Special thanks to JF and a polite proposal

Status
Not open for further replies.

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,352
1,935
Nachukua fursa hii kuwashukuru sana wenzetu wanaomeneji, kuratibu na kuendesha JF kwa jinsi walivyoifanya hii kazi kwa uaminifu na bidii kubwa tangu ianze na hata tunapoenda kuuaga mwaka 2007. Niwashukuru kipekee kwa jinsi walivyohakikisha kuwa mtandao huu unabaki imara katika kipindi muhimu cha uchaguzi wa Kenya. Baada ya shukrani hizi naomba nitoe pendekezo hili.

Kwa muda mrefu sasa tangu kuanza kwake JF imekuwa ikiendeshwa kwa kujitolea kwa baadhi ya wenzetu chini ya usimamizi makini wa ndugu yetu Invisible. Hata hivo naogopa kwamba hapa tulipofikia tupo juu sana na chochote kikitokea kama kile kilichotupata kule bcs itakuwa ni pigo kubwa kwa watanzania popopte pale walipo katika dunia hii. Nafikiri kwamba hapa ilipofikia JF inahitaji iendeshwe kitaasisi zaidi kuliko kutegemea watu wachache kujitolea pekee. Ni kwa sababu hii napendekeza kuwa wakati sasa umefika wa kuiendesha JF kitaasisi zaidi. Ninapendekeza mambo mawili yafuatayo ili kuhakikisha JF inabaki na kuimarika zaidi:

i) Pamoja na aina ya membership system iliyopo, tuwe na subscription membership. Hii itatusaidia kuwa na operating fund wakati wote -wa raha na shida-na hivyo kuhakikisha kuwa panapotokea matatizo ya kiufundi yanayohitaji mapesa, JF inaendelea bila kuwabebesha wachache wetu mzigo. Subscription membership iwe open kwa yeyote anayetaka na anayependa. Napendekeza kwa kuanzia tuanze na subscription fee ya US$100 kwa mwaka. Modalities za kukusanya hii nawaachia wengine kama wazo litakubalika.

ii) Tuwe na ka-board of directors ambao watawasiliana kutoa maamuzi critical yanayohitaji consultation kuhusu maendeleo ya JF. Wajumbe wake watoke miongoni mwa fully paying subscribing members.

Lengo la pendekezo langu hili ni kuifanya JF iwe endelevu zaidi na kuifanya ikae kitaasisi zaidi. Ili kufanikisha hili tunahitaji pia kuangalia jina lake na pengine kufikiria uwezekano wa kuiandikisha rasmi. Pengine tungeweza kuwa na jina: JF Internationa Online Centre for Public Debates, etc etc.

Of course najua kuna pending issues: eg t-shirt, sijui hii imefikia wapi?

What do you think?
 
Mkumbo wazo lako ni zuri, mapendekezo yangu ni kwamba iwe chini ya taasisi isiyolenga kupata faida (Not for profit organisation) iwe ni foundation yenye jina kwa mfano Jambo forums Foundation, etc, etc,na isajiliwe katika mojawapo ya nchi za huko ughaibuni USA, UK etc. Ikisha sajiliwa wajumbe wa bodi wataona namna ya kuweza kuiendesha kwa michango ya hiari au kupitia wafadhili mbalimbali kwa nia ya kuimarisha demokrasia katika nchi za afrika mashariki. Hili linaezekana sana tu.

Nawatakia heri ya mwaka mpya 2008
 
Kitila,

Wazo zuri sana.Ni vizuri kuipa nguvu JF kwa namna yoyote ile ili iweze kuwafikia wengi.JF imetusaidia sana kupata habari hasa katika kipindi hiki kigumu cha kutaka kujua ukweli...

-Wembe
 
Mkuu umeniwahi...:) lakini halijaharibika neno. Pia nilitaka kuuliza swali je akitokea kibopa anataka kuinunua JF kwa nia ya kutunyamazisha itakuwaje? Maana kama mnavyofahamu baadhi ya magazeti yamenunuliwa na vibopa na magazeti hayo yakabadilisha kabisa mwelekeo wa habari zake kiasi ambacho wapenzi wa magazeti hayo hawataki kuyanunua kabisa. Mimi naunga mkono wazo lako, lakini kuna wenzetu wengine kiasi hiki cha $100 kitawaongezea mzigo mkubwa mno katika gharama zao za kila siku za maisha. Hivyo tufikirie pia ni jinsi gani ya kuwasaidia wanachama hawa ili nao waendelee kuwa wanachama na kuweza kuchangia katika mijadala mbali mbali.
 
