani sijui ukoje!" Sandra akasema kwa kuudhika.

"Sandirito!" Sophia akasema.

"Na we usiniite hivyo!" Sandra akasema na kufanya wote wacheke.

"Haya punguza kuni basi, moto mkali mno. Ntaifuta, sawa?" Xander akamwambia.

"Ole wako uache. Nakupa saa moja, la sivyo nami nita... nitajua la kufanya," Sandra akasema.

Kisha kwa jazba, akaichukua glasi ya soda aliyoshikilia Isiminzile na kuinywa yote kwa kishindo, halafu akamrudishia Isiminzile glasi kwa nguvu.

"Iiiih jamani! Sasa soda ya mwenzio imekukosea nini?" Xander akasema.

Sandra akasonya kidogo na kuondoka hapo upesi. Sophia na Xander wakabaki wanacheka.

"Hilo jina umelitoa wapi?" Sophia akauliza.

"Ahahahah... kuna animation fulani inaitwa Condorito, inachekesha sana. Ndiyo nika-mend jina lake kama hivyo. Sasa... hapendi kwa sababu Condorito ni kituko kwo' anaona ni kama namharibia jina..." Xander akaeleza baada ya kumwachia Isiminzile.

"Mh... haya bwana. Nyie wawili mnafurahisha sana," Sophia akasema.

"Vipi mama?" Xander akauliza.

"Anaendelea vizuri Xander. Wameshaanza matibabu na habari ni nzuri," Sophia akasema kwa furaha.

"Sasa je, nilikwambia, she's a survivor. Utamwambia namsalimia," Xander akamwambia.

"Ahahah... asante mwaya. Unaenda home sa'hivi?" Sophia akauliza.

"Hapana, kuna sehemu napita kwanza. Halafu... nahitaji kuwahi. Wewe wapi?"

"Me naingia bweni kulala. Sandra atakuwa ameshaondoka hivyo maana hatuna zoezi leo."

"Okay. Baadae eti?"

"Poa."

"Oa... Simi, asante. Kesho," Xander akamwambia.

Isiminzile hakutoa jibu bali akawa amemtazama tu. Xander akaondoka upesi na kuwaacha wawili hawa hapo.

"Simi? Unaitwa Simi?" Sophia akamuuliza.

Lakini Isiminzile akawa anamtazama tu kama vile mtu aliyepigwa na bumbuazi. Sophia akamwona kama mtu wa ajabu-ajabu tu na kuamua kujiondokea hapo. Isiminzile akabaki amesimama, huku akiwa ameshikilia glasi yake mkononi, naye akawa anapumua kwa njia iliyoonyesha hofu kubwa.


JE, UNADHANI NI NINI AMBACHO ISIMINZILE AMEFANYA?

★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Mahaba, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

Rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA SABA

★★★★★★★★★★★★★


Baada ya kuwaacha Isiminzile na Sophia, Xander alielekea mpaka walipokuwa Lucas na Bernard na kuwakuta wanapata msosi kwenye mgahawa mmoja maeneo hayo. Wakamkaribisha na kumwambia na yeye achukue chakula, lakini Xander akakataa na kumwambia Lucas akimaliza aichukue pikipiki yake kwa muda fulani, kisha baadae ataipeleka nyumbani kwao. Lucas akauliza kwani yeye alikuwa anaenda wapi, naye Xander akasema ni sehemu ambayo hangehitaji pikipiki, hivyo atumie kwa muda kisha baadae aipeleke kwao; kwa kuwa alipajua. Akampatia funguo, naye akawaacha wawili hao wakiendelea na makamuzi.

Kutoka maeneo hayo ya chuo, Xander alichukua usafiri na kuelekea maeneo ya kati zaidi ya jiji, na hapo akaingia kwenye mgahawa fulani wa starehe na kuagiza kinywaji kimoja tu. Kisha akamtumia ujumbe Valentina kumwambia alikuwa sehemu gani, hivyo akitoka tu huko chuoni ampitie hapo ili wote waende kwake "kuichukua boxer." Alikuwa anajichekea mwenyewe tu huku akiwa na hamu sana ya kutaka kufanya jambo lingine kubwa siku hii. Baada ya kama dakika 10 hivi, Valentina akajibu ujumbe huo akisema sawa; alikuwa anamalizia mambo fulani kisha ndiyo angempitia.

