Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,991
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Jumaa Mubarak 😀🔥

----
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amedai kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiongezea mishahara yao kutoka milioni 13 waliyokuwa wanapata hapo awali hadi kufikia milioni 18 kwa mwezi, hiyo ikiwa ni nje ya posho ya vikao anayopatiwa Mbunge kila anapohudhuria kikao kimoja cha Bunge

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 21.2024 Babati mjini, mkoani Manyara Mbowe amesema kuwa mara nyingi viongozi wa serikali wamekuwa wakijitokeza hadharani na kueleza kuwa uchumi umekua hapa nchini, jambo ambalo anakubaliananalo kwa kutumia kipimo cha pato la Taifa (GDP) lakini ameeleza kuwa uchumi huo umekua kwa watu wachache walioko serikalini na sio kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla wake

Amesema viongozi walioko serikalini wamekuwa wakiendekeza maisha ya anasa ambayo kwa kiasi kikubwa hayaangalii maslahi ya nchi na wananchi wake ndio maana inawawia vigumu kukubali kufanya marekebisho ya msingi ya sheria za nchi kutokana na msingi wa uwepo wa Katiba mpya

Ametolea mfano kupitishwa kwa sheria ya mafao ya wenza wa viongozi kama sehemu ya anasa hizo kwa kuwa sasa mwenza wa Rais mstaafu analazimika kupokea asilimia 60 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, wakati Rais mstaafu akipokea asilimia 80 ya mshahara huo, hiyo ikienda sambamba na kupatiwa magari yanayobadilishwa kila baada ya muda, walinzi, nyumba na watumishi wengine binafsi.

Chanzo: Jambo Tv

Majibu ya Bunge - Bunge lakanusha Kauli ya Mbowe kuwa Mshahara wa Wabunge umepanda kutoka Tsh Milioni 13 hadi 18
 
Kunywa bia nitalipia
GBEFU-4WIAAQAyI.jpeg
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Source Jambo TV

Jumaa Mubarak
Mmmmmh ni yakweli haya?
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Source Jambo TV

Jumaa Mubarak 😀🔥
Nakumbuka what’s wao walijiongezea posho

Wakiwa nje wanauona San mchezo

Wakiwa ndani… watakwambia kwa ground iz ze difflenti
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Source Jambo TV

Jumaa Mubarak 😀🔥
Aliyewaongezea mishahara ni Rais hawana mamlaka ya kujiongezea mishahara hapa wa kumpa lawama ni Rais
 
Back
Top Bottom