Wasiwasi wangu tukii'formalise' itapoteza character yake. Iendelee hivi hivi nawale wanaopenda kuichangia wafanye hivyo. Tunazo taasisi nyingi za kutosha, hatuhitaji nyingine. Tukumbuke nguruwe walivyofanya kwenye Animal Farm. Tusielekee huko. Special privileges etc. etc.
 
Wazo zuri sana. Lakini nafikiri kwa njisi watu wanavyotumia majina ya bandia ili kuwa incognito humu sijui kama wengi watadhubutu kujiandikisha uanachama. Nafikiri wazo la Ngereja ni vizuri likafikiriwa na kufanyiwa kazi. sisi ma-incognito tujaribu kutafuta namna ya kuichangia JF!!!
 
Pamoja na mawazo mazuri, ila kumbukeni unajiandikisha then legally mnakuwa liable kushitaki au kushitakiwa kwa lolote litakalotokea hapa JF.

Pili kwa mafanikio tuliyoyapata tukishajiandikisha kuna watu, vikundi vya watu, mashirika watapenda kujiassocoate nasi kwa kutoa misaada kusaidia JF lakini itakuwa ndio kuinunua kidogo kidogo JF mwishowe itabinafsishwa.

Hivyo tujadili kwa undani tusikurupuke
 
If it is not broken, don't fix it. Kukiwa na ada, basi washiriki wengi ambao ni wanafunzi watajitoa.

Naona kuna fursa ya kuchangia kwa wale watakaopenda kufanya hivyo.

Naungana na wengine kuwashukuru viongozi wa JF kwa kazi nzuri na inayozaa matunda mengi. Kama kutakuwa na ULAZIMA wa kubadilisha mfumo wa sasa, basi naomba watushauri. Ifahamike lakini kwamba ni lazima kujua matokeo ya mabadiliko yatakuwa yapi kabla ya kubadilisha.
 
acheni hii JF ibaki kuwa freelance intelligency, ingekuwa registred K-T tusingempata na hawa intelahamwe tusingewajua, kwani media zote za kenya zimezimwa, hata hao reuters na AFP wako kimya. Mie nashauri ifunguliwe account ya siri tuweze kutuma fedha ya kusaport hii site na kuzawadia reporters kama K-T, tutatuma dola hata kwa siri kwenye bahasha.
 
Nakubaliana nawe Eddy kabisa .Wazo la Kitila ni jema sana sana lakini namna tunavyo pambana kwa fikra na kila kitu nasema tuendelee kuwa hivi .
 
Kitila,
Umetoa wazo zuri sana na hata huko nyuma limewahi kujadiliwa lakini bila ya uamuzi kutolewa.

Kuna mambo tunayopata kuzingatia wakati tunajadili hili. JF ni chombo kinachomilikiwa na watu binafsi, tukifikiria mabadiliko hayo lazima tuangalie hiyo ownership itakuwaje? Japo watu wachache watakuwa tayari kusaidia kuchangia lakini kama ownership itaendelea kuwa ya mtu au watu wachache naamini itakuwa ngumu sana kuwashawishi wanachama wengi zaidi kusaidia.

Tukitatua hilo suala la ownership ndipo mambo mengine yanaweza kujadiliwa ikiwa ni pamoja na kuunda board, kuisajili kama NGO nk.

JF inaweza kufanya mambo mengi makubwa hasa kwenye hili la kukuza demokrasia Tanzania lakini lazima kwanza tukubaliane masuala ya ownership na funding issues.
 
Mimi nimesoma maoni yote ya wenzangu na nakubaliana nayo kabisa.

Mawazo yote ni katika kujaribu kuimarisha forum hii ili iwe bora kabisa na iwe moto wa kuotea mbali.

Mimi wazo langu kuu ni kwamba, forum hii ijiendeshe kama ilivo kwa sasa ila wawepo watu maalumwa kuhakikisha forum hii inasimama kifwedha lakini isiwe taasisi.

Pia mimi binafsi nipo tayari kusaidia suala lolote kwa uwezo wangu kuhakikisha JF inaendeshwa kisasa lakini kama "donner".