Xander akahisi raha sana kwa kuwa ilionekana ni kama wanapanga kutoka "out" kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Alijiambia akilini mwake kwamba huyu mwanamke anataka muziki mnene, na yeye angempatia mpaka besi ya mwisho leo. Aliendelea kukaa hapo kwa dakika kadhaa, kisha simu yake ikaita. Mpigaji alikuwa ni Valentina, naye akamtaarifu kwamba alifika nje hapo, hivyo aende upesi. Xander akaachia tabasamu la kiburi na kuelekea nje, na baada ya kuliona gari la madam, akalifuata na kuingia upande wa mbele pembeni ya mwanamke huyu.

Valentina alikuwa anamwangalia kama vile anasubiri Xander aseme jambo fulani, lakini Xander akaonyesha kama anataka kutabasamu ila akajikaza na kuangalia mbele tu. Madam akaanzisha mwendo tena kuanza kuelekea nyumbani sasa. Baada ya kama dakika mbili za ukimya, Xander akaona amsemeshe.

"Hivi ile nyama ya jana bado ipo?" akauliza.

"Nyama gani?" Valentina akauliza pia.

"Niliacha... jana nilinunua nyama, nikakuachia nyum..."

"Ipo. Utaikuta kama na yenyewe unataka kuichukua," Valentina akamkatisha.

Xander akajitahidi kubana tabasamu lake, kwa kuwa aliona Valentina alikuwa anajifanya amekaza. Valentina akamwangalia na kukuta anamtazama kwa njia ya tabasamu.

"Nini?" akamuuliza.

"Nothing," Xander akajibu.

"Funguo yangu unayo?"

"Yep."

"Iweke hapo."

Xander akaiweka huku anacheka.

"Unacheka nini?"

"Nothing."

"Unaniona kama kituko eti?"

"Never. Nakuona kama mtu special sana kwangu."

"Kama girlfriend wako?"

"Ahahah... anakufanya uone wivu?"

"Nini?"

"Niambie kama anakukera. Tutasaidiana kuchimba shimo. Hatasikika tena," Xander akatania.

Valentina akacheka kidogo.

"Mimi siyo mtu wa kuona wivu," Valentina akasema.

"Mmmm kweli?"

"Sasa mimi nimwonee wivu Ramla msichana mdogo kweli nitakuwa na akili?"

"Inawezekana. Sikumbuki kukuambia jina la girlfriend wangu, na hata kama ulituona pamoja, sikuwahi kukwambia huyo ndiyo girlfriend wangu... ikimaanisha umefanya utafiti..."

"Hakuna haja ya utafiti, nyie ni... wanafunzi wa darasa ninalofundisha, kwa nini nisimjue? Na... kila mtu anajua hilo... kuhusu wewe na yeye..."

"Kumbe? Kwa hiyo... unasema kwamba kwa kuwa nina girlfriend, siwezi kukuona wewe kuwa special?"

"Ah me sijui bwana. Naomba tusiongelee hayo..."

"Lakini we si ndiyo umeanza kumtaja..."

"Mimi ni mtu mzima Alexander. Nina experience na mambo mengi, hivi siyo vitu vya kunichanganya. Na nilikuweka wazi kwamba kilichotokea kati yetu ilikuwa kimakosa. Nilikuwa nimelewa. Full stop. Tunaenda so ukachukue nguo yako, then... uende nyumbani," Valentina akasema bila kumwangalia.

"Kumbe... kumbe una experience na mambo mengi eeh?" Xander akamwambia kiutani.

Valentina akamtazama kimaswali.

"Yaani katika yote niliyokwambia, umesikia hilo tu?"

"Ahahah... ndiyo la muhimu kwangu. Nataka nijionee hayo mambo mengi," Xander akasema kiutongozi.

"No. Haiwezekani..."

"Kwa nini?"

"Kwa sababu Alexander, wewe ni... mimi... yaani hata sijui ni kwa nini nataka kujielezea kwako!"

