Je, Wabunge Wasaliti 19 watang'olewa Bungeni?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,703
218,246
Kuna Dokezo kwamba Wabunge wale 19 Wasaliti, waliojiuza na kuapishwa na Job Ndugai kwenye eneo la Gereji ya Bunge, huenda Wakaondolewa Bungeni kwa vile waliingizwa kinyume cha Sheria, inadaiwa kwamba hawana tofauti na lile zuio la mikutano ya hadhara lililoondolewa hivi karibuni .

Taarifa zaidi zinasema kwamba Jambo hili la kuondolewa bungeni kwa Halima Mdee , Sophia Mwakagenda na wenzao NI SEHEMU YA MARIDHIANO baina ya CCM na CHADEMA, na kwamba utekelezaji wake waweza kuwa ndani ya siku chache zijazo.

Uwezekano wa Wasaliti hawa kufukuzwa Bungeni ni zaidi ya 100% , Hii ni kwa sababu waliingia kwa kufoji , hata ile KESI YAO WALIYOFUNGUA MAHAKAMANI inapinga kuvuliwa Uanachama wao tu , HAIHUSIANI NA UBUNGE , hivyo basi wakivuliwa ubunge bado wanayo nafasi ya kuendelea na kesi yao , na ikiwa watashinda basi watarejeshewa uanachama wao (japo uwezekano wa kushinda ni kama hakuna).

Usaliti ni laana, Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu, Laana ya Usaliti yaweza kukikumba hadi kizazi cha nne cha Mhusika .

INASIKITISHA SANA!
 
Sasa kama kesi iliyoko mahakamani haihusiani na wao kuondolewa ndani ya bunge, BUNGE LITAWAONDOA KWA VIGEZO VIPI?
Kesi yao inapinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, kwahiyo inaweza kuendelea tu ili wapiganie uanachama wao , uanachama hauhusiani na Ubunge, ndio maana mimi pamoja na uanachama wangu wa Chadema lakini si Mbunge .

Kingine unachopaswa kukumbuka ni kwamba Wao ndio wameishitaki Chadema wakipinga kuvuliwa uanachama , kwa madai kwamba hawakupewa nafasi ya kusikilizwa.

Kingine unachotakiwa kukifahamu ni hiki ,kwenye maridhiano uongo , uzandiki na hila zote huwekwa kando , kinachoangaliwa ni Ukweli pekee , imebainika wazi kwamba mchakato wa kuwaapisha hawa kuwa wabunge ulikuwa batili , hakuna asiyejua , sasa ili kulinda Maridhiano ni lazima hawa ubatili wao uishe
 
Kwamba CDM rasmi inamtambua sa100 baada ya maridhiano!!

Hapo sasa COVID wataondoka automatically. Bt b4 that zilikuwa kelele tu, wasingeondoka Hadi 2025.
 
Kuna Dokezo kwamba Wabunge wale 19 Wasaliti, waliojiuza na kuapishwa na Job Ndugai kwenye eneo la Gereji ya Bunge, huenda Wakaondolewa Bungeni kwa vile waliingizwa kinyume cha Sheria, inadaiwa kwamba hawana tofauti na lile zuio la mikutano ya hadhara lililoondolewa hivi karibuni .

Taarifa zaidi zinasema kwamba Jambo hili la kuondolewa bungeni kwa Halima Mdee , Sophia Mwakagenda na wenzao NI SEHEMU YA MARIDHIANO baina ya CCM na CHADEMA, na kwamba utekelezaji wake waweza kuwa ndani ya siku chache zijazo.

Uwezekano wa Wasaliti hawa kufukuzwa Bungeni ni zaidi ya 100% , Hii ni kwa sababu waliingia kwa kufoji , hata ile KESI YAO WALIYOFUNGUA MAHAKAMANI inapinga kuvuliwa Uanachama wao tu , HAIHUSIANI NA UBUNGE , hivyo basi wakivuliwa ubunge bado wanayo nafasi ya kuendelea na kesi yao , na ikiwa watashinda basi watarejeshewa uanachama wao ( japo uwezekano wa kushinda ni kama hakuna )

Usaliti ni laana, Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu, Laana ya Usaliti yaweza kukikumba hadi kizazi cha nne cha Mhusika .

INASIKITISHA SANA!
Umeiandika kishabiki sana..
Hapo hapo kuna tetesi kuwa CHADEMA wanatarajia kuanza kupokea ruzuku ya wabunge hao unaosema wanataka kufukuzwa
 
Kesi yao inapinga kuvuliwa uanachama wa Chadema , kwahiyo inaweza kuendelea tu ili wapiganie uanachama wao , uanachama hauhusiani na Ubunge , ndio maana mimi pamoja na uanachama wangu wa Chadema lakini si Mbunge...
Unapoteza wakti mkuu.Mambo yote huamuliwa na "mheshimiwa"?
 
Mkuu si utafute jambo jingine kwa maana hili kwanza liko mahakamani; pili hamna namna ya kuwatoa zaidi ya kulilia huruma za watu wengine ndiyo wawatoe; hawa 19 mpaka 2025 take my word
Wewe ndiyo nani nchi hii?? Mbona mnajikweza Sana wanaJF mkiwa nyuma ya keyboard? Eti take my words!!!.

Shieee!!! (Mshangao wa kimasai)

Usikute unaishi kwa kuuza mbogamboga toka bonde la Msimbaxi.
 
Wewe ndiyo nani nchi hii?? Mbona mnajikweza Sana wanaJF mkiwa nyuma ya keyboard? Eti take my words!!!.

Shieee!!! (Mshangao wa kimasai)

Usikute unaishi kwa kuuza mbogamboga toka bonde la Msimbaxi.

Kwani wewe umecomment hapa kama nani nchi hii? Ulitakiwa ujiulize hivyo pia, kabla haujatoa maoni..!
 
Mkuu si utafute jambo jingine kwa maana hili kwanza liko mahakamani; pili hamna namna ya kuwatoa zaidi ya kulilia huruma za watu wengine ndiyo wawatoe; hawa 19 mpaka 2025 take my word
Kwani kesi ya Mbowe haikuwa mahakamani? Rais akiamua tu hao majaji wataskiliza kesi kwa spidi ya mwanga na hukumu kutolewa chap Chap!

Au umesahau issue ya Lissu kuvuliwa ubunge ama umesahau Lipumba alipowavua wabunge wa CUF viti maalum!! Kuwa kwao mahakamani hakukuzuia wao kuachia ubunge.
 
Umeiandika kishabiki sana..
Hapo hapo kuna tetesi kuwa CHADEMA wanatarajia kuanza kupokea ruzuku ya wabunge hao unaosema wanataka kufukuzwa
Eeh baada ya kamati kuu kuteua wabunge kihalali na sio hao waliojipeleka wenyewe. So watatimuliwa kupisha listi halali so walitaka kuwepo ni kheri waombe radhi na wajiuzulu Ili wateuliwe kihalali wakiendelea na ubishi yatawakuta magumu na 2025 watastaafu rasmi siasa.
 
Back
Top Bottom