Spika Anna Makinda achimba mkwara mzito wabunge

Spika Anna Makinda achimba mkwara mzito wabunge

Nilishangazwa na muda wa uchangiaji, walikuwa wanapewa muda wa dakika 5 kuchangia. Lakini nadhani saa zilizokuwa zinatumika kupima muda zilikuwa tofauti. Akiwa anachangia mbunge wa upinzani saa inatumika ya tiGO (inakula sekunde fasta fasta) lakini akichangia wa CCM saa inayotumika ya Airtel (taaartibu) yaani dk 5 zilikuwa kama dk 10 za muda wa kawaida!

Makinda/Ndugai tendeni haki la sivyo ndonga mtindo mmoja!
 
Mama yangu Anna Makinda pole sana kwa utovu wa nidhamu ya wabunge wako, nilidhani kwa baadhi ya wale waliotoka jeshini wangekuwa na nidhamu kumbe hakuna kitu kama hicho nikatafakari kwamba huenda miezi mitatu haikutosha kuwatia adabu nadhani ni kweli ni kipindi kifupi sana hawajaiva hao. Mtu unatarajiwa kwamba ni muungwana kwa muonekano kumbe ukiguswa tu unahazina ya matusi tena matusi ya nguoni ukiwa kwenye TV LIVE mmetia aibu sana. Juma Nkamia nilimheshimu sana tangu akiwa Radio Tanzania, alikuwa ROLE MODEL Wangu lakini kuanzia jana sitaki hata kumsikia. Leticia Nyerere mtoto wa Baba wa Taifa mtu mwadilifu aliyewalea watoto wake leo hii unasimama Bungeni na kuliomba Bunge eti kuwe na chuo cha kuwafunza wanaume namna ya kutongoza wanawake. Hivi kweli tupo serious kweli. Are you there for jokes, people trust you that you are there to discuss on how you could solve their problems, you sit and start thinking of the "Southern Part"

Bubu Msemaovyo,
Kwanza naunga mkono hoja yako. Hata hivyo naomba kuweka rekodi sahihi kwenye hizo red. Moja, wabunge vijana wakiwemo vinara wa siasa za matusi, kejeli na lugha zisikuwa na staha (Lusinde na Nchemba) walienda jeshini kwa week tatu na sio miezi mitatu.

Pili, bwana Juma Nkamia, mbunge wa Kondoa Kusini jimbo ambalo mwaka jana limepandishwa hadhi na kuwa Wilaya mpya ya Chemba, ni kati wa wabunge wenye uelewa mdogo sana na wasio na mchango wowote katika maendeleo ya nchi yetu. Anapenda kusifu kuwa ametembelea nchi nyingi sana duniani (so what???). Kwa kujua kuwa hakubaliki tena kwa wapiga kura pamoja na nguvu kubwa ya pesa aliyotumia katika chaguzi kuu mbili zilizopita (2005 aliposhindwa na 2010) anachofanya sasa ni kujifanya mtetezi wa CCM ili yamkini akumbukwe kwa hilo. Ya kwamba amewahi kuwa 'role model' ni swali ambalo linahitaji ufafanuzi.

Tatu, Leticia Nyerere, sio mtoto wa baba wa Taifa bali aliwahi kuolewa na mtoto mmoja wapo wa mwalimu.
 
Akiongea kwa uchungu Spika wa Bunge Mama Anne Makinda amewashambulia wabunge wanaovaa suti baadae wanatukana matusi ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana na mdomo wake hauwezi kutamka hayo. Pia amesema ametumiwa sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda ajifungie chumbani.

Analalamika nini wakati amewalea mwenyewe? Mpaka atumiwe sms na mwananchi ndio ashtuke kuwa the so called waheshimiwa wanatukana. Upendeleo wake umemponza na bado wataja mtukana na yeye wazi wazi ndio ataelewa maana ya kuwajibika kama kiongozi ni nini!
 
Kweli huyu mama anayasema haya sasa wakati yeye ndiye anayeshabikia matusi? Kwa hili na mahali lilipofikia, nimetokea kumdharau sana huyu mama. Tatizo huwa atumii akila zake, ni zile za kupewa tu. Hana budi kukemea na kuchukua hatua, si kusema kwa uchungu. Ukiwa unabeba upande mmoja na kukandamiza mwingine au kusimamia kiti kwa woga wa wale waliokuweka, jamii yote inakudharau. Hadi leo hii namheshimu sana Sita kwani alikuwa anatumia akili zake vizuri. Sidhani hapa ni taaluma ya sheria aliyonayo Sita pekee uwezo binafsi ni muhimu. Makinda si amezisoma na kuzielewa kanuni za bunge?. Nilikutana na Mbuge mmoja wa CCM akawa anamlaumu sana huyu mama na kuonyesha ni jinsi gani anawafanya hata wao waonekane hawana maana kwa waliowachagua. Mama, kuwa makini na fuata taratibu, utaheshimika!!! Otherwise, Bunge linakuwa kongamano la wanafunzi wa O-level. Hii nchi si ya watu wa chama fulani. Kuna watu wengi hawana vyama na wanadhurika pale hoja za kitaifa zinapotupwa kwa ushabiki wa kisiasa.
 