"Kwa sababu unataka... full stop."

Valentina akamwangalia machoni sana, naye Xander akatabasamu kwa mbali. Kisha madam akaangalia mbele tu na kubaki kimya.

"Ninakuelewa sana madam V. Najua hatujayaanza mambo haya sehemu nzuri, lakini nataka mwisho wake uwe. Umenivutia sana madam... kila time nakuwaza tu... it's such a good feeling..."

"Alexander acha... acha tafadhali..."

"Kwa nini? Nakufanya ujihisi dhaifu? Nakufanya... uhisi raha ambayo umekuwa ukijaribu kuikimbia kwa muda mrefu eti? Hakuna haja ya kuikimbia madam V... nifungulie mlango wako niingie..."

"Ahah... unafaa kuwa mtunga mashairi. Hizo swagger hazitanikamata lakini..."

"Siyo swagger... ni ukweli. Ulikuwa umeufunga mlango wako wa kihisia kwa sababu... unaogopa kuumia. Lakini madam V... maumivu ni sehemu ya maisha, na maisha siyo fair kwa kila mtu. Kwa hiyo usijizuie kupenda kwa sababu unaogopa... la sivyo unaweza hata kulipuka..."

"Kulipuka na nini?"

"Si hivyo unavyoyafungia mahisia ndani? Yakijaa sana mwisho wa siku puuf! Watu wanakuja kuokota vipisi vipisi... ila me ntakimendea kimoja tu... kile kipisi..."

Valentina akajikaza asitabasamu kwa kuwa Xander alimtania kiuchokozi sana. Sasa hakuweza kujizuia kufurahishwa na kijana huyu, lakini bado akaona asimwachie sana acheze na akili yake.

Wakawa wamefika nje ya nyumba yake hatimaye. Bila kuambiwa, Xander akachukua ile funguo na kushuka, akielekea getini kufungua. Akalifungua lote na kuanza kumwonyesha Valentina ishara kwa kiganja chake kuwa aliingize gari ndani polepole; kama anamwita. Valentina akatabasamu kidogo huku anatikisa kichwa chake kwa kufurahishwa na vituko hivi, naye akaliingiza gari ndani.

Baada ya Xander kulifunga geti, akaelekea usawa wa gari na kusimama, lakini akashangaa kwa kuwa Valentina hakushuka. Akaona achungulie kupitia kioo na kumwona akiwa ameweka simu sikioni, hivyo akajua alikuwa anaongea na mtu. Wazo la kwamba huenda alikuwa labda anazungumza na askari aje kumkamata likamwingia, naye akatabasamu kwa sababu aliliona kuwa wazo la kipuuzi. Lakini akaufungua mlango wa gari na kuketi ndani yake tena, ili amwangalie madam wake akiongea.

"... na ni sawa kwa sababu itakuwa Jumamosi, mipango yote imekamilika tunasubiria tu tamko la TUSA... ndiyo... eeh ndiyo, bado ila.. wako tayari kwa hiyo we piga tiki tu... Asante sana kwa msaada wako Millie, unastahili lunch ya nguvu kutoka kwangu mpenzi... ahahahah...."

Xander alikuwa anamtazama tu kwa kuvutiwa na sura yake alipocheka. Akaamua kutumia nafasi hii kumchokoza ili aone angeitikia vipi. Valentina akiwa bado anaongea na "Millie," Xander akatumia kiganja chake kuanza kuzichezea nywele za kichwa cha madam. Kisha akaanza kutembeza vidole vyake kutokea begani mpaka katikati ya mkono wake, huku akimwangalia. Valentina hakumtazama, lakini Xander aliona wazi kwamba alihisi vyema kile alichofanya, ila akakaza tu, akionyesha kama hajali.

Baada ya kukata simu, Valentina akataka kufungua mlango wa gari ili atoke, lakini Xander akauzuia kwa kuurudisha ufunge haraka. Hii ilifanya ainamie kumwelekea Valentina alipounyoosha mkono ili kufanya hivyo, kwa hiyo akawa amemkaribia zaidi usoni. Valentina hakumtazama, ila akaweka uso ulioonyesha dhahiri kwamba alikerwa na jambo hilo.

