Spika Ndugai amtaka Mbowe aache tabia ya kujipima ubavu na Mkuu wa nchi Rais Magufuli, aache kabisa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,922
141,888


Up dates;

Spika Ndugai amesema Mbowe kama KUB ni mtu muhimu sana pale bungeni na ni mjumbe wa kamati zote muhimu ikiwemo ya Uongozi, kamati ya haki, kamati ya kanuni na kamati ya bajeti.
Pia kama KUB Mbowe anaruhusiwa kusimama bungeni wakati wowote na kuuliza au kushauri chochote tofauti na wabunge wengine wote.

Spika Ndugai anasema ni utovu wa adabu na nidhamu kwa kiongozi yoyote kujibu hotuba ya mkuu wa nchi mara tu amalizapo kuhutubia, Mbowe kama alikuwa na maswali au ushauri utaratibu anaopaswa kuutumia anaujua ila kiukweli Mbowe ni mtoro sana wa bunge na hata vikao vya kamati haudhurii kabisa.

Ndugai amesema tatizo lake na Mbowe limeanza pale alipomtaka KUB arudishe posho ya sh 2,040,000 aliyochukua bila kuifanyia kazi baada ya kujiweka karantini.

Ndugai ameapa Mbowe ni lazima atarudisha hiyo fedha liwake jua au inyeshe mvua, wabunge wengine wamesharudisha kasoro Mbowe na wengine wawili au watatu.
 
Ndugai amepanic
Ndugai hatomuweza Mbowe hata afanyeje !

FB_IMG_1589397986327.jpg
 
Hivi Bunge la sasa sio muhimili tena unaojitegemea eeeh!!!??

Kwa maana spika tu anaonekana hajiamini akiwa ndani ya bunge analoliongoza.

Prof.Assad aliona mbali sana , muhimili unaojitegemea na ambao una meno ya kumuwajibisha hata prezidaa leo umekuwa kibogoyo kabisa.

Wao wanaogopa kuwajibishwa na prezidaa badala ya prezidaa awahofie wao.



sent using Simenzi mayai
 
Back
Top Bottom