Ni upumbavu kuwafunga watu midomo eti kwa sababu tu hawajui lugha fulani. Ni watu wajinga tu ndo wanaoweza kupitisha sheria inayosema lugha ya mawasiliano iwe lugha wasiyoijua. Kwa hili sishabikii. Narudia tena kusema, ili Tanzania iendelee tunahitajia Kiswahili na lugha nyingine za makabila tu! Ni upuuzi kulazimisha tuongee Kiingereza wakati watu waliopo kilomita 20 kutoka Dodoma mjini hawaelewi Kiswahili chenyewe. Ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kuwawakilisha watu kwa kuongea lugha wasiyoijua. Sioni mantiki yoyote. Mamikataba yote mabavu yametokana na vilaza wetu kutojua lugha ya Kiingereza.
Tujifunze kwa waarabu, mikataba kwa Kiarabu, mabunge yao wanaendesha kwa Kiarabu. Sisi Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kihispania. Ni aibu. Hatuna siri, hatuna utamaduni. Tunahaha tu. Narudia tena kuandika miswada, kuongea Kingereza bungeni, kuongea kiingereza kwenye mikutano ya kimataifa ni ukosefu wa akili!