"Unafanya nini?" Valentina akauliza bila kumwangalia.

"Taking a moment to mesmerize your beauty (nachukua muda mfupi kuutathmini uzuri wako)," Xander akamwambia kwa sauti ya chini.

"Umemaliza?" Valentina akauliza.

"Bado," Xander akamwambia.

Kisha akaisogelea sehemu ya shingo yake na kuibusu kidogo. Valentina akamwangalia kwa njia iliyoonyesha kama hakupendezwa na hilo. Sasa midomo yao ikawa karibu zaidi, naye Xander akatabasamu kwa mbali.

"Unataka kunichezea Alexander?" Valentina akauliza kwa hisia.

Xander akawa makini kidogo.

"Hapana madam V. Hapana. Ninavutiwa nawe ukweli. Sina... sina mambo mengi... au vitu vingi navyojua kama wewe... lakini hii ndiyo njia yangu ya kukuonyesha jinsi navyoku-feel... Siwezi kukuchezea... siwezi," Xander akamwambia kwa kubembeleza.

Valentina akatazama mbele na kusema, "Hivyo ndivyo nyie husema. Lakini mkishapata mnachotaka... ni kama tu inavyokuwa kwa Ramla, si ndiyo?"

"Achana na habari za Ramla madam V. Niangalie mimi... sisi," akasema Xander.

Valentina akatoa tabasamu la kuguna, kisha akataka kufungua tena mlango, lakini Xander akauzuia kwa mara nyingine, kisha akaanza kuibusu shingo yake. Valentina akawa kama anamsukuma huku akisema aache, lakini Xander akaendelea. Akajaribu kumzuia kwa nguvu lakini kijana akamshinda na kumbananiza kwenye sehemu hiyo ya mlango, akiibusu kimahaba sana shingo yake. Valentina sasa akawa akipumua kwa nguvu sana.

"...Alexander... acha... stop... don't... ohh God..."

"Don't fight it... don't fight it... let yourself go... let it go..." Xander akamwambia kwa kunong'oneza.

Aliendelea kumbusu sehemu hiyo ya shingo huku amembana kwa kutumia nguvu kiasi, kisha akapandisha mpaka mdomoni mwake na kuanza kuibusu. Valentina hakuweza kujizuia kurudisha busu hii pia kwa sababu hisia kali kumwelekea kijana huyu zilikuwa zimempanda, na ni kama alifurahia sana njia hii ya kupatiwa mapenzi.

Xander alitoka mdomoni kwa madam wake na kushuka tena shingoni, naye taratibu akaanza kumpatia mwanamke huyu mapenzi ndani ya gari lake. Kijana akaisawazisha miili yao vizuri ili Valentina apitishe mguu wake mmoja upande mwingine wa siti, yaani awe katikati ya jamaa. Mambo haya yote Valentina aliyaruhusu kabisa, ikionyesha ni kitu alichokuwa anataka kama Xander alivyomwambia.

Wawili hawa wakaendelea kuonyeshana upendo wao kwa dakika kadhaa ndani ya gari hilo. Valentina akamshangaza Xander kiasi baada ya yeye kuonyesha alitaka mchezo huu uendelee. Tabasamu la furaha likaonekana mdomoni mwa Xander, naye akaendelea kumpa raha mwanamke wake.

"Te amo, cariño..." Xander akanong'oneza sikioni kwa madam.

Dakika chache baadae Xander akajiachia kwa kuhisi mridhiko wa mwanzo. Valentina alikuwa amemshikilia kwa njia ya kumkumbatia huku akipumua kilegevu, kisha taratibu akajivuta na kumtazama usoni. Xander alikuwa anamwangalia kwa hisia sana, kisha akalishika shavu lake na kuanza kuchezea nywele nyuma ya shingo yake.

"Nina-note hili. Zamu hii haujalewa," Xander akasema kiutani.

"Hivi ninafanya nini?" Valentina akauliza kwa sauti ya chini.

"Unanipa utamu," Xander akamwambia.

