Spika Ndugai: Mbowe alikuwa Ulaya sasa katumwa na watu wake anapotosha kuhusu ripoti ya CAG

Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
Hivi ni Mbowe au Zitto aliyechambua hoja za CAG?
 
hivi ZZK huyu mbona huwa wanaomwogopa sana? af all the things aliezungumza mambo mazito ni Zzk ila speaker kakomaa na Mbowe..nahisi watu kama kina ZZK na kina Mbat100 waliwekwa kuwa wapinzani feki
 
Ndugai akapambane na maandamano ya bodaboda aliosema wachapwe viboko
Hilo halikwepeki baada ya kumsema vibaya Jpm kuhusu bandari ya Bagamoyo
Wana Ccm tuungane tumngoe huyu
 
Sasa amejuaje kama inapotoshwa wakati yeye hajaisoma, hajui chochote na hao wabunge wanaounda LAAC na PAC hawajaichambua?

Ndugai ni Speaker wa HOVYO sana kuwahi kutokea katika historia ya Bunge letu tukufu. Ameiharibu sana taswira ya Bunge na sasa kila zuzu yeyote anatamani kuingia kule
Namuunga mkono ile kauli ya asad
 
hivi ZZK huyu mbona huwa wanaomwogopa sana? af all the things aliezungumza mambo mazito ni Zzk ila speaker kakomaa na Mbowe..nahisi watu kama kina ZZK na kina Mbat100 waliwekwa kuwa wapinzani feki
Utaendelea kuwaza bila ya majibu sahihi ila Zitto anajulikana kitambo
 
Spika wa Bunge Job Ndugai, amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya CAG na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne, kwa kuwa inapotoshwa huku akimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kuwa mmoja wapo

Spika wa Bunge Job Ndugai amezitaka kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) zichambue ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuiwakilisha bungeni katika mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano, kwa kuwa inapotoshwa.

Akizungumza leo Jumatatu Aprili 12 2021, Ndugai huku akimtaja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amedai kuwepo upotoshaji wa ripoti hiyo.

Kauli ya Spika imekuja siku moja baada ya Mbowe kuhutubia kupitia mitandao ya jamii, ambapo pamoja na mambo mengine alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

“Watu wanabeba tu mabilioni yameibiwa sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe alikuwa Ulaya huko sasa katumwa na watu wake huko anapotosha mambo,” amesema.

Amesema sio watu wengi wenye uelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu na hivyo kunaweza kukawa na ujenzi wa kituo cha afya wa Sh 500milioni lakini Sh 499milioni zimetumika vizuri kabisa.

Hata hivyo, amesema lakini kati ya fedha hizo Sh1milioni ikikosa kiambatanisho fulani ni kawaida wakaguzi wanahoji fungu zima la Sh 500milioni.

Amesema kwa hiyo unaposoma mtaani unaona sh 500 zimeibwa lakini kumbe pale ni Sh milioni moja ndio hazina risiti.

Amesema kamati hizo zitaanza mapema kuchambua ripoti hizo ili waangalie ratiba yao na kuwaelimisha watu kuhusiana na ripoti ya CAG ambayo ni taarifa nzuri lakini baadhi ya watu wanabeba na kupotosha tu.

Mwananchi
Aliyeweka pich ya kwamba watu wa ulaya wanawivu au wanataka kutuua ndio aliyetuharibu wa africa tunalia kila siku wazungu mabeberu na huku tunategemea wao kuanzia kwenye mikopo, technolojia , madawa pamoja na policy zote na huku sisi wenyewe ndio tunaokula pesa za nchi yetu..waafrica tunatakiwa kuangalia ni wapi tuna kosea na kujirekebisha
 
Kwa hiyo Mbowe ndiyo anasababisha taarifa za hizo kamati kusomwa mkutano wa 4 badala ya wa 5, na siyo ratiba ya Bunge?

Halafu hizo kamati zina wataalamu kiasi gani kuwazidi wale wa ofisi ya ukaguzi? Lakini hizo kamati ndiyo zitajibu hoja za CAG na siyo taasisi husika zilizotuhumiwa, na mwisho kwa mabadiliko haya ya Ndugai haoni kuwa hizo taarifa za kamati zitakuwa hazina uhalisia zaidi ya kujibu hoja za kumbagaza CAG kama alivyoanza yeye, bunge likiitwa dhaifu tusisikie kutisha watu pingu na maazimio ya kutofanya kazi na CAG maana ndiyo kawaida yake

Ndugai kanunuliwa na WACHINA lazima achunguzwe!! Kwavile yeye kanunuliwa anafikiri kila mtu ni corrupt kama yeye!! Hawa wagogo ni watu wa kuomba omba sio watafutaji hivyo huwaoneo donge wenzao wanaotafuta!!
 
mangi hizo ni audit queries na opinions sio final conclussion.
Mkuu mimi ni auditor na nilishawahi kushiriki audit za CAG. Audit queries huwa zinakuwa communicated kwa wahusika kabla ya final audit report haijatoka ili kama wana majibu ziweze kuondolewa. Audit queries zikikosa majibu ndio hapo audit report inakuwa finalised na kupewa mhusika. Kwa hiyo kile kilichomo kwenye audit report hakina queries zozote bali ni final audit report (final findings). So, please acha kupotosha.
 
Sasa amejuaje kama inapotoshwa wakati yeye hajaisoma, hajui chochote na hao wabunge wanaounda LAAC na PAC hawajaichambua?

Ndugai ni Speaker wa HOVYO sana kuwahi kutokea katika historia ya Bunge letu tukufu. Ameiharibu sana taswira ya Bunge na sasa kila zuzu yeyote anatamani kuingia kule
Ndugai ajue kuwa Hayati anamuangalia huko aliko kwa jinsi alivyomsaliti mapema .... Kumtupia hilo zigo Mbowe haitamsadia. Actually, yeye ndiye aliyelianzisha kwa kudai kuwa Rais alishauriwa vibaya.
 
Back
Top Bottom