Kwenye kutangazwa mshindi ndio penye tatizo, hapo ndio ccm panapo wafanya waendelee kubaki madarakani, sasa wewe ambaye ulikuwa unasubiria kumzidi ccm kwa kura nyingi kwenye uchaguzi ndio nakuuliza nani atakutangaza wewe kuwa ndio mshindi au ndio yale ya marehemu Maalim Seif ya kujitangaza mwenyewe?
Ndiyo maana nakwambia kuwa ccm wamejimilikisha hiyo nafasi ya urais kuwa ni yao tu kivyovyote vile, watu wanasema ccm wanategemea dola kubaki madarakani watu wanataka tume huru ya uchaguzi yote hayo kwa sababu wameona tatizo lilipo. Ila wewe unaniambia mie napotosha na kwamba et upinzani kura zao zilikuwa zinaongezeka hivyo unaamini ingekuja kutokea upinzani kupata kura nyingi za urais na kupata urais!
Elewa kwamba tatizo sio ccm kuiba kura tu bali ni kwamba ccm wanatumia njia zozote zile ili kubaki madarakani, we kubali tu ukweli wa kwamba ccm wanawaanchia ubunge na udiwani ndio mgawane ili kubalance ila sio urais.