Valentina akacheka kwa sauti ya chini na kulaza paji lake la uso shingoni kwa Xander. Xander akatabasamu kwa furaha pia.

"Sijui ni kwa nini unanifanya naishiwa nguvu," akasema Valentina kwa sauti yenye deko.

"Na bado. Nataka nikumalize nguvu zote kabisa," akasema Xander.

Valentina akanyanyua uso wake na kumwangalia machoni.

"Unapenda kujisifu sana," akamwambia.

"Hiyo ni lazima. Inafurahisha sana mwanaume akijua mwanamke wake anafurahia kile anachopewa," Xander akasema.

"Mhm... mwanamke wako? Vipi kuhusu Ramla?"

"Ramla... nitaongea naye. Nimekuwa nikijitahidi ku-keep up na mambo yake mengi yenye kukwaza, lakini, sa'hivi itabidi ni..."

"Alexander sisemi umwache... kwa sababu yangu. Haujui ni jinsi gani ataumia," Valentina akamwambia.

"Oh no! Sisemi kwamba ni kwa sababu hii tu. Kwa muda mrefu nimekuwa nikitaka kufanya hivyo ila basi tu kwa sababu nilitaka kutulia na mtu mmoja. Lakini kwa alichokifanya juzi..."

"Kwani alifanya nini?"

"Alinizingua. Alidai nina-cheat na rafiki ya dada yangu kwa kuwa aliniona naye tu kwenye pikipiki. Wivu kwenye mahusiano ni kawaida lakini yeye anaenda mbali sana kwenye kulalamika... hataki kusikiliza sababu, anajali anachofikiria yeye tu. Hii siyo mara ya kwanza ananitendea kwa njia ya dharau, anafanya iwe kama nimemuoa kumbe ni girlfriend tu," Xander akaeleza.

"Anaonyesha anakupenda sana..."

"Hata kama. Tume-date karibia miaka miwili, anapaswa kukua, siyo kila kitu abembelezwe, anyenyekewe... nimejitahidi sana ila sasa hivi I can't... nataka kuwa na wewe tu," Xander akamwambia huku anapapasa kiuno chake.

"Na mimi najua utafika huo wakati kama ilivyo kwa..."

"Usiwaze hayo madam V, furahia tu wakati huu. Hatujui kesho itakuwaje," Xander akamwambia na kuliminya kalio lake.

Valentina akavuta pumzi na kusema, "Alexander..."

"No. Mimi kwako siyo Alexander tena. Niite Xander mpenzi..." Xander akasema huku akimkonyeza.

Valentina akatabasamu na kuuliza, "Yale maneno... uliyoniambia... yarudie tena..."

"Te amo, cariño," Xander akasema.

"Maana yake?"

"I love you, darling," Xander akajibu.

Valentina akatabasamu, kisha Xander akaanza kumnyonya ulimi kimahaba kwa mara nyingine tena. Wakati huu Valentina pia alimwonyesha kwamba alijua kutoa penzi la mdomo kwa kuirudisha denda hii vyema.

"Vipi tukienda ndani?" Valentina akauliza katikati ya busu yao.

"Wazo zuri," Xander akajibu.

Wakapeana busu fupi, kisha wakaanza kujisawazisha ili watoke nje ya gari. Xander alipandisha suruali yake, naye Valentina akalivaa vizuri gauni lake kisha wote wakatoka na kuanza kuelekea ndani. Walikuwa wakitazamana kihisia sana, naye Xander akaubana mwili wa mwanamke huyu kwake huku wakitembea pamoja. Giza lilikuwa linaanza kuingia kwa mbali, saa moja ikikaribia.

Walifika ndani ya nyumba na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha madam na kuendelea na penzi lao. Wakati Xander alipokuwa akiendelea na kazi yake, alihisi mjio wake ukitoka, naye alipokuwa ameanza kujivuta ili ajitoe kwa Valentina, Valentina akamng'ang'ania ili kuzuia hilo. Ikiwa imekuja kwa njia ya sintofahamu, Xander akajiachia ndani ya Valentina.

Xander akatulia kidogo na kuendelea kumlalia kwa juu, huku Valentina akipumua kichovu na kupapasa mgongo wa mpenzi wake mpya.