Kuna vitu vingi tu vinahitajika kama kuboresha kama "server" "memory" na "HDDs" ambazo ndio nguvu kubwa ya uendeshaji wa jambo kama la JF.

Ila suala la malipo au mchango kidogo sio baya kwani ndio litaendesha forum hii kwa uimara zaidi.

Napendekeza JF iwe na Account maalum na mimi nikiwa mmoja wa wanachama ntakuwa tayari kutumbukiza fwedha humo kwa uwezo wangu iwe kwa mwezi au kwa mwaka.

Kuna vitu vingi tu vya kuongezea katika JF kama E-news, na mijadala hai "Live Discussions" ambazo zitavutia wanachama wengi na kutoa masuluhisho mablimbali kwa jamii.

Lakini vitu hivi vinataka watu kama Invisible na "dedication" kama ya wenzangu na wengine.

Ila suala la "Annonymity" sio tatizo kwani kuna njia nyingi tu ambazo ntajaribu kumshauri Invisible na ma-expert wengine katika PMs zao.

Mimi ntapenda kubakia na jina langu la Richard na naona ni zuri tu, kwani sioni kama mawazo yangu ni ya kutukana watu au ni utovu wa adabu, bali ni kuonyesha msimamo wangu wa mawazo na kusema kile nnachofikiria nikipanga mantiki na vigezo.

Mwisho napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wanachama na wageni wote katika forum hii kwa kuweza kuwa pamoja katika mwaka huu wa 2007.

Kama binadamu labda kuna waliokuwa na doubts na mawazo yangu na wako wale ambao wameyapenda. Lakini mimi ntajaribu kuboresha mawazo yangu ili yawe na "clear picture" zaidi.

Nawatakia kila la kheri katika mwaka ujao wa 2008 uwe wa mabadiliko makubwa katika JF na Idumu JF!
 
Good things in life are free...napendekeza kinyume cha pendekezo la kulipia wa mwaka. Wanachama waendelee na utaratibu wa kuchangia kwa hiari.

Naunga mkono hoa ya 2 ya Mhe KM na pendekezo la Mhe A. Moshi.
 
Nashukuruni sana kwa mawazo haya chanya. Labda nifafanue mambo manne yafuatayo:

i) niliposema kuwe na ada simaanishi kwamba basi wale ambao hawakulipa hawatakuwa wanachama. Lahasha, ila tu kuwa wale watakaolipa watakuwa na added advantage, eg., kuwa na membership card, kuweza kuwa wajumbe wa bodi, etc. Lakini kila mtu ataendelea kuwa member kwa maana ya kuchangia kama ilivyo sasa. Vilevile haina maana kwamba watu watalazimishwa kubadilisha majina na kutumia majina yao halisi, lahasha. Lengo ni kufanya uendeshaji wa JF uwe endelevu na wa kitaasisi zaidi.

ii) Wazo la ownership: na hapa ndipo wasiwasi wangu ulipo. So far tumetegemea good will ya owners wa hii forum ambao kwa kweli wengi wetu hatuwajui! Sasa maanake ni kwamba siku hawa wa bwana/mabibi wakapata matatizo ya kifedha, kiufundi au good will yao ikaisha, utakuta JF inapotea ghafla, halafu ndio utakuwa mwisho wetu. Tunakumbuka sana yaliyotukuta bcs (nafafanua zaidi hapo chini (IV).Wasiwasi wangu ni kwamba hiki chombo sasa kimekuwa cha maana mno kiasi kwamba kukiacha kwa mtu mmoja pekee is a bit risk.

iii) "If it is not broken, dont fix" (A. Moshi). This is only partly true. Tunapaswa pia kuweka mipango ya kuendelea zaidi. Sasa kwa sababu nguo haijachanika haina maana kwamba usinunue ingine. Kuna methali zingine nyingi zinazoweza ku-counter hii methali.

iV)More importantly, tuna mfano au uzoefu wa kutisha kwa yale yaliyotukuta kule bcs. Ile forum ilipamba moto kama hii, lakini ghafla ikajifia na tukapotezana na hadi leo kuna watu hawajawahi kuamini hizi forum tena wakidhani kwamba ipo siku itakufa tu. Ile forum ilikufa tu kwa sababu aliyekuwa anaiendesha (business times) alijiunga na CCM na akapata ubunge na hivyo akaona kwamba mawazo mengi hayakuwa na tija kwa CCM na hivyo akaamua kuifunga. So, unaweza ukaona umuhimu wa kuifanya kitu kama hiki kikubwa kikaendeshwa kitaasisi zaidi kuliko mtu moja.

