Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Spika Makinda achezea Kibano - Bungeni Live!

Ni upumbavu kuwafunga watu midomo eti kwa sababu tu hawajui lugha fulani. Ni watu wajinga tu ndo wanaoweza kupitisha sheria inayosema lugha ya mawasiliano iwe lugha wasiyoijua. Kwa hili sishabikii. Narudia tena kusema, ili Tanzania iendelee tunahitajia Kiswahili na lugha nyingine za makabila tu! Ni upuuzi kulazimisha tuongee Kiingereza wakati watu waliopo kilomita 20 kutoka Dodoma mjini hawaelewi Kiswahili chenyewe. Ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kuwawakilisha watu kwa kuongea lugha wasiyoijua. Sioni mantiki yoyote. Mamikataba yote mabavu yametokana na vilaza wetu kutojua lugha ya Kiingereza.
Tujifunze kwa waarabu, mikataba kwa Kiarabu, mabunge yao wanaendesha kwa Kiarabu. Sisi Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania. Ni aibu. Hatuna siri, hatuna utamaduni. Tunahaha tu. Narudia tena kuandika miswada, kuongea Kingereza bungeni, kuongea kiingereza kwenye mikutano ya kimataifa ni ukosefu wa akili!

Ni upumbavu zaidi kupeleka wawakilishi wa nchi wasiokidhi vigezo vinavyotakiwa. Labda ungeshauri bunge la SADC liendeshwe kwa utamaduni wa kitanzania ungeeleweka. Kwa hili there is no way to avoid "ngeli." Labda kama tunataka kuendeleza kale ka utamaduni ketu cha kuchagua wansinziaji bungeni!
 
Wenje ajishushie hadhi kwani TZ tuna hadhi bado? Kama nchi yenyewe haina hadhi tunaigawa kwa masultani wenje ashushe hadi gani tena?
 
Jamani mnaofuatilia Bunge huyu mama Makinda analiongoza bunge kwa Kulazimisha hawezi.Nimekuwa nikimsikiliza sana kiingereza chake Jamani kama namuonea mtanisamehe.Mama hawezi anatakiwa akae na wataalam wa Lugha hiyo manake napata mashaka kama anawezakushiriki kwenye International forums na nchi ikawakilishwa vizuri.kiingereza chake ni cha hali ya chini Kabisa.
 
kwa mtindo huu yangu macho tu, nasubiri mikono ianze maana ni bonge la muvi
 
Wewe hata Lugha yako ya mama inakushinda/huelewi.Hili ni jukwaa la Siasa ambalo linajadili tatizo la lugha kwa wabunge wanaogombea nafasi za kutuwakilisha nje ya Tanzania
You just want to argue blindly, this is a chat-zone/forum, where people just use any slang and say anything
My friend, I seriously want you to re-think this analogy you are attempting to make.I am not talking about accent/speaking style - simply basic grammar and correct pronunciation. It isn't too much to ask, is it?
it isn't.
 
Kilichotokea leo bungeni kwa Mh. Wenje kulazimishwa kufuta usemi wake kimemtia aibu sana mbunge huyu, kwani ameonekana ni mtu asiye na msimamo na ni muoga pale anapo kemewa, na hasa pale alipoambiwa kuwa atatolewa nje ya bunge, kama si hekima na busara za Zitto za kumuomba Mh. Spika amvumilie hakujua asemalo kwa kuita kikao cha kamati ya uongozi kilichokaa ni ‘black market' . Hii imemshushia sana hadhi yake !
cHILDISH!
Jivue Gamba wewe!
Naona tokea jana uko kwenye kazi maalum...Payroll inakaribia kutema nini?
 
Ni upumbavu kuwafunga watu midomo eti kwa sababu tu hawajui lugha fulani. Ni watu wajinga tu ndo wanaoweza kupitisha sheria inayosema lugha ya mawasiliano iwe lugha wasiyoijua. Kwa hili sishabikii. Narudia tena kusema, ili Tanzania iendelee tunahitajia Kiswahili na lugha nyingine za makabila tu! Ni upuuzi kulazimisha tuongee Kiingereza wakati watu waliopo kilomita 20 kutoka Dodoma mjini hawaelewi Kiswahili chenyewe. Ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kuwawakilisha watu kwa kuongea lugha wasiyoijua. Sioni mantiki yoyote. Mamikataba yote mabavu yametokana na vilaza wetu kutojua lugha ya Kiingereza.
Tujifunze kwa waarabu, mikataba kwa Kiarabu, mabunge yao wanaendesha kwa Kiarabu. Sisi Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania. Ni aibu. Hatuna siri, hatuna utamaduni. Tunahaha tu. Narudia tena kuandika miswada, kuongea Kingereza bungeni, kuongea kiingereza kwenye mikutano ya kimataifa ni ukosefu wa akili!

Kichaa huwa anafikiria watu wote ni vichaa kama yeye ama wengine zaidi yake. Mjinga hufikiria watu wote ni wajinga kama yeye au zaidi yake.Werevu hufikiria watu wote ni werevu na huwa makini na kila mtu hasa asiyemjua. Hapo ndipo ilipo tofauti ya maamuzi ya watu. Kweli Tanzania lugha yetu kuu ni kiswahili lakini hatuwezi kupeleka wawakilishi wasiojua lugha inayotumika huko. Haitakuwa na maana. Kuhusu mikataba mibovu, asikwambie mtu, hiyo mikataba imepindishwa makusudi na watu werevu kabisa katika nchi hii kwa sababu ya uchu na ubinafsi wao. Tatitozi siyo ukilaza au uelevu, Welevu wa nchi masikini wanatumia werevu wao kuwaibia masikini walio wengi. Lakini yana mwisho.
 
Kama alidhani ni kazi raisi imekula kwake
na wale waliomtuma kukaa kwenye kiti!!!!!!
Kutaka Sitta to Makinda.....!!!
 
Watu msisahau hapa ni kwenye forum,Bungeni ni ofisini.Naona hapa watu wazima wanaropoka tu
Mambo ya kutinga suti ufukweni
 
cHILDISH!
Jivue Gamba wewe!
Naona tokea jana uko kwenye kazi maalum...Payroll inakaribia kutema nini?

yeye alidhania bunge ni sehemu ya kuvua samaki kule mwaloni wanajisemea maneno yoyote, wajuzi wa mambo wamemuumbua
 
Wawakilishi wetu, naomba mtumie busara. Najua mnalipwa mishahara mikubwa tu, lakini tumieni muda wenu vizuri. Sisi wananchi tunaumia sana na haya maisha!
 
cHILDISH!
Jivue Gamba wewe!
Naona tokea jana uko kwenye kazi maalum...Payroll inakaribia kutema nini?

Hakuna mabadiliko hata wakijivua gamba. nyoka akijivua gamba sumu yake iko palepale.
 
Back
Top Bottom