"Madam V... nafikiri nime... nime...." Xander akawa anaongelea shingoni kwa Valentina.

"Usijali. Kuna dawa nitakunywa," Valentina akamtuliza.

"Ahah... wewe ni mtamu sana madam V..."

"Mhm... wewe pia..."

"Ahahah... asante kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya maisha yako..."

"No. Mimi ndo' nikushukuru. Sijataka kuwa na mwanaume kwa sababu... kama ulivyosema... niliogopa. Ila sasa ngoja nijionee safari yetu itakavyokuwa..."

"Asante madam V..."

"Karibu. Na mimi kwako kuanzia sasa siyo madam V tena... niite Valentina..."

Xander akatabasamu na kumbusu mdomoni, kisha shingoni, halafu akabusu na kifua chake kiutundu. Valentina akacheka kidogo.

"Nahisi njaa..." Xander akamwambia.

"Oh... hukula?"

Xander akatikisa kichwa kukanusha.

"Basi wacha nika-fix kitu, sawa?" Valentina akasema.

"Sawa... Valentina," Xander akamwambia.

Wakapiga busu laini tena, kisha Valentina akaingia bafuni kujimwagia maji kidogo. Baada ya kutoka akaelekea jikoni akimwambia Xander amfuate baada ya yeye kujimwagia pia.

Usiku ukawa umeingia sasa kufikia mida ya saa 2, na mvua ndogo ikaanza kunyesha. Xander na Valentina walikula pamoja huku wakiongea mambo yenye kufurahisha. Xander akamwelezea pia kuhusu maisha yake; kazi za mama na baba yake, ukaribu wake na Sandra, mdogo wake wa kike Azra, na hali walizopitia kama familia. Alimwambia jinsi alivyovunjwa moyo na baba yake, lakini hakumchukia, bali alitaka tu kuwa pamoja naye zaidi kama ilivyokuwa zamani. Valentina akamtia moyo kwamba bila shaka mambo yangekuwa sawa siku moja kuhusiana na hilo.

Kwenye mida ya saa 3 baada ya wawili hawa kutumia muda kula na kuongea, Valentina akamwambia Xander kwamba angempeleka kwao. Xander akasema alitaka kulala hapo hapo siku hiyo ili wafurahie kuwa pamoja zaidi, lakini Valentina akakanusha na kusema wangepanga kuwa pamoja wakati mwingine mzuri; hasa kwa kuwa hakutaka mama yake amzingue. Ijapokuwa Xander alimshawishi kuwa mama yake hakuwa na tatizo hata akilala kwa rafiki, bado Valentina akasisitiza kumrudisha kwao kwa leo. Xander hakuwa na kipingamizi tena, hasa kwa sababu kwa leo mwanamke huyu alimridhisha. Hivyo baada ya kukubaliana, wakatoka pamoja na kuondoka kwa kutumia gari la madam.

Mvua bado ilinyesha kwa kuongezeka na kupungua, kukiwa na mianga ya radi pia, mpaka Valentina alipomfikisha Xander kwao kwa mara ya kwanza. Kijana akamwambia kuwa angefurahi sana kama mpenzi wake huyu angekuja kwenye sherehe ya mama yake, naye Valentina akasema wangeangalia na jinsi mambo yangekuwa.

Wakapeana busu fupi ya kuagana, kisha Xander akaelekea getini kwao akijaribu kuwahi ili asilowane sana. Valentina akabaki kumwangalia tu huku anatabasamu, kisha akaligeuza gari na kuanza kurejea nyumbani kwake.



Baada ya kufika ndani....


"Mbona uliitelekeza pikipiki? Kaileta rafiki yako, wewe ulikuwa wapi?" Alice akamuuliza kwa njia ya kawaida.

"Aam... pikipiki ilipatwa na shida kwo'... nikaiacha kwa fundi. Baadae nilikuwa na marafiki zangu, kwa hiyo nikamwambia Lucas aipitie maana niliona uvivu kuifata," Xander akadanganya.

"Si ungeniambia mapema?"