Nasisitiza tu hapa kwamba wazo la kutoa michango halina maana kwamba litawafanya wale wasiochangia wasiwe members. Bali ni kujaribu kuwa na njia ya uhakikia na institutionalised ya kuwa na source of income kuliko kutegemea tu michango ya hiari na appeal za akina MKJJ pale tatizo likitokea. Wafadhili pia kama akina mhe Richard na Yeboyebo wataendelea kuwepo na kupewa nafasi.

More ideas please? Kufikia tarehe 3 Januari nita-compile mawazo yote na kutoa summary hapa kwa ajili ya wayfoward. Na pia tutawashirikisha wamiliki ili kuona wao wana mawazo gani kutokana na yale wananchi watakuwa wamependekeza.
 
Tuwe Makini, mpngo wa kujisajili rasmi una hatari zake.. Angalieni namna yahoo walivyobreak privacy yao kwa watawala wa CHINA..Jamaa wanaozea NDANi sasa.
Najua kwa utaratibu wa sasa Admin akikamatwa na WATAWALA ili atoe data za wachangiaji wote humu ndani, atlast anaweza wataja wote au akarelease hizo details, kufuatilia issues za IP sio tatizo kwa watawala wakiamua wamtafute nani...
Namna ya JF kujiendesha nafikiri wasamalia wema waendelee, pia matangazo ya Kugoogle kila liktokea kila mmoja a-click atleast 10-20 times...JF itapata pesa. Admin hajasema kiasi gani chahitajika kuioperate na kuisimamia. ALAU AJE ATUPE overal cost kiasi gani na namna Gani AD za google zinavyoweza kuraise Funds...
 
i) niliposema kuwe na ada simaanishi kwamba basi wale ambao hawakulipa hawatakuwa wanachama. Lahasha, ila tu kuwa wale watakaolipa watakuwa na added advantage, eg., kuwa na membership card, kuweza kuwa wajumbe wa bodi, etc. Lakini kila mtu ataendelea kuwa member kwa maana ya kuchangia kama ilivyo sasa. Vilevile haina maana kwamba watu watalazimishwa kubadilisha majina na kutumia majina yao halisi, lahasha. Lengo ni kufanya uendeshaji wa JF uwe endelevu na wa kitaasisi zaidi.

Mimi humu ni mgeni kwa hiyo pengine sifahamu inside story. Kilichonivutia na kinachonifanya niendelee kuchangia hii Forum ni usawa uliotawala. Kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake hata kama ni pumba. Kama ni pumba watu hawasiti kukueleza hivyo bila kujali nafasi yako. Watanzania kwa bahati mbaya tunapenda elitism, ndiyo maana kwenye shughuli zetu hapakosi high table kuwatofautisha wageni. Wabunge wetu baada ya kuitwa waheshimiwa nao wamekuwa waheshimiwa, hawataki kabisa kulinganishwa na mwananchi wa kawaida. Wasiwasi wangu ni kuwa hili pendekezo linaelekea hukohuko. Haitoshi wengine kuitwa Expert Members, Senior na Junior sasa mnataka vitambulisho na meza zilizopambwa vitenge na maua! I share your concerns kuhusu sustainability lakini tuangalie tusije tukapoteza kile kinachoifanya JF unique. Nimeelimishwa sana na hao nisiowajua. Mara nyingi tu nimesahihishwa nilipokosea na ninawashukuru kwa hilo. Wakati mwingine tumekubali kutofautiana bila natumaini kuweka uadui. Ni hapa tu inapowezekana.

Nimejenga heshima kubwa kwa wale ambao ni public figures wanaodiriki kuchangia na kubadilishana mawazo katika hili pori. Nimetambua kuwa nchi yetu imebarikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa na watu ambao wanauchungu nayo kwa kiasi kikubwa hata wakati wanakuwa critical. Kwa yote haya nawashukuruwakina invisible na wenziwe nisiowajua. Mungu awabariki sana.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom