Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,647
CHADEMA,
Kwa vile sasa mmeshakiri rasmi kwamba CCM wamewacheza [played you], hamna budi kujaribu mbinu nyinginezo katika harakati zenu za kuleta mabadiliko ya kisiasa.
Civil disobedience na passive resistance.
Hamasisheni watu waanze kugomea matendo ya serikali ya CCM.
Mifano:
1. Msishiriki kabisa chaguzi zozote zile zilizopangwa kufanyika chini ya mazingira yaliyopo hivi sasa. Wahamasisheni na watu waache kushiriki. Wahamasisheni waache kujiandikisha kupiga kura. Pia, vishawishini na vyama vingine vya upinzani visishiriki kabisa katika chaguzi zozote zile.
2. Washawishini wananchi waache kujitokeza kwenye sherehe zozote zile zilizoandaliwa na serikali.
3. Washawishini wananchi waache kujitokeza kwa wingi sehemu ambazo viongozi wa CCM wanakuwepo. Mfano, kama Rais ana ratiba ya kwenda kufungua mradi sehemu, wananchi wasiende. Wamwache rais na maCCM wenzake washiriki peke yao.
4. Natamani sana waajiriwa wote wa serikali kufanya migomo inayolenga kuipa shinikizo serikali ya CCM ili yapatikane mabadiliko ya kweli ya kisiasa.
Mbinu zingine mtachangia na wengine. Ila ni lazima ziwepo kwenye wigo wa civil disobedience na passive resistance.
Natambua kwamba kuyatimiza yote hayo si kazi rahisi, hususan kwenye hii jamii yetu ambayo imejaa uoga wa kupitiliza.
İli yote hayo yatimie, ni lazima wengi wetu tuwe on-code. Bila ya kuwa codified, hakuna kitakachotimia.
Kwa wale waliopo Marekani, nawatakia siku njema ya mapumziko ya sikukuu ya MLK Jr. hapo kesho Jumatatu tarehe 16.
Binafsi ninamkubali sana MLK Jr. He was super brilliant.
MLK day ndo imenipa hamasa ya kufungua mjadala huu kwa sababu Dr. King na wenzake walitumia hizo mbinu za civil disobedience na passive resistance katika kuishinikiza serikali ya Marekani kuufuta ubaguzi wa rangi wa kitaasisi [institutional racism].
Mwamko huo wa kuipa shinikizo serikali ya Marekani ulichochewa na mwanamama Rosa Parks ambaye siku moja anatoka kazini akiwa amechoka, alikataa kuachia siti yake kwenye basi ili kumpisha mzungu akae kama ambavyo sheria ilivyokuwa inasema.
Kukataa kwake huko ndo kukazaa Montgomery Bus Boycott iliyodumu kwa mwaka mzima. Mgomo huo pia ndo uliomweka Dr. King kwenye chati za uanaharakati na mengineyo yaliyobaki yakawa ni historia.
Mgomo huo pia ulipelekea mahakama ya upeo ya Marekani [US Supreme Court] kutoa uamuzi kuwa sheria za jimbo la Alabama na za mji wa Montgomery zilikuwa zinaenda kinyume na katiba ya nchi.
Pata picha endapo watu wanagoma kupanda ndege za ATCL. Wanagoma kupanda mwendokasi, n.k., mwisho wa siku serikali haitakuwa na jinsi zaidi ya kuwasikiliza watu kwa umaanani.
Najua kuandika tu na kutoa mawazo huku umekaa nyumbani kwenye kiti chako ni rahisi zaidi kuliko kutenda.
Lakini pia, hakuna tendo la kibinadamu linalotokea tu bila kuanza kama fikra kichwani.
Katika jitihada za kuleta mabadiliko nchini, ni lazima kujaribu mbinu mbalimbali.
Civil disobedience na passive resistance ni mbinu ambazo zimeleta mabadiliko sehemu nyingi tu hapa duniani.
Na kama huko kwingine mafanikio yalipatikana, basi naamini hata hapa Tanzania inawezekana pia.
CHADEMA, NCCR, and others, add this arrow in your quiver. It works.