Spika Anna Makinda achimba mkwara mzito wabunge

Spika Anna Makinda achimba mkwara mzito wabunge

Kwani Spika hakuwa na kanuni za kuwashughulikia Wabunge wanaokiuka kanuni? Au yeye ndiye ameshindwa kuzisimamia kwa kujaa upendeleo kwa Wabunge wa ccm na kuwaonea Wabunge wa upinzani.
 
Akiongea kwa uchungu Spika wa Bunge Mama Anne Makinda amewashambulia wabunge wanaovaa suti baadae wanatukana matusi ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana na mdomo wake hauwezi kutamka hayo. Pia amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.
Je anakubali kuwa anaongoza vikao vya MBWA?.
 
Angewataja tu majina mbona yako wazi? Na yeye ndo anayalea?
1. Mwigulu Nchemba(gaidi)
2. Lusinde
3. Juma Nkamia
4.
5.
Ongezeeni kwenye hiyo LIST OF SHAME

You must be a good supervisor indeed!
 
Ipo haja ya kutengenezwa sheria ya kuruhusu wananchi kuamua kufanya tasmini ya kuona kama mbunge wao aendelee kuwawakilisha au la kila baada ya muda fulani ndani ya kipindi cha miaka mitano(Kwa kufuatilia uwakilishi wake bungeni na pia anachokifanya jimboni kwake) huenda inaweza kusaidia kurejesha nidhamu-Hii pia kwa mtizamo wangu itarejesha heshima na nidhamu ya wabunge hawa kwa waajiri wao ambao ni wananchi. Hali ilivyo sasa mtu akisha upata ubunge anakuwa bosi mwenyewe na kuona anaweza kufanya chochote bila ya bosi wake(wananchi) kuweza kuamua chochote juu ya uwajibikaji wa waajiriwa (wabunge) katika kazi wanazotarajiwa kuzifanya hata kabla ya kipindi cha miaka mitano.Bunge halina mvuto tena wa kulifuatilia na kuona unaweza kujifunza kitu kutoka kwao badala yake vinavyoonekana ni vituko tu kama wako mtaani(Hawaoneshi kuwa na malengo ya dhati kusaidia wananchi kuondokana na kero na changamoto za maisha zinazowakabili)
 
Spika wa bunge bi Anna makinda amewapiga biti waheshimiwa wabunge leo asubuhi na kuwaambia suti zao walizojitupia haziendani na maneno yanayowatoka ktk vinywa vyao, amesema matusi ndiyo yamekuwa yakitawala katika midomo ya wawakilishi hao na kuacha hoja inayojadiliwa hewani, amekwenda mbali zaidi na kuwatia mkwara wabunge hao kwamba hataangalia chama endapo mbunge atavunja kanuni za bunge. Kwa kuwa kanuni za bunge zinampa nafasi ya kuita police na kuja kumchukua mbunge huyo kwa hatua za kisheria,


........Refarii mzuri katika mechi haangalii rangi ya jezi..... kama ni kadi nyekundu na njano anatoa hata kwa timu nzima ................. Kwa kweli Mh. spika na uongozi mzima wa bunge unastahili lawama ... mambo ya matusi na lugha za kuudhi mmezilea wenyewe ndani ya bunge kwa kulinda maslahi... kanuni zipo lakini zinakiukwa... kama hatua zingechukuliwa muda mrefu nidhamu ingetawala... kwa maana hiyo mnavuna mlichopanda.. mmengia katika kumbukumbu za historia kwa viongozi wa bunge ambao mamba ya ajabu ajabu yamepita na kutokea mikonon mwenu.........mtakumbukwa daima na milele

 
Kama kanuni zinaruhusu sawa. Lakini anatakiwa pia aende shule ili kujua maana ya neno tusi, vinginevyo anaweza kumchukulia hatua mbunge wakati neno alilotumia sio tusi. Maneno kama kutongoza, Kikwete dhaifu, kiherehere, mjinga, waziri mkuu mwongo, mbwa, spika dhaifu, nk kama yalivyotumiwa na wabunge sio matusi ila yanaweza kumkera mtu kulingana na muktadha na hadhi.
 
Aache utoto, kuiba aibe yeye halafu awe wa kwanza kulalamika? hii hali ya mjengoni ameiruhusu mwenyewe!
 
Mbona yule mbunge (CUF) kutoka Zanzibar (Akiwa amevalia suti ya rangi ya "Malai") amewaona wote pamoja na MAKINDA kuwa wako UCHI kwa vile hawajajisetiri MAUNGO?

​Nilisikia akisema mtu kajamba!
 
Mbona yule mbunge (CUF) kutoka Zanzibar (Akiwa amevalia suti ya rangi ya "Malai") amewaona wote pamoja na MAKINDA kuwa wako UCHI kwa vile hawajajisetiri MAUNGO?

kwenda huko- be specific! Malai come in different colors.
 
Bottom line ni kwamba Bunge halina leadership! Kuna figures tu zimeassume position pasina kujua wanatakiwa kufanya nini hasa kama viongozi wa Bunge.