"Sikuona haja. Me kwanza nilikaa kusubiri maana fundi aliniambia ingetengemaa mapema lakini akawa anazungusha tu... kwo' mvua ilipoanza nikaona tu niiache..."

"Yaani liongo hili! Unachanganya story nyuma-mbele," akasema Sandra, aliyekuwa pembeni.

"Ulikuwepo?" Xander akamuuliza.

"Tunakujua we huna lolote, ulikuwa na mtu wako tu huko mmechelewa kutoka kufanya yenu ndiyo ukatunga hiki kisingizio," Sandra akasema.

"Ila Sandra..." Xander akasema kwa hofu kiasi huku akimtazama mama yake.

Alice akatikisa kichwa chake, kisha akauliza, "Umekula?"

"Yeah..." Xander akajibu.

"Sasa je, si nilikwambia? Anapikiwa huko... hahaaa..." Sandra akasema kiutani.

"Nenda sasa ukabadilishe nguo," Alice akamwambia Xander.

Xander akaanza kuondoka huku akitabasamu kwa njia iliyomfanya aonekane mwema, ila alipomgeukia Sandra, akamwonyesha ishara ya kumcheka na kumzomea kimya kimya, naye Sandra akamwonyesha kidole chake cha kati bila mama yao kuwaona. Baada ya kujikausha maji na kuvaa nguo zingine, Xander akarejea tena sehemu ya sebuleni kuketi pamoja na Sandra na mama yao. Salome na Azra walikuwa wameshakwenda kulala.

Watatu hawa wakakaa hapo kwa kama saa zima wakipiga story za hapa na pale, kisha baadae kila mmoja akaondoka kwenda kwenye vyumba vyao vya kupumzika.



Mvua bado iliendelea kunyesha familia nzima ilipoingia kujipumzisha. Hali ilizidi kuwa mbaya kwa sababu iligeuka na kuwa kama dhoruba kadiri muda ulivyokwenda. Mapazia yalipeperushwa kwa nguvu ijapokuwa madirisha yalifungwa vyema, na mianga ya radi ilimulika mara nyingi sana na kufanya paonekane kama vile mchana. Ngurumo za radi ziliendelea kutawala, na hii ilimsumbua sana Alexandra ambaye alipata shida kusinzia kutokana na kuhofishwa na hali hii. Alijiona ni kama vile yuko ndani ya filamu yenye kutisha aliyowahi kutazama kipindi cha nyuma, na haikuonekana kama ingepita ndani ya muda mfupi.

Baada ya kufikiria kwa kina, akaona anyanyuke tu na kuchukua simu yake, naye akaona ilikuwa ni saa 6 na nusu usiku sasa. Akavaa kikaptura chepesi chini ya T-shirt lake refu alilokuwa amevaa na nguo ya ndani pekee, kisha akatoka chumbani kwake na kuelekea kwenye chumba cha pacha wake. Akaugonga mlango taratibu, kisha akausukuma kidogo na kuchungulia ndani. Sikuzote waliheshimiana hivyo ilikuwa ni lazima kugonga mlango kabla ya kuingia kwenye chumba cha mmoja na mwenzake ili kuepuka kukutana na hali zisizotazamiwa. Lakini kwa kuwa mvua ilikuwa kubwa, Alexandra akaona tu atumie zaidi sauti yake.

"Xander... Xander uko macho?" akauliza kwa sauti iliyosikika vizuri.

"Sandra? Ndiyo niko macho. Vipi?" Xander akajibu.

Sandra akasita kidogo, lakini akasema, "Naogopa."

"Unaogopa mvua? Ni kubwa kweli... siyo rahisi kulala..."

"Ndiyo. Naweza kulala huku? Kule nahisi kama vile kuna kitu nyuma ya shuka kinanivuta..."

"Ahahahah... Nsyuka eti?"

"Acha basi Xander!"

"Ahahah... sorry. Haina shida. Njoo ulale hapa. Usisahau... anything for you..."

