Spika Ndugai: Wabunge 19 waliofukuzwa CHADEMA wapo kwenye mikono salama

TLS na mzee Warioba na Jenerali Ulimwengu nyie ni wabobezi wa sheria inakuwaje mnakaa kimya kuona chombo muhimu kama bunge linachezewa na mtu mmoja tu. Hili sakata la kufukuzwa uanachama wabunge 19 wa Ndugai ndani ya CHADEMA linapoteza kbs umuhimu wa kufuata sheria na katiba...
Mimi sio mwanasiasa,kama wangepita wao kwenye majimbo hawa viongozi wa Chadema yasingetokea haya!Katiba mpya ndo mwarobaini.
 
Leo Bungeni baada ya kipindi cha maswali na majibu, Spika wa Bunge Job Ndugai amesimama na kumkemea Nape Nauye, Mbunge wa Mtama ambaye hivi karibuni alitoa maoni yake binafsi kuwa wale wabunge 19 waliotimuliwa na CHADEMA sio wabunge halali.

Ndugai, akonekana mwenge wasiwasi na aliyepoteza mwelekeo akaanza kwa kujisifu kuwa yeye ni mzoefu, hivyo asipangiwe cha kufanya.

Ameenda mbali zaidi kwa kutaka kuonesha kuwa akina mama hao 19 wanaonewa na mfumo dume uliopo CHADEMA. Ndugai anasahau yeye na Profesa Lipumba walichowafanyia akina mama wa CUF walipovuliwa ubunge kwa kimemo cha Lipumba.

Mzee Ndugai atabaki katika historia kama SPIKA DHAIFU kuwahi kutokea. Tunazitaka Mamlaka za kulinda Katiba kuhakikisha KATIBA inalindwa.

Ikiwezekana kila NDUGAI atakapoonekana hadharani azomewe kwa aibu anayoiletea Taifa.
Naomba nikukosoe. Ndugai hakuonekana mwenye wasiwasi bali mwenye kujiamini na aliongea kimamlaka.

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Anachokifanya Spika ni kuonyesha dharau na jeuri yake wazi wazi kwa Mama. Hili suala kwani kuna mtanzania asiyelijua kwamba ulikuwa ni uhuni uhuni tu uliofanyika huku mwendazake akichekelea.

Ni aibu.
 
hili swalala wabunge 19 haliwezi kuanzia kwenye vyama/chama chao kuwafukuza bali linatakiwa kuanzia kwenye kosa walilofanya hawa.

na kosa lao hawa ni chama kutangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi wa 2020 na wao kubaini msimamo wa chama hauwazuii kwenda bungeni kutumikia wananchi.

chama kikaamua kuwaadhibu kwa kosa hilo.

hebu wanasheria tuelewesheni maana tunasikia kila siku katiba inavunjwa, katiba inavunjwa.

je katiba inamlazimisha kila mtu kugoma hata kama taratibu zipo zinazomruhusu kutokugoma ? (hapa nina maana ya kwamba kama hakuna sehemu inayosema kufanya hivi ni kosa mana yake kufanya siyo kosa)

lakini pili hivi kwa mrorongo ulivyokwenda, chama kiliwawajibisha wabunge kwa kosa la kwenda bungeni, je bunge au serikali inaweza kusema kosa la kuwawajibisha kwetu siyo kosa hivyo hatukubaliani na maamuzi yenu?

yawezekana ndani ya chama kuna taratibu za rufaa lakini ukitazama nia ya viongozi wanaotakiwa kutizama rufaa hakuna maamuzi ya haki yanayoweza kutendeka kutoka kwao.

je ni maamuzi yapi yanayozingatia katiba ya nchi?
 
Bungeni hupaswi kujipeleka kwa matakwa yako bali unapelekwa na matakwa ya Chama chako, kama chama chako hakiko tayari kuingia bungeni wewe huwezi kuingia bungeni. Mbunge anawakilisha chama chake kwanza kabla ya kuamua kumuwakilisha mtu yoyote. Na chama chako kikikuvua uanachama papo hapo unapoteza sifa za kuwa mbunge.

Msimamo rasmi wa CHADEMA mpaka sasa ni huu.
1. Hawatapelekea wabunge wa viti maalum bungeni.
2. Hawajakaa chini kama chama kuteua wabunge wa viti maalum.
3. Wamewavua uanachama wale Covid 19.

Hakuna hata chembe moja ya kisheria, kikatiba au kiuhalisia inayoweza kuwatambua au kuwalinda wabunge wa Covid 19. Wale wanawake hawakuteuliwa na CHADEMA na sio wanachama wa CHADEMA. Wale Covid 19 wako bungeni kwa matakwa binafsi ya ulevi wa madaraka wa spika wa bunge.
 
Kwa hapa Ndugai ni Mkuu kuliko katiba iliyompa uspika!!

Jobo hili analo!!
Asipojiangalia na kujirudi akaendelea kuishupaza shingo yake hili litamdhuru.

Kisingizio cha utetezi wa wanawake kimebuma BAWACHA haoo wanakuja DOM. Polisi watawapa ulinzi waandamane salama!!

Chama (CCM) kiinaanza kujitenga na hii jinai!!
 
Habari wadau!

Sisi binadamu tuna wivu sana, na roho mbaya kiukweli hata kama sheria zilikiukwa lakini hawa wabunge 19 ni muhimu sana pale bungeni kuwepo maana wanachangamsha bunge na kutetea masirahi mapana ya watanzania wengi.

Nikiangalia yule Nusrat Hanje anavyojenga hoja na wale wengine inaonyesha wazi wasipokuwapo hawa bungeni kutakuwa na gap kubwa sana la uwakilishi bungeni.
 
Mimi sijawahi ona hii obsession ya kuwafukuza watu

Watu hawataki hata kujadili katiba mpya.

Wao wanataka kuona hawa wadada wanapigwa chini haraka.

Wakati kuna options ya mahakama.

Hawa kina Halima wakienda mahakamani, kesi inaweza kwenda hata miaka mitano.
 
Wewe umetumia hisia zako binafsi ku judge hili jambo. Lakini umesahau kuwa kuna utawala wa sheria.

Sheria haitaki prejudices mkuu lazima ifuate mkondo wake hata kama unaona tofauti lakini as long as sheria inasimamia usawa wewe utajua mwenyewe.
 
Wewe umetumia hisia zako binafsi ku judge hili jambo. Lakini umesahau kuwa kuna utawala wa sheria.

Sheria haitaki prejudices mkuu lazima ifuate mkondo wake hata kama unaona tofauti lakini as long as sheria inasimamia usawa wewe utajua mwenyewe.
Sheria yenyewe inasemaje?nani anayeisimamia?
 
Back
Top Bottom