Naomba niseme kuwa siku tutakapopata viongozi kuanzia raisi,spika, naibu spika na mawiziri bila kushikwa mikono (vyeo vya kupewa) mambo yataanza kwenda. Kwa sasa tutaendelea kushuhudia mambo ya ajabu yasioweza elezeka. SHAME
 
Mama yangu Anna Makinda pole sana kwa utovu wa nidhamu ya wabunge wako, nilidhani kwa baadhi ya wale waliotoka jeshini wangekuwa na nidhamu kumbe hakuna kitu kama hicho nikatafakari kwamba huenda miezi mitatu haikutosha kuwatia adabu nadhani ni kweli ni kipindi kifupi sana hawajaiva hao. Mtu unatarajiwa kwamba ni muungwana kwa muonekano kumbe ukiguswa tu unahazina ya matusi tena matusi ya nguoni ukiwa kwenye TV LIVE mmetia aibu sana. Juma Nkamia nilimheshimu sana tangu akiwa Radio Tanzania, alikuwa ROLE MODEL Wangu lakini kuanzia jana sitaki hata kumsikia. Leticia Nyerere mtoto wa Baba wa Taifa mtu mwadilifu aliyewalea watoto wake leo hii unasimama Bungeni na kuliomba Bunge eti kuwe na chuo cha kuwafunza wanaume namna ya kutongoza wanawake. Hivi kweli tupo serious kweli. Are you there for jokes, people trust you that you are there to discuss on how you could solve their problems, you sit and start thinking of the "Southern Part"

Si afadhali hata hiyo ya chuo cha kutongoza hebu tafakari kauli hizi ambazo zimetolewa tu hivi majuzijuzi na wabunge
-Bangi ihalalishwe
-Mbowe kaja hapa kajamba kisha akaibukia Kibaha
-Mbona unawashwa washwa?
-Siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa
-Serikali ni -------
-Chadema wakija Nzega nitaongoza kuwapiga
-Sisi ni maskini kwa kuwa noti zina picha za wanyama
-Chadema ni wauaji, magaidi nk
-Mchungaji Msigwa ni mchungaji wa nguruwe
Sasa hilo bunge gani labda bunge la mataahira
 
Greatest tusi ni kuwaibia watanzania mabilioni kupitia mikataba ya ajabu ajabu, mengine yote side show tu.
 
Yeye ndiye aliyeruhusu! Aende akaongee na mwenye mbwa na aache kuongea na mbwa
Kiuungwana kabisa mheshimiwa Juma Nkamia alitakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu si na bunge tu bali na chama chake cha CCM kwani amekifedhesha mno .
 
Si afadhali hata hiyo ya chuo cha kutongoza hebu tafakari kauli hizi ambazo zimetolewa tu hivi majuzijuzi na wabunge
-Bangi ihalalishwe
-Mbowe kaja hapa kajamba kisha akaibukia Kibaha
-Mbona unawashwa washwa?
-Siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa
-Serikali ni -------
-Chadema wakija Nzega nitaongoza kuwapiga
-Sisi ni maskini kwa kuwa noti zina picha za wanyama
-Chadema ni wauaji, magaidi nk
-Mchungaji Msigwa ni mchungaji wa nguruwe
Sasa hilo bunge gani labda bunge la mataahira
Huyu aliyetamka hivi si muungwana/mstaarabu hata kidogo.
 
Katika hali isiyo ya kawaida ukiwa noti za Sh 10,000 na Sh 5000 unaweza kukosa huduma kwa sababu ya kukosekana kwa fedha ndogondogo. Moja ya sifa nzuri za fedha ni kuweza kugawanyika katika sehemu ndogondogo. Napata hofu juu ya hali hii, yawezekana bidhaa zote zikauzwa kuanzia sh 5000 hadi 10000. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania
Hili nalo ni neno mkubwa! Nimeshangaa sana tumepanda Daladala abiria kama 7 hivi tulikua na noti za kuanzia elfu 2000/5000/10000 tukamlipa Konda, konda akadai eti tunamkomoa wakati sio kweli! Naanza kupata picha sasa noti yakuanzia 2000/1000/500 hazitakua kwenye mzunguko tena! Lets wait and see!
 
:Suti mbona siku hizi ni vazi la kawaida..
Yeye mbona anavaa suti na hatendi haki...

Aache hizo spika
lazima ngumi zipigwe ili tuwe sawa...
Eti anasema atakaetukana atampeleka polisi...!

Huu ni ujinga...!
wabunge wetu msiogope endeleeni kuwaumbua.


Watu wengi tuliacha kuangalia bunge mpaka tupate kiongozi mpya wa kuliongoza. Bora wanaotukana kulio wanafiki wa kusema ndiyo kila kitu na kugonga meza. Wabunge wengi wapunbavu sana tunajua hiki ni kipindi chao cha kupokea rushwa. Natamani kuwatukana hata mimi! ase! kitugu kyab'o
 
Back
Top Bottom