Mama yangu Anna Makinda pole sana kwa utovu wa nidhamu ya wabunge wako, nilidhani kwa baadhi ya wale waliotoka jeshini wangekuwa na nidhamu kumbe hakuna kitu kama hicho nikatafakari kwamba huenda miezi mitatu haikutosha kuwatia adabu nadhani ni kweli ni kipindi kifupi sana hawajaiva hao. Mtu unatarajiwa kwamba ni muungwana kwa muonekano kumbe ukiguswa tu unahazina ya matusi tena matusi ya nguoni ukiwa kwenye TV LIVE mmetia aibu sana. Juma Nkamia nilimheshimu sana tangu akiwa Radio Tanzania, alikuwa ROLE MODEL Wangu lakini kuanzia jana sitaki hata kumsikia. Leticia Nyerere mtoto wa Baba wa Taifa mtu mwadilifu aliyewalea watoto wake leo hii unasimama Bungeni na kuliomba Bunge eti kuwe na chuo cha kuwafunza wanaume namna ya kutongoza wanawake. Hivi kweli tupo serious kweli. Are you there for jokes, people trust you that you are there to discuss on how you could solve their problems, you sit and start thinking of the "Southern Part"
Hapo kwenye red huyu si mtoto wa Nyerere na hana uhusiano wowote na familia ya Baba wa Taifa..
 
Spika wetu anachemka sana; chanzo cha wabunge kutukana na kuzungumza upuuzi ni yeye na naibu wake Ndungai. Niseme wazi Anna anatuaibisha sana

EJL
 
Amedai kuanzia sasa marufuku kama Wabunge wanatukanana kwenye vyama vyao wabakie hukohuko bunge ni pahala patukufu siyo jumba la mipasho. Namuunga mkono kuna vyama matusi ni lugh yao wanajijua
 
Yote yanatokea kwa sababu spika mwenyewe kashindwa kutimiza majukumu yake. nashangaa viongozi wetu sijui ni wa namna gani? yaani sioni tofauti kati ya walioenda shule na ambao hawajaenda.. hivi huwa hawaangalia mabunge ya wenzetu? ndiyo hugombana ila kwa maslahi ya nchi na wananchi wake si ushabiki wa kipumbavu wa wabunge wa aina ya Lusinde! simshangai Lusinde na wenzake wanaofanana naye ila HAO WALIYOMPIGIA KURA, CHAMA chake PAMOJA NA BUNGE ANALOONGOZA MAKINDA MWENYEWE IT A SHAME.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Foul-mouthed MPs face expulsion from House [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 16 April 2013 22:34 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
By Peter Nyanje
The Citizen Reporter
Dodoma.

MPs who use foul language in Parliament risk expulsion from the debating chamber, Speaker Anne Makinda warned yesterday.

Expressing her dismay over the conduct of some MPs on Monday, Ms Makinda said she was fed up and would now use her powers to discipline errant lawmakers.

“I don’t know what got into some of you last evening. What you did was disgraceful and from now on, if any MP attempts to use such language I will not hesitate to order the sergeant-at-arms to immediately remove them from the debating chamber,” said a vividly perturbed Ms Makinda.

She said she had for a long time been accused of failing to use the Standing Orders to keep wayward legislators in check, adding that the rules would now be applied to the letter to restore discipline in the House.“I will make sure that abusive MPs are immediately kicked out of the House. If they want to appeal they will have to do so from outside, not inside this chamber,” Ms Makinda said. She reminded MPs that being on different sides of the political fence was not a licence for them to hurl abuse at one another.

“We did not establish political parties to be platforms for some people to attack their rivals. Political differences should not be regarded by some as a reason to insult one another. I have powers to hand you over to police and I will do that,” Ms Makinda said.“If people fail to behave themselves in this House we will establish another chamber for them to exercise their uncouth behaviour.”

Ms Makinda said what MPs did or said in the House was broadcast live across the country, adding that people were appalled by lawmakers’ behaviour.

“I have received a text message from a person who watched yesterday’s session. This person says: ‘Parliament is now out of control...from now on I will not watch Bunge sessions together with my children...I will watch them in the privacy of my bedroom’,” she said.

