Stephen Byabato awahamasisha wadau wa nishati kushiriki mkutano na maonesho ya petroli ya Afrika Mashariki

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MHE. STEPHEN BYABATO AWAHAMASISHWA WADAU WA NISHATI KUSHIRIKI MKUTANO NA MAONESHO YA PETROLI YA AFRIKA MASHARIKI

Wadau mbalimbali katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia nchini wamehamasishwa kushiriki katika Mkutano na Maonesho ya 10 Petroli yanayotarajiwa kufanyika nchini Uganda mwezi Mei mwaka huu yatakayoshirikisha nchi zote za Afrika Mashariki.

Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato (aliyemwakilisha Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba) amewahamasisha wadau hao jijini Dar es Salaam katika Mkutano maalum uliolenga kuwafahamisha na kuwahamasisha ili waweze washiriki katika mkutano huo muhimu utakaofanyika Uganda kuanzia tarehe 09 hadi 11 Mei 2023.

Byabato amesema, lengo la Mkutano huo wa Uganda ni kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia kwa kutangaza shughuli za utafutaji na uzalishaji wa mafuta na Gesi Asilia zinazoendelea ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Tanzania itapata fursa ya kueleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa mabomba ya Gesi Asilia na Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG).

“Mkutano na Maonesho hayo yataonesha watu mbalimbali wanafanya nini kwenye kuchimba, kutafuta, kwenye teknolojia, utoaji wa huduma na ni hatua gani ambayo nchi shiriki zimefika katika Sekta ya Mafuta na Gesi, hivyo leo tumewaelimisha na kuwafahamisha wadau wetu faida ya kushiriki katika Mkutano na Maonesho hayo.” Amesema Byabato

Kuhusu Gesi Asilia ameeleza kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye uchimbaji na uendelezaji wa Gesi Asilia kwani tayari inatumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo viwandani, majumbani na kuzalisha umeme ambapo asilimia 60 hadi 70 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na Gesi Asilia.

Ameongeza kuwa, Tanzania imejipanga kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya kupeleka Gesi nchini Kenya, Uganda na Zambia, hivyo itatumia Maonesho hayo pia kwa kutangaza soko la gesi nchini ili kupata wawekezaji zaidi si katika kuchimba tu, bali pia kuiendeleza Gesi Asilia.

#Nishati
#ByabatoKazini
#KaziIendelee
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-06 at 16.45.54.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-06 at 16.45.54.jpeg
    42 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-03-06 at 16.45.57.jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-06 at 16.45.57.jpeg
    42.8 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-03-06 at 16.45.55(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-03-06 at 16.45.55(1).jpeg
    36.7 KB · Views: 4
Back
Top Bottom