Spika Ndugai: Mnaogopa nini kuleta viambatanishi ili tuwavue Ubunge kwa Haki?

Baada ya kile kikao cha kujifanya wanawavua uanachama Mdee alitokea hadharani akasema wao siyo watoto kwahiyo kina Mbowe wajaribu kuwa wastaarabu...
sawa kabisa mdee nakumbuka alisema hivyo kwahiyoi wasifikiri wakina mdee hawana akili mbowe anahusiuka
 
Ndugai kajificha chini ya kivuli cha NEC maana majina ya Wabunge yanatoka NEC. Hili swali hata Ndugai mwenyeww atalirefer kwa NEC

Kwenye hayo madai ya forgery nadhani hata NEC wanaweza kujitoa ufahamu na kuitaka CHADEMA ikaithibitishe hiyo forgery kortini
Ccm ni kichaka cha maovu
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao
Atuthibitishie kwanza nani alipeleka majina ya hao wabunge NEC ikiwa chama kimakanusah halafu ndio tuone nani mvunjaji wa sheria
 
Hapa mbona hakukua na figisu?? Au kichaa kimezidi?

IMG_20210507_133359.jpg


IMG_20210507_133407.jpg
 
Vyovyote Iwavyo HAO wabunge wameshaharibikiwa mambo yao ndani ya chama chao cha chadema spika hata angewalinda naamini Hawana nafasi tena kwenye chama chao.

KAMA wangekua na busara wangewafuata wakuu wao wamalizane nao waishi kwa amani.

Kwa sasa hata wakitumia dirisha la Mfumo Dume na kwamba wanaonewa ni wanawake hiyo wala haina maana wala nafasi yeyote.

Siku ndugai hayupo aje spika mwingine anajali sheria za nchi mnapigwa. Jipangemi msimtumainie Mtu.
 
Kuna jambo moja ambalo Ndugai analikwepa, na pia kuna kosa Ndugai anafanya, hivyo naweza kusema anafanya makosa makubwa mawili kwa makusudi.

1.Spika huwezi kutoa agizo au maelekezo kwa chama cha siasa kwa mdomo bali anapaswa kufanya hivyo kwa kuwaandikia CHADEMA barua rasimi licha ya ukweli kuwa hata haki hiyo ya kuhoji maamuzi ya CHADEMA hana.

2.Pili, kama anataka nyaraka za kuwafukuza uanachama wabunge hao, atuonyeshe au ahoji pia nyaraka za wabunge hao kuteuliwa na CHADEMA kuwa wabunge wa viti maalumu kutoka kwa Mamlaka iliyowasilisha majina hayo kwake(NEC).

CHADEMA mawasiliano yote kuhusu hili sakata yako kimaandishi ila Ndugai anapiga porojo tu(naona anakwepa maandishi ingawa ana kinga na zaidi anafikiri CHADEMA watafanya anachokitaka).

Viatu alivyovaa Ndugai si size yake.
 
Mimi sio mwanasheria lakini nina uwezo wa kutambua tu kwamba Ndungai ni mzigo kwa bunge na ni spika ambaye hana uelewa wowote kuhusu sheria

Unawezaje kuomba

1: Katiba ya Chadema

2: Mutasali wa vikao vya chadema

na mambo mengine juu ya kifukuzwa kwa wanachama wa chadema wakati unafahamu kabisa.

Hawa wabunge 19 hawakuwai kuteuliwa na chama chini ya katibu mkuu Myika Je wewe ulipokea barua ya kuteuliwa kwao kutoka kwa katibu mkuu?

Kwanini hawa wabunge hawakuapa ndani bunge mbele ya wabunge wengine kama sheria inavyotaka wafanye?

Kwanini majina ya Viti maalumu ya ccm ulipewa kwa mkurugenzi wa tume na barua za kuteuliwa kwao zilikuwa zimesainiwa na Bashiru? Je za hao 19 zilisainiwa na nani?

Ndungai ni MTU hatari sana na anautia doa pakubwa utawala wa Mama Samia adhibitiwe lasivyo Taifa linaanguka na yeye hana cha kupoteza.

Tumkemee adui mamba moja wa democracia kwa sasa nchini ni Ndungai.
 
Mpaka hapo inaonesha wazi spika anajua chadema walikosea wapi kisheria ndio maana kila siku anawataka wapeleke

Maybe kwenye hiko kikao akidi ilikuwa haijatimia au kuna mapungufu kutokana na Katiba yao
Kawa kona- bonge la kabari
 
Back
Top Bottom