Special message to Mama Janeth Magufuli

Special message to Mama Janeth Magufuli

Habari mama,

Pole sana kwa msiba wa mumeo!, alikuwa great leader na wananchi wengi wanamkumbuka kwa utumishi wake ingawa ulikuwa mfupi kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi yetu.

Hiyo Pole niliyotoa ni ya kawaida kwasisi binadamu maana wote tumefiwa wapendwa wetu lakini lengo kuu ni Pole kwa unayosikia na kuona kejeli na kubagazwa kwa marehemu mume wako hadharani bila woga tena kwa mambo mengine yasiyo msingi.

Sikia mama, mume wako alitimiza wajibu wake bila kujali pale alipokosea lakini wewe u hai ubavu wake ukisikia maneno magumu sana. Pengine unalazimika kuwatia moyo watoto lakini wewe mwenyewe umebeba mzigo mzito.

Imagine hata leo maneno yaliyotamkwa mbele yako! Tushukuru mama Samia walau kutuliza moyo wako baada ya maneno magumu leo lakini sio rahisi.

Endelea kuvumilia malimwengu, endelea kuipenda Tanzania! Jipe moyo kama Bikira Maria alivyojipa moyo alivyoshuhudia mwanae akiteswa na kufa msalabani!

Endelea kujipa moyo kama Bikira Maria alivyovumilia hata waliomtenda ubaya Yesu walipoeneza uzushi dhidi yake kuwa wanafunzi wake wamemwiba hakufufuka. Haikuwa rahisi ila moja ya tunu tunayojifunza juu ya Bikira Maria mara nyingi ni yote aliyaweka moyoni!

Kasome utenzi wa Bikira Maria Luka 1: 46-55 Ukutie nguvu. All shall be well
Leo CCM wamedhihirisha namna walivyo.

Mwenyekiti wa CCM Taifa alichokifanya ni kupoozesha hali na siyo kukemea upuuzi wa wazee wa chama ambao wamemtuma Makamba aseme kuwa wao ndo waliamua kukataa na kumtaka mungu wao afanye kilichomtokea JPM

Watanzania tunapaswa kutafakari sana haya maneno ambayo akina Nape, January na hatimaye yanasemwa kwa umma kupitia mkutano wa Kikatiba ws CCM.

Kuna maana kubwa sana kwa CCM kuendelea kushika madaraka. Nina mashaka namna vyombo vya dola vinavyonufaika na huu utawala wa kikatili wa CCM

Tutafakari. Tusiache kutafakari sana

2025 siyo mbali
 
Acha uchochezi na uchongqnishi mleta mada. Hakuna aliyemnanga jiwe leo. Hayo ni mawazo yako tu.

Hebu mtaje mtu aliyemtaja jiwe kwa jina lake. Vinginevyo ni uzushi na uzandiki tu unaojaribu kuueneza.
Unajaribu kujificha kwenye shamba la karanga.
 
Man,

Hao akina MTAZAMO wanajiona wao ndo wana uchungu zaidi na JPM kuliko hata Mama Janeth mwenyewe!!

Ni kutokana na hilo ndo maana wakiona mtu anaongea wasichotaka wao kukisikia basi wanamuona ana chuki dhidi ya JPM

In short, source ilikuwa hotuba ya Mzee Makamba, na kama kawaida yao, akaanza kumwagia sifa Samia! Wakati akiendelea na hizo sifa, ndipo akasema maneno haya:-

Baada ya kuongea hayo hadi JK akashika kichwa...

Sasa Mzee Makamba akaona amekosea kusema "Ukiondoka kabla ya 2025 Mungu atatupa mtu mwingine" na katika kujikosha, ndipo akasema maneno haya:-

Sasa akina MTAZAMO ndo wanaona Makamba kamaanisha Magufuli alikuwa mtu mbaya ndo maana amekufa kumbe alikuwa anajikosha kutokana na kauli yake kwa SSH kwamba akiondoka kabla ya '25 Mungu atawapa mtu mwingine...

Cha ajabu, hata Mzee Mkapa amefariki... lakini kutokana na paranoia, wao wanaona kasemwa JPM...

Msikilie mwenyewe hapa...


Sawa
 
Leo CCM wamedhihirisha namna walivyo.

Mwenyekiti wa CCM Taifa alichokifanya ni kupoozesha hali na siyo kukemea upuuzi wa wazee wa chama ambao wamemtuma Makamba aseme kuwa wao ndo waliamua kukataa na kumtaka mungu wao afanye kilichomtokea JPM

Watanzania tunapaswa kutafakari sana haya maneno ambayo akina Nape, January na hatimaye yanasemwa kwa umma kupitia mkutano wa Kikatiba ws CCM.