“Please, behave yourselves... there are some things which, according to your status, you are not supposed to say in public,” Ms Makinda said, noting that voters did not send MPs to Parliament to abuse one another.
Ms Makinda’s sentiments were echoed by Science, Technology and Communication deputy minister January Makamba, who noted that what happened on Monday was “very unfortunate”.

“It is amazing that when we are working in our committees, or even when we meet at the canteen, we are cordial to one another, but when we come here, when the TV cameras are on, we change completely,” Mr Makamba said when debating the Prime Minister’s Office’s 2013/14 budget estimates.

He said MPs could make their voices heard without being abusive. Ms Makinda’s rebuke followed fierce verbal exchanges between MPs from CCM and CUF, on one side, and Chadema on the other.

Instead of debating the PMO’s estimates, some MPs from the two camps attacked one another, and some went as far as using unprintable epithets to the chagrin of Prime Minister Mizengo Pinda, whose budget speech was being discussed.

Attempts by Deputy Speaker Job Ndugai to appeal to MPs to observe civility were ignored and some lawmakers stepped up their verbal attacks.

At one point, State Minister in the Prime Minister’s Office William Lukuvi stood up and told Parliament that they were aware that the Chadema camp had planned well in advance to attack their CCM counterparts.

“We know, for instance, that Chadema substituted two MPs who were supposed to contribute this evening with other legislators, who said what they have said,” he said.

MPs who used language that riled others include Livingstone Lusinde (Mtera-CCM), Rev Peter Msigwa (Iringa Urban-Chadema), Juma Nkamia (Kondoa South-CCM), Ezekiel Wenje (Nyamagana- Chadema), Khatib Said Haji (Konde-CUF) and Muhammad Amour Chombogo (Magomeni-CCM).

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
images
​
Matusi ya Wabunge wa CCM:
Juma Mkamia (Kondoa - CCM).​


  • [*=1]Alimtukana Mbunge wa Chadema Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) kuwa ni mbwa na hawezi kuzungumza naye bali na mwenye mbwa.
    [*=1]Alimtukana mbunge wa NCCR Mageuzi Mbunge wa Kasulu Mjini Moses Machali kuwa si mtu makini hivyo hawezi kutilia maanani hoja zake.
Livingstone Lusinde (Mtera - CCM).
​


  • [*=1]Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde alitoa lugha ya maudhi kwamba ndani ya bunge kuna watu wana mimba zisizotarajiwa.
Mohammad Amour Chombo (Magomeni - CCM).
​


  • [*=1]Mbunge wa Magomeni Mohammad Amour Chombo alimtukana Mbunge Wenje kwa kusema: "Serikali yetu haina nguvu za kiume, lakini niseme wewe Wenje ni sawa na uzi wa kulainisha kabla ya kuingizwa kwenye tundu la sindano."
    [*=1]Aliunga mkono tusi la Mbunge wa CUF Khatibu Said Haji kwamba Mchungaji Msigwa yawezekana ni mchungaji wa wa nguruwe.

images


Wabunge wa Chadema waliotoa lugha za matusi:
Ezekiel Wenje (Nyamagana - Chadema)
​


  • [*=1]Mbunge wa Mwanza Ezekiel Wenje alisema the government is impotent, incompetent, kauli ambayo ilitafsiriwa na baadhi ya wabunge wa CCM kwamba amesema serikali haina nguvu za kiume.
Mchungaji Msigwa (Iringa - Chadema)​


  • [*=1]Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa alitumia maneno ya biblia kutoka kitabu cha Mithali 27:22; "Mpumbavu ukimchukua, ukimchanganya na ngano kwenye kinu atabaki na upumbavu wake." Hivyo utendaji wao wanaofanya ni sawa na kuruhusu akili ndogo kuongoza akili kubwa.
    [*=1]"Tatizo ninyi Wazanzibar hamtaki kuguswa, kuhoja mambo mnayofanya likiwepo la kila mwananchi anayeishi Zanzibar afunge wakati wako watu wa dini tofauti. Mimi nawaambieni kamwe hamuwezi kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya kiislamu."

Matusi ya Mbunge wa CUF:
Khatibu Saidi Haji (Konde - CUF)
​


  • [*=1]Alimtukana Freeman Mbowe mbunge wa Hai kwa kusema "Mbowe kaja hapa anajambajamba tu" akilalamikia hoja ya Mbowe kuhusu idadi ya watu wa visiwani.

    [*=1]Amtukana Mchungaji Msigwa: "Wewe Msigwa ni mchungaji wa watu au mchungaji wa nguruwe? Alitoa tusi hilo kutokana na Mchungaji Msigwa kutoa kauli ya kwamba Zanzibar kuna udini.

 
Huwa namuonea huruma sana Bi Kiroboto anavyopata wakati mgumu hasa pale mbunge wa upinzani akiwa anachangia. Sura yake inatibuka zaidi.
 
Back
Top Bottom