Sandra akatabasamu kwa kuhisi ahueni, kisha akaingia na kuufunga mlango. Kulikuwa na giza lakini bado mianga ya radi ilifanya sehemu kubwa ya chumba ionekane. Sandra akatembea mpaka kitandani na kupanda, kisha akajilaza karibu kabisa na mwili wa pacha wake. Xander akalala kwa kumpa mgongo, hivyo Sandra akajibana nyuma yake na kupitisha mkono wake mmoja ubavuni kwa pacha wake; kama amemkumbatia kwa nyuma. Xander hakuwa amevaa kitu juu, ila chini alikuwa amevaa kaptura nyepesi ya ndani. Wakalivuta shuka na kuifunika miili yao vizuri.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa mapacha hawa kulala pamoja namna hii, lakini ni muda mrefu ulikuwa umepita. Binti akajibana vizuri kwenye mwili wa kaka yake, huku kichwa chake kikiwa nyuma ya shingo ya Xander, na hali hiyo ikamtuliza kwa kumfanya ajihisi salama sana, na pole kwa pole usingizi ukawajia wote wawili.

Dhoruba hii kali iliendelea, na ilionekana ni kama iliiandama nyumba hii ya Meja Casmir tu. Baada ya muda fulani, ilipiga radi kubwa sana, na mwanga mkali kupita maelezo ukakitawala chumba walicholala mapacha hawa. Lakini walikuwa mbali sana kiusingizi kuweza kusikia, kisha hali ikaanza kutulia. Haukupita muda mrefu na sehemu hii ikatulia kabisa. Dhoruba ikapita.


★★★★


Asubuhi Ikafika. Xander ndiye aliyekuwa wa kwanza kuamka. Kulikuwa na mwanga wa mbali wa jua, na angalau sasa chumba kiliangazwa. Akajigeuza kivivuvivu na kujinyoosha akiwa amefumba macho yake bado. Lakini akaanza kujihisi utofauti fulani hivi. Kwanza kabisa, sikuzote alizoea kuamka na kuhisi msuli wake ukiwa mgumu haswa, lakini leo hakuhisi hilo. Ajabu. Akajinyanyua na kujiangalia kifuani.

'Nilivaa T-shirt saa ngapi?' akawaza. 'Subiri. Mbona kama upande niliolala siyo... What the hell?!' akajishangaa.

Alihisi ni kama labda alikuwa anaota. Kwa nini? Alikuwa na matiti kama mwanamke! Akatikisa kichwa chake kwa nguvu, lakini haikuonekana kuwa ndoto. Akajishika kwa chini, mashine haipo. Nini kinaendelea? Akatazama pembeni yake kwenye kitanda na kukuta amelala na mwanaume. Mwanaume huyo alikuwa ni yeye mwenyewe! Akatoa macho kwa mshangao.

Akamtikisa mtu huyo na kumwambia kwa sauti, "Wewe amka!"

Mh! Mbona sauti ya kike? Alishindwa kuelewa.

Mtu huyo akanyanyuka huku akisema, "Xander nini? Mbona una..."

Kabla hajamaliza kuongea, akatoa macho pia kwa mshangao. Lakini Xander alikuwa anamwona mtu huyu kuwa ni yeye akiuliza 'Xander nini?' Aliyeuliza hivyo akataka kupiga kelele, lakini Xander akamwahi na kumziba mdomo.

"Usipige kelele. Mama atazingua!" akamwambia.

Xander alikuwa ameuziba mdomo "wake" mwenyewe huku uso "wake" huo ukimwangalia kwa hofu sana. Kisha akaushusha taratibu mkono wake.

"Nini kinaendelea? Mbona mwili wangu... mbona nauona uko huko?" mwili wa Xander ukauliza.

"Sijui. Kwani ninafanana na..."

"Mimi! Sura yangu! Mwili wangu!"

Xander akatafakari kidogo, kisha akauliza kwa sauti ya chini, "Sandra?"

"Nnn..diyo..."

Xander akabaki mdomo wazi akishangaa sana. Alikuwa ametambua sasa kwamba mwili wake na wa dada yake ilikuwa imebadilishana. Ni nini kilikuwa kimetokea?


★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★

Follow me WhatsApp for full story. Misimu yote mitatu ya hadithi hii iko tayari.

WhatsApp +255 787 604 893
 
Back
Top Bottom