Kuna maana kubwa sana kwa CCM kuendelea kushika madaraka. Nina mashaka namna vyombo vya dola vinavyonufaika na huu utawala wa kikatili wa CCM

Tutafakari. Tusiache kutafakari sana

2025 siyo mbali
Pamoja na kumpa faraja Mama Janeth, tumuombee afahamu neno hili la maarifa, Mungu ana upande mmoja tu, hakunaga habari ya vugu vugu..mikutano ya ccm ni sherehe za kukufuru Muumba, ukitafuta sabab hasa ya kualika watu wenye hadhi kama yake Mama Janeth haionekani..lakini ukikubali kushiriki sherehe za aina hiyo, siku Mungu anapindua meza hutasalimika itakuwa bahati mbaya kwake..tumuombee ajue neno hili sherehe hizi si njema kwa maisha yake baada ya maisha ya hapa duniani.
 
Wako na Slaa toka kwenye Ukatoliki
I see...

Uongozi kazi sana aisee

Yaani nilivyokuwa namkubali MTAZAMO miaka ile, wallah kama ningekuwa Kiongozi wa CHADEMA ingekuwa nimeshampa madaraka bila kujua kwamba kumbe allegiance yake haikuwa kwenye chama bali kwa mtu!

Mi bhana wala sitaki kuwa mnafiki... binafsi sikutaka kabisa kumwelewa Mbowe kwa hatua yake ya kumwengua Slaa na kumleta EL, kwa sababu yule mzee nilikuwa namkubali sana!

Lakini kwa upande mwingine, nilitoa heshima kubwa sana na heshima hiyo itaendelea kubaki kwa wana-CHADEMA ambao hatimae walikuja kumgeuka Dr. Slaa pamoja na ukubwa wake kwenye chama!

Heshima yangu kwao ilikuwa ni ile kuonesha NO ONE IS BIGGER THAN chama kwa sababu haya mambo, weka mahaba yako kama yote kwa mtu wako lakini mwisho wa yote, CHAMA FIRST, mengine ndo yanafuata!
 
..hotuba nzima ya Mzee Makamba hii hapa.

..naomba muisikilize ili kutenda haki.

..kwa mtizamo wangu kuna baadhi yetu wanaikuza au kuipa tafsiri potofu kauli za Mzee Makamba.

..kinachoendelea hapa ni sehemu ya michezo michafu ya siasa.

 

Ukweli ni kwamba leo mtu mzima amekosea, ameropokwa na ametia aibu.
Kauli yake haikuwa ya afya na Rais amejua alimaanisha nini na ndio maana akashindwa kuikalia kimya.
Hawa wazee madaraka yamewalevya
 
Kuna siku niliwahi kumuuliza ikiwa hivi kweli alikuwa mfuasi wa CHADEMA au alikuwa mfuasi wa Slaa!

Back in the days niliamini kabisa kwamba MTAZAMO alikuwa Mfuasi wa CHADEMA Kindakindaki!!

Baada ya Dr. Slaa kuondoka CHADEMA ndipo nilipokuja kugundua kumbe hakuwa mfuasi wa chama bali mfuasi wa mtu, na tangia hapo, ukiongea jambo tofauti kuhusu JPM tu basi lazima aku-brand kwamba una chuki...
Umenikumbusha makala za mwanakijiji enzi za JK mpaka niliamini ni mpinzani...

.....kumbe hakuwa mpinzani ila mpenzi wa Ccm aliyechoshwa na utawala wa JK tu ndio maana enzi ya JPM alirudisha majeshi.
Erythrocyte
 
..hotuba nzima ya Mzee Makamba hii hapa.

..naomba muisikilize ili kutenda haki.

..kwa mtizamo wangu kuna baadhi yetu wanaikuza au kuipa tafsiri potofu kauli za Mzee Makamba.

..kinachoendelea hapa ni sehemu ya michezo michafu ya siasa.


Huenda mahasimu wake wanajaribu...... "ku-capitalize hii kauli for political gain and public sympathy"....ila siasa mchezo mchafu Sana...

Ila ni vyema kuchunga kauli zetu tunapoongea mbele ya hadhara.
Chige Tindo Pascal Mayalla
 
Mungu amempa neema ya kuishi yule mzee leo anatukana wafu, baba tenda muujiza... iwe barabarani, au hata akinywa maji apaliwe, au hata akilala tu tuone imeisha iyo...
 
Back
Top Bottom