Spika Anna Makinda achimba mkwara mzito wabunge

Spika Anna Makinda achimba mkwara mzito wabunge

Akiongea kwa uchungu Spika wa Bunge Mama Anne Makinda amewashambulia wabunge wanaovaa suti baadae wanatukana matusi ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana na mdomo wake hauwezi kutamka hayo. Pia amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.


Aanza kumshughulikia Juma Nkamia kwa matusi aliyomtukana Sugu jana. Bila aibu alijaribu kuyafanya kama nahau za Kiswahili!
 
Hatimaye na mwenye mbwa(sp...ika) naye kaamua kuchachamaa.
 
:Suti mbona siku hizi ni vazi la kawaida..
Yeye mbona anavaa suti na hatendi haki...

Aache hizo spika
lazima ngumi zipigwe ili tuwe sawa...
Eti anasema atakaetukana atampeleka polisi...!

Huu ni ujinga...!
wabunge wetu msiogope endeleeni kuwaumbua.

Hivi we unatumia nini kufikiri?humo ndani ya mviringo uliopo juu ya shingo yako,mwenyewe unaita kichwa ndani yake kuna ubongo au sifongo?
 
Akiongea kwa uchungu Spika wa Bunge Mama Anne Makinda amewashambulia wabunge wanaovaa suti baadae wanatukana matusi ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana na mdomo wake hauwezi kutamka hayo. Pia amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.

suti bongo!
 
:Suti mbona siku hizi ni vazi la kawaida..
Yeye mbona anavaa suti na hatendi haki...

Aache hizo spika
lazima ngumi zipigwe ili tuwe sawa...
Eti anasema atakaetukana atampeleka polisi...!

Huu ni ujinga...!
wabunge wetu msiogope endeleeni kuwaumbua.

Anza kumpiga kwanza huyo aliye karibu yako kwanza halafu uone kama kutakuwa na usalama.jitafakari upya wewe!
 
bi kiroboto km mama thatcher kwa roho mbaya! Aangalie watu wasijefanya sherehe siku akindei
 
Wakati wabunge hasa wa CCM wanapoporomosha matusi wabunge woote wa CCM hasa hasa mawaziri hushangilia na kupiga makofi... hii inamaanisha kua matusi yanapendwa hasa hasa kama yanaelekezwa kwa wapinzani!! rotten paliamenti!!
 
Mama huyu nimeshamkatia tamaa, anaacha kushangaa watu wanavaa suti na kuongeza 0 kwenye 14,000 na mpaka leo hatujasikia Jairo kafanywa nini
 
Akiongea kwa uchungu Spika wa Bunge Mama Anne Makinda amewashambulia wabunge wanaovaa suti baadae wanatukana matusi ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana na mdomo wake hauwezi kutamka hayo. Pia amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.

Hana lolote huyo Bi Kiroboto zaidi ya kuendekeza unafiki na kutumikishwa na mafisadi waliomweka kwenye hiyo nafasi kwa faida yao. Akumbuke kuwa madhila yote yanayotokea hapa Tanzania kwa sasa na siku za usoni yeye kama kiongozi wa mhimili unaotunga sharia za nchi atakuwa anahusika na kuwajibika kwa kiasi kikubwa na hiyo hali. Ni vyema atambue pia kwamba uovu anaowafanyia watanzania hautakuwa na msamaha hata kidogo na hiyo dhambi itamtafuna maisha yake yote.
 
Huyu mama ana chekesha. Ingekua hao waliotukana ni wa upizani tu angewataka kwa majina ila kwa vile kuna wa CCM amekwepa kutaja majina. Ila huyu mama mwanzo alikua anatia hasira sasa hivi ana sikitisha tu maana inawezekana tunamlaumu bure kumbe mama mzigo alio "wezeshwa" umemshinda. Juzi wabunge wa CCM wametukana alikua anachekelea na kudai "mkuki kwa nguruwe" leo anakuja na kudai ana sikitishwa. Hii sera ya "kuwezeshwa" kweli inabidi iangaliwe upya.
 
Katika hali isiyo ya kawaida ukiwa noti za Sh 10,000 na Sh 5000 unaweza kukosa huduma kwa sababu ya kukosekana kwa fedha ndogondogo. Moja ya sifa nzuri za fedha ni kuweza kugawanyika katika sehemu ndogondogo. Napata hofu juu ya hali hii, yawezekana bidhaa zote zikauzwa kuanzia sh 5000 hadi 10000. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania

Mkuu, kwema????
 
Akija Njombe anasali sana ibada ya asubuhi na jioni kila siku.Lakini matendo yake?! Mungu tuhurumie.
 
Breaking News:Spika wa Bunge la
Jamhuri ya muungano wa
Tanzania,Anna Makinda,amesema
kuanzia leo,Aprili 16,2013,Mbunge
yeyote atakayetoa lugha ya matusi
bungeni atawaita polisi kumtoa nje
ya ukumbi wa bunge na taratibu
nyingine zitafuata baadaye.
 
Elli, nchi yetu imejaa walalamikaji, yaani hadi raisi wa nchi ni mlalamikaji. Madaraka wanayo, wafanya vurugu wanawajuwa, wauza unga wanawajuwa, waliorudisha hela za wizi wa EPA wanawajuwa, mafisadi wanawajuwa, magamba wanawajuwa, ma meremeta wanawajuwa, mandege ya jeshi ya kuiba twiga na wanyama wengine zaidi ya 100 wanawajuwa, maloliondo wanawajuwa, maTanpower resources wanawajuwa, ma IPTL wanawajuwa, ma Richmond wanawajuwa, ma siongei na mbwa bali na mwenye mbwa wanawajuwa, ma mimba zisizotarajiwa wanawajuwa, ma majizi ya bandarini alisema list anayo hivyo wanawajuwa, kwa nini hawawachukulii hatua?

Hawachukuliwi hatua kwa sababu wanaopaswa kuchukua na kuchukuliwa hatua ndio hayo hayo majizi! Kikubwa tuige mifano ya Libya na Misri tuwafurushe wote tuweke watu safi
 
Breaking News:Spika wa Bunge la
Jamhuri ya muungano wa
Tanzania,Anna Makinda,amesema
kuanzia leo,Aprili 16,2013,Mbunge
yeyote atakayetoa lugha ya matusi
bungeni atawaita polisi kumtoa nje
ya ukumbi wa bunge na taratibu
nyingine zitafuata baadaye.
Amesahau kuwa wabunge wana kinga kisheria ya kutoshitakiwa kwa lolote wasemalo wakiwa bungeni? Achukue maamuzi magumu ya kufuta hiyo kinga kisheria ili mtu akitukana akamatwe na kuburuzwa mahakamani ndio bunge litakuwa na nidhamu!
 
Back
Top Bottom