Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.
Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; Na wanyonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake;
Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele.